mtangazaji wa radio uhuru fm na mjumbe wa baraza la vijana wa ccm mkoa wa Dar violet mzindakaya mpogolo (sister v) akirejesha fomu ya kugombea ujumbe wa halmashauri kuu taifa (nec) kwa kaimu katibu msaidizi wa mkoa wa rukwa ndugu hamis kibonde jana. waandishi na hata wanamichezo kibao wanawania ujumbe wa nec ambapo leo mwanariadha nyota wa zamani filbert bayi na katibu mkuu mstaafu wa simba michael wambura wamefanaya hivyo pia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2007

    KIGUMU Chama Cha Mapinduzi!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2007

    Michu huyo ni Vailet Crisant Mzindakaya au Mpogolo au ndio wanaficha majina kuogopa majungu. Ila poa tuu Siasa haina urithi bali ni umahili wa mtu binafsi. Ila maji hufuata mkondo.

    Wambura namfagilia mpiganaji huyo Rage nae wapi? Tabora hajachukua kweli ahaaa na Ndolanga nae Lindi. Du kweli chama cha mapinduzi kikubwa kina beba kila aina ya Wa TZ, Yaani wanamichezo, wafanyakazi. Ila ile alama ya jembe na nyundo imepitwa na wakati kwani wakulima ni wachache sana walitakiwa waweke na Ngoma kuonyesha alama ya WASANII

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2007

    hiyo computer kule ni ya mwaka gani? mbona iko mbali hivo inaelekea ni pambo

    ReplyDelete
  4. Bado Jangala,Bi Kidude, Kingwendu, Bambo na wengine wa aina hiyo. CCM chama cha wasanii bwana! Usanii mtupu we humuoni Mgosi alivyo?Ah! Tanzania, haki ya nani wallah!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2007

    ...............Wallahi nikirudi lazima na mimi nikachukue fomu mambo yenyewe haya, easy access 2 every thing in TZ + usisahau VX za bure na posho kibao just 2 sleep on the cozy seats in DOM. Mungu Ibariki TZ

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 30, 2007

    Ndio dalili haswa za kushuka kwa heshima ya NEC; Kambarage angekuwepo utani huu usingekuwepo... wale wasiojua NEC ndiyo inayoongoza nchi hii, ndio inachagua rais,,, alafu wanachi wanapiga mhuri...

    Haya, Kimkandamkanda tutafika

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 30, 2007

    Mbona Califonia , Minnesota viongozi wao walikua kwenye entartaiment industry.
    Kama mtu yupo tayari kufanya kazi basi usimjudge kwa vile past career yake ni gani. Mbona walio na professional backgrounds hatuoni wanachofanya?

    Kama qualification zina pass basi wape watu chance. Kama ni kuengeza quality ya hiyo NEC ni kuongeza qualifications ziwe high. mfano mgombea must have a high school diploma na kama ni wengi wanayo basi a diploma with all A's au 10 yrs experience etc. Hapo hutawaona wengi wanaenda kuomba hizo forms. Other wise bado tutawaona wengi tu

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 30, 2007

    Michuzi tuwekee picha ya Ridhiwani Kikwete alivyoenda kuchukua fomu ya kuomba kuwa mjumbe wa NEC. Atamenyana na Sumaye jimbo la DAR. Kazi kweli kweli mtandao wote. Mangula naye bado analia na mtandao, anagombea uwenyekiti wa CCM mkoa Iringa. Kasheshe mwaka huu!

    ReplyDelete
  9. Kuna wasanii na kuna 'usanii' tunaposema ndani ya NEC ni usanii mwenye akili timamu ataelewa inamaanishwa nini. Huko Calfonia na kwingineko wasanii wanaingia katika siasa lakini hawafanyi usanii ndani ya siasa.NEC ya CCM kwa hali ya sasa ni chombo cha juu sana kimaamuzi ya nchi hii.Ni mahali pasipowafaa WAENDEKEZA NJAA NA WATU WA POROJO NA BLABLA.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 31, 2007

    jamani hebu nisaidieni,kuna dadaangu mmoja anitwa NEEMA SITA alikuwa anafanya kazi IPPMEDIA zamani akatimkia marekani. Sasa mpaka hii leo sijui yuko wapi?? please kama kuna mwana blogu ana habari zake na email yake anipe thru this blogu.

    ASANTE

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 31, 2007

    Wewe unayemtafuta dada yako kwenye blog ya Michuzi kweli dada yako huyo au umbeya tu.

    Na kama hajakupa mawasiliano yake kwako ina maana hataki kusikia kutoka kwako. Mwache mwenzako.

    Wewe kwa nini usiweke email yako huku kwenye blog unataka yeye aeke yake huku. kama unahamu sana ya kuwasiliana naye weka email yako itamfikia popote alipo.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 31, 2007

    Regan na Schwarzenegger huwezi kuwafananisha kabisa na hao wasanii wetu. These people have accomplished a lot before they started in politics. Maria Shriver asingemuoa CA governor kama asingekuwa as successfull as he is. FYI, Schwarzenegger worth more than a billion dollars as we speak now.

    Record ya Mzee Regan speaks for itself as a CA governor and as the US president. I think it is very unfair to compair CA politicians with our artists. You may sometimes want to read people's biographies before you talk about them.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 01, 2007

    Ni kwa vile nchi yetu haiwalipi wasanii wetu vizuri. Wote wanaakili na vipaji tu sawa na wengine. Ni umasikini tu unatumaliza. Schwarzenegger hiyo billion yake asingeweza kuitengenezea Australia. Kwa hiyo kuwa ana hela sio kuwa na akili. Hata wasanii wetu ni wajuzi sana tu ila nchi yetu ni maskini ndio maana nao wanaishia hohehahe.

    Kama watu wanaqualification zinazohitajika mimi sioni tatizo liko wapi. Ila kama wanataka huo uongozi kwa maslahi yao ndio tatizo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 01, 2007

    You need to be smart to live in a coutry as an immigrant, graduate from college, get married to the Kennedies, be a successfull movie star, make wise investments, and be CA governor. Rember, one needs to be smart to make money. This man is used as a case study in sociology and many other classes. If you are just like Anold, show us whatchu got.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 01, 2007

    Ndugu yangu mtoa maoni (June 1st,-7:27pm), nimejaribu kusoma maoni yako lakini sielewi ulikuwa na maana gani.
    Sijui kwa sababu umechanganya lugha na kujikuta umejichanganya mwenyewe kiasi cha kushindwa hata kucheck SPELLING ya maneno yako uliyotoka kutueleza.
    si vibaya ukarudia tena kwa lugha yoyote uitakayo(English, France, Swahili or Spanish) huenda tukakuelewa vizuri. Pengine una hoja nzuri lakini hukuipangilia itakiwavyo....MLALAHOI, MBAGALA KIBONDE MAJI, DAR.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 01, 2007

    Ok, I hope this will help.

    Vous avez besoin d'être intelligent pour habiter en un pays étranger comme un immigrant, un diplômé de l'université, obtenez épousé au Kennedy, êtes une star de cinéma réussie, une marque un investissements sages, et être un gouverneur de Californie. Se rappeler, l'un a besoin d'être intelligent pour gagner de l'argent. Cet homme est utilisé comme une étude de cas dans la sociologie et beaucoup de classes autres. Si vous êtes juste comme Arnold, nous montrez que vous avez.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 02, 2007

    weew anoy hapo juu kama unamtetea mtiu hivyo unatakiwa ujue mambo yake zaidi. Gov wa CA hakusoma USA. Amekuja mtu mzima na kazi yake ya kwanza likua road construction kusupport body building career yake. Ndio akapata movie gig ndio akaonana na maria. Na kwataarifa yako Califonia wanasema anayeiongoza ni mkewe kwa vile mambo mengi ndio anamwambia yeye.

    Nawakilisha

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 02, 2007

    Arnold was a millionair before age 22 and he earned a B.A. from the University of Wisconsin-Superior, where he graduated Business and International Economics in 1979.

    Maria as a CA first lady does not lead CA but she is just playing a first lady's role to advise her husband.

    CA wanasema anayeiongoza ni mkewe, mimi ninaishi CA wala sijamuona hata siku moja Maria akifanya kazi za Gov zaidi ya tangazo lake la redio jinsi ya kujiandaa na baa la moto au tetemeko la ardhi.

    Muwakilishi wakilisha na ukweli wala usiwakilishe with "he said she said"

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 02, 2007

    Schwarzenegger moved to the United States in September of 1968, having little money and still weak in English. There he trained at Gold's Gym in Santa Monica, California, under the patronage of Joe Weider. From 1970-1974, one of Schwarzenegger's weight training partners was Ric Drasin, the bodybuilder and professional wrestler who designed the original Gold's Gym logo in 1973. Schwarzenegger also became good friends with professional wrestler "Superstar" Billy Graham.

    He was just 20 years old when he moved to the US.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...