MIGOMO YA CHUO KIKUU INAEPUKIKA?
Chuo Kikuu cha Dar es salaam, katika siku za hivi karibuni kimekuwa katika chati kubwa sio kwa sababu zinazofurahisha, hivi niandikavyo Chuo hicho kimefungwa na wanafunzi wamewekewa masharti mazito wanayotakiwa kuyatimiza ili waweze kurejea. Kwa kadri nionavyo, kuna walakini mkubwa kwenye suala zima la mikopo ya wanafunzi. Kwa tafsiri na nadharia nyepesi, mkopo ni msaada anaopewa mtu kwa lengo la kuurudisha baadae lakini tunavyoona sasa hakuna mazingira kama hayo kwenye utaratibu wetu. Leo nimeona tujadili suala hili kwa kirefu ili kuweza kuishauri serikali ya sasa na kusaidia kuepuka migomo hii inayotokea mara kwa mara:
Vyuo vikuu duniani kote inafahamika ndio msingi mkuu wa uchumi wa nchi husika kwani kwa kiasi kikubwa wahitimu wa vyuo husika huingia katika uchumi wa nchi ama kwa ajira katika idara na makampuni au kujiajiri wenyewe.
Kwa mazingira ya sasa, takriban kila mwanafunzi aliesoma Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika miaka ya hivi karibuni, historia yake ya chuo haiwezi kukamilika bila kukutajia ushiriki wake katika mgomo! Kwa asilimi kubwa mikopo na fedha za wanafunzi ndio imekuwa ni tatizo kuu.Kama hatua madhubuti hazitachukuliwa, kuna hatari ya kuwa na wahitimu nusu nusu kutokana muda mwingi kupotea kwa wanafunzi kuwa katika migomo. Kwa vile tatizo ni mikopo nadhani ni bora kuangalia mfumo mzima kwa lengo la kuutafutia marekebisho maridhawa…
Vyuo vikuu duniani kote inafahamika ndio msingi mkuu wa uchumi wa nchi husika kwani kwa kiasi kikubwa wahitimu wa vyuo husika huingia katika uchumi wa nchi ama kwa ajira katika idara na makampuni au kujiajiri wenyewe.
Kwa mazingira ya sasa, takriban kila mwanafunzi aliesoma Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika miaka ya hivi karibuni, historia yake ya chuo haiwezi kukamilika bila kukutajia ushiriki wake katika mgomo! Kwa asilimi kubwa mikopo na fedha za wanafunzi ndio imekuwa ni tatizo kuu.Kama hatua madhubuti hazitachukuliwa, kuna hatari ya kuwa na wahitimu nusu nusu kutokana muda mwingi kupotea kwa wanafunzi kuwa katika migomo. Kwa vile tatizo ni mikopo nadhani ni bora kuangalia mfumo mzima kwa lengo la kuutafutia marekebisho maridhawa…
Kwa maelezo zaidi www.saidiyakubu.blogspot.com
Migomo katika vyuo vikuu nchini Tanzania inaweza kuepukika ikiwa watawala wetu watalipa kipau mbele swala la Elimu ya juu.Nchi haiwezi kuendelea kwa kutokuwa na vyuo vikuu.hawea ndio wasomi na wajenzi wa Nchi wa kesho.
ReplyDeleteIkiwa watawala wataendelea kusababisha migomo katika vyuo vyetu basi wana ajenda yao binafsi ya kutotaka wengine kupata Elimu kwa manufaa ya nchi bali wanatka kuonekana wao tu ndowenye degree wenye maisha bora na familia zao tu.
swala la Elimu ya juu lisiwe la kisiasa nchini Tanzania liwe swala la kijamii.wtawala wasilitizame swala la mgomo katika mboni moja ya jicho.
Mfano mzuri ni huu:kuna mwanafunzi mmoja namfahamu amefiwa na wazazi wake wote na ni watu tu wa pembeni wanamsaidia kulipa karo.je unaposema alipe asilimia 40% je atasoma???!
watawala wawe na akili wasitumie yale yanayowazunguka kuwaumiza watoto wa matonya wa watanzania
Dons say students` claims genuine
ReplyDelete2007-05-01 10:18:25
By Guardian Reporter
Members of the University of Dar es Salaam academic community have said the loan-related concern raised by students now suspended were genuine and required serious attention and have called on the government to address the issue ``in a timely manner and through an open and free dialogue``.
The stand is contained in a press statement issued in Dar es Salaam yesterday by the university`s Academic Staff Assembly (UDASA).
The university`s management on April 17 suspended indefinitely all main campus undergraduate students after they had boycotted classes for two days, protesting the government`s insistence that they bear 40 per cent of the costs of their stay at the university.
The suspension letter also covered all undergraduate students at the university`s constituent colleges, including the Institute of Journalism and Mass Communication.
Arguing that most of them come from poor families and therefore cannot raise the amount required, the students want the government to revisit its policy on loans in respect of institutions of higher learning and possibly cover the 40 per cent using its own coffers.
``While UDASA recognises the willingness on the part of the government to consider students` demands, we call upon it to seriously look into the matter and commit itself to providing a lasting solution,``the statement, a copy of which was availed to The Guardian, reads.
It calls on the government to initiate a public debate on how education in general, and higher education in particular, should be funded.
The statement notes further that the assembly, as an organ of academic members of staff, would like to see the university functioning normally.
UDASA has also expressed its concern over the manner in which the students were ordered to vacate the premises ``within a short time in the evening, when they were totally unprepared`` and appealed to the university management to revisit its position on the conditions the suspended students are required to fulfil before being allowed back.
Prior to students` suspension, the university�s administration had considered the students` demands, says the statement, adding: ``It is prudent that the University Administration revert to its earlier offer because the situation has not been altered by the suspension of students and perhaps for many students the situation has worsened.``
In the assembly`s view, the conditions for reinstatement ``are punishment to students, most of whom had not wanted to take part in the boycott of classes but were rather forced out of classes by their fellow students``.
Consequently, UDASA has deplored attempts by some students to suppress their colleagues who have dissenting views on how to achieve the goals they intend to achieve.
The assembly has also urged the university`s management to ensure that the reopening of the university does not cause inconveniences to students, staff and learning programmes.
Sidhani kama kuna haja ya kuongelea sana kwa sasa suala hili tatizo kubwa la elimu ya tanzania ni serikali zetu zimeingiza siasa ktk suala zima la mikopo.
ReplyDeleteMengi yana yameongelewa hata hapa kwa michuzi. Wataalamu wengi wanaongelea suala hili sema tu nilichogundua serikali zetu haziko tayari kusikiliza vilio vya wananchi wake.
Katika nchi zetu tumebakia kushindana masikini kwa masikini ukisha panda ngazi moja unajaribu kuhakisha mwenzako hainui hata shingo ndicho tunachokiona. Mikakati kabambe ya serikali imeisha sahau watu wa kawaida inaangalia matajiri wa Dar es salaamn, na mijini kuliko kuangalia ukweli wa mtanzanzania.
Kama wewe ni mbunge, mfanya kazi yeyote ulisoma kipindi bure huna budi ya kuchangia katika mfuko wa elimu hili wapate fedha za kukopesha wanafunzi wa kitanzania. Viongozi hawawezi kutunga sheria zinazowanufaisha wao tu ni lazima zinufaishe taifa la tz.
Wafanyakazi waunga mkono wanafunzi Chuo Kikuu
ReplyDeleteNa Mussa Juma, Arusha (www.mwananchi.co.tz),02/05/2007
SHIRIKISHO la Vyama Huru vya Wafanyakazi Mkoa wa Arusha (Tucta) limepinga uamuzi wa kuondolewa vyuoni wanafunzi wa vyuo vikuu waliokuwa wamegoma na limeitaka serikali kuvifungua chuo vyote vikuu bila masharti mapema iwezekanavyo.
Tamko hilo, lilitolewa jana katika risala ya Tucta mkoa, katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani mkoani hapa, yaliyofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo mkuu wa Mkoa wa Arusha, Samweli Ndomba alikuwa mgeni rasmi.
Akisoma risala hiyo, mratibu maadhimisho ya Mei mosi mkoani hapa, Soud Madega, alisema kitendo cha kufungwa vyuo vikuu vya serikali ni cha kulaaniwa na kila Mtanzania mwenye uwezo wa kutafakari.
Madega alisema hata kama viongozi wanaona maamuzi yao ni ya mwisho, lakini wanachodai wanafunzi ni haki yao na wala si upendeleo.
_"Wakati vyuo vinafungwa serikali ina ziada ya matumizi yake ya Sh900 bilioni katika matumizi hivi wangetuambia kuna matumizi ya zaida kugharamia elimu nani angelalamika?"_ alihoji Madega.
Alisema kuondolewa wanafunzi hao ni uonevu mkubwa na Tucta haipo tayari kuvumilia kwani watoto wa wafanyakazi maskini hawawezi kupata asilimia 40 ya kugharamia elimu hiyo.
Shirikisho hilo limeitaka serikali iepuke siasa katika masuala ya msingi na isikwepe kufanya mazungumzo na wanafunzi wa vyuo vikuu ili kuepuka migogoro.
Tucta imeishauri serikali idhamini wanafunzi wote wa elimu ya juu kwa kuwapa mkopo wa asilimia 100 kwa sababu wataalam hao watakapohitimu masomo watafanyakazi ya kujenga taifa.
TUCTA pia iliendelea kulalamikia makato makubwa ya kodi katika mishahara ya wafanyakazi licha ya kuwa wanalipa kodi ya asilimia 20 kwa kila wanachonunua.