
Mzee Michuzi,
Salama muheshiwiwa, nimekuwa nikisubiri sana kusoma ripoti ya jamaa wa Muhimbili waliekosea kuwafanyia operesheni watu wawili kichwa na mguu, tangu jana nimekuwa nikitembelea hii blog kila baada ya masaa mawili au matatu, Cha kushangaza ni kuwa naona umekauka kabisa, hutaki hata kuzungumzia swala hili, swali langu ni kuwa, je unahusika kwa kiasi fulani ? au Madaktari ni washikaji zako ? naomba sana unijibu, na vile vile uipost hii issue kwenye blog yako (yetu) ili watu watoe maoni yao. Nimesoma sehemu fulani kuwa mmoja wa wagonjwa hawa amefariki dunia, Mungu Ailaze Roho Yake Mahali Pema.
Haya,
ni mimi mwana blog JP.
(naogopa kutaja jina langu zima nisije-tukanwa na kutolewa siri zangu zote hadharani).
mdau jp,
kwa ufahamu wangu ripoti ya awali ipo tayari ila haijatolewa kwa umma hivyo sina ubavu wa kufanya lolote hadi hapo taratibu zitapotimia - michuzi


Ripoti ya nini? uzembe umejionyesha wazi kinachotakiwa ni watu kuwajibishwa,hizo bla bla bla ni majungu matupu.
ReplyDeleteNi lazima watu wawajibike uhai wa mtu umepotea na madhahara au hata kifo chaweza tokea kwa huyo waliomfanyia kimakosa..ingekuwa ughaibuni kwetu hao madaktari wangekiona cha mtema..ila Bongo TAMBARARE mambo yataisha kimya kimya!!
Kwa kweli inasikitisha sana mungu amrehem na pole nyingi kwa wafiwa na waivalie njuga swla hili wahusika wawajibike kikamilifu. Na wewe ndugu yangu uliye comment hapo juu umenichekesha sana EE bwana inabidi uogope wabongo tusingekuacha!!
ReplyDeleteVIPI MNASUBIRI RIPOTI IPOWE ILI ISIJE IKATUUNGUZA? HIYO KATIBA YA CCM INAFANYA NINI HAPO JUU? AU NDIYO RIPOTI YENYEWE.
ReplyDelete