msanii langa (pichani) anatoka na album karibuni. hivi sasa anatesa na kibao kipya kilichoanza kupigwa redioni hivi karibuni kinaitwa "Pipi ya kijiti"mistari yake mwanzoni inaenda kama hivi "...mademu wengine wanapenda maua ya waridi, si bora pipi ya kijiti unakula unafaidi..."
wadau wanaweza kujionea wenyewe www.myspace.com/langa255
Habari yake yake nyingine hapa http://michuzijr.blogspot.com/2007/06/langa.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2007

    Na hizo nguo za jeshi zimeruhusiwa siku hizi au?? Ni vema zikaendelea kukatazwa zitaeneza wizi tu na ujambazi.

    Maeneo mengi ya vijijini ukivaa hivyo hata kodi ya kichwa unaweza kudai na watu wakakata mshiko. Unaweza kusema umetumwa na Nyerere kuchangisha pesa za mwenge na watu waka amini. Kaaaazi kwelikweli!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2007

    mademu wanapenda sana pipi za vijiti siku hizi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 02, 2007

    Ebwana dogo mistari imeenda shule naona hubahatishi uko bado matawi ya juu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 02, 2007

    Ubunifu hakuna hapa amebadilisha wimbo wa 50 cent wa candy shop kuanzia rythm na kutafsiri loly pop kuwa pipi ya kijiti huo si utamaduni wetu na sijui wimbo wenyewe kam uta survive hauna maadili kabisa

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 02, 2007

    Hivi wasanii kama hawa mbona hawawikii kwenye chati za bongo flava. Bw mdogo got mad skillz, sijui ni nani huwa anamuandikia mistari yake, kama anaandika mwenyewe basi he has a great future ahead of him. Kama ule mwimbo wake wa "Problems.." unaweza kabisa ku-compete on a global level...Keep you head up kid..!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 02, 2007

    mwanangu uko juu, matawi ya juu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 02, 2007

    we anony wa Tarehe July 2, 2007 4:23:00 PM EAT, acha ushamba wewe kila kitu kishaimbwa katika ulimwengu huu....

    track ni nzuri na dogo amejitahidi haya sikiliza hiyo problem halafu sema kamuiga nani?
    au unataka kusema baada ya prof j kuimba pigamakofi busta alimuiga kuja na make clap? au yeye langa alipoimba matawi ya juu aliigwa na mims kwa kuimba this why am hot? kila kitu kisha imbwa na sometimes ni idea zinaingiliana ...
    kuwa mzalendo mshikaji na lazipa utoe cr pale panapotakiwa kutoa holla at ya...

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 02, 2007

    kijana yuko kamili ila hapati airtime anayostahili. alafu idea ya pipi ya kijiti tatizo liko wapi kama 50 kafanya?..huwezi kusema hamna ubunifu..alifikiri kuitoa kwa staili nyingine..and whoever said kuwa kila mwimbo lazima uwe na maadili ni nani?..lazima kuvunjika kwa maadili kuimbwe ili yeye kama msanii aguse ngwe zote za maisha au vipi mazee?? poa msela, jaribu kuimba conscious nadhani hiyo itakupendeza zaidi..jaribu style ya akina Common kuvaa suti, itawafunga midomo wasiopenda Army comourflage..haha..alafu subiri madongo mengine uyatoe KO...kila lakheri kijana!
    -akupendaye-

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 03, 2007

    ukweli uko palepale KAIGA! tena bora hata angebadilisha kidogo na maneno kayatumia yale yale acheni uvivu tungeni vya kwenu vi hela vya haraka haraka havita wafikisha popote bila kutumia akili. sina chuki naye dogo nikatika harakati za kumkomaza kimuziki msifikiri watu wanakurupuka tu na kwenda studio wanfikiri ndio maana wako mbali. muulize yoyo anayeujua mziki atawaambia

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 03, 2007

    Nyie ma anony wabishi hamjeaelewa mwenzenu anasema nini kabla hamjaanza kubisha hajaiga hebu kausikilizeni wimbo wa 50 cent wa candy shop ndio muanze kubisha. nimesikiliza nione kinacho jadiliwa ni kweli nikasikitika kaiga kuanzia rythm, sounds , maneno ila kongezea ya kwake kidogo na majibishano kama 50 alivyo fanya hiyo piga makofi na mifano mingine inaonyesha jinsi gani vijana wa kizazi kipya msivyo makini na kusoma na wala ukomavu katika muziki. Someni muziki msifikiri ukikimbia darasani unaweza kuwa mwanamuziki bila kuusomea

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 03, 2007

    Kabla ya kuendelea kubishana soma article hii

    When I wrote this column, I consulted with then UC Berkeley music Professor Ricky ‘Uhuru Maggot’ Vincent who wrote the excellent book ‘History of Funk’. He pointed out the blatant contradictions of some of these rap critics who would lambaste Hip Hop but give a pass to jazz, blues and even classic artists who always borrowed riffs and melodies from past works and added their own take. He noted that many jazz musicians called it riffing (borrowing) and vamping (twisting) and that everyone from Duke Ellington on down to Count Bassie to James Brown and Average White Band all engaged in the practice.

    Read the whole column here
    http://odeo.com/audio/633407/view

    ReplyDelete
  12. NDIO AMEIGA ME WANANIBOA KWELI BAADHI YAWASANII WA BONGO HAWAJITUMI.EBU KUWENI SERIOUS NA KAZI AU MTAISHIA KUENDESHA VIBALUNI TU WAKATI WENZENU WANAPAA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...