balozi wetu geneva mh. marten lumbanga (tai, shati jeupe)akipozi na wachezaji na viongozi wa taifa staaz timu hiyo ilipomtembelea jana huko uswisi. kulia kwa mh. balozi ni kiongozi wa msafara na makamu mwenyekiti wa tff jamal bayser. jana staaz ilishinda 1-0 dhidi ya timu ya kuwait na habari zinasema wachezaji kadhaa huenda wakaitwa kwa majaribio na timu za huko baada ya mechi na msumbiji septemba 8

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. ingekuwa vyema kama taifa stars wangepata timu pinzani bora zaidi ya hizo walizocheza nazo

    ReplyDelete
  2. exposure...blaza issa wafikishie ujumbe vijana chansi za kujifagilia ndo hizi...waoneshe kalufundi...alafu kumbe mshua ni namba wani apo ee?

    ReplyDelete
  3. Huko kina baba (Taifa Stars) fanyeni marembo na nakshi (show off) ili kujiuza. Mkirudi nyumbani ngumi jiwe chinga asitoke jamani msituangushe. Mind, body and soul muwe uwanjani sie pia tunajua mko under pressure, but we still want u guys to deliver.

    ReplyDelete
  4. Bwana Michuzi Lumbanga ni balozi wetu huko USWISI na sio Balozi wetu huko geneva.
    Geneva ni sehemu moja tu ndani ya nchi ya Uswisi.
    Nawasilisha

    ReplyDelete
  5. NAMWONA DADA HAMISA MKOMA HAPO KULIA MWENYE CRAZY COLOUR HAYA WASALIMIE HUKO,

    ReplyDelete
  6. Wajameni mimi naomba kusema hivi: Taifa stars imekuwa ikialikwa kwenye sehemu mbalimbali kusalimia waheshimiwa ikiwa ni pamoja na Bungeni, na Balozi mbalimbali. Hivi haiwezekani walu kuvaa suti au kuwa smart kidogo badalaya kuvaa hayo matrack suti. Wakati mwingine unatoka mchicha bwana. Anyway mimi nasema tu inawezekana wanamichezo ndivyo walivyo.

    Mzee wa TBS

    ReplyDelete
  7. WE ANNON WA 9.32PM UMECHEMSHA. LUMBANGA NI BALOZI NA MWAKILISHI WA TANZANIA KWENYE MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA YALIYOPO GENEVA. BALOZI WA TANZANIA USWISI NI AHMED NGEMERA AMBAYE ANA MAKAZI YAKE BERLIN, UJERUMANI AKIWA PIA NI BALOZI WETU HUKO. HATUNA RESIDENT AMBASSADOR USWISI.

    ReplyDelete
  8. i support 'mzee wa TBS' 100 percent...enough with jezis now ...suti ya nguvu average dola 100...let us try...it is possible...

    ReplyDelete
  9. Mzee wa TBS umenikuna, nimekumbuka hata kina Beckham wakiwa nje ya uwanja huvaa suti bwana, ee jamani doli 100, jiachieni bwana...anyway labda ndo kutokasimple huko. Lakini ndo na uniform, heeeteheteheteheeeeeeeeeee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...