maegesho ya magari ya wanja jipya la neshno. cheki magari yalivyotengewa sehemu zao juu ya nyasi. si vibaya ukapitia tovuti ya tff hapa:http://tfftanzania.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. hayo maegesho yanaywezo wa kuchukua magari mangapi kwa wakati mmoja

    ReplyDelete
  2. Michuzi, shukurani kwa kutubonyezea hiyo link ya TFF. Ila naomba uwashauri TFF wazingatie ufasaha wa lugha katika tovuti yao mfano mdogo ni kiingereza kilichotumika kama caption ya PICTURE OF THE WEEK, hakika wanahitaji mtu makini wa ku-proof read kabla ya kupost articles zao online. Inasomeka hivi "taifa stars fan's in dar es salaam city, showing there support by signing there names ."

    ReplyDelete
  3. Ningetarajia iwe kinyume chake, yaani magari yawe kwenye concrete slabs na si juu ya majani! Au ndo utaratibu mpya? Nina wasiwasi kuna uchemkaji hapo! Wanamazingira nitoeni dukuduku!

    ReplyDelete
  4. Nakubaliana na Mawenge, kuna uchemkaji maana hali ya hizo nyasi itakuwaje baada ya muda kama magari yataegeshwa juu yake.

    ReplyDelete
  5. Michuzi usituchezee hivi ni kweli magari yako juu ya majani? so wonderful, ndio kina Mwakalebele hao? ni aibu, magari hayapaki kwenye majani. mmevaa chupi kichwani!

    ReplyDelete
  6. Baada ya kuiangalia picha kwa karibu najiwa na mawazo hizo si nyasi kama Michuzi alivyoandika bali ni rangi imepakwa kwenye maegesho. Hivyo, kama hiyo ni sahihi basi comment yangu ya awali isipewe umuhimu wowote!

    ReplyDelete
  7. Linavutia ila hii itafanya cost za matengenezo ziwe high.

    Mfano hardwood floor ni ghali kuweka lakini maintenance yake ni cheap na carpet floor ni cheap lakini maintenance yake ni ghali.

    Ningewaomba tu wafikirie hilo in a long run itakuaje? Je walikubali cheap thing (grass) compare to expensive thing (concrete) parking? Hii isipokuwa na good maintenance itakua kama uchafu vile.


    Pia wangefikiria parking za juu kwa juu au hata 5 minutes kutoka kiwanjani na kuwe na shuttles za kupeleka watu au kama sio mbali kwa kutembea basi watu watembee. Hawafikirii miaka kumi au ishirini parking zitatosha? Ndio maana jiji letu linasumbua barabara zake hazipitiki kwa vile watu walio design hawakuwaza miaka 10 au ishirini ..itakuaje? Hamna pa kuengeza barabara

    ReplyDelete
  8. HIVI NI KWELI HAYO MAGARI YAPO JUU YA MAJANI AU MACHO YANGU? KAMA NI KWELI MHH TANZANIA TUNA SAFARI NDEFU. YAANI HAMNA MTU HATA MMOJA TANZANIA NZIMA ALIEONA HIYO?

    ReplyDelete
  9. Nakubaliana na Ano hapo juu kuna haja ya kupata mtu wa proof-reading articles za TFF kabla hazijatundikwa vinginevyo lugha ya malikia itakuwa haina maana bora waandike kiswahili.

    "taifa stars fan's in dar es salaam city, showing there support by signing there names"

    ReplyDelete
  10. Waambie hao maana kama MAGARI yata kuwa yanaegeshwa kwenye nyasi, itakuwa ni kuvumbua tairi upya, ushamba usio na mfano ni sawa na mshamba aliyeona bunduki kwa mara ya kwanza akachungulia kwenye tobo aone risasi inavyotoka...

    ReplyDelete
  11. Jamani hivi TFF hawajawaona watu wanaotengeneza website nzuri, website hiyo imetengenezwa na nani imekaa hovyooo, jamani tujifunze Mwakalebela na Wanzako please angalieni website za vyama vya soka vingine zinavyopendeza, theFA.com etc. ni hayo tu Michu make sure TFF wamepata hii comment for them to change.

    ReplyDelete
  12. parking yenyewe hapo mechi iliyopita ilikuwa 5000/= tena kwa wale tu wenye tiketi za VIP.

    Sijui kwenye mechi hii ya Msumbiji itakuwaje, labda 10,000/=.

    ReplyDelete
  13. Huo si unyasi bali rangi angalieni kwa karibu!

    ReplyDelete
  14. BWANA MICHUZI TUNAOMBA UTUPE LINK AMBAYO TUTAWEZA KUONA LIVE MECHI YA STARS KWA SISI TULOKUWEPO UGHAIBUNI COZ TUMEONA TIDO KATIA MKATABA NA GTV KUONA LIVE TVT,RDT NA PRT TUNAOMBA UTUJUILISHE AU MTU YEYOTE ANAYEJUA WEBSITE GANI ITAONYESHA GAME YA STARS LIVE.

    ReplyDelete
  15. Majani Majani Majani! eee mama weeee! Na hii mambo ya Blogger warming!
    Atanaye Kijiko

    ReplyDelete
  16. HEE MAGARI YANA EGESHWA KWENYE NYASI @#%&! ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...