Mzee Michuzi,

Salama muheshiwiwa, nimekuwa nikisubiri sana kusoma ripoti ya jamaa wa Muhimbili waliekosea kuwafanyia operesheni watu wawili kichwa na mguu, tangu jana nimekuwa nikitembelea hii blog kila baada ya masaa mawili au matatu, Cha kushangaza ni kuwa naona umekauka kabisa, hutaki hata kuzungumzia swala hili, swali langu ni kuwa, je unahusika kwa kiasi fulani ? au Madaktari ni washikaji zako ? naomba sana unijibu, na vile vile uipost hii issue kwenye blog yako (yetu) ili watu watoe maoni yao. Nimesoma sehemu fulani kuwa mmoja wa wagonjwa hawa amefariki dunia, Mungu Ailaze Roho Yake Mahali Pema.


Haya,

ni mimi mwana blog JP.

(naogopa kutaja jina langu zima nisije-tukanwa na kutolewa siri zangu zote hadharani).


mdau jp,
kwa ufahamu wangu ripoti ya awali ipo tayari ila haijatolewa kwa umma hivyo sina ubavu wa kufanya lolote hadi hapo taratibu zitapotimia - michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ripoti ya nini? uzembe umejionyesha wazi kinachotakiwa ni watu kuwajibishwa,hizo bla bla bla ni majungu matupu.
    Ni lazima watu wawajibike uhai wa mtu umepotea na madhahara au hata kifo chaweza tokea kwa huyo waliomfanyia kimakosa..ingekuwa ughaibuni kwetu hao madaktari wangekiona cha mtema..ila Bongo TAMBARARE mambo yataisha kimya kimya!!

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli inasikitisha sana mungu amrehem na pole nyingi kwa wafiwa na waivalie njuga swla hili wahusika wawajibike kikamilifu. Na wewe ndugu yangu uliye comment hapo juu umenichekesha sana EE bwana inabidi uogope wabongo tusingekuacha!!

    ReplyDelete
  3. VIPI MNASUBIRI RIPOTI IPOWE ILI ISIJE IKATUUNGUZA? HIYO KATIBA YA CCM INAFANYA NINI HAPO JUU? AU NDIYO RIPOTI YENYEWE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...