
mwenyekiti wa yanga imani madega (chini,kati) akiwa na makumbi juma 'homa ya jiji' (chini shoto) na sekilojo chambua (chini kulia) na romario, mohamed hussein, abubakar kombo na salum sure boy katika hafla ambayo imeandaliwa na wachezaji nyota wa zamani kuwapa moyo wadogo zao wafanye vyema ilofanyika hoteli ya sea cliff usiku huu

mshambuliaji hatari wa yanga wa zamani mohamed hussein mmachinga akiwa na wachezaji wa staaz

mkurudenzi msaidizi wa simba hagila akiwa na baadhi ya wachezaji wa staaz
Lovely! Nefagilia sana kitendo kilichonyeshwa na wakongwe. Hii inaonyesha wazi kwamba soka ya Tanzania sasa imesheni baraka zote za wakongwe wa soka nchini. Sio kama wakati uleee soka ilivyokuwa inaendeshwa na Wanajeshi. Kulikuwa hakuna baraka kama hizi tuzionazo sasa kwani wakongwe walikuwa hawathaminiwi. Nikiwa kama Mtanzania mwenye machungu na soka letu napenda kuwapongeza TFF na Wakongwe kwa kuandaa Tafrija hiyo. Pili ningependa kutoa hoja kwamba kama ikiwezekana hata mara moja au mbili kwa mwaka Wakongwe wawe wanaandaliwa kitu kama hiki ili kuwaenzi. Ukiangalia juju juju huwezi kuona mchango wa hawa jamaa katika maisha ya Mtanzania lakini ukweli ni kwamba ni hawa wakongwe ndio waliokuwa na uwezo wa kusimamisha mizozo ya kisiasa na hata kifamili japo kwa masaa mawili ili watu waangalie au wasikilize mpira!! Ukiangalia hilo basi utaona mchango wao katika jamii yetu hii. Hongera sana kwa hilo! Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Taifa Stars!
ReplyDeleteMohamed Hussein Daima Mmachinga! Moja ya namba tisa hodari katika historia ya soka. Naomba TFF waweke rekodi za huyu jamaa ina wezekana ni mmoja ya Wachezaji wenye magori mengi katika historia ya Soka Tanzania kama sio Mogella. Tusipo fanya hivyo jamaa ataishia hivi hivi kama wengine wakati ikumbukwe aliwahi kuongoza kwa ufungaji si chini ya misimu minne. Good stuff Chinga Boy you're the icon!!
ReplyDeleteKuhusu wachezaji naona they look healthy! lakini nauuliza kwa nini Maximo hamuiti Njohole. Ninani hakubaliani nami kuwa yule kijana anakipaji cha jabu. Inabidi aitwe kuongeza nguvu katika mechi ya Mozambique. Ikumbukwe watanazania hata hao wenzetu sio kwamba wachezaji wao wote wanacheza Div I hapana ni hao hao wakuokoteza katika vidaraja vidogo vya huko Ulaya lakini ni wakulipwa. Wanaupeo mkubwa kiasi kulinganisha na wnaocheza local league hapo nyumbani. Mfano tumeuona Stars wamekwenda nje wamefungwa na timu za mdaraja ya pili na tatu. Hii inaonyesha kuwa wachezaji wa madaraja ya pili na tatu wa nje wana uwezo kiasi wa kuzisaidia timu zao za Taifa. Kwa kumalizia naomba TFF na Kocha Maximo kulingalia upya swala la Njohole.Aksanteni!!
ReplyDeleteMdau hapo juu, Njohole haitajiki kwa sasa, bwana mdogo Nizar anafanya vitu si mchezo, kwa hiyo nadhani kwa namba yake saa hizi haitajiki hata kidogo
ReplyDeleteHii inatia moyo sana kuona watu wa generation ile bado wanaishi maana ni karibu nusu ya watu waliokuwa maarufu miaka ile Tizii hatuko nao, wameondoka na ngoma.Wadau mnasemaje?
ReplyDeleteAlexandria ,VA
Bruv Michuzi,unaonaje ukiwashauri waanzishe chama chao cha wachezaji wa zamani ili wadau tupate kuwachangia chochote kidogo kilichopo na serikali pia ikawakumbuka kwa kuwasaidia.Jamaa nawakubali waliiletea sifa nchi yetu.Enzi East Africa tulikuwa wababe na Africa yote walitugwaya.
ReplyDeleteNi wazo tu nawakilisha.
ANON WA 1O:22 USHAURI WAKO MZURI NA KWELI UMETILIWA KIPA UMBELE NA WADAU WENGINE. UPO MFUKO MAALUM UMEANZISHWA KATIKA KUWASAIDIA MASHUJAA WETU WA ZAMANI.
ReplyDeleteHIYO PIA ITASAIDIA KUWAFUNGUA MACHO WACHEZAJI WA SASA WANAOJIFANYA WAMESHAJUA MPIRA WAKATI NDIYO KWANZA WANAJIFUNZA. THUMS UP KWA SAAANA NYOTA WETU WA ZAMANI. NYIE MMELILETEA TAIFA HESHIMA ENZI ZENU NA MLITESA.
NAKUMBUKA ENZI HIZO KILA MTOTO ANAYECHEZA MPIRA ALIKUWA ANAJIPACHIKA MAJINA YA WACHEZAJI HAWA.
WENGINE WALIJIITA PONDAMALI, OMAR MAHADHI, ATHUMAN MAMBOSASA, WENGINE KOMPYUTA (KITWANA), MIE ENZI HIZO NILIJIITA GEORGE KULAGWA, WENGINE MARTIN KIKWA. ILI MRADI TU KUJIFANANISHA NA HAO JAMAA NA HAKUNA HATA MMOJA ALIYETAKA KUITWA MAJINA YA WACHEZAJI WA NJE KWANI YA KWETU YALIKUWA YANATISHA. IDUMU "ORIGINAL" TAIFA STARS.
HATA KLABU HUSIKA KAMA SIMBA NA YANGA ZILIZOKUWA ZINATAMBA NA WACHEZAJI HAWA, NAO WANGEANZISHA FUNGU MAALUM LA KUWASAIDIA HAWA JAMAA KWANI HAWANA PENSHENI WANAPOFIKIA UMRI HUO.
TFF NAYO INGEKUWA INAWEKA ANGALAU SH.50 AU SH. 100 KWA KILA TIKETI WANAYOUZA IENDE KWENYE MFUKO WA "OLD IS GOLD". BENDERA FANYA JUU CHINI HAO WALIKUWA VIJANA WAKO NA NDIYO WALIOKULETEA SIFA KUBWA ENZI HIZO. WASAIDIE KWA WAZO HILO LA ONGEZEKO LA SH. 100 KWA KILA TIKETI IENDE KWA HAO JAMAA.
MICHUZI HIYO SNAP YA JUU YA AKINA ABUBAKR KOMBO NA WENZAKE, HUYO JAMAA WA KWANZA KUSHOTO ALIYESIMAMA SIYO ABDALLAH ALIYEKUWA AKICHEZEA SIGARA NA BAADAYE SIMBA?
ReplyDeleteNAKUMBUKA SALEH "ROMARIO" WA YANGA HAKUWA HIVYO NA HADI SASA BADO ATAONEKANA YANKI TU KWANI BADO MTOTO MDOGO. YANGA WALIMCHUKUA TOKA SHULE AKIWA BADO KINDA. KAMA KWELI TUREKEBISHIE MANAKE JAMAA ALIKUWA NA MBIO KAMA SURE BOY.
MICHUZI NAONA UMEWAPIGA CHINI CRDB NA KUWACHUKUA EASY FINANCE. ANGALIA UNAWEZA KULAMBA KOTE (NA CRDB PIA) KWANI BADO UNA NAFASI KUBWA CHINI YA UKURASA WAKO.
ReplyDeleteCHA MSINGI NI KUWAWEKA CRDB UPANDE WA PILI WA UKURASA HUU ILI KILA MTU ANAPOANGALIA PICHA KWENDA CHINI, ATAONA TANGAZO LA CRDB. NIA NI KUKUPA MAWAZO TU KWANI ILE SURA YA YULE WA DADA WA CRDB, INANIACHA HOI. AHSANTE.
Kuhusu NJOHOLE!
ReplyDeleteNjohole hachezi tena mpira. Na ameshaondoka hapa Austria kuelea UK, siyo kucheza mpira, bali kuhangaika na maisha kwa njia nyingine. Hivyo sidhani kwamba anaweza kusaidia sana Taifa staz
Siyo nawakilisha ni nawasilisha, jamani Kiswahili kifundishwe vipi?
ReplyDeleteEEEEEE BWANA EE MICHUZI UMENIFURAHISHA SANAA SANAA NA KUNILETEA MAJINA KAMA SEKILOJO CHAMUBA,ABUBAKAR KOMBO,PETER TINO,MAKUMBI JUMA(HOMA YA JIJI),HAHAHAHAAAA NIMECHEKA NA KWELI HAPO NDIO NAJUA TUMETOKAA MBALI ENZI HIZO RADIO MOJA TENA RTD HALAFU HAISIKIKI VIZURI MHHH KILA MTU ANANG'ANG'ANIA AWEKE SIKIO KWENYE SPEAKER HALAFU MTANGAZAJI ANANG'ANG'ANA NA KILA JINA LA ALIYEKAMATA MPIRA ALITAJE BASI BALAA LAKE SI DOGO......
ReplyDelete