nzaeli kyomo (mbele) na mosi ali wakichuana katika mbio za mita 100 uwanja wa sheikh amri abeid arusha mwaka 1978. madada hawa ni baadhi ya nyota wakubwa wachache wa riadha bongo imepata kuwa nao na walikuwa mahasimu wakubwa kwenye nyanja hiyo. hivi sasa nzaeli ana shule ya msingi hapa dar wakati mosi ali anaishi na familia yake nchini norway na ni mwalimu wa riadha anayeheshimika sana huko. alikuwa bongo kwa mapumziko na anaondoka kesho akiwa na ndoto ya kurejea na kufungua shule ya michezo. mosi na nzaeli watakumbukwa kwa kuwakilisha nchi kwenye olimpiki na pia kuwa na kuweka rekodi katika mbio fupi kwa kinadada ambapo nzaeli aliweka ya sekunde 11:2 katika mita 100 na mosi aliweka ya sekunde 11:4 ambapo hadi leo hakuna aliyezivunja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 10, 2007

    Kaka Michuzi naomba picha ya Nzael Kyomo alivyo sasa. Alikuwa akiishi Houston, Texas. Nina miaka mingi sijamuona nasikia amerudi bongo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2007

    Ni vizuri sana kuwakumbuka watu kama hawa, waliolipa Taifa letu letu heshima siku za nyuma, sidhani kama wengi wanawakumbuka akina mama hawa, wengi wanamkumbuka BAI labda kwa vile yuko na shule yake pale Dsm,na akina Anna Ndege wanaochipukia kwa sasa, ni naomba hostoria zao zaidi na ikiwekezekana picha zao zaidi pia!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...