mambo yanazidi kunoga na wadau wa pembe zote za dunia wameamua kufanya kweli kwa kutuletea mavituz wanayofanya huko waliko. nawasifu na kuwapongeza sana na pia kuwashukuru kwa kuwa na imani na blogu yetu hii. mambo ya australia ni kama ifuatavyo hapo juu na chini


SO it is that moment again in Sydney where the Muuungano day is celebrated by having a Kanga Party in the heart of Sydney. Kanga Party portrays the beauty of an African women in so many ways, dressing, dancing, etc.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Balozi wa Tanzania nchini Uingereza amesema serikali ya awamu ya nne imedhamiria kivitendo kuuimarisha muungano ambao hivi sasa umetimiza miaka 43.

    Balozi Maajar aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na mabalozi wa nchi mbali mbali waliopo nchini Uingereza na wageni wengine waalikwa.

    Alisema serikali ya Rais Kikwete imeanza kushughulikia kero mbali mbali za muungano sambamba na ahadi zilizokwishatolewa awali, ‘’ Serikali ya awamu ya nne imeanza kutekeleza hatua mbali mbali katika kuudumisha, kuulinda na kuuendeleza muungano. Hatua hizo ni pamoja na kuipa majukumu rasmi ofisi ya Makamu wa Rais kushughulikia muungano. Tayari kuna waziri wa nchi katika ofisi hiyo aliewekwa mahsusi kushughulikia muungano. Kuna tume ya pamoja yenye wajumbe toka pande zote za muungano inayoshughulikia masuala ya fedha katika muungano na pia namna rasilimali zinavyogawanywa’’ alisema Balozi Maajar.

    Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia masuala ya Mazingira, Professa Mark Mwandosya na ujumbe wake ambao upo nchini hapa kwa ziara ya kikazi pia walihudhuria sherehe hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Uingereza na watanzania wengine mashuhuri akiwemo mmoja wa wahasibu wakuu wa Kampuni ya Pricewaterhouse Coopers nchini Tanzania, Dr. Edmund Mndolwa na Makamu Mkuu wa Chuo cha Kiislamu cha Morogoro, Mama Mwantumu Malale ambae pia ni Katibu Mkuu Mstaafu katika wizara ya elimu.

    Sherehe hiyo iliyofanyika katika ubalozi wa Tanzania nchini hapa ilihudhuriwa na mabalozi toka nchi za Zambia,Namibia, Kenya, Afrika ya Kusini na nyinginezo na pia kuhudhuriwa na Wafanyabiashara mbali mbali maarufu wa Uingereza akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa kampuni kubwa ya Marks & Spencer, Stuart Rose ambae alikaa Tanzania wakati wa ujana wake.

    Balozi Maajar alitumia fursa hiyo kuwaeleza mabalozi hao namna watanzania wanavyoishi kwa pamoja licha ya ukweli wapo makabila zaidi ya 120, ‘’wakati tulipopata uhuru nchi yetu ilikuwa na makabila 120 kila moja likiwa na chifu wake,utamaduni wake, na lugha yake lakini sasa tunajivunia umoja tulionao kupitia Muungano ulioasisiwa na viongozi wetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Amani Abeid Karume ambao walifanikiwa kuyaunganisha makabila haya na kuishinda sera ya gawanya utawale iliyokuwa ni mbinu ya kikoloni iliyofanikiwa sana katika nchi nyingine,leo hii wananchi wetu wanajitambua kama watanzania kwanza kabla ya ukabila,dini au eneo wanalotoka’’ aliongeza.

    Aidha Balozi Maajar aliendelea kusisitiza kuwa Muungano huo utadumisha huku Tanzania ikiendela na mshikamano wake katika jumuiya za kimataifa kama vile SADCC na Umoja wa Mataifa.

    Wengi wa wageni waalikwa katika sherehe hiyo walivutiwa sana na vyakula vya kiasili vya Tanzania kama vile Sambusa, kuku wa kuchoma, na vinginevyo ambao viliandaliwa na Jumuiya ya Wanawake wa kitanzania [TAWA].

    Wakati huo huo katika kusherehekea sikukuu hiyo ya Muungano, Kampuni ya Chombeza yenye makazi yake mjini hapa imeandaa sherehe maalum kwa watanzania wote itakayofanyika siku ya Jumamossi ambapo miziki ya kitanzania na vyakula mbali mbali vya kiasili vitakuwepo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...