
kundi linalojiita 'fans of simba' limeibuka dar na kuanza kufanya vitu vyake kwa makeke ambapo leo wameweka hadharani gari ambalo litachezewa bahati nasibu maalumu katika harakati za kundi hilo kuinasua klabu ya simba toka katika lindi la utegemezi. pichani ni baadhi ya viongozi wa fans of simba na gari lao
Michuzi,
ReplyDeleteHongera kwa sura mpya na kupata mdhamini wa blogu. Haya ni matunda ya bidii na kazi yako nzuri, inatia moyo. Naam! Niko mjini, nimeingia jioni hii. Nitakutafuta kesho na keshokutwa.
Hawa bwana wa fans of Simba wamenifurahisha sana. Huu ni mfano ambao unapaswa kuigwa na klabu nyingine katika kuinua sekta ya michezo hususan mpira wa miguu. Klabu nyingine kama Yanga zisiogope kuiga ubunifu wa namna hii kuchelea kuchekwa!. Mimi nitakuwa mmojawapo atakayecheza bahati na nasibu ya namna hiyo kwani naamini katika kufanya hivyo nitakuwa nachangia maendeleo ya michezo Tanzania.
ReplyDeleteRiganda.
Nawapongeza sana kwa ubunifu, sio kama klabu inayotegemea fedha za mtu binafsi na siku akipata mafua kidogo wanatafutana, akipata maralia ndio kabisaaa klabuni amani inatoweka. Analosema hakuna mtu wa kutia neno. Hongera sana fans of simba!!!!
ReplyDeletesawa nyie fans of simba kweli mnataka kuendeleza timu au mnataka kufanya miradi kwa kupitia mgongo wa klabu aya tutaona mwisho wake
ReplyDeletemambo haya mi ndo huwa yananiudhi kwenye mpira wa bongo.leo mara kuna friends of simba,kesho oh kundi jipya la fans of simba.hivi kuna ubaya gani hawa friends of simba wakiunganisha nguvu na fans of simba ili kujenga kitu imara.kuna mahali nimewasikia fans of simba wakiapa kwamba kamwe friends of simba hawatewa timu,ndo nini mnafanya/ujinga mtupu.wwatu mnajenga nyumba moja,ya nini kugombea fito? issa acha ku promoti mambo ya ujuha haya.
ReplyDeletemambo ya kiswahili swahili tuu ndio maana hakuna maendeleo yoyote na kitakachofuata ni ugomvi mpaka kiama na wajanja hapo watatoana macho kwa ulafi ....kesho wataibuka wengine na keshokutwa wengine na wengine,haya mabo yanatakiwa yaende kisheria na utaratibu unaokubalika katika nchi sio uhuni uhuni tuu kama kina jack Pemba,please shut down this shit maana naona watu watalizwa tuu
ReplyDeleteHAWA FANS OF SIMBA HAWANA LOLOTE ILIYOBAKI NI MISHAUO TU !!!! SIE TUNAOWAFAHAMU NI FRIENDS OF SIMBA !! NA HAWA NAO WAMETOKA WAPI WEEEEH MISUPU WA KUCHUMPAAAAAAAA !!!!
ReplyDelete