kundi linalojiita 'fans of simba' limeibuka dar na kuanza kufanya vitu vyake kwa makeke ambapo leo wameweka hadharani gari ambalo litachezewa bahati nasibu maalumu katika harakati za kundi hilo kuinasua klabu ya simba toka katika lindi la utegemezi. pichani ni baadhi ya viongozi wa fans of simba na gari lao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Hongera kwa sura mpya na kupata mdhamini wa blogu. Haya ni matunda ya bidii na kazi yako nzuri, inatia moyo. Naam! Niko mjini, nimeingia jioni hii. Nitakutafuta kesho na keshokutwa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2007

    Hawa bwana wa fans of Simba wamenifurahisha sana. Huu ni mfano ambao unapaswa kuigwa na klabu nyingine katika kuinua sekta ya michezo hususan mpira wa miguu. Klabu nyingine kama Yanga zisiogope kuiga ubunifu wa namna hii kuchelea kuchekwa!. Mimi nitakuwa mmojawapo atakayecheza bahati na nasibu ya namna hiyo kwani naamini katika kufanya hivyo nitakuwa nachangia maendeleo ya michezo Tanzania.
    Riganda.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 02, 2007

    Nawapongeza sana kwa ubunifu, sio kama klabu inayotegemea fedha za mtu binafsi na siku akipata mafua kidogo wanatafutana, akipata maralia ndio kabisaaa klabuni amani inatoweka. Analosema hakuna mtu wa kutia neno. Hongera sana fans of simba!!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 02, 2007

    sawa nyie fans of simba kweli mnataka kuendeleza timu au mnataka kufanya miradi kwa kupitia mgongo wa klabu aya tutaona mwisho wake

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 02, 2007

    mambo haya mi ndo huwa yananiudhi kwenye mpira wa bongo.leo mara kuna friends of simba,kesho oh kundi jipya la fans of simba.hivi kuna ubaya gani hawa friends of simba wakiunganisha nguvu na fans of simba ili kujenga kitu imara.kuna mahali nimewasikia fans of simba wakiapa kwamba kamwe friends of simba hawatewa timu,ndo nini mnafanya/ujinga mtupu.wwatu mnajenga nyumba moja,ya nini kugombea fito? issa acha ku promoti mambo ya ujuha haya.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 03, 2007

    mambo ya kiswahili swahili tuu ndio maana hakuna maendeleo yoyote na kitakachofuata ni ugomvi mpaka kiama na wajanja hapo watatoana macho kwa ulafi ....kesho wataibuka wengine na keshokutwa wengine na wengine,haya mabo yanatakiwa yaende kisheria na utaratibu unaokubalika katika nchi sio uhuni uhuni tuu kama kina jack Pemba,please shut down this shit maana naona watu watalizwa tuu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 04, 2007

    HAWA FANS OF SIMBA HAWANA LOLOTE ILIYOBAKI NI MISHAUO TU !!!! SIE TUNAOWAFAHAMU NI FRIENDS OF SIMBA !! NA HAWA NAO WAMETOKA WAPI WEEEEH MISUPU WA KUCHUMPAAAAAAAA !!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...