WADAU WAPENDWA. LEO NIMEPATA HABARI ZA KUSIKITISHA KWAMBA MDAU MAGGID MJENGWA KAHARIBIKIWA NA KAMERA YAKE NA SASA AMEBAKI HANA NONDO YA KUFANYIA KAZI. HAPO CHINI KUNA UJUMBE WA MWALIMU MAZARA AMBAO KAUTUMA KWANGU BAADA YA KUGUNDUA HABARI HIZO KWENYE BLOGU YA MAGGID. MAGGID NAYE KATUMA UJUMBE KUTHIBITISHA HAYO NA KUTUPA ANUANI YAKE ILI WADAU WENYE MOYO WA KUSAIDIA WAMSAIDIE KWA HALI AMA MALI. KWA KUANZISHA HARAMBEE HII MUHIMU MIMI BINAFSI NACHANGIA SH. 50,000/- NA NATUMAI WADAU WENGINE MTANIUNGA MKONO. KUTOA NI MOYO, NA HUU NI MCHANGO WA HIYARI YA MOYO. HARAMBEE WADAU NA SHIME TUMSAIDIE MAGGID ILI AENDELEZE LIBENEKE!
WAKATABAHU
MICHUZI M.I.
ujumbe wa mwl. mazara huu chini:
WAPENDWA WATANZANIA WENZANGU KOKOTE DUNIANI.
KAMA MMOJA WA WASOMAJI NA MSHABIKI MKUBWA WA KAZI NZURI ZINAZOFANYWA NA WAANDISHI WETU HUKO NYUMBANI IKIWA NI PAMOJA NA NDUGU MAGGID MJENGWA, ISSA MICHUZI NK., JIONI HII KATIKA KUPITIA "BLOG" YA MWANDISHI MAGGID MJENGWA INAONYESHA CAMERA ALIYOKUWA AKITUMIA NA AMBAYO IMWEMWEZESHA KUCHANGIA KUMBUKUMBU NYIIIIIINGI ZA MIAKA HIYO HADI SASA IMEHARIBIKA NA LABDA PENGINE IKAWA VIGUMU KUTENGENEZWA. NA ANAHITAJI INGINE HARAKA IWEZEKANAVYO ILI AENDELEE KUTUTUMIKIA.
MCHANGO WAKO WA $ 1-$ 10 KUPITIA "WESTERN UNION"( AU ZAIDI KUTEGEMEA NA UWEZO WAKO BINAFSI), KWA NDUGU MJENGWA UNAWEZA KUMWEZESHA KUJIPATIA CAMERA NYINGINE YA NGUVU, ITAKAYOMWEZESHA KUENDELEA KUFANYA KAZI YAKE KWA UFANISI NA UFASAHA ZAIDI.***IKUMBUKWE YA KWAMBWA, NI KATIKA UPENDO, KUJALI NA KATIKA UTAMADUNI WA KUJITOLEA KATIKA HALI NA MALI UMEENDELEA KULETA TOFAUTI KUBWA ZA KIMAISHA DUNIANI.
Mfano halisia: Leo tuonapo watu binafsi kama vile( Bill Gate), mashirika ya dini, biashara mbalimbali wakichangia katika katika maendeleo ya watu mbalimbali Duniani, si kwamba ni Wajibu wao, bali ni kutokana na kujali na upendo wa kutaka kuleta tofauti za kimaisha, kielimu, kijamii nk.
Huu ni utamaduni mzuri mno wa kuigwa.Ndugu Mjengwa, natumaini ujumbe huu utawagusa wengi na hasa wale wenye nia ya kusaidia kama mimi, na hivyo kupata SULUHISHO LA KUDUMU WA CAMERA YAKO.
Mawasiliano yako, ikiwa ni pamoja na ni wapi pa kukutumia michango yetu ya hiari itasaidia sana. Ni wenu katika Kujali, Kuthamini na Kuendeleza Vipaji/Wataalamu( Huko Nyumbani), bila kutegemea Bajeti ya Serikari au Wahisani wa Kigeni.
Mwalimu Mazara
tamko la maggid mwenyewe ni hili chini:
Nami namshukuru Bw. Mazara kwa wazo na moyo wake huo. Hakika, nitashukuru kupata mchango wowote ule wa hiyari. Unaweza kutuma mchango wako kwa njia mbili; Benki ya NBC au Western Union. Anuani yangu kamili ni:
Maggid John Mjengwa
Box 2414,
Iringa,
Tanzania
NBC LTD,
NBC LTD,
Iringa Branch.
Acc No: NLCBTZTH 0282010 37642
Kama unatuma kwa Western Union unaweza kunijulisha code numbers kwa email: maggid@hotmail.com au kunitumia sms: + 255 713 858582
Natanguliza Shukrani.
Maggid
Michuzi, Maggid mi nipo UK hapa na nautambua mchango wenu hivyo kesho nitatuma mchango wangu..
ReplyDeleteTatizo la Watanzania wanapenda sana vya bure na ukitoa issue kama hii watafunga macho na wakati huo huo wanategemea uwape habari kwenye blog... na jambo likienda kombo tu utaona wanavyo chonga.. Wananikera wabongo wapenda vya bure..
Wabongo tungekuwa kama mataifa mengine tungeendelea sababu wengi tu wanafanya mambo ya mazuri na kuchangiana lakini wapiiii wabongo wanataka vya bure tuuuuuuuuuuuuuu.
Waungwana tumchangie ndugu yetu Maggid mchango wake naujua na ni mkubwa kwenye jamii..
Tubadili tabia na tuwe na moyo wa kusaidiana na kuchangia..
Are you serious!!?
ReplyDeleteAngalia hi blog isijekuwa ni sehemu ya kila mtu kuomba msaada hata kama hauitajiki....ila ukiwa na tatizo sema, watu wenye roho nzuri watasaidia....ila MSIZOEE SAANA KUOMBAOMBA
ReplyDeleteMtu kama anataka kuchangia achangie sio kutoa kashfa mara wabongo sijui nini au nini. Mbona yako mambo muhimu sana ya kuchangia kuliko hiyo kamera ya Maggid? Kuna masuala ya watoto yatima,walemavu nk lakini hao wadau wa huko UK mbona hawachongi kama hilo nalo ni muhimu.Tuchangiane lakini tuache sifa
ReplyDeletenajua wewe anon Tarehe July 5, 2007 9:38:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous
ReplyDeleteunataka sifa
Hivi niambie kuna blog gani TANZANIA itakuletea picha kama hizo anazopiga MAGGID? mjengwa blog yake inatupa REALOITY on the ground na siyo maharusi na sherehe za wakubwa DAR so please hebu get a grip. N a kama unataka kuchangia MAYATIMA fine lakini mbona HULALAMIKI wakati OFISI YA WAZIRI MKUU INATAKA KUTUMIA BILIONI 3 KUFANYA UKARABATI?
acha hizo
maggid tegemea mchango wangu kesho panapo majaaliwa na uhai
Jamanii eeh bla bla bla hazisaidiii chochote. Na ndio maana imesisitizwa kuwa ni hiari yako. Hivyo badala ya kuanza kukumbushiana omba omba au kusaidia yatima, ingekuwa vizuri either kutoa au kunyamaza tuu. Wewe unaesema kuchangia yatima au walemavu wewe ni lini umeshawasaidia hao?? Du kuchonga tuu!!! kaka sina uwezi ningekununulia brand new kabsaaaaaaaaaaaa.. pole sana!!
ReplyDeletemmh yamekuwa haya tena??? Tunachangishana hivi hivi???does this man work anywhere??? Pse fanya maarifa yako kuna vitu vya kukuchangia lakini si zana za kazi(jembe). We tafuta kivyako wachangishe akina Michuzi au funga blog!! we vipi!!
ReplyDeleteHuu ujinga, sasa hivyo kamera aliipataje kwanza? Kama ni ya mwajiri wake kwanini tuchange? kama hana hela basi atafute fani ingine. Michango imezidi jamni kila siku michango mara utasikia mchango wa kuchangia kununua kalamu yake ya kuandikia.
ReplyDeleteHihi hapa kuna mambomnei ya kusema sio tatizo mchango ila kama Maggid amefanya kazi siku nyingi n , je kwa nini ameshindwa kununua ingine maana ndio kazi yake kupiga picha na si kweli amekuwa na hiyo camera muda mrefu pia ana ajira so haombe kwa hao kampuni yake sio kutumia hii blog kwa kuomba hii ni aibu , kwenye wewe Michu utasema kuwa hata wewe unaitaji camera , lol, na kama zipo kame nyingi kwa kazim kama yako yaani 35 mm au ndio unataka digital ya bei baya maana kana ni 45 mm nitakutumia hata leo hii , zipo nyingi kwenye maduka bei poa na inategemea ni aina gani so watu tunajua upotografi pia aina za camera na hizi blog kamaunaona unafanya kazi bure sema kuna vitu kama matangazo so wambia watu kama benk hii inayotumia blog ya Michu wakusaidia ili wakupe camera na wewe utangaze matangazo yao kwa muda fulani fulani maana hakuna vya bure ....na unataka camera ngapi ? lol hii michu usipotoa nitajua na wewe upo kwenye deal hiii lakini tutamngangia huu ndugu yetu ila siku ignine plz plz tuletea michango ya vifo, kusaidia watoto yatima, AIds na vilema sio kwa vipi kama hivi .... asnate mkereketwa..
ReplyDeleteKWANI BLOG BILA PICHA HAIWEZI KUSOMWA KILICHOKUSUDIWA KUANDIKWA!
ReplyDeleteMJENGWA UMEKAA UGHAIBUNI MIAKA MINGAPI KIASI CHA KUSHINDWA KUWA NA KAMERA ZAIDI YA MOJA.
KAMA KWELI WEWE NI MPENDA FANI YA SHUGHULI ZAKO, LAZIMA UWE NA NYENZO NYINGI ILI MOJA IKIENDA KOMBO, NYINGINE HUCHUKUA NAFASI.
MICHUZI NADHANI ANA KAMERA ZAIDI YA MOJA LICHA YA ZILE ZA KAZINI KWANI DAILY NEWS.
HII TABIA YA KUOMBA OMBA IMEKUA MBAYA NA ITAPELEKA WENGI PABAYA. TUJIFUNZE KUJITEGEMEA. SITOI MCHANGO KWAKO NG'O LABDA UNGEKUWA KILEMA UNAYEHITAJI MSAADA WA KWELI.
KWAHERI...KINATI
huyu magidd alikuwa haweki savings?? hiki kifaa ni sehemu ya kazi yake, huu ni ubabaishaji wa hali ya juu. Kuchangia ni kuendekeza uzembe, ingawa kwa upande mwingine ni vyema kuchangia vitu kama hivi kuliko kuchangia harusi.
ReplyDeleteSITATUMA MCHANGO.........
Jamani michango,michango,michangoooo,itatuua.Sasa uhabari gani huo nyenzo imekufa unaomba mchango?ina maana soon michuzi nae ataomba mchango.Wabongo mgrow up mambo ya michango yanaturudisha nyuma.Au vipi funga blog si HUNA NYENZO ZA KUFANYIA KAZI?ya nini kupitisha bakuli?Sichangi ng'oooo
ReplyDeleteMh! Wabongo bwana! Sijui tukoje, Maggiji keshaona sisi ni watu wa kuongopeeeeeeewa!!!!! Yaani umekaa Sweeden kwa miaka yote hiyo ushindwe kununua kamera ambayo kwa hapo bongo haiwezi kuzidi laki nne? Mi nadhani ni kujidhalilisha, ni vizuri nyie watu wa blog mjue kwamba kutembelea blog zenu na kufurahia sio tiketi ya kuombwa fedha za kumalia nyumba zenu!
ReplyDeleteHebu tuendee jamani.......
KUTOA NI MOYO NA NI HIYARI YAKO. LAKINI WATANZANIA TUTAJIFUNZA LINI NENO KUJITEGEMEA? KWANINI KILA KITU TUNATAKA TUCHANGIWE? MWISHO TUTAANZA KUCHANGIA CHUPI ZA WATU. KAMA UANDISHI NI KAZI YAKO KWA NINI BASI HUWEZI KU SAVE NA KUMAKE SURE UNAJIDHATITI HASA KATIKA HILO. JE KESHO UTATUAMBIE TUCHANGIE MAFUTA YA GARI AU NAULI YA DALA DALA KISA HUNA YA KUKUFIKISHA KAZINI ILI UENDELEZE HIYO BLOG YALO. KAMA HUWEZI BASI FANYA HIYO GLOB WATU WA SUBSCRIBE ILI UWEZE KUPATA HELA. LAKINI TUACHANE NA TABIA TEGEMEZI HII, LETS BE LEARN TO BE INDEPENDENT FOR ONCE. TUACHE KUOMBA OMBA NDIO MAANA TUNASHINDWA KUENDELEA, HATA WALE WALIO ENDELEA KIDOGO WANARUDISHWA NYUMA NA TABIA HII YA KUOMBA OMBA UTAKUTA MTU HAWEZI KU SAVE HATA SENTI MOJA KWANI KILA KUKICHA KUNA BAKULI LA NAMAN MOJA AMA NYINGINE LINATEMBEZWA. KUENDELEA KUCHANGIA HAYA MABAKULI NI KUENDEKEZA UJINGA. LET'S STOP NOW! EBWE!
ReplyDeleteMaggid kabla sijatuma mchango sema kama na hela ya kula imeisha basi niongezee kidogo, husione aibu ni maisha ya kawaida..lakini Maggid niulize...ngoja niache heheh hehe..Maggid bwana,hehe!!! mbavu sina...Alafu na wewe Michu kwa kusakizia sikuwezi hehe....
ReplyDeleteSijasoma maoni yote lakini kama yote ni ya like 3: 26 basi hata hamu inakua hamna. Wewe kukosoa watu ni yanini kama mni mchango toa wewe malumbano ya nini? Hii ni kukatishana moyo na midomo isiyo na akili kichwani ila kukosoa tu.
ReplyDeleteWewe toa mchango wacha maneno. Waosha vinywa au wew ndio mchoyo roho inakuuma sas unashindwa pa kusemea. kama alivyosema Michuzi kutoa ni moyo sasa kama unatoa toa na ukae kimya.
Mimi nitakutumia soon
Ukweli ni kwamba watanzania hatujui mambo ya msingi.Mko radhi kuchangia mafuta ya waziri mkuu kuzurura nchini lakini mnajidai kuhoji kwanini brother Maggid achangiwe kununua kamera ambayo ndio chanzo cha habari muhimu za nchi yetu.Hivi tukoje sisi wabongo?Vichwa kama maandazi.Kama mtu huna unasema sina.Sio aah,sichangi,sijui angesave,sijui nini.Maneno maneno mengiiiii,kaa kimya kama huna,hujalazimishwa kuchanga.Waache wenyenazo na wenye hela wachange.Maggid utapokea kutoka kwangu kaka.Achana na hawa watu uchwara ambao wanadhani maneno ndio mtaji.**8%#@#@#@#@@@@ zenu.
ReplyDeleteNADHANI HUU NI UTANI TU KWANI KAMA HILO OMBI LA MCHANGO NI LA DHATI BASI NADHANI TUNAKOELEKEA SIO KUZURI.KINACHOWAFANYA HAWA WENZETU WA MAGHARIBI WATUPIGE BAO NI ILE SENSE YA KUJITEGEMEA AMBAYO JAPO SIE TULIKUWA TUNAIHUBIRI ENZI ZA UJAMAA BADO KUNA MAELFU KWA MAELFU YA WANAOSUBIRI VYA DEZO.SIWADISCOURAGE WANAOTAKA KUCHANGAKWANI HUO NI UAMUZI WA MTU BINAFSI LAKINI HUYU MUUNGWANA MAGGID ANACHEKESHA
ReplyDeleteMI NINAWAUNGA MKONO WABONGO WOTE WANAOPINGA HII TABIA YA KUPITISHANA MABAKULI YA OMBAOMBA KILA KUKICHA.
ReplyDeleteMJENGWA YA NINI KUJIDHALILISHA NA KUJIWEKA SAWA NA WALE OMBAOMBA WA BARABARANI.
KUNA FAIDA GANI YA KUWA NA BLOG WAKATI NYENZO ZA KUFANYIA KAZI HUNA.
NI SAWA NA KUWA NA MWANAMKE HALAFU UNAOMBA WATU WAKUSAIDIE KUMKANYAGA WAKATI MWENYEWE HUWEZI KUMHUDUMIA.
ELIMIKA BWANA MDOGO PIGA KAZI UPATE NYEZO. NUNUA HATA KAMERA NDOGO UTAKAWEZA KUWEKA PICHA KWENYE BLOG. JIFUNZENI KUJITEGEMEA.
Wabongo hacheni k... zenu hapa maggid kaomba msaada na mwenye nacho atoe na sio kupiga domo humu.
ReplyDeleteMnapenda sana kuletewa huduma za bure ngoja siku Michuzi nae aseme hakuna blog sijui mtafanyaje.
Mijitu mna mambo ya kis....*2 utafikiri hamna kazi. Roho mbaya tu.. umezoea kuwa na mitandao ya bure tu. Kiwanja kila huduma lazima ujiandikishe kwa malipo ndio uipate. Ipo siku bongo itafikia hilo na sijui mtafanyaje!!!!
Maggid nakuunga mkono kwa hili swala.
Tuendelee kumchangia ndugu yetu Maggid.
Hivi nyinyi mnaosema wenzenu (Maggid)wanapenda vya bure, mbona na nyinyi mnasoma blog yake bure,mnafikiri habari na picha zinajibandika easy tu! Kama huna kitu na uko majuu rudi haraka ujiunge na Maggid Kijijini na ataendelea kukusomesha blog bure.Cha msingi hapa ishasemwa ni hiari-sasa hiari manake kama unacho TOA na kama huna au hujisikii kutoa kata kona usiwavunje moyo wenzako kwani sio suala la mjadala.Maggid nakupa Big UP...
ReplyDeletetehe tehe tehe........ maoni matamu..
ReplyDeletevihi kandoro atawaweza ombamba kweli, tehe tehe ombaomba on line!
hivi hawa wadhamini wa blog wameona hili ombi? na udhamini maana yake nini nisaidieni.
hivi hii blog haitembelewi na WACHUMI? wamfundishe basi huyu mgogo nini maana ya biashara.
hivi.... mabilioni ya KIKWETE YAMEISHA? very interesting
BOTTOM LINE ni kuwa SICHANGII HATA THUMNI.
ReplyDeletehuyu mtu aliyotuma comment yake ya saa na tarehe hii July 6, 2007 3:10:00 AM ni mpumbavu maana Maggid kazi yake ni kupinga picha so watu wanasema kama ni kazi yake wanini asijuwe kuwa inaitaji kusave au kuwa na camera nyingi na pia blog kusign ni bure na kama anaweka news plus thanx kwa hiyo lakini sio kutake adventage ya watu kama kumsaidia tutamsaidia ila lazima tuwambia hii ndio yale mambo ya michango kila siku bongo hata kwa faida ya yule mtu mwenyewe pia michu ni rafiki yake na mfanyakazi mwenzeke anaweza kumsaidia camera mmoja kati ya zile zake na hii pia ni aibu maana hii blog mara nyingi uwa ninaacess na marafiki zangu hambao wajue kiswahili je nitawafahamishaje kuwa jamaa maggid ni mpiga picha mzuri na anafanya kazi safi leo ina ana camera na pia aliokuwa nao ametumia miaka mingi lol na tena anaomba kumsaada kwetu. sina ya kusema ila michu watch out plz sio kuweka kila kitu wanakuomba vingine fikiria kwanza au free of speech , rite ....
ReplyDeleteMichuzi, I like ur Blogg. Majid, I always truly likes ur Articles. lakini kwa hili naona kama mmejishusha hivi, maana mmerudi kule kule wabongo tulikojifikisha. kupenda ufadhili....samahani lakini.
ReplyDeletee bwana Magidd
ReplyDeletehivi ni kweli Camera umepoteza au ndio unataka mchango wa kumalizia nyumba. Mbona hujatoa breakdown ya kwamba unataka kununua Camera ya bei gani?? na kwamba wewe utachangia kiasi gani??
Nafikiri umejiabisha sana kuomba omba namna hii.
Mtoa maoni July 6, 2007 1:45:00 PM EAT, kwani rafiki zako Mungu? unawasujudu sana. kwani wakiona mtu anaomba kusaidiwa la ajabu nini. Mmezidi.
ReplyDeleteWenye nazo watatoa nyie msionazo kaeni kimya. Mnasema mishango imezidi na huku nyie kila siku mwapitiza vicard kwa watu. Ni circle of life. Leo mchangie kesho atakuchangia.
Usipomchangia na wewe ukiwa na lako wala usichange.
Magidd mimi naomba usisahau japo thank you note card