kama nilivyoahidi awali hii ndo hali halisi ilivyokuwa leo udsm baada ya chuo kufungwa na amri ya kuwataka madenti waondoke kampasi ya mlimani kabla ya saa 12 ilivyokuwa. huo juu ni waraka ambao wana solidariti waliubandika dakika chache kabla ya mstari mfu waliopewa.
hali ilikuwa shwari na hakukuwa na vurugu zozote na madenti wote waliondoka kabla ya muda waliopewa kutimia. foleni za magari ilikuwa kubwa mithiri ya siku ya mahafali. mie nilifika mlimani mida ya saa kumi na kuondoka kiasi cha saa mbili kasorobo kutokana na hiyo foleni ambapo ilibidi trafiki kibao waletwe kuweka mambo sawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. wanacheza hao.
    hapo wataambiwa anaetaka kurudi chuo arudi na asiyetaka asirudi utaona kama solidarity hiyo itakuwepo kama wanavyodai. watu wana background tofauti hapo, mwingine hiyo 60% inatosha kabisa, mwingine anataka atunze familia kwa hiyo hiyo pesa ya chuo, wapi na wapi. mkishatimuliwa shule hakuna cha solidality tena, ndiomshavunjwa nguvu. Poleni mwee

    ReplyDelete
  2. Hawa wanafunzi ni wajinga. Huyu mwandishi naye hata kuandika hajui ndio wanalilia 100%? Jamani tusipoanglia kazi zote hapo town zitashikwa na waKenya au Waganda. Serikali itabidi ijitoe kwenye maswala ya mikopo. Hao wanafunzi wakakope kwenye Mabenki wanapotaka kusoma waone kama huko unaweza kuwalazimisha kiasi cha kukopeshwa.

    Huwezi cheza na Serikali, mie nakumbuka wakati tupo Tambaza fujo ilikuwa mtindo mmoja. Wee, serikali ilvyoamua kututhibiti unafanya mchezo. Wote tulitupwa mikoani ndani ndani huko na shule ikabadilishwa kuwa High school na mchanganyiko na mademu. Mkono wa serikali ni refu huwezi shindana nao.

    ReplyDelete
  3. Wewe ni nani kuipiga mkwala Serikali...Yaani we ndio Bush alafu Chuo/Serikali ndio Al-Queda??? Tumia lugha endelevu kufikisha hoja yako

    ReplyDelete
  4. Hii barua inaonyesha ni kwa namna gani akili za hawa wanafunzi au wawakilishi wao walivyo. Wewe msomi wa chuo kikuu utawezaje kuchanganya lugha mbili katika barua muhimu kama hii. Kama walitaka kuandika kiswahili waandike kiswahili na sio kuchanganya na maneno ya kiingereza ambacho bado kinawapiga ugoko

    ReplyDelete
  5. Michu naomba uwape pole zangu vijana. Tatizo ni kubwa kuliko tunavyo fikiri. Wizara ya Elimu ya Juu ina watu wenye kinyongo hawataki kubuni mbinu za kuishauri serikali kutatua matatizo ya wanafunzi. Wamekariri kuwa wanafunzi ni wakorofi, wanapenda dezo etc. Je ni kweli? Unajua hiyo 40% ni kiasi gani? Watu wameandaliwaje kukabiliana na hayo mabadiliko?
    UPANDE WA WANAFUNZI nao wamepoteza dira. Front liners ni wale wasiojua kutumia lugha ya kiungwana. Kwanini wasichague watu prudent wawasemee badala ya mabango ya kashfa? Tatizo lina eleweka. Walau kwa miaka kumi hivi mkopo uwe 100% kauchumi kakue!! Niko Ulaya ila I feel for these GUYS.... Mungu ibariki Tanzania!!

    ReplyDelete
  6. asilimia kubwa ya wanafunzi wa chuo kikuu hiyo pesa wanaitaka kwa ari na mali ili waende kwa wanganga wa kienyeji kulogana darasani ili wafauru mitihani sasa kikwete kashtukia deal. mimi naona kikwete awachape fimbo tu matakoni na awapake pilipili kwanza ndiyo heshima itarudi.

    ReplyDelete
  7. Unajua hawa wanafunzi wanaponzwa na Mob Psychology, kuna wengine hata hawajui wanataka nini!! naungana na Anonymous wa Tarehe Tuesday, April 17, 2007 10:26:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous, jamani tufikirie tulipotoka serikali ina mambo mengi ingawa lenu muhimu ila kuna njia ya kufikisha ujumbe mmekuwa mkisikia wenzenu wanagoma kila mara na nyie ili mradi muonekane mpo mkagoma haya serikali ni kama mashine ya saa kick moja inazungusha nyingine hatimaye mshare!!! anaamua mwingine, anatekeleza mwingine, tena mshukuru FFU hawajakuja!!

    ReplyDelete
  8. Mnacheza nyie, kama serikali isingekuwa na hela hapo sawa, sasa serikali inaendekeza anasa, na kubwaga huduma muhimu kama elimu, afya na miundombinu. Wanafunzi pekee ndo wanaipa adabu serikali. Mkapa alijitahidi sana, mishahara ya walimu ikaanza kufika on time mwisho wa mwezi na mikopo kutolewa on time, na ni 100%. Hapo bado alikuwa analipa madeni ya nje na ndani. Sasa uswahili umeingia serikalini, yangu macho.

    ReplyDelete
  9. Kuna mtu ana particulars zozote kuhusiana na hii mikopo wanayoigomea? Hii mikopo ni ya duration miaka yote mitatu/minne ya mwanafunzi kuwa chuoni au ni ya mwaka mmoja mmoja? Ni shilingi ngapi kama ni kwa miaka yote au ni kwa mwaka mmoja? Na katika hiyo amount, asilimia 40 wanazozigomea ni shilingi ngapi na asilimia 60 serikali inayolipa ni shilingi ngapi? Vilevile, duration za kulipa ni za muda gani?

    Lakini nao wakome(samahani kusema hivyo)Sasa sijui wanamkomoa nani - wao au serikali? Wameamua kum-diss rais JK kwani nadhani aliwaambia analishughulikia hili swala. Sasa warudi kwa kijijini wakatafakari walicho fanya na kusuffer the kwensekwens za action zao.

    ReplyDelete
  10. Tatizo kubwa la watanzania waliowengi ni umimihakuna cha kuiendeleza nchi. Nina wasiwasi hii nchi kila mtu inabidi apigane alipo vinginevyo wahaya usema "MWafa-bwana" Wakati nci zilizojirani zetu ambazo tunapigana kujiunga nazo zina uwezo wa kukopesha mwanafunzi wa PhD watanzania hata First year University hatujaweza. Wasomi wa kitanzania ni wangapi? Nafikiri mababa wetu wamezeeka wanastaili kupumzishwa hili vijana wajaribu kuweka mawazo endelevu.

    Kwa speed tunayokwenda nayo, tumeshindwa kufika kibaha maili moja, Je tukipewa kwenda Geita, Muheza na Nyakahanga tutaweza?.

    Hii nchi tuiombee kwa mungu tu mwenye neema...... Amina.

    Michuzi tafadhali sana najua unapenda haki.

    ReplyDelete
  11. of all the people wameamua kutumia stupid george Bush line ambayo ni very unpopular ...people knew bush is a madman alipotumia hiyo line either you're with us or...sasa naona wamefanya the same hawa na hivi wanamtishia nani hawa ng'ombe kwani kama huna hiyo 40% sio kila mtu hana...inabidi hiyo change wanayozungumzia ianzie kwao kwa namna wanavyofikiria na kusolve shida zao

    ReplyDelete
  12. HII KALI, LAKINI JUJIULIZE KWA NINI WANAGOMA KARIBU NA MITIHANI???MIMI NAONA HAO VINGOZI WAMEKOSA PA KUNUNUA MITIHANI THEN WAKAANZISHA HILO SHESHE. NASHAURI SERIKALI IPELEKE HIYO MIKOPO BANKI THEN WANAFUNZI WAKAKAKOPE KUTOKA HUKO HALAFU WATAJUA MIKOPO NI NINI

    ReplyDelete
  13. HAWA WANAOANDIKA INFORMATION ZA KIPUUZI NAMNA HII BAADAE WAKIWA VIONGOZI WA SERIKALI NDIO WAKATAOFUKUZA WANAFUNZI!! WANSEMA CHUO KIFUTWE KAMA HAWAPEWI HIZO PESA, JAMANI, WATANZANIA TUNA MATATIZO GANI? HAWA KWELI HAWAJUI PR, NA WALA HAWAWAHESHIMU WATANZANIA WENZAO (WALIOKO SERIKALINI). KWANINI WATANZANIA TUMEKOSA STAHA HIVI?

    TALKING LIKE THAT TO AUTHORITIES SHOW LUCK OF INTEGRITY, CORRUPT MORALITY, AND ASTONISHING LUCK OF RESPECT FOR YOUR FELLOW CITIZENS. FOR THOSE IN THE GOVERNMENT ARE, IN THE FINAL ANALYSIS, FELLOW TANZANIANS. NOW, IS THIS THE WAY TANZANIANS COMMUNICATE? ARE THESE STUDENTS OUR LEADERS OF TOMMORROW?. TUNA KAZI KUBWA HASA!

    ReplyDelete
  14. Huyo aliyeandika hiyo barua ya ajabu tayari amekwishapelekwa USA kusoma na wazazi wake. Shauri zenu nyie watoto wa wakulima mliomskiliza! Na yeye aliondoka Chuoni na ride safi. Mlie tu!

    ReplyDelete
  15. we anon Wednesday, April 18, 2007 8:16:00 PM kasome inglishi kozi pumbavu au andika kiswahili kwenye mabano ni masahihisho- Punctuation yako ni mbovu sana nimeshindwa kuirekebisha. siku nyingine andika kiswahili
    TALKING LIKE THAT TO AUTHORITIES(authority) SHOW LUCK(lack) OF INTEGRITY, CORRUPT MORALITY, AND ASTONISHING LUCK(lack) OF RESPECT FOR YOUR FELLOW CITIZENS. FOR THOSE IN THE GOVERNMENT ARE, IN THE FINAL ANALYSIS, FELLOW TANZANIANS. NOW, IS THIS THE WAY TANZANIANS COMMUNICATE? ARE THESE STUDENTS OUR LEADERS OF TOMMORROW(tomorrow)?. TUNA KAZI KUBWA HASA!

    ReplyDelete
  16. nimesoma maoni yaliyochangiwa na waliotangulia hapo juu. ukweli kabisa ninaingiwa na wasiwasi na wachangiaji watanzania wanaoishi nje ya nchi. WENGI WAO( SIO WOTE) wanaonyesha kukurupuka na kuchangia hata kitu hasichojua. Tujaribu kuwa wastaarabu. Fanya tathimini kabla ya kukurupuka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...