mdau asanterabi malima akienda kupokea nondo zake baada ya kumaliza mastaz yake huko uturuki hivi karibuni. naona wabongo wamecharuka siku hizi kwa kula nondo mpaka kieleweke na hamna noma wala nini...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2007

    Hongera sana,salam nyingi kutoka birmingham

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2007

    Babao,
    Hongera sana. Naona umekamilisha masomo yako kama ulivyodhamiria.
    Sasa vipi? Bado una ule mpango wa kuja huku Jep?
    Kaka yako wa JP.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 09, 2007

    Aisee Asante hongera mzee

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 09, 2007

    Congrats bro!!! Its so amazing kwa jinsi vijana tunavyojituma siku hizi. Ombi ni kwamba mrudi kulitumikia taifa labda mtaleta maendeleo. Michuzi asante kwa hiyo picha imenikumbusha class yangu ya Oysterbay, asanterabi alikuwa mdogo halafu mtundu sana..

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 09, 2007

    Hongera kaka kwa kumaliza masomo yako. Kama Michuzi kweli Mpakanjia anaumwa??? Yu hoi Muhimbili??? Nitashukuru sana ukijibu swali.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 09, 2007

    Ustaadh Asante, hongera saana mwana. As usual you've done what you always do best "MSHUKO", very proud of you brother. Keep on aiming for the sky.
    MMK

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 09, 2007

    Kaka Hongera - Mshamma Jr

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 09, 2007

    du product ya O/bay primary hii!!Kijana anapiga nondo huyu!!Kila la kheri nami sirudi bongo mpaka nimekamata gamba la pili!!Wabongo majanki tupige buku tukawang'oe akina Balali na sampuli nyingine zote za namna hiyo!!!Hongera Asanterabi,
    O/Bay mate, UK

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 09, 2007

    Babao sasa inabidi ukamilishe ikiwezekana Panda hadi Darini(PhD) kama Steel.Mshuko uendelee!Hongera sana ustaadh salamu toka kwa mzee Bozi.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 09, 2007

    Naona Vijana wa Mama Ng'ambi O/Bay Primary wanazidi kung'aa ndani na nje ya nchi...

    JOAN umenikumbusha mbali sana kwa kulitaja jina la O/Bay. umenikumbusha enzi za shule za Halmashauri.

    Hak-ya-nani, shule za halmashauri zilikuwa na raha zake enzi hizo.

    Japo fimbo za walimu ndo zilikuwa zinanikera,dakika za majeruhi nilijenga usugu wa bakora za walimu. walimu wa O/Bay ninaowakumbuka akiina NyagaBona, Mwalimu Kipa, Mwalimu Bahati (wa Hisabati), Mama Ngole (mwalimu wa Kiingereza), halafu kuna yule mwalimu mzuri mzuri jina nimelisahau lakini alikuwa akiitwa Madonna.

    mnamkumbuka yule mlinzi aliyekuwa akiitwa MCHAMBAWIMA... jamaa akijambishwa anaruka na kuwa mkali kama Shehe aliyelishwa kitimoto hadharani.

    Good old days....
    michuzi, ukipata nafasi jaribu kutembelea hizi shule za halmashauri. wengi wetu tumepitia huko na hatuna updates ya shule zetu. tutafurahi sana kupata ma-snepu ya shule zetu zilivyo sasa huko home.

    ReplyDelete
  11. Hongera sana kwa kugraduate - mdau wa bondeni

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 09, 2007

    Kaka michuzi hongera sana kwa kututumia picha za maendeleo ya wabongo huko ughaibuni hasa katika maswala ya elimu. keep it up the good work. tunawaomba wakumbuke kurudi nyumbani kusaidia nchi yao

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 09, 2007

    Duh! Mshikaji anaitwa AsanteRabi? Hongera Asante Mola!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 09, 2007

    COOOK Tebrikler abi.Mtoto wa nyoka ni nyoka.Nyoka azai mjusi.Mwana huyu kawatesa Mabata(waturuki) vibaya sanaa kuanzia 1st degree hadi 2nd degree.Saluti broo.Nasi watutia moyo wabongo wengine kwa mfano wako huu.
    Mwanao kimz

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 10, 2007

    Asante aka Babao HONGERA SANA!!!
    Yani kama nawasikia vile jamaa wanayoshangilia hapo..baada ya mtangazaji kutangaza jinsi ulivyopasua pasua vibaya SANA

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 10, 2007

    iste boyle abicim.TEBRIKLER! kushangaza mabata.
    MLUGA

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 10, 2007

    Anon@ 4:24pm
    Good memory, umekumbuka mpaka majina ya walimu? we kweli ulikuwa mwanafunzi bora! kwa nini mlimwita mwalimu madonna? any specific reasonz? N'wayz yote tisa, kumi... MCHAMBAWIMA?
    I love swahili!

    Hongera sana kaka kwa ku-gradueti! yap! you should (Phd) panda hadi dalini or pull heavens down, ili ujue zaidi hata vilivofichika huko juu.

    Congrats!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 11, 2007

    mbona hatuoni picha za wasicha....hey jamani mpooooooo
    onyesheni nyundo senu au kama ndio mpenda mpaka darini mtuchungulie chini kidogo tu jamani tuwaone

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 11, 2007

    MBona kama ukumbi wote wako eksaitedi ,ni kwa sababu wana mshangaa huyu mweusi kuchukua hiyo digirii, au sababu ana vutia?

    Obay wow sijui nianzie wapi , yani those were dayz, nikikumbuka kitenesi na lile chuma kule sijui madarasa ya tatu, ambako maji huwa yana jaa wakati wa mvua ,so tuna panda lile chuma kucheza kidali po.


    Nakumbuka kina Mwal Kazoza,Liwali,Apson,KIpa,Ngole,Musya,Manguku,Temba,Nchimbi,Bombuli,MUzoh,Toroka(Marehemu),Shayo,Kitipwi,Mbwambo,Kadebe(beutiful),Omary,Nyangabona,Kulwa,Shigela,Mihayo,Lubuva,Kirigini,Sichembe,Nyoni,Masanja,Musikula,(Marehemu),Kashaga,Mwamanga,Kikove,Bonda,Ngambi(Marehemu),Ng'osha, na wengine wengi!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 11, 2007

    I am very very proud of you! you are so gorgeous!!!!! the picture it self says it,doen't it?.Huyu (Asanterabi)ni mashine kubwa kabisa msidhani ni mchezo, kama hamuamini ingieni hapa http://www.sabah.com.tr/2005/06/28/gnd119.html afu katafute dictionary ya kituruki mtajua aliwafanya nini Waturuki mwaka 2005 (alipomaliza first degree) na aliipeperusha vipi bendera ya TANZANIA uturuki!(Nazar değimesin) seninle gurur duyuyorum abi

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 12, 2007

    hongera sana Asante!!!
    Nakuaminia kaka. Endelea kukamua. Chukua hadi PhD ya Mechatronics uje uintroduce Bongo hiyo field kaka.

    Inafurahisha kuona wana O'bay mmetuma msg kemkmem kumpogeza mwenzetu. Safi sana... natumai wote mnaendelea kupiga bao kisawa sawa wherever u r. Asanta toka primary alikuwa anatisha. Infact mwaka wao wote walikuwa vichwa.. kina Swere, Kija, Sekwao, Mgulu, Tumaini, etc!!
    (class of 92). Walituinspire na sisi kufanya mambo kwa kwenda mbele !!

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 12, 2007

    well done bro.we real appreciate for what u did.inshallah mwenyezi mungu akupe wepesi zaidi katika masomo yako kama wafikiria na kukamua na hiyo ya
    phd.kwa kile ulichokipata kiwe basi faida ya jamii yetu changa ambayo bado ipo katika wimbi la umaskini.jamii ifaidike na kile ulichokipa hapa uturuki.sir.buru upo kaka?.
    well done bro.asanterabi

    wise A.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 13, 2007

    Annony wa July 11, 2007 5:54:00 AM EAT
    nimeikubali Memory yako. Umetaja majina ya walimu amboa binafsi nilishayasahau kabisaaa.

    hiyo habari ya chuma la kule karibu na nyumba ya mwl mkuu nalo pia limenikumbusha mbali sana. niliwahi kuanguka na kuumia vibaya ktk hilo chuma sitolisahau.

    Nimekumbuka mambo ya kujiita LY "Last Year" ukiwa darasa la saba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...