Home
Unlabelled
nadra
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Ni kweli jambo hili nilakujivunia sana. Itapendeza siku moja ikiwa Raisi hajatoka CCM halafu mahusiano yawe hivihivi.
ReplyDeletewote wanatoka chama kimoja na wote ni wezi,michuzi tukuambie mara ngapi?hii picha ulishaitoa zamani kwenye blog yako,tatizo la mtu mweusi na wewe michuzi mmoja wao ukiona watu wanacheka kama hivyo unadhani mambo ni shwari,asilimia 85 ya wadanganyika wanateseka kwa huduma za sirikali mbovu,ni nchi ya kishenzi kabisa familia yangu yote naiamishia USA,eti wanafurahi?wanafurahia ujinga?
ReplyDeleteMimi nina uchungu sana na hawa watu.Nyerere alikuwa ni kiongozi shupavu sana hata kama ilichukua muda kuona kwamba alifanya makosa kama kuleta Azimio la Arusha na kuundwa kwa vijiji vya ujammaa. lakini hawa jamaa watatu mimi sijui niwaiteje. huyo mzee ruksa yeye 'was ignorant' kabisa kauza nchi yetu kwa waarabu na karuhusu watu waibe na kuua uchumi wa nchi yetu kabisa.Huyu Mkapa katufanya tuwe maskini kuliko tulivyo kuwa miaka arubaini(40) iliyopita. kaleta wezi wa kutuibia kwa ticket ya kuwekeza akiamini kwamba watabadili hali ya maisha yetu. nchi yetu inaibiwa sana na makaburu na wawekezaji uchwala. Hana uchungu na nchi yetu kabisa. hivi kweli huyo Mkapa ni Mtanzania?. kanunua radar ambayo kwa sasa ni outdated wala hatuitumii kwa sababu hatuna matumizi yake makubwa huku watoto wetu wakifukuzwa shule kwa kuto lipa ada ya shule. Huyu kikwete tuliona kwamba sasa Nyerere kapata mrithi wake na sasa atapumzika vizuri huko aliko. Mara ghafla kawa 'The Most World Tourist President na high spender". kateuwa viongozi kwa kuwalipa fadhira ya kumpigia ndogo ndogo kasahau watu walio mpigia kura kuwatumiki kwa bidii. serikali yake haina agenda, kama kuna mtu anajua agenda ya serikali ya kikwete aseme- kutalii duniani na kundi la walaji ambao wanakwenda shoping? hana sera zozote, sera zake niza kushutukiza tu hana alicho panga kutimiza katika utawala wake. Nyerere alipanga kuleta usawa na Elimu kwa wote.Alileta elimu ya watu wazima na alipigania uhuru wa Africa. Mzee Ruksa yeye alipanga kuua uchumi na kuleta waarabu kununua nchi yetu kule loliondo. kauza viwanja vya umma(open space pale Golden Tulip Hotel- kaowa watoto wa shule). Mkapa kaleta Umaskini zaidi, kauza nchi yetu kwa wawekezaji feki ambao ni wezi. Kanunua radar huku watu hawana dawa muhimbili. Kikwete sijui anachofanya No Idea kabisa....
ReplyDeleteSamuel Sitta na Adam Malima pia uliwabandika wanacheka kwa furaha pamoja.
ReplyDeleteHawa wahuni tu, wanarithishana umaskini tu hakuna lolote. Maana kama amani wanayoizungumzia halafu haileti manufaa kwa jamii kiuchumi na kujikomboa kimaisha hakuna lolote.
ReplyDeleteTehe!tehe!si unaona Bw.Ben zilikuwa kelele tu,oh eti Rada sijui nini,tehe tehe!!wasahaulifu sana hawa watu si unakumbuka Loliondo?tunapeta tuu hata hayo ya Richimundi bwana mdogo we kamua baba! yule mshamba wa DP akileta za kuleta,mtafutie kesi hata ya `kuvaa suti kama waziri` kisha Ukonga mwaka.Tehe!!tehe.
ReplyDeleteHawa wote wajinga lakini walau Ben pamoja na kaujinga kake he had a weak vision na ka akili kidogo.
ReplyDeleteHuyu wa katikati ndio zuzu kabisa. Hajui kitu na ninafikiri anatatizo au la kisaikolojia au la kiafya...
Tukubali tusikubali Tanzania yetu haitosongo mbele chini ya uongozi wa JK. Kama mna kumbukumbu mtakumbuka hili.
Yaani hapo jamaa kikwete kamwambia 'Kaka Ben usihofu mi issue ya rada wala siifuatilii we kula nchi tu watasema watalala teh teh teh na baba yangu mzee mwinyi usiwe na wasi mi siwageuki kama rais wa Malawi teh teh'' Ila na ninyi msijifanye kuninyerere kwenye serikali yangu chuneni tu si mnajua twawala teh teh teh nchi mali yetu hii sasa nini tena teh teh''
ReplyDeleteyaani hayo ndio yanayoendelea hapo hamna lolote la maana. Ila siku moja watakuja jibu mashitaka hata wakiwa kaburini.
ahahahahahha hahahahahahaha we dogo fala sana hapo juu!!
ReplyDeleteMichuzi hata wachawi usiku wakiwa pamoja kula nyama za watu wanacheeeka.Usishangae!
ReplyDeleteteh teh, haluuuuuuuu sijui nani kachekesha hapo..., ni vizuri inapendeza
ReplyDeleteHakuna mwenye afadhali hapo.Ni sawa na kusema kipofu,kiziwi,bubu nani kile???Wote walemavu tu.
ReplyDeleteMzee wa Ruksa,mzee wa Rada na mzee wa kutalii na kulipa fadhila.Nani bora?
Utashangaa 2010 JK mzee wa kutalii na kulipa fadhila rais tena.
wasukuma wanasema hivi 'myete ya mnagugwa mafi mhingo' yaani kwamba 'panzi huwa anaonekana smart sana kwa nje lakini ndani mwilini amejaa mavi mpaka shingoni'
ReplyDeleteMimi nadhani hao ma-annon hapo juu wanajifanya kuwa wana uchungu na nchi kwa kuwachukia vingozi wao hao wapendwa ni malimbukeni na wajinga kupita ujinga wenyewe!
ReplyDeleteWenyewe wanataka nini Dunian hapa zaidi ya Tanzania yenye kheri na neema namna hii? Watu hawa wanatakiwa wafungue macho na akili zao kutambua kuwa nchii hii, kama zilivyo zote kusini mwa Jangwa la sahara zinaendeshwa na WEST na sis kwa sisi wenyewe kutaka.
Alichofanya Mwinyi na mawazo yake na wahauri wake, lakini kwa shinikizo la WEST!.
Mkapa kuuza au kugawa bure mashirika ya yetu ni mawazo yake, lakini pia shinikizo la WEST! Amejitahidi kama yeye lakini hawezi tawala kama yeye, lazima aimbe wimbo wa kimataifa!
Kikwete kaja na mbwembwe kibao! Wala Rushwa, control ya over-expenditure, kasi, hari na nguvu mpya! Zote hizi haziwezi kwenda bila ya remote ya WEST. Ndo maana alikuwa na maana nzuri kuwaambia wanafunzi wa vyuo vya juu kuwa atafikiria kihusu 40%, lakini aliporudi Ikulu na kuangalia ma-file ya WB/IMF, akagundua kuwa haiwezekani! Kafyata mkia na wanafunzi wanagoma sasa!
Inatakiwa watu waelewe kuwa tunapita katika kipindi kigumu sana ambazo hata nchi zilizo mbele yetu kama zile za ASIA zimetoka humo siku chache zilizopita. Watu wasitarajie maajabu eti kwa kuwa Tanzania ina reources kibao. It takes time to transform your resources into ECONOMIC growth!
Watanzania tuwe wachambuzi na wa kufikiria kwa akili sana. Tusiruke ruke tu na kuropoka ropoka hovyo. Kama kuna raia wa nje anasoma baadhi ya comments katika hii blog nzuri ya Michuzi, lazima atadhania kuwa sisi wote ni wajinga wajinga kama baadhi ya watu kulingana na comments zao hapo.
SI ajabu sana sana kuwasikia watani zetu wa jadi akitamba na wakituambia sisi hatujasoma kabisa kama wao! NI kwa sababu a maoni ya kipuuzi kama ya baadhi yetu.
Tulieni watanzania, someni muelewe, fikirieni mchambue. SI kukurupuka na kusema chochote kama vile tumekumbwa na RVF kwa pamoja.
Kama ni control ya WEST, uchaguzi wa gharama kubwa hivyo wanini!!!! eh!! Si huyo WEST achague na kusema huyo ndiyo RAHISI wenu. Kwa sababu siyo RAIS tena.
ReplyDeleteUsiwapuuze watu bwana, wewe unadhani huyo TB & GB ndiyo watakupeleka huko kunako maendeleo!
Mimi nakuhakikishia hii nchi ikipata kiongozi MGUMU miaka miwili CHINA hii hapa (unacheka!)
Wewe tangu lini kupiga picha na hao WEST ikawa kuimarisha uchumi.
Katika yoooooooooooooooooote iliyoyaandika hapa juu point ni
watanzania TUCHAPE KAZI, Lakini kazi ni lazima iwe na malipo ya kulinda AFYA.
Hata mkulima alipwe fedha ya kutosha kwa mazao yake ili aweze kulipia ada hadi elimu ya juu. SIYO USANII.
Hivi hilo bakuli huwa linategemewa ndiyo lisomeshe. Sasa wanapogoma kulijaza si ndiyo hayo madhara ya wanafunzi kugoma.
Waambieni basi hao wanafunzi kuwa TB amegoma kutujazia bakuli letu. tujue kabisa, kumbe! tunalipiwa na MJOMBA TB!!!!
We Annon hapo juu wa tarehe 19 April 7:29, uwe mwangalifu sana.
ReplyDeleteChina unayoifahamu sasa hivi haikuamka tu na kuwa na kasi unayoiona sasa hivi. Wamepitia turbulence kibao, tena kuliko hata zetu. Uisahau kuwa pia China ina watu Million mia 900 ambao wanaishi chini ya dola moja kwa siku, ambayo ni idadi ya watu wote Africa mara mbili! Lakini kwa kuwa wachache wa China wana hela sana ndo maana GNP yao iko juu mara kadhaa kuliko yetu!
Ukiweza ku-analyze huu mfano wa China, unatweza amini kuwa sisi Africa ni matajiri sana! Wengi wa watu huwa kitu hiki hawakiangalii na ndiyo maana nikasema, tuwe waangalifu, tusikurupuke hovyo hovyo tu na kusema ohh, Mkapa kaiba au kafanya vile. Pima, chambua then jilinganishe ndani na kimataifa.
Politcs zisiwafumbe macho Wabongo wenzangu. Tuwe makini sana sana kufikiria. KUna siku niliwahi kusema hapa hapa kwenye hii blog kuwa wakati wa uchanguzi, Wa-TZ wote huwa mbumbu! Chochote waambiwacho, ili mradi ni kuelezea machungu yao wanashangilia tu.
Machungu yako utayatatua mwenyewe na si mwenzako au kiongozi wako. Wewe kama wewe, hasa wewe unayesoma hapa kwenye hii blog. Mpaka, Kikwete au hata aje nani, wewe usipocheza utakufa kama wewe.
Anon wa 1:13pm utakuwa mzee wa compasator ya madhabahu nini umejuaje mimi ni dogo ahahahahahahahaha
ReplyDeleteWe Anon unayetaka kuhamishia familia yako USA, ni mufilisi wa mawazo. Tanzania si nchi ya kishenzi kama unavyosema wewe, ila wewe ndo mshenzi kwa sababu huna shukurani kabisa. Mama yako aliyekuzaa, alikalia ardhi ya Tz, na wewe mwenyewe umekulia tz, leo unajifanya kuitukana nchi yetu kisiwa cha amani. Kumbuka ndugu yangu kuwa Tz ina miaka 45 tangu izaliwe kama nchi, sasa huwezi kuifananisha na nchi kama USA yenye umri wa zaidi ya miaka 200 kama taifa. Acha kutukana TZ, we baki huko huko USA na umanamba wako, unadhani umepata kumbe umepatikana. Ngoja baada ya miaka 20, halafu jilinganishe maisha yako na wenzako uliosoma nao na wakabaki TZ, utajikuta masikini wa kutupwa hata kama unajifanya unaishi USA. Ughaibuni ni manamba tu ndugu, usidhani kazi za kuosha wazee na kubeba mabox ndo maendeleo. Mungu ibariki Tanzania
ReplyDeleteJe kicheko hicho ni cha mafanikio waliyoyaleta kwa nchi au kicheko chao cha mafanikio yao binafsi?
ReplyDeletesikatai kufanya kazi lakini iwapo pesa zinaibiwa na kununua rada na kutembea duniani na kununua lexus cars, hakuna mabadiliko yoyote yatakayo weza kutokea hata kidogo. watoto hawana masoma na Elimu ni ufunguo wa Maisha lakini kwa Mtanzania ujinga ndio ufunguo wa maisha na umasikini. Hatuwezi kupata maendeleo Tanzania mpaka tuondokane na utawala huu mbuvo.
ReplyDeleteHiyo rada watanzania wangapi wanaitumia au kujua tu kwamba kuna rada ya Mamilioni?. je kama tusinge nunua rada hiyo hizo pesa zingenunua dawa na kusaidia ada ya watoto. wezi sana hao ..lakini huwezi ukafanya watu Million 39 wote wapumbavu kuna siku haya yote yatakuwa na mwaisho.
kwanini wa bongo tunatukana wazee wetu kwani hakuna njia nyingine ya kuwakosoa ni kweli kila rais anamapungufu yake lakini unapotukana wewe ndio unaonyesha ni jinsi gani usivyo mtaarabu.vilevile lazima tukumbuke hawa jamaa hawaendeshi uchumi ila wanafuata amri za IMF na WB. ni nyerere peke yake katika bara la africa alijaribu what we call the african type of economy which were totally based on traditions and culture of the african people. but what we are doing right now is immitation of western countries type of economy,and keep in mind capitalistic economy does not have humane face,so what is happening now in tanzania is the maximum exploitation of resources and poor people by rich. the matter of the fact is few rich people are exploiting poor majority.
ReplyDeleteMsiwasingizie wa WEST bwana. Kwani Msumbiji inayopiga hatua kiuchumi iko sayari gani? Hizo safari za rais wenu msanii wanaziandaa watu wa WEST? Na hiyo mikataba mibovu nayo mtasema ni kwa sababu ya WEST? Hivi posho za wabunge kwa kikao kimoja cha Bunge kuwa Tshs 100,000/- wakati kima cha chini kwa Mwezi (sio siku)ni nusu tu ya kiwango hicho na elimu ya mgogoro nayo ni kwa sabubu ya WEST? Kama viongozi wenu wanafuata mambo ya WEST hata wanayoyajua kuwa yana madhara kwa raia wao na kuyatekeleza basi ni mazezeta, wapumbavu wasiostahili kuongoza nchi! Ni lazima tuseme bila woga kuwa viongozi wetu ndio wanaoharibu nchi. Hata wakionekana wanatabasamu kwa nje, ndani mioyo yao inawasuta kwa ufidhuli wanaoufanya kwa nchi yetu.
ReplyDeleteSir Issa..Naona kwa maranyingine tena unatuonyesha mambo ya lugha ya picha. PICHA INAPENDEZA HII KAKA..NAONA WOTE WAMESIMAMA KWA HESHIMA NA TAADHIMA..MIKONO YAO IMESHIKILIA MATUMBO YAO...KUNAULE MSEMO USEMAO.."......IS ON YOUR HAND"
ReplyDeleteUJUMBE KWA WANAFUNZI NA PIA KWA RAIS KIKWETE...
ReplyDeleteWATU WENGI HUMU MNAPIGA YOWE ISIYO YA MSINGI SERIKALI ILITAMKA MAPEMA KABISA KWAMBA MWAKA HUU KILA MWANAFUNZI ATALIPA ASILIMIA 40, NA KAMA HUWEZI BASI ACHANA NA SHULE SASA IWEJE WANAFUNZI ZAIDI YA MILLION MOJA HAWANA HIYO LAKI NANE WAKATI KILA KUKICHA WATU WAKO BAA WANAENDESHA MAGARI MAZURI SASA NI KWELI KILA KIJANA WA CHUO KIKUU KAKOSA ADA? HUU NI UPUMBAVU KUONA KILA MWANAFUNZI ANAANDAMANA INGEKUWA VIZURI WALE WACHACHE WASIYO JIWEZA NDIYO WAGOME LAKINI MIJITU MIZIMA NA AKILI ZAO YANAENDESHWA NA HAYO YANAYOJIITA ETI PUNCH, PUNCH MY ASS...SORRY MICHUZI KWA LANGUAGE YANGU, KAMA HUNA UWEZO WA KULIPA BASI JALIBUNI NJIA MUUAFAKA YA KUDAI HIZO HELA NA WENGINE WENYE UWEZO WA ENDELEEE NA MASOMO KAMA KAWAIDA KULIKO KUSABABISHA WATU WENYE UWEZO KUKOSA MASOMO KUNA WATU WANATOKA NJE YA NCHI WANA SHOLARSHIP ZAO LAKINI WAABIDI WAKOSE MASOMO KWA SABABU YA ISSUE ZA KIPUNGUANI.
KIKWETE... NA WEWE KIKWETE UNAKOSAJE HELA ZA WANAFUNZI WAKATI UNAPATA HELA ZA KUWALETA WACHOVU REAL MADRID KUCHEZA DAKIKA TISINI KWA POUND MILLIONI 150? JALIBU KUFIKILIA KWANZA KABLA YA KUWATIMUA HAO WANAFUNZI. TIMUA REAL MADRID NA DEAL ZAO FAKE, HAO WALIO KUTAPELI RADA WAMBIE WAKURUDISHIE PESA UWAPE WANAFUNZI, HAO WALIOINGIZIA HASALA TAIFA KWA MIKATABA FAKE YA MADINI WAMBIE WALIPE FIDIA UWAPE WANAFUNZI,HIZO RUSHWA NA UKWEPAJI KODI ZA KUINGIZA MAJENERETA WAMBIE WALIPE KODI WAPE WANAFUNZI WASOME... ACHANA NA USANII KIKWETE WATHIBITISHIE WANAFUNZI HAKUNA HELA KABLA YA KUWATHIBITISHIA REAL MADRID KUNA PESA YA KUWAKODISHIA NDEGA NON STOP FROM SPAIN!
Mawazo ynu yote mazuri,sasa tupate mtu/watu wa kuyachambua na kuyaweka kwenye aidha Jarida au Kitabu ili yasiwe kama maongezi ya kijiweni kama baadhi ya wachangiaji wanavyofikiri.
ReplyDelete