
peter tino akiweka sahihi juu ya mpira maalumu ambao wachezaji wote wa zamani wa staaz walimwaga wino. mpira huo ulitolewa na spia mbwembwe mkurugenbzi wa kampuni ya vifaa vya michezo ya ab sports

mastraika wawili wakubwa kupata kutokea bongo; peter tino na kitwana manara popat

starika nyota wa taifa staaz na pan africa peter tino akipongezwa na makocha wa timu ya taifa huku kitwana manara akishuhudia. tino yupo kwenye vitabu vya historia kuwa baada ya kuifikissha bongo kwenye fainali za afrika huko lagos mwaka 1981 kwa goli lake la pekee alilowafunga zambia kule ndola
Huyu jamaa alikuwa bonge la striker,ingekuwa enzi hizi labda angekuwa Arsenal au Man U,zama hizo mpira bongo ulikuwa hauna kitu na sio bongo tu hata huku ughaibuni.Jamaa namkubali toka akiwa African Sports ya Tanga na Pan African,vijana wa leo wangekuwa kama yeye bongo zamani tunachekea Ghana.Big up Peter Tino,tunakukumbuka baba.
ReplyDeleteNamkumbuka sana Peter Tino akiwa African Sports alikuwa hatari bi balaa .... na Mohamed Salum wa Coastal Union!
ReplyDeleteWako wapi
Omari Hussein 'Keegan',
Leopald Tasso 'Mkebez',
Charles Boniface Mkwasa,
Thuweni Ally,
Celestine Mbunga 'Sikinde', Zamoyoni Mogella,
Elisha John
Said Mrisho Zico
n.k.
Sikuwaona katika picha!?
Pongezi kwa aliyebuni, na waandaaji wa 'ghafla' hii ya wachezaji wa zamani wa staaz!!
ReplyDeletePia wasaidiwe kutokana na viingilio hivi vya mechi za taifa ili waishi maisha ya hadhi ya kibinadamu. Maana wengi wao wanapata matatizo sana kimaisha mfano mzuri ni ule wa picha ulizotuonyesha kuhusiana na mchezaji Chuma kule Mtwara!!!
Tino
ReplyDeleteChoka mbaya !
Peter Augustino ukipenda Peter Tino, nakumbuka sana goli lake alilowafunga Wazambia Sheikh Amri Abeid miaka ya 80 wakati wa Kombe la Challenge. Tino alikuwa anatisha! Somo kwa vijana nguvu ni kitu cha kwisha wekeza fedha kwa maisha ya baadae kama vipi na shuke pia mpige nyie wachezaji wa sasa!
ReplyDeleteDas ist mir!
Ndugu yangu hapo juu, fedha ya kuwekeza kwa maisha ya baadae kwa mpira wa Bongo hakuna.Waulize wachezaji wenyewe wakuambie.
ReplyDeleteNINI HAO ULIOWAKUMBUKA WAPO WENGI TU NANADHANI WENGINE MAREHEMU KWA SASA.JE UNAMKUMBUKA PITA MUHINA SAMLI AYUBU,ABDU NTILA SANIFU RAZALO 'TINGISHA' MINZIRO 'MAJESHI' NA MHANDO MDEVE? wapowapi jamani watu hawa na wengine wengi hebu misupu anzisha kitu kinaitwa historia fupi ya wachezaji wetu wa soka wa zamani ktk blog hii tafadhali
ReplyDeletePita Tino bwana, yanshomeza kweli! Yatake three position kwa one time!
ReplyDeleteTeh teh teh.
Ali nka Fumo Felician bwaana?
ReplyDelete