
hii ndo kamati ya miss tz. toka shoto ni jason tall (mjumbe), prashant patel (mwenyekiti), hashim lundenga (mkurugenzi wa lino international, waandaaji wa miss tz), dk. ramesh shah (mshauri), aidan ricco (afisa habari) na mkuu wa itifaki makoye. nafungua mjadala wa kuijadili kamati hii pamoja na nini kifanyike ili bongo ifanye vizuri kwenye miss world. mjadala huu pia upo www.bongocelebrity.com
mimi nahisi kuna haja ya kufanya kama wenzetu wa Angola ambao wamevumbua ujanja wa kuchagua miss kutoka nje ya nchi pia, miss angola ambae analikuwa miss world africa, anaishi U.K,na huyu wa sasa alikwa anaishi portugal na hivi sasa anaishi U.K pia,
ReplyDeletekuna vipaji vingi pia nje ya Bongo ambao inatakiwa pia miss Tanzania wa kila nchi ya za bara la ulaya ingelikuwa vizuri kupambana ili apatikane miss TZ Europe pamoja na mwenza wake ili waje kupambana fainali na wenzao wa bongo, vile vile washindi wawili kutoka america na canada,asia,na australia,hapo nadhani atapatikana mshindi wa nguvu ambae atatuwakilisha vizuri ktk nchi,
zaidi mamiss wetu wanatakiwa kujua talent yao ni nini, sio tu kuvamia kusema mimi nacheza mpira wa miguu, hali ya kuwa hujawahi hata siku moja kucheza mpira,unadhani mazoezi ya mpira wiki moja ktk maisha yako yataweza kukufanya kuonekana mchezaji, zaidi ni bora kuonyesha kipaji kwa jamii kama kwenda kuwasaidia wafanyakazi unicef msaada ambao hauhitaji kulipa kitu,au unhcr ktk kambi za wakimbizi kama vile kusaidia kupika au kusaidia kusambaza huduma muhimu kama ambavyo miss ataelekezwa na wafanyakazi ,pamoja na mambo mengi ya jamii, kwenu wadau,
MIMI BADO SWALI LANGU LIPO PALE PALE MICHUZI MBONA UKWENDA KUMPOKEA SISTA WAKO JANA ROHO MBAYA HIYO MMECHANGIA KUMUAIBISHA DADA WATU MASIKINI WAKATI MLIJUA KABISA ANA NAFASI YOYOTE KULE HATA ROUND YA KWANZA WALIMPENDELEA INGEKUWA MIMI HATA ROOM ASINGE CHECK IN NINGEMRUDISHA NCHINI KWAO NINGEONA NCHI YAKE WAMEFANYA UTANI KWAMBA HAWAKUWA SERIOUS NA USHINDANI
ReplyDeletehawa Jamaa bwana ni wababaishaji haina maaana kuendelea kuwa nao maana hatuoni jipya kila siku warembo wanalalamikia maandalizi na ukiangalia kuna a bulk of money inatoka kwa sponsor sasa kuendelea kuwa nao upuuzi
ReplyDeletehuu ni mtazamo wangu jamani
Kwanza mbona hawa wahindi wengi wanajaza kiwingu tunataka masista na mabraza vijana.Sasa hawa waheshimiwa mbona sana kweli watajuwa katika umii nini kinatakiwa au fashion ni zinaenda vipi.Yaani wakina patel kweli watuamulie mambo haya?Hivi mlio ughaibuni tushaurini maana mnaona mengi huko mliko na hasa mavazi,maana hata Flaviana matata hatukumvisha nguo ya maana akashindwa ingawa alikuwa mzuri sana angeshinda kumi bora kwenye miss world.Huyu Richa tulishajuwa asingeshinda kwanza kazubaa sana,hakuwa shapu kama wengine.Tusichague mamiss waliozubaa majaji wanataka mashapu na wajanja,tuchague sura za kiafrica na hapa sizungumzii ukabila,richa aneshinda lakini legelege mno hata picha anaona aibu.Mambo ya umodo unatakiwa uwe mbabe fulani na picha unatakiwa uwe strong.Hawa watu wazima mambo ya umodo hawayajui tutafute vijana sio wamama watu wazima,na vile vile tupate mashapu wanaojuwa nini kinaendelea duniani sio lazima wawewameishi majuu lakini wawe watu wa fasheni.Sasa wamama wanaochagua mamodo wenyewe hata kuvaa hawajui,nyele kutengeneza ndio basi tu,wanabaki wakituchagulia masepetu matupu kama basila mwanukuzi,hivi walikuwa wamelala nini,of all the people you give us basila? zero?
ReplyDeleteHawa jamaa wazee hata fashion hawazijuwi hebu waone.Mbona hakuna majike.Ughaibuni hebu tupeni majina ya wadada huko tuanze mikakati maana ujinga huu,wadada wazuri na miili mizuri wako huko,hebu rudini tukomboe jahazi.
ReplyDeleteHivi mimi nina swali,hela wanyo wahindi tuu au waswahili tunapuuzia vikwanja.Mara dewji mara patel,mko wapi waswahili matajiri.Tumeona kwenye forbe magazine tajiri wa ghana katambuliwa na wazungu wememkoma.Tanzania vipi jamani,mbona uchumi tunao lakini tyumeukalia,mitalenti tunayo lakini hatuipatii pesa.Huyo mghana katajirika kwa biashara ndogo sana na kachunguzwa sasa maana walidhani ni poda lakini jamaa ujuzi na kuivest sehemu basi makaratasi anayo lakini kaamua kuishi ghana kwao na kutumbua mamilioni ya kimarekani hapo ghana.Mamiss hata nguo za maana hatuwanunulii basi wanavaa vioja huko nchi za watu na kututia aibu.Umiss sio sura tuu na bongo pia,tabasamu,mwendo,pozi,vitu kibao.
ReplyDeleteMbona hiyo kamati haina hata mwanamke mmoja??? Hivi nyie wanaume tupu kweli mtaweza kuwaanda hao wanawake vizuri mnaowachagua kama Mamiss??
ReplyDeleteMi nadhani kutokuwepo wanawake katika hiyo kamati ni pengo dhahiri na la wazi.
Najua wazee mnalinda chakula chenu katika hiyo franchise yenu na Miss World Corporation, lakini mkumbuke ubinafsi ni msingi mkuu wa kushindwa katika biashara. Ingizeni miss mmoja aliyefanya vema huko nyuma awe member wa kamati (kama Hoyce hivi). Pia wekeni mwanamke mmoja mtu mzima (m-mama mama kama Mama Terry hivi) kwa ajili ya kuwashauri hao mamiss.
Nakumbuka maneno ya MC Taji Liundi, ..." Mashindano ya mwaka huu yanamuonekano tofauti mtaona mabadiliko..." eeh! Kweli!!! Tumeyaona sasa wadau, mimi naona hiyo kamati wameota pembe, wasafiri kwenda nchi za wenzetu kama SA, Venezuela waulize siri ya urembo jamani, hata wakiruka mashindano kwa mwaka mzima ili maandalizi ya mwaka unaofuata yawe bomba si mbaya hao wanaopenda kushiriki wajiande ili wa meet market ya urembo
ReplyDeleteSalaaam... Duh kweli Miss Tanzania ni kijiwe/biashara mazima!! Wewe kamati ya Miss Tanzania halafu wote ni maMr?? Sijawahi ona.... Pili hao jamaa wanajua mambo ya "uzuri" na "urembo" na "ubora" manake mdada mrembo sio lazima awe mzuri au bora jamani!!!! Ina maana hakuna watu wenye hata mawazo ya kuwapangua hawa jamaa na kuweka sura ambazo zinaweza tusaidia tukapata watu kama kina Nancy Sumari tena.... Jamani lazima tukubali kuna kuchoka (mfano wazee wetu hapo juu kwenye picha) hivyo basi tuwapumzishege etiii!!!!
ReplyDeleteMungu Ibariki Tanzania na Watu wake..
VIPI WADAU RICHA AMERUDI?
ReplyDeleteNilikuwa Loliondo kwa Mtoto wa Mfalme wa Urabuni anayemiliki eneo huko...Mmh!
Hi Michuzi?
ReplyDeletemie nadhani hii kamati ivunjiliwe mbali,iundwe kamati ya watu ambao wako serious, wenye kufahamu, nini maana ya urembo? mrembo anatakiwa awe vipi?,na apatikane mrembo ambaye anakuwa na manufaa zaidi kwa jamii yetu ya kitanzania, nasi, si tuwe tunanga'ngania aende akashinde, tu bali pia tuwe tunashirikiana nae,iundwe kamati ambayo haina malalamiko,kashfa kama hii....bye 4 now soup, cya dec 16th when u'll walk alone
Kwani jamani hii kamati huwa inachaguliwaje??? na mbona hawa jamaa wako muda mrefu sana?? kwani hakuna watanzania wengine wanaofaa kuibadili hii kamati...labda tupate timu mpya itakayo kuja na nguvu mpya, ari mpya na mambo mapya...kila siku haohao tu!!Duh
ReplyDeleteInabidi wawe seriou kwanza wao wenyewe Anon hapo juu siuliona walichagua MISS TZ UK lakini ilikuwa vile vile tena bora wale wa bongo yeye ndio alikuwa amechoka kuliko wa home waache kufavor kama mtu anakiwango hakuna kumregister kabisaaaa yaani hata form wasimpe this time wananchi tumeumia roho sanaaa hashimu lundenga tunakuheshimu sana
ReplyDeleteHAWA JAMAA NI KWELI KABISA WANAFANYA MAMBO AMBAYO SIYO YA KUFANYA MISS TANZANIA AWE KWELI MISS TANZANIA AMBAYE HATA AKIFIKA HUKO MISS DUNIA BASI AFANYE MAMBO AMBAYO YATAKUWA KATIKA KULETA USHINDI NYUMBANI,NADHANI WAMEFANYA HUU KAMA MRADI TU WA KUWANUFAISHA WAO NA JAMAA ZAO KWA NJIA HII AMBAYO INAONEKANA KUWA NI HALALI.
ReplyDeleteVIPI KAKA MICHUZI LILE SHINDANO LA MAN UTD NA ARSENAL LA UTABIRI ULISEMA MFADHILI KASAFIRI JE HAJARUDI TU ILI MSHINDI APATIKANE AU NDO HALIJOJO SIYO.
nadhani kuna haja wa majaji wanaoteuliwa kujudge the contest kutoka nje ya nchi, and be experienced poeple. otherwise ukichukua mtanzania, yatakuwa yale yale, keshachukua rushwa, anampendelea mtu fulani, upeo wetu wa kuchagua ni finyu, hayo ni maoni yangu. swala la kuchukua miss kutoka europe ni gharama, hata vijijini mbona kuna binti warembo, just like face of africa, wanaweza kwenda deep inthe villages and choose the girls they think are qualified,
ReplyDeletehayo ni maoni yangu
Wizara husika ya Habari, Utamaduni na Michezo ishirikiane kwa karibu na Wizara ya Jinsia, Maendeleo ya Jamii na Watoto kusimamia NGO zote zinazosimamia urembo. Kwa sasa hivi NGO hizi ni za ubababaishaji, ulaji na kujinufaisha, na hazizingatii maslahi ya nchi na hawa wasichana. Mbaya zaidi wakati mwingine hata viongozi wa NGO hizi wanaendekeza mabo ya ngono kwa hawa wasichana, kuwaomba wao wenyewe au kuwauza kwa "mapendejee". Na hawa WaHINDi walioja huko kazi yao kutumia Miss Tanzania kufanikisha biashara zao, nasikia hata kuvusha UNGA!!!
ReplyDeletenamuunga mkono huyo aliyesema kuwa kwenue hiyo Kamati kuwe na m Mama flani hivi wa kuwashauri hao maMsiss.
ReplyDeleteLakini sikubaliani na ena pendekezo lake la mama Terry.
Mi nampendekeza Mama GETRUDE RWAKATARE.
hii kamati ivunjwe,tupate kamati itakayo jumuisha watu ambao niwa somi,wenye exposure na wenye uzoefu na haya mambo ya ulimbwende kuwataja wachache ni LUCY KIWELE,MARIA SARUNGI,JENERALI ULIMWENGU,HOYCE TEMU,H.LUNDENGA(AWE MJUMBE TU)NK
ReplyDeletekwani hawa wahindi tunaowaona sahivi wapo kwa maslahi binafsi wao na akina Lundenga.
RX: hii Kamati,
ReplyDelete1. Ina utapia mlo wa tunda la utambuzi wa usawa wa jinsia.
2. Ina mtindio wa madini aina ya 'rika la ujana'
3. Imelemewa na uzito wa tuhuma (ambazo huenda wasingekuwa nazo)tokana na Lundenga kuhodhi kwa muda mrefu kitekinikali mamlaka na hati milki ya kusakanya walimbwende na kusababisha michoko, kebehi na ushiriki hafifu wa Wananchi katika maboresho ya kuwapata Warembo ambao wangetoa ushindani mkubwa duniani.
4.Inauguza macho yaliyozingwa na utando mzito wa ÚDARESALAMISM, kiasi cha kutoona mbali ya wigo bandia.
MNGT:
1.Kamati hii ifutwe hasilani. Iundwe nyingine kwa ushindani wa kuchaguliwa kwa sifa zinazopaswa kila baada ya miaka mitatu chini ya wizara yenye dhamana ya michezo, utamaduni na starehe.
2. Nakubali kuwa ikibidi tusitishe mashindano hata kwa miaka miwili ili kuandaa shindano la nguvu na lenye kumpata modeli mwenye taranta anuawi na kumuandaa vyema.
aidha ndani ya miaka hiyo miwili mjadala na mashauriano yaliyokwenda shule yafanyike ili yumkini SMZ iridhie na kukubali mabinti wao kshiriki katika hii fani.
3.Mashindano ya Kitaifa sasa yaanze mwendo wa mzunguko mpaka kila mkoa uwe mwenyeji wake ndipo turudi Dar -es- salam. Majariwa ya Mola, wenzetu wakiridhia, kituo kifuatacho kiwe Zanzibar!
4. Fani hii iwekewe mkakati wa Kitaifa ikiwa ni pamoja na kufungua mchepuo wa ulimbwende, urembo, mavazi na utanashati mfano katika Chuo chetu cha kule Bagamoyo au kwingineko kuinua vipaji na mwamko nchini.
Ah! wengine nao wamalizie kumponya huyu mgonjwa!
Nyakatakule Unyilisya Echalo
Mimi nahisi hawa watu wamejisahau na majukumu yao na pia kuna wengine hapo wamekuwa humo kwa muda mrefu inabidi wapishe watu wengine watoe michango yao kwa vile yao haisaidii tena. Allawi
ReplyDeleteAnnon number moja hapo juu nkufagilia sana. Umeongea. Mimi binafsi huwa sielewi kwanini Lundenga anang'ang'ana na vibinti hiv vya mitaani wakati kuna wasichana wengi sana walioko ndani na nje ya nchi wenyewe vipaji. Wa ndani kwa Lundenga kwa kweli hawezi kuwalazimisha, lakini kitendo chake kwa mfano, kukataa miss Tanzania aliyechagualiwa UK wa mwaka juzi kuwa eti kuwa hawakufuata utaratibu nilishangaa sana! Wale wa UK wali-organise kama ilivgyo kwa Miss Kinondoni au Arusha. Ilikuwa mufahaka kumruhusu aungane na wenzake kumsaka MISS Tanzania.
ReplyDeleteSijui kiwango cha shule cha LUNDENGA, lakini kama ni form 4 au six au Diploma, tusitegemee mambo ya Angola hata siku moja. Tunahitaji mtu mwenye kuelewa.
michuzi!
ReplyDeletenianze kwa kusema kwamba NANI ANAKUMBUKA FAT? kuna watu walijifanya FAT ni ya kwao mpaka serikali ikawa inawaogopa kabisa lkn leo kidogo mafanikio yameanza kuonekana na utemi aupo tena kwenye mchezo wa mpira wa miguu na sasa tuna TFF safi ingawa wachezaji wetu bado ni walewale hila tunakuwa na moyo sana na timu yetu kwa sasa
USHAURI
naomba sana wadau tubadilishe wakina bugabe wa kamati ya UMISS TZ wakitoka na ukiritimba utaisha na mamiss wa mikoani watashiriki tena wazuri tu lkn kwa sasa wanajua tu wakishiriki ni wasindikizaji kwahiyo wanaona wanapoteza muda wao bure kwenye umiss na sasa ni zaidi ya mwaka wa 6/7 atujapata miss kutoka mikoani kwahiyo inakatisha tamaa kabisa hila tatizo ni mara rushwa ya ngono marahuyu ameadiwa gari mara huyu ajapewa nyumba yake wakati wadhamini ni wengi na viingilio ni vikubwa sasa mimi nasema yafuatayo
1.kuwe na taasisi kamili na sio kamati
2.tuwe na majaji walienda shule sio hawa kila siku na wakuokota tu mitaani
3.kiwe chombo huru kwa kila kitu
nafikiri ujumbe umefika kwa walengwa
ni mimi john mvaa viatu wa michuzi blog
Jamani naomba mnisaidie,naomba kujua hii kamati:
ReplyDelete1.What are their qualifications and skills (specificaly kwa hivyo vyeo mfano mwenyekiti)
2. Wanachaguliwa na nani?
asante
Mdau
Toronto.
Hii kamati itoke kusimamia mashindano haya kwani kwa kuacha umri wa kila mtu na uzee walionao nadhani hata kamati yenyewe ni zee yaani imezeeka miss tz inahitaji ubunifu mpya na si wao tena.....
ReplyDeletewakati wanaanza naamini kwa miaka ya mwanzo walikuwa kila mwaka wanakitu kipya ila walipofikisha mwaka wa nne wakatak na baada ya hapo wanapolomoka hii ni kudhihilisha kwamba upeo wao kwa maswala haya umefika mwisho ...wapunzike jamani hata kama LINO yao.
ReplyDeleteThis is something of national interest, for that reason i suggest:
ReplyDelete1.Skills and qualification of the team to be reviewed- hii itahakikisha tunaweka watu wenye skills na kazi na wanajua nini wanafanya
2.Responsibility bearing- kamati ya sasa hivi haina uwajibikaji hata wakiboronga watu watalaumu tu lakini wenyewe wanaendeleza libenele la ulaji. Lazima kuwe na njia ya kuwa punish ili ku-encourage perfomance.
3.kuwe na limit duration of time to be in kamati and shouldnt be exceeded for no reason.
4. many more..............
*.I hate ponjoro's, kama wanataka kutoa zawadi ya mshindi sio waje na visheria nyao vya kumchagua mtu wao asiye na vigezo ili tu zawadi ibaki kwenye familia yao.
I think zawadi ya gari last year ndo imesababisha yote haya, kama hakuna mzalendo atayetoa zawadi bila masharti ya kumchagua mtu wake bora kusiwe na zawadi lakini tuchague mtu atayeenda kuwakilisha vema.
Michuzi ,
ReplyDeletekamati hii ni vyema ivunjwe kwani imejaa kashfa kubwa za zinaa tupu .
Waziri husika , wadau ni vyema tushirikishwe ili kuiletea taifa katika fani hii ya Miss Tanzania. Kama kamati hii iliweza kukosea kutuma DVD ya Ms Richa to U.K badala China they have to resigne kuonyesha kuwa wamewajibika .
Mdau , Hashimoto
Mimi naona hii kamati yote ivunjwe..haina maana yeyote..nashauri iundwe kama ambayo itajumuisha wtu wa masuala ya urembo wanaojua nini urembo..sio mnatuwekea watu waajabu..toeni hao maponjoro..huyo mhindi ila siku yeye na hakuna mafanikio
ReplyDeleteMbona Lundenga afya inayumba?
ReplyDeleteMniwe radhi nitakaowaudhi. Mimi nimewahi kujihusisha kwa karibu na hizi shughuli za urembo, sasa hivi niko pembeni. Nimeshahudhuria na kushiriki kwenye level ya taifa na kwenye Miss World yenyewe. Inaelekea wengi hamjui mnachokisema. Tanzania si nchi pekee inayoshindwa, kuna zingine hazijawahi kufikia hata Tanzania ilipofikia katika miaka hii michache. Hii Kamati inafanya kazi kama chombo binafsi, na waandaaji wa Miss World wanashirikiana na watu binafsi kwa misingi ya kibiashara na uendelezaji au uhamasishaji wa vipaji vya urembo. hii ni sanaa huria. Hakuna kitu kama hawa ni akina nani, wako wanaume watupu au wazee. Fikira potofu. Anayewaona hawafai aanzishe ya kwake kama alivyofanya Maria Sarungi ambaye mwaka wa kwanza tu kupeleka mrembo Miss Universe, ametikisha dunia. Hakuna nafasi kwa Mtanzania yeyote kupeleka msichana Miss World, hiyo muijue na hakuna mwenye haki ya kuwapora hawa jamaa, walibuni wenyewe na wameijenga wenyewe. Watanzania tuache kulalama bila hata kuelewa tunasema nini. Dunia haiendi hivyo na naamini akina Hashim watakuwa tayari wana haki miliki. Hii Miss Tanzania kama title na fursa ya kushindana ulimwenguni ni hawa jamaa - kwisha. Asanteni.
ReplyDelete"Champions make decisons that create the future they desire.....
ReplyDeleteLoosers make decisions that create the present they desire".
Haya yote ni matatizo ya rushwa ya .... Hao wazee hawaondoki hapo labda muwapige mabomu maana wanajua watakosa kula na ...
ReplyDeletetatizo lao ni watu wa totozi! naona this time waliamua wampe bosi wao chance! we uliona wapi mashindano ya wasichana wadogo, warembo lkn waandaaji ni wanaume tena watu wazima! Albert tulia sasa umri umekwenda, totozi haziishi!!
ReplyDeleteNanukuu msemaji aliyesema yafuatayo:
ReplyDelete"Hakuna nafasi kwa Mtanzania yeyote kupeleka msichana Miss World, hiyo muijue na hakuna mwenye haki ya kuwapora hawa jamaa, walibuni wenyewe na wameijenga wenyewe"
Ndg yangu pamoja na uzoefu wako na uhiari wa wawashiriki katika fani hii, napenda kukuonya kuwa Jamii na Serikali kwa ujumla lazima ihakikishe kuwa misingi ya utu, haki za binadamu, amani na umoja wa kitaifa vinalindwa katika shughuli yeyote ile inayogusa utambulisho wa kitaifa au umma. Haijalishi inaendeshwa na wafanyabiashara au wasio wafanyabiashara. Haijalishi kama una hati milki, umeazima au umepewa kibali au unalipa mrahaba n.k
Makanisa na misikiti yamesajiriwa kwa hiyari yao na si watanzania wote ni wanachama wao lakini bado Serikali lazima ihakikishe kuwa hawahubiri ubaguzi wala chuki wala kuzuia watu kwenda hospitalini wala wasishauri wanachamma wake wasifanye kazi eti mwisho wa dunia umewadia n.k
Wasanii kwa hiyari zao hutunga na kurekodi nyimbo zao na kupata hati milki lakini inafika wakati wanapigwa 'stop' kuimba au kuonesha usanii wao endapo watakuwa wanakiuka niliyoyataja hapo juu.
Tena isitoshe miss Tanzania hupewa bendera ya nchi na mkono wa kheri na kiongozi / viongozi wetu pindi anapokwenda katika mashindano ya Dunia je mpaka hapo bado unaona tu kuwa mazungumzo yeyote ya maboresho kuhusu hii kamati ni ubatiri simply kwa sababu wana hati milki?
Ok! sasa na hati milki yao leo serikali ikitangaza kama Zanzibar kuwa hakuna kuendesha hayo mashindano hapa wala kutumia jina la Tanzania (maana nao wana hati milki yake), Lundenga & the Fellows wataweza kuwakilisha nchi gani?
Nadhani ufafanuzi wako sasa unaunga mkono maneno mazuri ya Anony Nyakatakule kuwa hii kamati ina mtindio na utapiamlo wa aina fulani!
Mkata issues!
Wewe mdau unayejifanya unajua sana Miss World hilo la kwamba Miss World Tanzania ni franchise ya watu bianfsi wenye exclusive rights tunalijua.
ReplyDeleteLakini usisahau kuwa hawa jamaa licha ya kuwa na Exclusive rights za kuendesha Miss World hapa Tanzania pia wana Moral obligations za kufanya shindano kwa haki na busara. After all mwakilishi wanayemchagua anabeba bendera ya Tanzania na anatuwakilisha duniani. Akiwa kule kwenye shindano la dunia hakuna mtu anayemjua Lundenga na hao washkaji zake. Mwakilishi wetu akiwa kule watu wanachoona ni nchi ya Tanzania.
Kwa hiyo hawa jamaa hata kama wana exclusive rights wakiendeleza usanii tunaweza kuwadhibiti kupitia Serikali. Kwani wao nao wako chini ya serikali yetu vile vile.
Kama hujui ni nini nasema uliza Ndolanga na FAT yake ambao walikuwa wanajidanganya kuwa kujificha chini ya exclusive rights za FIFA kungewasaidia kuendeleza uozo.
Richa hakuwa na sifa za kuwakilisha Tanzania, hata kama Kamati ya Lundenga wanataka tuamini tofauti. Mwakilishi wa Tanzania inafaa kuwakilisha Watanzania kama tunavyofahamika ulimwenguni kuwa ni watu weusi, na tunaongea Kiswahili fasaha kabisa duniani.
ReplyDeleteNafikiri ni vema tukaiga mfano wa watani zetu wa jadi Kenya ambao kwenye Miss World Kenya wana kipengele cha Miss India Kenya.
Huyu Richa anafaa kuwa Miss India Tanzania
Lundenga, you can truly borrow a leaf from your conterparts in Kenya. The Miss World Kenya committee has a sub-title called MISS INDIA KENYA which is held together with Miss World Kenya.
ReplyDeleteRicha should be re-crowned as Miss India Tanzania 2007. And who ever was the 1st Runner-up (assuming she's not Indian) must be given her righful title of Miss Tanzania 2007.
Thanks
haya ni mambo ya nuksi tuuuuuuu
ReplyDeletekote duniani wanaohusika na haya mashindn ni mushkush
soma hapa uone kioja cha miss califonia 2007 http://www.abcnews.go.com/Entertainment/BeautySecrets/wireStory?id=3966217
hawa jamaa,hawana jipya. kazi ao kula hela za sponsor kwa manufaa yao. heri iundwe kamati mpya yenye kutuletea maendeleo. huyo lundenga kwanza hata english hajui na nina fikiri huyo lundenga hana hata elimu ya kutosha ameka kiswahili mno. miss world ni kitu sio cha kuchezea inataka uwe exposed enough to the world, which lundenga he doesnt have that.
ReplyDelete