
njenje plaza a.k.a ambassador plaza a.k.a gogo hotel ndiyo hiyo inapigwa nyundo kupisha kikwangua anga cha kampuni moja ya simu (jina kapuni hadi kieleweka). lakini wapenzi wa kilimanjaro band wana njenje waliokuwa wakiduarika hapo kila jumamosi wasikonde kwani tayari waziri na wenzie wameshahamia bwalo la polisi ostabei ambako watakuwa wakitumbuiza kila siku ya ijumaa kuanzia ijumaa hii ya tarehe 27 julai. nyote mnakaribishwa huko ijumaa hii na nyingine zote kuanzia ijumaa hii. nani kasema mduara wa njenje utakufa baada ya hili?
Watakao kuja kuchezea mduara hapo ni waboreshaji maisha
ReplyDeleteBwana Michu bwalo la polisi mbali kishenzi huko wataenda hao wenye nazo. Japokuwa wapo wapenzi wa njenje wengi kwenda huko itakuwa tabu kwanini wasihamia Laprima maeneo ya Victoria? Pale pamekaa safi.
ReplyDeleteKweli wewe ni kiboko! Kikwangua anga!. Hili ni neno brand new. Du! Kaka, tafsiri zako ni mwanana kweli kweli
ReplyDeleteKwa kifupi ni kwamba CELTEL wamechukua eneo lote hilo wanajenga ofisi zao mpya ambazo zitakuwa hapo i think wameamua kuachana na TTCL kila mtu awe kivyake.
ReplyDeleteMichuzi, kweli una camera nzuri. Nakumbuka ulivyopiga hiyo snap ya ubomaji wa UWT hostel kipapparazzi hasa, huko unendesha gari.
ReplyDelete