majaji wa miss tz 2007

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. Aahaa! Kumbe hawa ndiyo waliomchagua MISS INDIA!

    ReplyDelete
  2. Kwa vile Miss Tz imekuwa burudani la nguvu na lenye shughuli pevu na hisia kali baada ya kila yasomwapo matokeo basi iwekewe muundo wa kitaasisi wenye ufanisi zaidi chini ya wizara husika ya utamaduni na taratibu zinazoongoza kama ilivyo TFF na Viongozi wake wa Kitaifa na Kikanda wawe wanachaguliwa kwa kura kila baada ya miaka 3. Dar itoe mwakilishi mmoja tu sawa na mikoa mingine yoye. Teknolojia ya kisasa ya Watanzania kupiga simu itumike badala ya hii ya majaji!
    Eti mpaka Ma-miss waliopita ama walilia au walilalama!Hivi kuna nini ambacho hatuambiwi waziwazi?

    Nyakarungu wa Coast

    ReplyDelete
  3. Anon September 4, 2007 9:55:00 unfortunatelly ni ngumu sana Dar kutoa mwakilishi mmoja tatizo sio ushindani wa ki mikoa ila tunataka mrembo mzuri ambaye hatafaa kuwakilisha nchi ndio muhimu masikini unaongea kwa machungu sana pole kama mimi nilivyonamachungu walivyomnyima miss Tanga

    ReplyDelete
  4. Maayo neneee!

    ReplyDelete
  5. Simuoni aliyekuwa MC Taji Liundi, maana mi nilidhani na yeye alikuwa jaji, nashangaa hata kabla matokeo hayajatangazwa tayari alishaongea kama mara tatu hivi kwamba "mwaka huu tunaahidi kuwaletea tofauti" alivyosema hivyo mi nilijua tu tofauti yenyewe ni huyo miss india badala ya miss Tz. Sawa lakini maana watanzania na sisi tumezidi kulala usingizi.

    ReplyDelete
  6. Kama kweli miss Tz anaiwakilisha TZ basi waachwe watanzania wenyewe wamchague miss Tz kwa kura na si hilo kundi la watu wachache hapo wanaojiita majaji, kutuchagulia watu wasiotakiwa. Ili kijua ni watu wangapi wanamsapoti huyu miss wa mwaka huu, ebu kafanyike kazoezi kadogo tu kakupata kura za watu, tena mpaka kule vujijini maana hata wao ni watanzania, halafu uone kamati ya lundenga itakavyoaibika. maskini wa TZ, Mwee.

    ReplyDelete
  7. hongera majaji kwa kumchagua miss atakaye wakilisha tanzania nasio atakayekwenda kutembea.

    Watanzania wamefanya hili ni topic kwa ushamba wao mbona watu wanabadilisha urai wao ili kuwakilisha nchi za wengine sasa huyo dada anakosa gani kuwa mtanzania au nyie shida yenu ni huo weupe wake????????????? kuna wakenya kibao ambao wamenunuliwa kukimbia nchi za watu huko na ni wangapi kati yetu hapa ni watanzania halisi wengine warundi wengine waluo wengine machinga wengine wanavizazi vya kisouth africa kwa hilo basi hakuana aliye mtanzania asilimia mia moja au tatizo ni kuwa mweupe????????
    Tunapokwenda mamisi hadi wachina watachaguliwa maana asasa hivi wanauza karanga sasa nyie mnashanga nini na nchi imeshauzwa hiyiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. haina mwenyewe mzungu sawa mchina sawa wahindi sawa wote nchi yao.kwani mmesahau kwamba watu wao sawa na hutakiwa kubagua mtu kwa rangi wala kabila hi ni siasa ya nchi waungwana.
    La muhimu ni kwamba tuone ni vipi atawakilisha nchi huko china lakin mengine ni bure tu.
    na huyo hasanali kuwashonea watoto nguo zinazowatelemka aache kabisaaa kwani huna tape measure??? watoto wakazi ya kupandisha magauni yanawapwaya haipendezi tunajua unajua kushona ila sasa ongeza ujuzi wako sio kubuluza hao wanawakilisha nchi.

    RICHA siku hazigandi kaza butiiiiiiii

    ReplyDelete
  8. Upuuzi mtupuu sasa ndo mmefanya nini huyo miss tz au miss india? anyway kwakuwa vodacom ni yenu ndo mnafanya mnachokitaka! Mmetuker sana watanzania na Muhindi wenu!

    ReplyDelete
  9. Hawa huwezi kuwaita MAJAJI, hawa sasa hivi wanaona hata aibu kujulikana kuwa ndio waliomchangua MISS INDIA. Kama uhuni huu utaendelea, kuna siku tutajua nini cha kufanya. Kwa hiyo wanasikia raha kwamba mwaka huu kwenye miss World kuna Miss India wawili? kudadeki.

    ReplyDelete
  10. Jamani WABAYA wetu hao MMEWAONAA? Waliotuletea Miss Tanzania Punjab hao. @~*%"><+_*@~!!! Kushnehi !!!

    ReplyDelete
  11. Tuwekee picha za harusi ya Hoyce Temu jamani na harusi ya Da Mija.

    ReplyDelete
  12. JAMANI TUNACHEMSHA, NAUNGANA NA ANON WA HAPO JUU, WAACHE WATANZANIA TUMACHGUE TUNAYEMTAKA. NCHI ZA WENZETU TUNAONAGA MASHINDANO KAMA HAYO, YANAENDA KWA KURA, KAMA VILE ZA KUMCHAGUA RAIS, WANANCHI WANAPIGA SIMU AU KUTUMA TEXT MESSAGE WANAPIGA KURA, WANATOLEWA MMOJA MMOJA MPAKA MWISHONI ANABAKIA MSHINDI.HEMU TUJIFUNZE, TUACHE KUENDEKEZA MAJAJI, MATOKEO YAKE WANATUCHAGUALIA HIZI KACHORI ZA KIHINDI.....

    ReplyDelete
  13. 1. Kamati iliweka viingilio vikubwa sana, na Vodacom wakaalika wafanyakazi wote wa Voda ambao ni maelfu, complementary za buuuureee!. Hivyo show ilikuwa too crowded, umati ulikuwa mkubwa sana. Na waliolipa pesa zao za jasho walionekana kama takataka. We mtu mmoja unatoa elfu75 kiingilio, halafu unagombea pa kukaa? Kweli?

    2. Huyu miss India alisha tuwakilisha Tanzania kwenye Miss Utalii sijui Universe na akafanya vibaya huko ugaibuni mwaka 2005 au 2006, sina uhakika na sasa na mwaka huu tena wanampeleka miss World, hivi akafanye nini huko? Ana uzuri gani?

    3. Mdhamini wa zawadi ya gari ni Ponjoro tena anamiliki kampuni ya kusambaza kadi za simu za Voada, jibu unalipata. Sisi walalahoi wenye nywele kama katani tulie tu.

    4. Miss India wa Tanzania hatufai hata kwa nini. Hata kipofu atagundua kuwa kuna dosari, tena kubwa.

    5. Hakuna mtu hata mmoja amefurahia ushindi. Labda awe ni mfanyakazi kwa wahindi au awe amesomeshwa shule za wahindi, Almuntazir, Mzizima, Shaban Robert, basi ataona is OK!!

    Sio swala la ubaguzi, wala swala la uraia, lakini ni bora mara mia elfu mzazi wake mmoja angekuwa ana asili ya kiafrika, tusingepika kelele hata siku moja. Kama vile Angela Damas, nani alichonga?

    ReplyDelete
  14. Michuzi kwa uchokozi tu sikuwezi! Yaani umemua kuwaanika majaji ili watu watoe maoni yao? Du! Hii imekaaje tena kaka?
    Halafu mie binafsi sikudhani kuwa Watanzania ni wabaguzi kiasi hiki! Huyu Richa nae ni Mtanzania kama walivyo Wadigo, Wasafwa, Wakwere, Wamatumbi na Wazaramo. Jamani acheni hizo! Mbona nyie mnalalama sana mkibaguliwa nchi za watu?

    ReplyDelete
  15. jamani, huyu mhindi ataweza pia kuonyesha utamaduni kwa kitanzania? Lundenga na team yako je mmemuandaaje bibie huyu kuonyesha image ya mtanzania huko kwenye mashindano maana kama ninavyojua mashindano hayo pia yanasaidia kupromote Tanzania na utamaduni wake.......

    ReplyDelete
  16. jamani, huyu mhindi ataweza pia kuonyesha utamaduni kwa kitanzania? Lundenga na team yako je mmemuandaaje bibie huyu kuonyesha image ya mtanzania huko kwenye mashindano maana kama ninavyojua mashindano hayo pia yanasaidia kupromote Tanzania na utamaduni wake.......

    ReplyDelete
  17. Inasikitisha kama sio kinyaa!

    Hivi watanzania kwanini tunasinzia kiasi hiki?? HII ilishapangwa mwanawane, Hata Taji Liundi alisema leo lazima tutoe mshindi tofauti. Kwa hiyo naomba ili swali wanijibu majaji wa Tanzania. Ni hongo, kujipendekeza au nini? Lundenga wewe bora ujiuzulu hufai hata kwanye ubunge wewe utatoa pesa za rushwa ili ushinde. mmenyima mtoto wa watu Miss Tanga ushindi kwa tamaa zenu za hongo. HAYA MKIFIKA CHINA MSEME KUWA HUYO NI MUHINDI (SUNCHE) WATANZANIA HALISI HAWAKUSHIRIKI. MLIJUA KUWA NI AIBU MKAANZA KUMFUNDISHA ASALIMU KWA KISUKUMA. NA KWANINI HAMKUMUULIZA SWALI KWA KISWAHILI ILI TUONE LUGHA ATAKAYO ONGEA, HILO MLILIJUA ANGEBORONGA NI MTANZANIA GANI AMBAYE AJUI KUONGEA KIWAHILI? BORA MASHINDANO HAYA YAANGALIWE UPYA MNAWASUMBUA WATOTO WA WATU BURE KUMBE MSHINDI MMESHA MTAYARISHA WENYWEWE. JANI MUHINDI, VIONGOZI WAHINDI, HATA UFUNGUO WA GARI ALISEMESHWA KWA KIHINDI. HAYA MPELEKENI HUYO SUNCHE WENU NDIVYO MLIVYOTAKA.

    ReplyDelete
  18. annoy wa 11:41 kumbe na wewe ulimsikia jamaa alivokuwa akikazana kusema mwaka huu wanatuletea mambo mapya kabisa!! na mimi pia niliishitkia hiyo kauli.halafu watu walipochukia na kuanza kuondoka akabaki kukazana kuwataka watu wabakie vitini!! wabakie vitini kwa Upumbavu kama huo?? Yaani wabantu wote hao wamezidiwa akili na hao Maponjoro wawili tu?? kweli Bongo sasa haina mwenyewe....!!

    ReplyDelete
  19. tumewaona! ndio mana tyson akamng'ata sikio holyfield...pia kuna world cup ya if i am not mistaken ya '90 ROGER MILLER akagusa arm yake akiashiria rangi yake...wengi tulimsapoti...what i want to say here is that sometimes there is nothing like FAIRPLAY...blaza michu i guess you are a football fan au hata kama siyo but nature ya kazi yako unafuatilia...hivi umafia wa kwenye world cup pamoja na kuwa WABANTU wamejaa WANACHEZA PROFESSIONALLY huko maulaya sioni siku timu ya nchi ya afrika itatwaa kombe la dunia...kwenye hili kombe la dunia fairplay haipo kwa vinchi vyetu hivi huwa vinazibitiwa mapeeema havifurukuti!!!...mambo ya huu umisi hata kwenye ngazi za miss tabata au misi mwananyamala fitna iko basi tu hatufuatilii...majaji tumewaona WAS THERE FAIRPLAY?...kingine...kwani lazma utumike ung'eng'e kwenye "kujieleza"?...mbona mamisi wengine huko duniani who prefer not to speak (au hawajui) english huwa wanatumia wakalimani? na inakubalika?...why should huku kwetu english iwe lazma???...anaetaka kujieleza kwa language atakayo si aachiwe tuu? matokeo yake wanakuja ng'ara a privilaged few ambao hawakukalia matofali mpaka sketi zikajaa viraka kwa makalio warembo weeeengi english hawako comfortable kuzungumza kutokana na standard yetu ya elimu tokea msingi...i conclude an injustice has just occured...

    ReplyDelete
  20. Kwa aliye kuwa ana fuatilia masuala ya urembo wa mwaka huu atakuwa anajua tuu kuwa walio kuwa na nafasi kubwa ya kushinda ni Lilian Abel,Richa Adhia na VIctoria Martin,hilo halina ubishi, hata wandaaji wa wilaya za Dar wak#likuwa wana mhofia Miss Tanga ambaye ni Victoria martin.

    tatizo linalotusumbua ni kwamba sisi waBongo badoni wa baguzi na hiyo ni kwa yeyote aliye hisikubaguliwa ,kawaida hufanya ubaguzi kiwazi wasi bila kuficha.

    Richa Adhia ni ana haki zote za kushiriki na kushinda,kwanza ni Mrembo,Raia na piani mwenye uiwezo mzuri wa kujieleza, hivyo ni vigezo tsha vya kumpa ushindi.

    Tukija kwa Mrembo MIss Tanga ,kwlei ni mrembo sana, na ila aliwasikitisha wartu pale alipokuwa akijibu swahihuku akisita sita,hapo ndio palipo muangushakwakiasi kikubwa.

    Kuhusu kupangwa matokeo hilo sina uhakika nalo ila kuna habari nime zipata muda mfupi ulio pita ambapo zinasema kuwa swali alilo ulizwa miss Tanga ambaye ni Victoria Martin pamoja na Queen David ambaye ni Miss Temeke , haya kuwepokwenye orodha ya maswali walio pewa kutakiwa kujibu siku ya oneysho, kawaida huwa wana pewa maswali kujiandaa kwanza , na hiyo ili mfanya Miss Tanga na Miss Temeke kubaki na mshangao na kuanza tustruggle kujibu swali kwani hawakutegemea kama watauliswa maswali wasio yajua.

    Kama hii habari ni kweli nampongeza warembo hawa kwa kuwa calm na kutolketa vurigu siku ya onyesho, hiyo imeonyesha utaarabu mkubwa walio nao.

    Mc ambaye ni Taji Liundi , aliposemakuhuzu kuleta tofauti ni kwamba,kila mtu hata mimi niliye kuwa hapo,nilikwua na uhakika Miss Adhia ni ana shinda kwani tumemfuatilia muda mrefu na kujua uwezo wake kuliganisha na wenzake, hata hivyo Liundi alikuwakimaanisha utofauti wa uandaaji waonmyesho sio utofauti wa Mshindi.

    Ms Adhia nakupngeza sana ,kwani nilijua tuu utashinda na pia nime shinda sh 1,000,000 usiku huo baada ya ku bet mimi na wenzangu ambao wote walisema ni Lilian mimi nikasema Richa na ukashinda , nakupongeza na najipongeza.

    ReplyDelete
  21. Naomba Majina ya Majaji na Shughuli wanazofanya. Inahuzunisha sana sana jamani acheni tu.

    ReplyDelete
  22. Jamani nyie mnafikiri lile gari la 45m + 8m walizotoa wahindi zingeenda kwa mswahili? mweeeeeee!!! Kitu kingine huyo sijui JAJI mkuu alishasema tangia mwanzo kuwa hajawahi kuwa JAJI sasa mlitegemea nini? MAJAJI wengine akina Klynn unategemea nini mtu kama yule eti ni JAJI. Naungana na anon mmoja aliyependekeza haya mashindano yawe RASMI hakuna cha LUNGENGA mhuni wala Prakash wajinga watupu. Ni aibu kuambiwa eti miss tanzania wakati mchakato wenyewe ni informal bali serikali inaambiwa eti huyo ndo miss wenu.

    Hapa sio cha ubaguzi wala nini, watu wana machungu. Mbona wahindi kama sio wabaguzi wanasoma shule zao hawachanganyiki na waswahili? mbona wafanyakazi waswahili wananyanyaswa huko ofisini na viwandani vya wahindi, kuna mifano mingi tu. Yaani ubaguzi unaonekana leo wakati HOYCE TEMU alipolalamika. Jamani tuwe fair mambo mengine ni aibu tupu. Kwanza ukimwuliza huyo ponjoro aimbe wimbo wa taifa nadhani hawezi, mwulize historia ya Tanzania hajui, sana sana atakwambia mlima kilimanjaro, na vitu ambavyo ni obvious. SHAME ON YOU ALL--

    ReplyDelete
  23. kazi kweli kweli i dont wish to be any of these judges right now!jamani WATANZANIA wenzangu punguzeni hasira try and focus on important things like how tutaikuza nchi yetu kuliko kustress na mambo ya mamiss.its only a competition. come down guys relax!!!!mtoto wa watu will have a tough year sababu kila kona atakuwa anasemwa.she will definately hate her self for being miss TZ!halafu next time wawe na two to three judges manake wengine hapo wanajaza nafasi tu.Ten judges for What!OH BLIMEY!

    ReplyDelete
  24. Kwa hakika inasikitisha sana...na hasa unapokuta watu unaowafahamu kwamba wamehusika na ubaradhuli huu wenye kutia kinyaa...km Mr Mc nilimjua na kumheshimu sana ...ila imenishangaza licha sikuwemo ukumbini kusikia ati alianza kuweweseka na kutamka kumjua mshindi...mwe!! lakini pia hao majaji tunaomba picha zao...close ups... majina na kazi zao...ndiyo... tuwajue na daima tuwalaani...

    ReplyDelete
  25. Mi jamani bora niendelee kubakia ulaya nibebe maboksi wee, nikizeeka, wakaniweke nyumba za wazee wa kizungu basi, bora nife na aibu yangu hukuhuku, kuliko kuja kuishi tena kwetu..maana kitakachofuata, tutaletewa rais Kachori,Ponjoro,...nchi yetu yenyewe, hatuheshimiani.., hili swala bwana, watu tulikazanie,,Richa abakie kuwa Miss 2007, lakini wananchi walalamike na kutoa maoni, ili kosa hili lisirudiwe..2008 hatutaki ngozi ya mwana wa Patel kwenye mashindano..mmnajifanya Ari mpya, nguvu mpya kumbe ndo mana yake hii eeh? sawa bwana, na RANGI MPYA...ngozi chapa ya Patel.Wacha niende kazini nikamtumikie mzungu mie, kuliko kurudi kwetu ambako babangu(Tanzania) amenitelekeza...

    ReplyDelete
  26. Anon wa hapo juu, umesema UKWELI TUPU,nchi imeshauzwa, Tumetelekezwa mshikaji wangu, wacha tukae huku ulaya, tuendelee kumtumikia kafiri......labda na sie siku moja tutaibuka Miss Europe (thubutuuuuuuuuuuu)

    ReplyDelete
  27. MICHUZI

    NIMEFURAHIA SANA KUWA NCHI YETU IMEONYESHA KUWA HATUNA UBAGUZI WA RANGI

    IMAGINE WATANZANIA WEUSI MKAA WANADAI ASINGEPEWA MHINDI SABABU ANA ASILI YA KIINDI

    SHAME ON ALL OF YOU MNASEMA WAZUNGU WABAGUZI HATA WAO WAMEWASHINDA

    HII NI AIBU SANA NA NI PICHA MBAYA TUNAIPA TANZANIA, HONGERA KWA MAJAJI MMEFANYA KAZI NZURI YA HAKI.

    HAYA YOTE MNAYOSEMA INGEKUWA MTANZANIA MWEUSI MKAA MNGESEMA NINI???????? WABAGUZI

    NCHI NYINGI ZA AFRICA ZIMEWEKA WEUPE KATIKA MASHINDANO NA HAKUNA MALALAMIKO

    POLENI NA MUENDELEE KULIA KAMA NDUGU ZENU HAWAKUSHINDA MAANA MIE NA WENGINE KAMA MIE TUNAWASIKITIKIA

    KWA UPANDE WANGU MISS TANZANIA 2006 HAKUWA MZURI WA KUWAPA WOW MAJAJI WA MISS WORLD MBONA HAMKUONGEA. MIMI HADI LEO NAJIULIZAGA Y ALICHAGULIWA KILA NIMUONAPO

    ACHENI UBAGUZI

    HONGERA MISS TANZANIA 2007.MTOTO WAKISUKUMA. USIWE NA SI WEWE NI MTANZANIA HASIRI. URAIA WAKO HAPO NA HAPO UTAZIDI KUSHINDA

    TUNASUBIRI KUKUONA NDANI YA CHINA. GARI VIPI I HOPE UNASIKIA RAHA NA RAV4 YAKO. HONGERA.

    NI MIMI MTANZANIA MWEUSI

    ReplyDelete
  28. UBAGUZI HAUNA NAFASI.
    YEYOTE MWENYE MAWAZO YA KIBAGUZI HANA NAFASI KATIKA JAMII.
    DHAMBI YA UBAGUZI ITAKUTAFUNA , IPO SIKU KAMA SIO WEWE KUBAGUA WATOTO WAKO BASI UTABAGUA WAJUKUU ZAKO, HILI HUTOLIKWEPA.

    TUKITAKA KUANZA KUBAGUANA BASI KILA MTU ALIYEKO DAR ARUDI KWAO. NA NINI DAR NI KWAO KAMA WENGI SIO WAHAMIAJI?

    HIVI INAWEZEKANA KWELI MZARAMO WA CHAMAZI AKAENDA KUGOMBEA UBUNGE MOSHI NA AKACHAGULIWA?
    AU AENDE KUGOMBEA UDIWANI KYELA AKACHAGULIWA?
    AU AENDE AKAGOMBEE UENYEKITI WA CCM KAMACHUMU AKACHAGULI?
    AU AENDE AKAGOMBE UENYEKITI WA CHADEMA TARIME AKACHAGULIWA, ITAKUWA NGUMU, NI SAWASAWA NA WAPEMBA KUMCHAGUA MWAKILISHI ASIYE MWANA - CUF.
    MWENYE MAWAZO YA KIBAGUZI NI MJINGA ANAHITAJI KUELIMISHWA ZAIDI.

    ReplyDelete
  29. Wakati India itakuwa na wawakilishi wawili katika Miss Universe/World, Tanzania itakuwa haina mwakilishi! Pole yetu Wadanganyika!

    ReplyDelete
  30. HUYO DEMU NI MZURI NA ALIJIELEZA VIZURI NA PIA NI MBONGO,TATIZO LIKO WAPI,HIYO NCHI NI MCHANGANYIKO WA MATAIFA MBALIMBALI,HUYO MSICHANA ANA HAKI ZOTE ZA KUSHIRIKI NA ANAJIVUNIA KUWA MTZ,MIMI NI MPOGOLO NAMUUNGA MKONO HUYO MSICHANA WATANZANIA ACHENI UBAGUZI NYERERE HAKUWALEA HIVYO.

    ReplyDelete
  31. Anony 4:20 awakilishe utamaduni wa TZ. Wewe umeshaona amepewa sare ya kipakistani basi jibu unalo...I am telling you the truth wala sio cha rangi au kwa vile ni muhindi lakini huyu hana ile unique fiture s za mamiss hawa....Akifika top 20 nitajiona mjinga sana... mark my words

    Much know - USA

    ReplyDelete
  32. Hawa ndio majaji waliochagua takataka kutuwakilisha?Yaani mtu alienda kushiriki Miss Earth akashindwa vibaya, leo anapelekwa kushiriki mashindano makubwa zaidi, Miss World??!Aiiiiibuuuu.
    Kama hao wahindi waliotoa gari walitaka kumpa mhindi mwenzao basi wasingelitoa tu, miss angepewa ka corolla basi,ilimradi tupate mwakilishi bora.
    Yaani mwanariadha kawa wamwisho jumuia ya madola ndio anapelekwa kuwakilisha ktk olympic?wakati hata vigezo hajafikisha?duh!hawa wahindi this time they have gone too far

    ReplyDelete
  33. Hongera Richa Adhia! Na sisi waTanzania tuache ubaguzi. Next tutakuwa na ukabila oh mHaya kashinda, oh Mbulu kashinda au Mchagga kashinda.

    Na huko mbele watu watamshangaa huyo Richa kama walivyomshangaa Flaviana na kipara chake. Watasema, kumbe Tanzania kuna wahindi na makibila wengine, kumbe mnaweza kumchagua kuwawakilisha. hamna ubaguzi kwenu. Ama kweli Tanzania tutageuza macho ya dunia kwetu. Tuwe na Umoja tumsupport Miss Tanzania.

    ReplyDelete
  34. Nimeshtuka wazee.....hizi comments zinazomsapot huyu mtoto wa kidosi zinaandikwa na wadosi wenyewe....hivi mnafikiri mtaweza kushindana nao wale kwa kukaa kwenye kompyuta siku nzima!!....anyway one day yes lakini.....

    ReplyDelete
  35. Hahaa wewe anonymous wa september 6, 2007 9:34:00 unachekesha, si wewe unaosema wahindi hajui kiswahili?

    Sasa kama ni wahindi wanaoandika wenyewe, kilichoandikwa hapo juu ni kihindi?

    Hamna jipya.
    Kwa taarifa yako mimi ni mweusi basi ila nimesoma na sio mjinga kama wewe.

    ReplyDelete
  36. wote wanaojikomba kwa richa ni magabachori wenzake, kazi yao ni kukaa kwenye internet siku nzima hawafanyi kazi yoyote zaidi ya kuchukua mkopo benki halafu wananunua hisa benki kuu wanaishi kwa interest. Poleni APES wa kibongo mna kazi. Hawafanyi kazi hao magabachori kazi yao ndio hiyo, kwa hiyo mjue walipa taz ni nyie na kutukanwa ni nyie nyie, mtakesha mkifanya kazi usiku na mchana mkichacharika kuiendeleza tanzania yenu, wakati wenzenu wanakula interest yenu benki kuu.

    ReplyDelete
  37. Chemmi, hakuna ubaguzi hapo Sis. ni fact tu. Aliyepanga kuwa kuwe na Bara la Afrika, Bara la Ulaya na Bara la Asia hakuwa mjinga. Kila ngozi ilipewa mahala pake pa kuishi. hii ingiliana ingiliana ya wa huku kwenda kule na wa kule kuzaliwa huku haiondoi ukweli huu. Watanzania tusijitie sisi tuna huruma sana. kwani watu wakitusifia kuwa hatuna ubaguzi ndio tunakuwa tumeshiba? Si wanatusifia hatuna ubaguzi halafu huku nyuma wanatung'onga? Hawa hawa tunaowatetea kuwa tusiwabague huwezi kwenda kwenye bara lao ukamiliki Duka Mtaani sembuse kuwa Miss ama Mbunge!
    Hivi Pamoja na Uingereza kuwa na raia kutoka kila pembe ya dunia, unategemea kuwa kuna siku utasikia Malikia wa Uingereza ni Mwarabu ama Mhindi???
    Kwa usugu huu wa kukosa uzalendo tuliojivika wenyewe, kuna uwezekano mkubwa sana kuwa miaka michache sana ijayo raisi wa Tanzania atakuwa Mheshimiwa sana Pratansi Parbhindal Bachchan!! Tuamkeni watanzania!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...