Wadau wapendwa duniani kote mnaosoma blogu hii!

Samahani kwa kuchelewa kuleta taarifa, kwa kweli jana mara baada ya mashindano kulikuwa na hafla ndogo lakini tulishindwa kuondoka mapema kwani Flavia alikuwa ni gumzo kila kona. Kila mtu alitaka kupiga picha naye na kila mtu alitupongeza.

Kama mnavyofahamu Flavia kaingia 10 bora! Nationalo director wengi wamenifuata na kuniopngeza wakisema kuwa Tanzania imekuw mfano bora kwani ni mara yetu ya kwanza na tumepenya 15 bor, na baada ya raundi ya kwanza tumeingia 10 bora! Nchi pekee iliyofika htua moja mbele kwa njia hii ni Botswana ambayo ilitoa mrembo Mpule kama Miss Universe.

Kwa kweli inbidi Tanzania tujipongeze sana, kwani mrembo wetu ameipeperusha vyema bendera. Ingawa nilikuwa mtanzania pekee kwenye ukumbi lakini baada ya kutangazwa 15 bora, waafrika na watu weusi kam vile Curacao na Bahamas walihamisha ushabiki wao Tanzania na walinisaidia kupeperusha bendera.
Lakini muhimu zaidi Flavia alishangiliwa sana na wenyeji wake watu wa Mexico! Mashabiki hawa waliposikia matokeo ya 5 bora na walipoona kuwa Mexico na Tanzania hawajaingia walianza kumzomea mrembo wa Marekani Rachel Smith.
Rachel alidondoka kwenye steji wakati wa mashindano ya vazi la jioni. MAshabiki wa Mexico waliendelea kumzomea mrembo huyu wa Marekani mpaka wakati wa kujibu swali. Ushabiki baadaye ulihama kwenda kwa Brazil na alipotangazwa mshindi kuwa Japan, watazamaji wengi walionekana kutofurahia sana matokeo.

watalaam wa masuala ya urembo wanaendelea kuchambua matokeo ya mwaka huu na wengi wamesema wazi kuwa mwaka huu bara la Asia lilikuwa lishinde. Hata hivyo kulikuwa na ushindi mkali sana kwani mrembo wa Korea alionekana kuwa na vigezo zaidi ya mrembo wa Japan.

Baada ya ushabiki na uzalendo kumalizika, watu wengi wamekubali kwamba moja wa warembo waliotia fora katika mashindano haya ni Flaviana Matata wa Tanzania. Mrembo huyu ana matumaini makubwa sana ya kuendelea kufanya vyema kimataifa hususan katika dunia ya ulimbwende (modeling).

Zawadi la Miss Photogenic limeenda kwa mrembo wa Ufilipno kwa mara ya 3 sasa, jmbo ambalo halijapokelewa vyema na mashabiki na watazamaji kwani wanadai kuwa ameshinda kwa wingi wa kura za uzalendo na si kwa kustahili
Zawadi la Miss Congeniality yaani mrembo wenye ucheshi na laiyepigiwa kura na warembo wenzake ni Miss China.
Maelezo zaidi nitakaporudi, Alhamisi. Flavia anategemea kutua tarehe 2 mijini Dar-es-Salaam. Asanateni sana Watanzania wote kwa ushirikiano na support mliyompatia mrembo wetu. Tanzania juu!!!

Zawadi la Miss Congeniality yaani mrembo wenye ucheshi na laiyepigiwa kura na warembo wenzake ni Miss China.

Maelezo zaidi nitakaporudi Alhamisi. Flaviana anategemea kutua tarehe 2 mjini Dar-es-Salaam. Asanteni sana sana Watanzania wote kwa ushirikiano na mliyompatia mrembo wetu. Hii imedhihirisha kweli kwamba kwamba Tanzania tunapendana na tunapenda mafanikio na Mungu akipenda iko siku tutapata makubwa zaidi - amen
Maria Sarungi-Tsehai
ukitaka kumuona flaviana alivyokuwa akijichanganya bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2007

    Maria - its the evening gown that killed her. Ilikuwa ugly and cheap, ilikuwa kama mfuko wa bluE. Kweli hapo sponsors mmemharibia binti wa watu. But she is gong to be just fine

    ReplyDelete
  2. she's very pretty, would love to work with her on modelling

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2007

    Akavae nguo huko, ebo! nitamsemea kwa shangazi!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2007

    Nakubaliana na annoy wa juu! what happen Maria??? Flaviana ana figure nzuri angevaa atleast something that hug her curves c'mon maria hebu tutajie fashionista tumuweke mtu kati kumvalisha Flaviana kama kapata mimba nje ya ndoa anajaribu kuficha. nina uhakika sasa hivi tungekuwa tunaongelea mengine!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2007

    The girl has the qualities but as u have said that dress was not a right choice and second I did not like the place they took her documentary it was not a good place, I believe they could find a more interesting place than that.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2007

    Hongera Flaviana,
    Me and my friends watched you last nite and you were kicking some asses! You are very pretty, thanx for carrying the most beautiful name "TANZANIA" on your shoulder high. Do your thing girl. You are going to replace Naomi Campbell.. She is done.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 29, 2007

    DA Maria,nakusalute kazi yako nzuri , basi mwakani mtuchagulie binti zuri kama huyu.hongereni sana.
    Ila Dada lile gown noma ,hivi ilikuwaje jamani.Mbona naona hata nguo za huyu Hasanali,mara nyingi twamwona hapa kwa blog nzuri sana. nadhani,ungefanya jambo la mbolea kumpa shughuli za kudesign ,jamani kile kitu alichovaa flaviana ah kibaya,lakini mwenyewe alijimudu nalo.All in all Congratulations to all especially wapiga kura wenzangu.Damn I love and miss Tanzania.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2007

    Tumemwona na alikuwa anashangiliwa sana... Miss USA alianguka na bado akaingia kwenye top 5, hapo ndio wa mexico wakaanza kuzomea. Ila kama mtu mmoja alivyosema hapojuu, Ile evening gown yaani ilikuwa michosho ndio iliyomwangusha. Hata Angola naye alikuwa poa sana ila hakuingia kwenye top 5 pia.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 29, 2007

    Flaviana dada, hongera,
    Sikiliza, wewe ni "supa modo"wa nguvu sasa hivi,Modelling agency yoyote utayowapelekea Resume yako kama mshindi # 6 kwenye miss universe atakunyakua kama keki ya moto. Ushauri wangu ni kwamba "Go For The Money". Usichukue mkataba njaa just because. Supa modo orijino mwenyewe Iman Abdul Maggid alishasafisha njia kwenu mamodo weusi kulipwa mapesa ya nguvu. She fought hard for this, so don go low honey, you do have the best resume already, now the sky is the limit for you.
    All the best.
    Subira.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 29, 2007

    Kwanza natoa hongera kwa miss huyo pamoja na tz nzima.Lakini huyo miss akupenda kwenye gauni la jioni yani lilikuwa baya sana sijui nani alichagua ilo gauni?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 29, 2007

    She was just great, absolutely confident with herself but everything came tumbling down when she showed up with that dress, My gosh! it was if she was going to a confirmation ceremony or something, please lets work on our evening gown!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 29, 2007

    Miss wa angola alitoka bomba gauni la jioni lakini swimsuit haikum[pendeza alivyokua anatembea alionekana mnene sana.

    Flavia alipendeza sana ni hilo gauni tu la jioni ndio limeharibu. Color size. nakumbuka kuna jingine TZ alivaa jekundu kwenye blog ya Michuzi hihi hihi lilikua kubwa sana tu. watu wakatania asije akaenda nalo hili Mexico kumbe alikwenda nalo bali color nyingine( just kidding)

    All in all hongera ila usikae bongo. Nenda ufaransa au USA kabla maji hayajapoa. Send your resume everywhere Iam sure kuna agenty atakuchukua. You are a real a model. Ukitua bongo alhamisi pumzika kidog chachamaa. Milango imeshafunguka top 10 sio mchezo.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 29, 2007

    She did great but hebu cheki gauni lilivo cheap and ugly, sio makosa yake ni makosa ya sponsor wake. You rock through it though next time voice your opinion if they give you such a dress

    http://news.yahoo.com/photos/ss/events/en/051007missuniverse/im:/070529/photos_en/2007_05_28t232449_295x450_us_mexico_missuniverse;_ylt=Aur07czMHTcdOZefivMRiZF.KcMA

    ReplyDelete
  14. Check pics here

    http://myafricatoday.blogspot.com/2007/05/miss-universe-tanzania-2007-part-1.html

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 29, 2007

    http://myafricatoday.blogspot.com/2007/05/miss-universe-tanzania-2007-part-1.html

    ReplyDelete
  16. Uwongo mbaya, ile gauni ilikuwa ill fitting. Haikum 'flatter' kabisa! Kweli ilikuwa kama kavaa gunia. Ile evening gown ya pink na black iliishia wapi? Ile ingempendeza, Miss USA asingekuwa kwenye top 5. Lakini gauni lile lilimponza.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 29, 2007

    Flavia nenda nyumbani kaage, usikae kabisa hapo. Umeshaweka CV yako nzuri sana. Changamkia tenda watu bado wanakuongelea na kukumbuka. Changamkia saa hivi maji bado ya moto. Kama huku chukua contact huko weka email yako mimi nitakuforwadia maagent kibao wa USA.

    Una skin nzuri unaweza hata kutangaza facial items na figure yako ndio model kabisa. I wish wangekua na the world next top model. Kweli ungewashinda wote.

    Usije ukaleta kabisa hao wang'aa macho hapo bongo wakuwahi au wakuweke ndani. Career yako ndio imeanza. Miss universe ni your bridge use it and use it wisely.

    Usione aibu kuuliza kama huna contacts post kwenye Michuzi wapo wengi tu tutakusaidia lakini cha muhimu ni kuwa usije uka model bongo tena kabisa. kama ni kuwafundisha na kuwaeleza yale uliyoyaona huko sawa do that lakini kumodel tena bongo never... you are bigger than that now.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 29, 2007

    nyie wadada Flaviana na sponsor wako Maria mkirudi Bongo mmshukuru sana huyu Brother Michuzi,kwani hii blog imechangia sana hapo ulipofikia bila hii hata hapo ingekuwa maajaliwa,ametuhimiza sana tupige kura.mie everyday ilikuwa nikitoka kwenye mabox lazima nipige three times kukuongezea kura,KEEP IT UP MICHUZI NEXT TIME MISS WORLD UTUPE TAARIFA HAPA.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 30, 2007

    Shukrani kwa Issa Michuzi kwa kazi hii kubwa sana. TUnashukuru sana maana sidhani kama sisi wengine tungemjua huyo Flaviana kama si hii blog. Ninaanzakuamini kwamba hii blog ni moja ya shule nzuri sana kwa watanzania wengi. Laiti kama wote wangekuwa wanatembelea, viwango vya ufahamu vingeongezekana mara dufu au zaidi.

    Keep it up Michuzi. Tuko pamoja

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 30, 2007

    Hapa Watanzania ndo huwa nawashangaa sana! Saa mijitu inaibuka na kuanza kukandia night dress aliyovaa Flaviana kwamba ndo imemwangusha, je wale ambao hawakufika hata 10 bora wenyewe ni dress gani iliyowaangusha?!!

    Imefika wakati watanzania tuwe wabunifu na si kudandiadandia tu innovations za watu. Tatizo la kudandiadandia ni kwamba unakuwa huna point hata moja kama mijtu iliyo-comment hapo juu. Mnatakiwa mfahamu kuwa hayo yalikuwa mashindano na Flaviana kajitahidi sana sana na katuwakilisha ilivyo.Sponodr hakufanya kosa kumchagulia dress. Huyo sponsor ndo kamfanikisha mpaka kafika hapo alipo.

    Tuanze uzuzu wa kukandiakandia kila kitu!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 30, 2007

    WEwe Anonymous Tarehe Wednesday, May 30, 2007 9:22:00 AM, Mtoa Maoni:

    Sio kwamba watu wanakandia, ila watu wametizama hiyo kitu live. Wameona baadhi ya mapungufu amabayo yamechangia Flaviana kutoendelea raundi ya tano bora. Sasa hapa ni watu tofauti kila mtu ameangalia na kila mtu ameona hiyo gauni sasa unabisha nini? Kuonyesha mapungufu sio kwamba ni kukandia ni kujifunza ili wakati mwingine afanye vizuri zaidi. Sio kwamba hakufanya vizuri ila alikuwa na uwezo wa kufanya vizuri zaidi ya hapo alipofika ya kumi bora. Usibishe GAUNI limemwangusha sana. Wakati anatoka alikuwa anashika matiti kuliweka vizuri sasa unataka watu wasiseme? Amefanya vizuri sana ila alikuwa na uweza kufanya vizuri zaidi ya hapo na kuongelea sio dhambi.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 31, 2007

    Sir Issa.. tunashukuru sana kwa mchango wako na vilevile shukrani zote ziwaendee woote waliopiga .”..KURA..” NA WAANDAJI WOOTE “NAMASHABIKI WAKE “FLAVIANA”WALIOKUWEPO HUKU MEXICO NA DUNIANI KOOTE....huyu kimwana “..FLAVIANA MATATA..” …emejitahidi saana. ”..KWA ALIYECHAGUA LILE GAUNI.. PALE SIO MAHALA PAKE..”...”..KAZU INAWEZAKUWA YA RANGI YOYOTE ILE..” kumradhi….Anon..Wednesday, May 30, 2007 9:22:00 AM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...