BIG BROTHER AFRICA II RICHARD LEO AMEONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA HOTELI YA HOLIDAY INN MILANGO YA SAA TANO ASUBUHI. IFUATAYO NI SEHEMU YA MKUTANO HUO KAMA NILIVYOAHIDI. MASWALI NA MAJIBU YALIKUWA KIBAO NAMI NIMECHAGUA MACHACHE AMBAYO NADHANI YATAKIDHI KIU YA WADAU KIASI...

Richard: Shikamooni… Kwanza nitaanza kwa kushukuru wananchi wa Tanzania kwa sapoti mliyonipa. Nawahaeshimu sana. Mmenionesha mapenzi ambayo sijawahi kupata. Na nitaendelea kutangaza nchi yangu popote pale nitapokuwa katika mambo yangu nitayokuwa nafanya. Na pia, jambo lililotokea jana, la vurugu kiasi cha kushindwa kusalimia wapenzi waliokuja kunilaki, naomba radhi. Naomba wananchi muelewe kwamba sio rahisi mimi kumsalimia kila mmoja wenu. Lilikuwa ni swala la usalama. Asanteni.

Lucy: Lilikuwa ni swala la usalama, lakini Richard bado yupo. Na wiki ijayo atakuwepo na tutatangaza utaratibu wa sehemu ya kwenda kumuona. Kwa kuanzia, kwa wananchi, sababu tunajua kwamba wote wanasubiria kutakuwa kuna party lakini Jumamosi saa sita mchana Richard atakuwepo ofisi za MultiChoice. Kwa wale watakaotaka kumuona, kwa ajili ya kusaini autographs na kila kitu ina maana watakuja pale na kupata opportunity ya kuongea naye na kupiga naye picha. Hii wiki yote tuta focus kwa wanahabari. Kesho Ijumaa atakuwa na ziara ya kutembelea vyombo vya habari vyote. Nyie hapa tunajua mnawakilisha lakini kesho atawafuata kule mnakofanyia kazi ili aweze kusalimia watu wote kwa pamoja. Baada ya hapo tutatangaza wapi wananchi wanaopenda kujirusha watakutana naye wapi. Kwa hiyo kwa sasa hivi tunaklaribisha maswali.

Swali: Umepanga kufanya nini baada ya kurejea na ushindi na pesa zote hizo

Richard: Ni swali zuri. Kama mnavyojua wote ndio nimeingia nchini na hata kupumzika sijapumzika. Kwa hiyo nitahitaji muda kukaa chini na kuangalia sehemu gani ya kuingia. Kwa kweli sasa hivi sina maamuzi kabisa. Lakini time ikipita nitapata mawazo na… yeah. Nahitaji muda. Lakini nataka niiingie kwenye career yangu ya mambo ya filamu. Na hilo ndilo swala la kwanza. Yaani kwa kuanzuia huo utakuwa ni mtazamo wangu wa kwanza kabisa.

Swali: Je Big Brother imekubadilisha wewe kama Richard?

Richard: Jinsi nilivyokuwa naishi mle sijabadilika na sidhani kama ningebadilika hata kama ningeambiwa leo niende tena. Kama ninagekuwa na nafasi ya pili ya kurudi kwenye nyumba ya Big Brother ningefanya mambo vile vile (vicheko kwa sana…) Mtazamo wangu nilioingia nao ndio ule ule. Lakini mimi niko wazi. Nilivyoingia na nilivyotoka bado niko vile vile. Nilipoingia sikuwa na plani. Sikupanga sijui nikienda nitamchezea huyu ama yule. Nilikuwa nimejiachia kama Free style. Ndo Richard huyu. Mimi ni kijana na kama kuna mtu ana idea nzuri tunakaa chini tunaongea. Kitu chochote kizuri mimi nitakichukua.

Swali: Katika mafanikio yoyote kuna changamoto zinazomkabili au anataraji kukabiliana nazo. Je unadhani mbele yako kuna changamoto gani inayokusubiri

Richard: Unajua, kwenye maisha, huwezi kutegemea kila mtu atakukubali. Unaelewa..? Mimi nimejiandaa.Kuna wengine watanichukia. Kuna wengine wataniponda. Lakini pia mke wangu. ni Challenge kubwa sana.

Swali: Umesema mkeo atakuwa changamoto kubwa kwako. Hebu fafanua

Richard: Sawa, si unajua nilivyoingia Big Brother nimeingia na ndoa. Na mambo yakatokea vile yalivyotokea. Kuna wengine wataelewa kwa sababu mazingira niliyokuwa naishi ni magumu. Kuna watu wengine watasema hamna. Kwa sababu wao hawajui. Hii opportunity ni yangu peke yangu. Unaelewa? Na experience niliyotoa mle ni yangu. Yaani nawaambia ukweli, sio wengi ambao wataelewa.

Mimi nampenda mke wangu sana. Sana tu. Na ningependa kuwa naye. Hiyo ndio itakuwa challenge yangu kubwa sasa hivi. I mean, hiyo ni challenge kubwa sana katika experience yangu yote katika nyumba na mambo ambayo yatatokea ni kumrudisha mke wangu. Lakini naamini…. Sijaonana naye. Sijaonana naye…. Kwa hiyo siwezi kuongea zaidi. Ok? Siwezi kuongea mengi (hapa vijichozi vinamlengalenga machoni).


Swali: Hebu tupe historia yako ya maisha kwa ufupi. Maana ulipokuwa kule mengi yamesemwa na yanaendela kusemwa..

Richard: Ok. Mimi bwana sio Mganda. Mimi Mzaramo. Mama yangu Mzaramo, alizaliwa Dar es salaam. Ok? Mzee wangu asili yake ni… eehh. Babu yangu upande wa baba ni Mdachi. Mama yake ni Mnyanrwanda. Sawa? Baba yangu alizaliwa Uganda. Mama yangu, wakati huo walipokutana, alikuwa anasoma Uganda. Kama Watanzania wengi wanavyokwenda huko kusoma. Wakakutana, wakapendana na nini nani…ikatokea ile ishu ya Iddi Amini. Mzee na mama wakarudi huku (Tanzania). Ndiyo yukazaliwa huku.

Nina umri wa miaka 25. Nimesoma shule ya msingi Makumbusho hapa Kijitonyama, Dar mpaka darasa la nne. Mama yangu akafariki tukahamia Sinza. Sina nikasoma shule ya msingi ya Mashujaa. Mzee akaamua kutupeleka Uganda. Uganda nikasoma mpaka form six. Uganda nilianza darasa la tano hadi form six. Kisha nikarudi zangu nyumbani. Nikamwambia mzee nimeshamaliza masomo, nataka kurudi nyumbani nikaanze maisha yangu. Nyumbani ni nyumbani. Unajua tena….Ndo hivyo nikakutana na Rikki. Nikaendelea na masomo yangu ya filamu. Nikapelekwa Big Brother, mpaka hapa leo…

Swali: Mlionana na kuongea na Tatiana baada ya kutoka Big Brother?

Richard: Ndio, nilionana na Tatiana. Hatukuongea mengi, kwa sababu sie wote hapa tuna matatizo mengi sana. Akarudi kwao, ana mambo yake. Na mimi na mimi ni mambo yangu nyumbani hapa. Na bado sijaonana na mke wangu mpaka hapa. Kwa hiyo sina mengi ya kuongea

Swali: kumekuwa na kelele kibao kwamba Big Brother ni mchezo ambao ni kinyume cha maadili katika jamii. Yaani immoral. Hii imekaaje kwako wewe ambaye wengi wanakulalamikia kwamba ulifanya mambo ya aibu mle

Richard: Ahh.. Big Brother sio immoral, kwa sababu huu mchezo wanavyotengeneza hawatwambii nenda kule ukafanye hiki na kile. Ile ni reality show. Wachezaji wa mchezo wanajikuta kwenye hali fulani na mambo yanatokea. so, ukisema ni immoral, inaonekana kama vile yaani imepangiwa iwe immoral. no, no, no... Hapana. Watu mnaenda na mnaishi kama mnavyoishi.

Swali: Watu wanaposema ile show ilikuwa immoral ni kwamba Richard ameoa. Lakini alichokuwa anafanya ni kinyume na maadili ya ndoa. Sasa je Big Brother inatufundisha nini sisi Waafrika?

Lucy: Big Brother haifundishi. Big Brother inaonesha. Sasa je tujiulize tuliooa au tulioolewa, hatujawahi kunanihiii.... nyumba ndogo? Tujiulize, hivyo vitu vipo havipo (makelele ya vipooo...vipooo...) Sasa tofauti hapa ni kitu gani...Na katika hayo kuna parental control. Yaani kinachokufurahisha wewe utakiangalia, usipokifurahia, haya....lakini ni kipi cha tofauti?







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Dah! Richard kashinda BBA, but, deep down, he is in deep shit! Hehehe! (a) Mambo ya ndoa (b) ku-control being a celebrity (c) Control over money. Haya mambo matatu asipoangalia, yanaweza kummmaliza kabisa na hatimaye kumuondoa duniani.....KALONGA!

    ReplyDelete
  2. Kwanza sio mtanzania.Mhindi mlipiga kelele.Richard ametoka mkoa gani???Ni wa kabila gani???Makabila ya Tanzania yanaeleweka.Nawasilisha.

    ReplyDelete
  3. Kama unataka kumrudia mkeo achana na dada yako. Yeye anaongea utumbo ili avunje ndoa yako wakati huo huo ndoa yake bado ipo sawa. Weka akili kichwani mara nyingi sana ndugu huwa wanaturudisha nyuma sana katika maisha. Sisemi uwatenge ila uweke mipaka ambayo hawaruhusiwi kuivuka katika maisha yako ya ndoa. Hakuna cha baba, mama, shangazi, mjomba, kaka, dada n.k. hao wote ni mzigo kwenye ndoa yako kama hutokuwa mkali. Uliyomuoa ni mkeo na sio mke wao, nafasi yao kwenye ndio yako ni ndogo sana.

    ReplyDelete
  4. He is a smart guy anajua kujibu maswali kwa ufasaha...big up Richard.I think utakuwa umewakata kilimi ma=haters.

    ReplyDelete
  5. Jamaa anaonekana hakuwa na lengo la nini atafanya kabla ya kuingia BBA na na baada ya kutoka BBA ni vile vile tu hakuna mabadiliko kama asemavo mwenyewe!
    ila kwa mnyakuo mkubwa huo alioupata ingekuwa vizuri akarudi shule ktk nchi ambazo ni expert wa mambo ya filamu kwani sasa uwezo anao.
    michuzi pia unatutia hamu kutaka kujua kuhusu nani atanyakua zawadi yako ya dola mia tano ya kuagulia matokeo ya mechi ya uengereza??

    ReplyDelete
  6. Interview nzuri na Richie kajibu vizuri,lakini Mwisho dada Lucy alipomalizia Mhh...!! kwa hiyo anaunga mkono watu kucheat?

    ReplyDelete
  7. NANUKUU
    " Swali: Hebu tupe historia yako ya maisha kwa ufupi. Maana ulipokuwa kule mengi yamesemwa na yanaendela kusemwa.
    Richard: Ok. Mimi bwana sio Mganda. Mimi Mzaramo. Mama yangu Mzaramo, alizaliwa Dar es salaam. Ok? Mzee wangu asili yake ni… eehh. Babu yangu upande wa baba ni Mdachi. Mama yake ni Mnyanrwanda. Sawa? Baba yangu alizaliwa Uganda. Mama yangu, wakati huo walipokutana, alikuwa anasoma Uganda"

    1. Rich jizoeze kujibu maswali kwa ufasaha. Hakukuwa na haja ya kuanza kujihami kuwa wewe si Mganda maana muulizaji hakusema hayo. Kama ulitaka kwenda katika kujisafisha au kufafanua juu ya maneno fulani yaliyosemwa ambayo una uhakika kuwa si ya kweli basi Ungeanza kwa kumuuliza ni yapi mengi yaliyosemwa ambayo yalihitaji ufafanuzi wako.
    2. Maelezo yako hayashawishi mtu kuwa inakuwaje sasa wewe uwe Mzaramo?
    3. Kwa hiyo baba yako anaendelea kuwa Mdachi au ni Mnyarwanda maana hukueleza alivyoacha huo uraia na kuwa Mtanzania ingawa hii haikuzuii wewe kuwa Mtanzania.

    4. Rich & Lucy immorality haipimwi kwa kigezo cha kupangwa au kutopangwa bali kwa kuhukumu hisia, neno au tendo lisilojali 'moral virtues' zinazothaminiwa na jamii husika in this case Tanzania au hata useme Afrika.
    5. We Lucy hufai kabisa kuwa Mshauri tena angalia utamwangamiza Rich sasa hivi! Yaani unahalalisha uozo kwa kuwa kuna watu fulani tumewashuhudia wanafanya uozo!!
    Aidha hiyo tasnifu ya eti Big Brother haifundishi bali kuonesha basi malizia kuonesha nini na kwa ajili ya nini au iweje? uone utakavyochemsha.

    Msilete vya kuleta hapa! Mtu mzima uliekwenda shule na mwenye hekima ukikosea unaomba radhi kama ulivyosema kuhusu kutoroshwa kwa ajili ya usalama wakati watu wanakusubiri Airport. Mbona hapo hukusema kuwa hiyo ndiyo reality kwamba wengi pia hufanya hivyo???

    Nyakatakule Unyilisya Echalo

    ReplyDelete
  8. ndio tunaona madhara katika jamii yetu ya Africa ya kuiga vitu vya wazungu visivyokuwa vya maana... Tuzidi kuiga tu tutakuja kuona madhara yake baadae kwa vizazi vijavyo na kadhalika

    ReplyDelete
  9. kuna maana gani kuiga show kama bb kwa sisi Africa??? Huhitaji kuwa rocket scientist kulisti madhara ya vitu kama hivi kwa jamii na maadili. Yani kweli waafrika tunatawaliwa kifikra mpaka kesho!! hatuna uwezo wa kuchuja nini cha kuiga na nini cha kutoiga. jamii yetu itazidi kuharibika tu, na vizazi vijavyo ndio hata sitaki kufikiria. Wazungu milele watatuona wajinga na they'll keep benefiting from our ignorance.

    ReplyDelete
  10. Jibu lako wewe sio mzaramo wewe ni mtanzania period....Hapo ukijiita mzaramo unajidanganya....watu wengi wamezaliwa hapa USA na mama wazungu na baba wabongo lakini hawajiiti wazungu wanakubalika kama raia wa USA lakini original yao inatokea huku bongo...that is simple...ukijishaua tutakuona mjinga na hujui au hukubali identity yako...

    ReplyDelete
  11. Tatizo la Richard ni kuwa bado mdogo. Alioa mapema kabla haja enjoy maisha kabisa sasa kila anachoona kinapita anatamani kukionja....

    Ndio maana watu wanaambiwa don't rush in anything...Wa USA hawaoi mpaka wamegonga 35 yrs old or up ....baada ya hapo kwa wengi wao (sio wote) huwaelezi kitu tena...kwasababu kila raha, uplay boy wote wameshapitia sasa wakisettle down ni kujenga maisha na vitu vidogo dogo kama TATIANA havitamsumbua kabisa.

    ReplyDelete
  12. Huyo Lucy ushindwe kabisa ana halalisha uasherati....ulegee dada yangu ....ndio maana ukimwi hauishi Tanzania....

    Richard omba msamaa yaishe...kubali udhaifu wako basi sio kusema nyumba ndogo zipo nyingi sasa basi mpeshapitisha kuwa ni jabo la kawaida...

    ReplyDelete
  13. Kweli nimejua kwanini watanzania hata huku marekani maisha yetu bado duni sana. Jamani tunawivu kupita kiasi. Mji naokaa mimi waafriaca wengine wemeshikilia kazi nzuri sisi wataanzania ni kufanya kazi za kupangusa.Simjui huyu Richard lakini watanzania tumezidi angeshinda nchi nyingine ndiyo mngefurahi?
    Pili according to my short survey nimejua kuwa watanzania wengi hapo Tanzania wanaangalia hichi kipindi na wanakingojea wiki nzima. Hamkujua kama iko immoral???????? Jamani watanzania wenzangu tuache hizo roho jamani this is too much. Kuhusu yeye na mke wake mumuachie mwenyewe nyie mmepungukiwa na nini. Naamini wewe mwenyewe au ndugu yako kwenye familia yako ameshawwahi kumuacha mke wake na kufanya uanasa. Naomba urekebisha ya nyumbani kwenu ndio mmuongee hayo.Too much. Hii big brother ipo muda mrefu hamkuwahi kulalamika hizo dola laki moja zinawatowa roho. Think please b4 u write shit. Unafungua comments kusikia sifa unakutana na watu wenye roho mbaya, huo ni ushetani na muombe mungu wako akusamehe. Kama Mnamuona Richard anamakosa basi kwa roho zenu kashasemehewa kwa mungu nyie wenye roho za korosho ndio mtabeba dhambi zake zote.
    Thumbs up Richard pamoja sikuangalia hicho kipindi. Walahi tumshukuru Nyerere kwa kuleta umoja kwa roho hizi zetu mbona tungekuwa zaidi ya vita vya warundi na wanyarwanda

    ReplyDelete
  14. Richard bwana atakuwa na kazi ngumu sana kumrudia mke wake, sasa mke wake sijui anafanya kazi gani hapo Bongo, kama anayo kazi nzuri basi nadhani Richard itabidi asahau lakini mkewe kama hana kazi nzuri ni lazima atarudi kwa Richard tu, fedha bwana

    ReplyDelete
  15. Dogo usikonde wala nini.
    Kama huyo Mkeo anakudengulia, RAY C si yupo?
    Asikubabaishe huyo!

    ReplyDelete
  16. Richard majibu yake kuhusu tatiana sijamuelewa, wakati yupo mle ndani alikua anasema anampenda sana tati na yuko tayari kwa kila kitu kwa ajili yake na kuna siku waligombana alisema yuko tayari hata kulala kwenye sakafu kwa ajili yake,sasa leo anarudi anasema anampenda sana mke wake jamani mbona haileti maana au anafikiri Rick hana nyongo? na yeye anawazazi jamani, kwakweli siwezi kumsema Rick lakini kwa binadamu wa kawaida, Richard hatakiwi kusamehewa hata kidogo, na kitu kingine ambacho richard alibugi step ni kutanga hadharani uwa ame fall in love na tati, What? hata kujibaraguza No way, Rick anatakiwa aangalie maisha yake na ajue mume aliyenaye ni wa aina gani, anaweza kufall na mwanamke mwingine hata kama rick yuko pembeni, na kwanini wasema wapenzi zao wakiwabwaga wao wataendelea ina mana walikua wanafanya vile makusudi ili kuwaumiza wanza wao?
    nonses hizo.

    ReplyDelete
  17. Kwa kweli tumpe Hongera Richard, sidhani kama ushindi wake umetokana na mapungufu aliyokuwa nayo bali yale aliyowafurahisha watazamaji. Kitu kikubwa alikuwa mcheshi sana na pili siku za mwanzo watu wengi walimwona kama yai bovu yaani hana kitu kichwani. siku za mwisho alishamiri sana na kuprove kwamba he is intelligent and with a creative mind alipoibuka kuwa kinara katika tasks walizopewa. Na hizi sifa ndio zilizompatia ushindi. Ninaamini ushindi wake ungekuwa wa kishindo isingekuwa mapungufu aliyokuwa nayo. Ila sisi wote ni wanadamu, na yale mapungufu tuliyonayo Mwenyezi ndie wa kuhukumu na sio sisi wanadamu. Huwezi jua kwa nini Mungu ametaka apitie aliyoyapitia. I foresee a bright future for Richard na Mungu ambariki. Ricki, ni ngumu kusamehe na kusahau lakini kumbuka huwezi jua Makusudi ya Mungu ya wewe kuwa na Richard. Ninakuombea Richard experience uliyopitia ikuwezeshe uwe a much better person in the future.

    ReplyDelete
  18. mhhh yangu macho

    ReplyDelete
  19. ni kijana mdogo, lakini amejibu maswali kwa upeo mzuri. na kuhusu ndoa yake, kumbuka angekuwa muhuni angemkandia mkewe,lakini ameonyesha upeo mzuri, kwamba sijakutana na mywife, lakini nampenda, and i cant talk much about her!!! bravo richard, u r a 25, but reasoning like a 35!!!

    ReplyDelete
  20. jamani yote mtasema watanzania bwana....!!!
    Wakati Rich hajakuwa mshidi hamkutaka kujua ni wa wapi ila sasa ndio vIherehere kutaka kujua kama kweli ni MTANZANIA yatawashinda na mtajiju.

    Richie kaka usisikilize ya watu ziba masikio na kujua maisha yako tu na mkeo yatakuwaje mungu atakujaalia mtajuwa pamoja na mkeo.

    Ila kuna wale wakina kaka wa mjini wanaoharibu wenzao kwenye uhuni na kwa sasa unapesa watataka urafiki kwako kila mtu sasa atajifanya anakujua vilivyo usiwape muda na wewe kabisa maana wao uhuni kwako upo mbele ya uso WA KAKA WA BONGO

    Namatumaini unaijua bongo vizuri ziba masikia kaka fanya kile unachoona kitakufaa katika maisha yako.

    wewe na rikki mpaka kufa nakuombea mungu atakusaidia tu mtakuwa pamoja.

    BIG UP...!!!!

    ReplyDelete
  21. JAMANI SIO SIRI NYIE WATU MNA WIVU SANA, YANI MTU AKIRUDI AKIWA AMECHEMSHA MANENO, AKIRUDI KASHINDA MANENO, WOOOTE MNAOTOA KASHFA KWA RICH HAMNA AKILI, WOTE WAPUUZI, TOENI BORITI KWENYE MACHO YENU NDIO MUONE VIBANZI KWENYE MACHO YA WENZENU!! KAZI KUKANDIA TU, KURA ZENYEWE HAMKUPIGA MLIMBANIA, TUACHIE SIE FANS WAKE TUSHEREHEKEE. NYIE MNAOJIFANYA NDOA KUTWA KUCHA MNAENDA KUNUNUA NANIHINO KINONDONI MAKABURINI!!
    KUDADADEKI!!!!

    ReplyDelete
  22. PIGENI MAKELELE WEEEEEEEEE TUKANENI WEEEEEEEE LKN NDO HIVYO RICHARD KASHAJISHINDIA MIJIHELA YAKE HATA MFANYEJE HANYANG'ANYWI NG'O!! BADALA YA KUFANYA MAMBO YENU MNAFATILIA MAISHA YA RICHARD. MWENZENU KAULA.. ANGALIENI MAMBO YA KUONGEA NA MUOMBEENI AFANYE MAMBO MAZURI ZAIDI KIJANA WETU, ACHENI KELELE ZA CHURA HAZIMZUII TEMBO KUNYWA MAJI NG'O!!!
    HONGERA RICHARD NA USISIKILIZE KELELE ZA VYURA!!
    CHIKI!

    ReplyDelete
  23. Katika mahojiano Richard kasema huyo tuliyemuona BBa 2 ndiye yeye wala hatabadilika. Kwa hiyo bado utaendelea kucheat sababu wewe ni binadamu. Je ungetoka huko ukute mkeo alikua na affair ungefanyaje?Ungemwita jina gani?

    ReplyDelete
  24. Mahela sio kitu, watu wanaangalia ubinadamu, kwa maana hio dada Lucy na yeye ana kabwana pembeni.
    Mambo ya nyumba ndogo ni kwa sie wakina waswahili, lakini kwa huyo mzungu itabidi akatubu kanisani, wazungu hawababaishwi na pesa, labda wale wazungu ukoko.

    Jingine, je jambo lakuonyesha ulimwengu nyeti zako ni maadili pia ya kitanzania?

    ReplyDelete
  25. Hivi ni salaam rasmi toka kwa niaba ya wadau wa London.

    Big Ron kwanza umerepresent ile kisawa sawa.At least sasa kutakuwa na heshima kidogo mana unathibitishia umma kuwa unaweza ukawa ulikuwa unafanya kazi pale ALDI ya EDMONTON lakini shule nayo ulikuwa unasoma na hata hiyo MBA yako haina utata hata kidogo tofauti na wengine

    Vile vile salaam toka kwa ma swahiba zako akina SAIDI JOHN,ABDALLAH ZIEBI,MANGI,ALEX MBAGA na bila kuwasahau wale masista PALE 21 A...na zaidi ya hayo tulikuwa tunakufanhamisha tuu kuwa sasa hao jamaa wa DSTV baada ya kumaliza kazi yako hapo inabidi ukae nao chini na urenegotiate new contract nao otherwise watakumilk kama wanavyofanya sehemu zinginezo Africa

    Tunajua kuna wengine wanalalamika kwa nini umevaa suti lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa hiyo suti inalipa na tai nayo ni mahala pake kwani IMAGE IS EVERYTHING!

    Mwisho ni ombi kuwa hebu fanya umsaidie kijana mwenzio GERALD MKASOYA ambaye kwa kweli taarifa zinazokuja huku zinasema kuwa hali yake si nzuri na kwa kweli hata YAYI lake lishaanza kuwa kama la KIMALAWI sasa hebu imagine MKASOYA ile cockney yake ya hapa na pale nayo ime go down the drain na mbaya zaidi hata KINDO naye nasikia kuwa yuko hoi..hebu wasaidie hao vijana ndugu yangu

    Kuhusu strategy ya kupata hilo fungu la RICHARD sidhani kama hapa ni mahala pake lakini nitajitaidi nikupigie baada ya kuangalia hatma yetu maana RUSSIA wakiwaunga ISRAEL ujue kuwa tumekweisha...btw omeona TOT'NAM tulivyorudi kwenye chati?

    -MDAU NORTH LONDON

    ReplyDelete
  26. Baraka naona bado ujazitupa suti zako za bairaiti za hapo LONDON

    ReplyDelete
  27. LUCY KIHWELE!! Did you real say that?? I dont believe it! So, do we take it that YOU also have a kibanda hasara and now and then you also cheat...?? my, my, my!

    ReplyDelete
  28. congrats rich u did it; because of u our country is a now hero; enyi watanzania wenye mioyo migumu ya kishamba na kiujima, isiyopenda mabadiliko wala maendeleo; who are u to judge others? if GOd can forgive why not u? i think its time to leave rich alone let him enjoy wat he deserve dears, or you want some? just speak out; why dont u concentrate on your affairs lather than keep on talking abt his personal n emotinal affairs?.

    Kiufupi napenda kuwashauri watanzania kuwa; badilikeni huu sio muda wa malumbano tumpongeze rich kwa kutuletea ushindi; mahusiano ni sehemu ya maisha ambayo kila mtu anayapitia na hakuna asiyelitambua hilo.
    Ni aibu kama nchi nyingine including SA; wanamkubali na wamefunga mjadala wa uhusiano wake na tatiana halafu nyinyi mnaenaendelea kujifanya vichwa ngumu kwa kumsakama,wakati hata kura hamkumpigia; acheni roho mabya mwacheni yeye aamue kuhusu maisha yake ya kimapenzi ebo;
    Asante lucy kwa kujibu vizuri hilo swali na hujakosea hata kidogo ila umekiri udhaifu wa kila mwanadamu.

    ReplyDelete
  29. Halafu mijitu mingine hovyo,how come mtu kaleta sifa kwenye nchi mnankandia??Linda mie niko nawe bwana hunijui sikujui lakini wanaokupiga madongo wengi ni wanawake they know how beautifull r u.dont worry someone somewhere support u.
    CHA CHANDU- UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...