jk akipiga stori na mama fatma abdallah mkali ambaye ni mlemavu toka kijiji cha mloka wilaya ya rufiji ambako jk alitembelea na kuhutubia wananchi katika ziara yake ya kikazi mkoa wa pwani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Shida ni nyingi kwa binadamu lakini ukiongea na Rais mmh! hata kama hajakupa shilingi unapata matumaini ya kuyakabili matatizo.

    ReplyDelete
  2. Napenda kuto shukurani kwa raisi jk kufika kijiji cha mlokaa,sijawahi sikia raisi yeyote kufika pale!!jamani jk anafanya kazi bwana...hongera baba..
    mdau kyekuu

    ReplyDelete
  3. Jamani Mkuu wa Mkoa wa Pwani (hayupo pichani) ananichekesha sana. Ongea yake bwana mmh! utafikiri anawadanganya watu sijui, au hajui kusoma vile.

    Lakini ningependa kujua historia yake na sababu zilizofanya ateuliwe kuchukua nafasi ya Marehemu Mhe. Amina Chifupa kule bungeni, kwanza umri wake unastahili? Pili mmh! katoka wapi kwa vijana toka lini? (Nashangaa kwenye hii picha hakuonekana.)
    Why not VK? at least mchango awake tumeuona.

    Kuna mtoto kule Ukerewe nadhani alitoa point sana, kwa nini mnasema mnaajiri vijana wakati mtu anakuu mkuu wa mkoa hapo hapo mbunge je hakuna vijana wanaostahili? Yule mtoto sijui yu wapi jamani? Ningempa zawadi nono?

    ReplyDelete
  4. Jamani JK siku hizi nae ANAJICHUBUA nini?
    Yaani anakuwa sio mweupe bali wa PINKI. Mpaka anatia raha.
    Kuku bwana! Haziongopi.
    Nakufagilia JK Babake!

    ReplyDelete
  5. Jamani tuwe serios kidogo na tunayosema. Kutembelea kijiji na kufanya kazi kuna uhusiano hapo au uwezo tu wa kutokuelewa. Mtu ukishindwa kuwaongoza Watz basi utakuwa na matatizo. Ni rahisi mno kuwadanganya na siku zikaenda.

    ReplyDelete
  6. ASILIMIA 95 YA WADANGANYIKA WANAISHI MAISHA DUNI NA HAWANA MATUMAINI YOYOTE.
    SWALI:JE JK ANALIELEWA HILI?SIO TU KIJU JUU,YAANI KWELI LINAMGUSA MOYONI??YAANI NDANI YA MOYO KABISA?KAMA NI KWELI NADHANI ANGEKUWA HANA USO WA FURAHA NA ANGEKUWA AMEKONDA KWA HILI LAKUFIKIRIA MAISHA YA WALALA HOI.
    NAREJEA MAISHA YA ALIYEKUWA RAIS WA MAREKANI HUYU SIO MWINGINE BALI NI ABRAHAM LINCOLN HUYU BWANA HAKUWAHI KUPATA RAHA HATA SIKU MOJA TANGU ALIPOINGIA WHITE HOUSE COZ USA NYAKATI HIZO ILIKUWA KTK MATATIZO MAKUBWA IKIWA NI PAMOJA NA VITA(CIVIL WAR) NATATIZO LA BIASHARA YA UTUMWA,HAYA MASUALA YALIKUWA YANAMPA WAKATI MGUMU KIAS KWAMBA ALIKUWA ANAHUZUNIKA WAKATI WOTE NA HILI WAWEZA PROVE KUTOKANA NA MIKUNYO MIKUNYO KWENYE USO WAKE NA HATA AFYA YAKE ILIKUWA NI SKINY(MWEMBAMBA SANA),HUYO SHUJAA ALIPIGANA KIUME KUHAKIKISHA MAREKANI INAKUWA MMOJA NA KUKOMESHA BIASHARA YA UTUMWA.LEO HII TANZANIA TUNA MATATIZO MENGI AMBAYO YANGEMFANYA RAIS MKWELI KUWA KTK HALI KAMA YA HUYO SHUJAA NILOMTAJA HAPO JUU BUT MARAIS WETU KICHEKO NJE NJE KANA KWAMBA HAWAONI MATATIZO MAZITO YANAYOIKABILI NCHI YETU NA NDO MAANA KUENDELEA ITAKUWA NI NDOTO YA MCHANA.NYERERE ALIWAHI KUTAMKA KUWA IKULU NI MAHALI PA GUMU,IWEJE WATU WANAPAKIMBILIA?LEO HII NI AJE MARAIS WETU WANANENEPA MARA BAADA YA KUINGIA IKULU??
    MNAOSEMA BONGO NI TAMBARARE NA WASIKITIKIA KWA SABABU HUO NI UBINAFSI WA HALI YA JUU,INAKUWAJE TAMBARARE WAKATI HALI YA MWANANCHI WA KIPATO CHA CHINI NI DUNI KIAS KWAMBA HANA UHAKIKA HATA WA MLO MMOJA??TAMBARARE MAANA YAKE NI KUWA KUNA HALI YA USAWA IN TERMS OF INCOMEWISE JE HILO LIPO?NCHI ZILIZOENDELEA TWAWEZA SEMA KUWA MAMBO NI TAMBARARE KWA SABABU RAIA % KUBWA WANA UWEZO UNAOLINGANA,SISEMI KIFEDHA BUT MAMBO KAMA MLO,MALAZI,ELIMU HILI NI KWAMBA KILA MTU ANALIMUDU.
    JAMANI TUACHE KUDANGANYANA,TZ MAMBO SI TAMBARARE BALI NI MILIMA NA MABONDE.
    NAWAKILISHA

    ReplyDelete
  7. Hali ya Watanzania kwa ujumla ni ngumu, sio utani, kwani kila siku gharama za kuishi kwa mahitaji yale muhimu tu inazidi kupanda kiasi kwamba shiling elifu kumi kwa sasa hivi haitoshi kwa mahitaji ya siku kwa mtu mwenye familia, yeye mke na watoto acha wategemezi. Hata hao wanaotuita wala mavumbi hawajakosea, kwasababu gani, kwasababu, tumewapa wenyewe kile walichokitaka kwa ahadi lakini hatujawauliza nini walichokifanya, na matokea yake wanatupita na magari yao na kututimulia mavumbi ambayo yanatuacha hoi kwa vikohozi na kukosa pumzi, wao hawoo wanatesa kwa raha zao. Sio wala mavumbi kweli sisi? Sio utani, inauma kwa yule inayomgusa rohoni. Watu wengi hali zao ni duni.
    Swali hapa, je ni nani wa kulaumiwa? viongozi, wananchi au serikali. Je ni nani kati ya hawa ndiye sababu ya kupanda kwa gharama za kimaisha, au kuwa chanzo cha uduni wetu? Huenda kosa tunalo wenyewe, na huenda chanzo cha yote haya ni sisi wenyewe!
    Kama ni viongozi wabovu ni sisi wenyewe tumewachagua, au sio? ni kura zetu ndio zimewaweka hapo walipo. Na kama serikali ndiyo yenye makosa ni kosa la nani, bado ni kosa letu. Serikali ni watu na watu ni sisi! Sheria mbovu, utekelezaji mbovu au tatizo ni nini hasa?. Tatizo ni sisi wananchi kwa kuwabeba viongozi wabovu. Hatuwajibiki kwa kuwauliza kwanini wanafanya hivyo, tunawaogopa kuwauliza, hata kudai haki zetu za msingi. Wapo wameanza kuwazomea, lakini haitoshi, bado tunahitaji moyo wa kijasiri wa kuwahoji, hiki kimeenda wapi, hiki kimetumikaje, na kwanini kodi yako haifanyi kile kilichokusudiwa, kwani wewe unalipa kodi kila ununuapo kitu, unajua hilo, basi iulizie kodi yako inafanyiwa nini.Na tufanye hivi tukielewa kuwa hiyo ni haki yetu. Vinginevyo tutaendelea kulala huku tunabembelezwa na mziki mtamu wa enzi na enzi,..zidumu, kidumu na wadumu..' wewe kalagabahwe...

    ReplyDelete
  8. WATANZANIA ACHENI KUMPIGA MUNGU MAWE. YATAWARUDIA WENYEWE. HALI NGUMU KIASI HICHO HUKO NYUMBANI HAIPO. ULIZENI WAHINDI HUKO UKIZALIWA MASKINI NI MASKINI TU.ULIZENI WAFILIPINO ULIZENI WARUSI,MABOSNIA ACHENI DOMO JAMANI HALI SIO MBAYA HIVYO. TATIZO LETU NI KUTOWAJIBIKA TU. TANZANIA SIO MASKINI MSIDANGANYWE. MTANZANIA YEYOTE AKIFURUKUTA RIZIKI YAKE ANAPATA NAFASI HIYO SEHEMU NYINGINE HAZIPO. NENDA NIGERIA MTU ANAKUTAPELI UKIMPELEKA POLISI UNAFUNGWA WEWE. JAMANI TUKAZE MSULI WAKATI WA KUSUBIRI RIZIKI UMEPITA

    ReplyDelete
  9. Hali ya maisha imepanda kila mahali kwa sababu ya kupanda kwa bei ya mafuta, huo ni ukweli watu wasiotaka kuukubali kwa sababu wameambiwa maisha bora kwa kila mtanzania.

    Na hata serikali ya Tanzania ifanyeje haiwezi kucontrol upandaji wa bei ya mafuta katika soko la dunia, kwa sababu linamilikiwa na wababe, nao hawajali chochote kuhusu maslahi ya watu wengine zaidi ya maslahi yao. Hebu ingieni kwenye mtandao muone hiyo bei ilivyopanda mnategemea hali ya maisha ya Tanzania itashuka wakati tunaagiza mafuta kutoka nje na tena tuna import vitu vingi kwa kutumia pesa za kigeni mpaka toilet pepa na dawa ya mswaki (kwa kuwa tunadhamini vitu vya kutoka nje ya nchi kuliko vya kwetu). Tunapeleka nini nje kutuingizia pesa za kigeni?
    Wengine watasema bidhaa za kwetu hazina ubora lakini hata hizo zinazoingizwa kwa kiasi kikubwa ubora wake unatia mashaka kama tulivyoona kwenye magazeti nyingi ni feki sasa pesa ngapi za kigeni zimepotea? Watu mpaka maziwa wanataka kunywa yaliyotoka nje uimport kila kitu bila kuexport kwa wingi unategemea nini ukichanganya na kupanda kwa bei ya mafuta ndio balaa kuanzia usafiri, usafirishaji wa mazao, viwandani wanakotumia mafuta kuendeshea mitambo kote huko athari ya kupanda bei ya mafuta itaonekana na mwisho lazima imfikie mlaji.

    Wachumi wanaliona hili na wengine wenye uelewa na masuala yanavyokwenda duniani pia wanalielewa lakini sijui kwa nini hawasemi wamekazana na JK sasa afanye amlazimishe Bush aache ubabe, ailazimishe Iran iache mipango yake ya Nuklia au afanyeje maana wagombanapo fahari wawili ziumiazo ni nyasi, sie tunaumia kwa malumbano ya wengine, wao wananufaika kwa kupanda kwa bei ya mafuta kila kukicha.

    Sikatai kuna sababu za ndani pia, (internal factors) ambazo nazo inabidi zifanyiwe kazi mojawapo ni uwajibikaji wa wananchi pamoja na viongozi wao. Hivi tungelikuwa tunafanya kazi kama hao tunaowacheka kila siku kuwa wanabeba maboksi nafikiri tija ingeongezeka, wengi wetu makazini ni wababaishaji, vijijini vijana hawataki kufanya kazi, walioko mijini wanataka kuwa wote wachuuzi, hivi hili taifa la wachuuzi litaendeleaje? Tizama nguvu kazi ya vijana inavyopotea bure mtu anashinda jioni na vitana vya mia tano anauza au sijui kakitu gani amekashika, kumbuka huyo hana mchango wowote katika maendeleo ya nchi haliingizii taifa kipato. Na walio nje nao hataki kuwekeza kwao japo kwa viwanda vidogo vidogo, na wahindi walio na viwanda dola wanapeleka kwao, yoote hayo na yanaleta huo mseto wa maisha magumu.

    Wakenye wenzetu wanaexport kweli nje ya nchi, maua, maharage (green beans) chai yao utaikuta iko kwenye fair trade, vinyago, vikoi, sie tumekalia kulia na JK sasa atufanyeje jamani wakati hatutaki kufungua macho kuona opportunities zilizo tuzunguka?

    Narudi kwa watu wa pwani Rufiji kuna bonde kubwa linamwaga maji baharini lakini watu wake bado masikini wakutupwa. Soko la mboga mboga na matunda liko kama km 170 hapo Dar es Salaam. Nawauliza soko la Kariakoo linalishwa na watu wa wapi kama sio Moshi, Tanga, Iringa na Mbeya kwa nyanya vitunguu, kabichi, hoho na ndizi kutoka huko. Kwanini Rufiji wasiilishe Dar kwa kuanzia na mboga mboga mpaka mchele? Tuunde tume kuchunguza au tulete mzungu aje kufanya utafiti hata hayo???

    Jamani eeh seriously tufanye kazi tuache ubabaishaji, (SIO WATU WOTE LAKINI) mtu unaingia asubuhi ofisini unasoma gazeti saa nzima unafanya kazi kidogo kisha unakunywa chai ya nguvu (kwa wale ofisi zao ziko karibu na feri kwa samaki na chapati na au chapati na mayai na mishikaki), Ikifika mchana unatoka kwenda lunch huko utamaliza saa nzima au na nusu, ukirudi jua limepanda joto balaa hata kazi haiwezi kufanyika, unazuga zuga kidogo kufanya kazi, unawapigia simu rafiki zako au unaingia blogu ya michuzi au JF uone kuna nini humo, hapo utachukua saa nyingine ukimaliza siku imetoka unafunga ofisi unaondoka zako kurudi nyumbani unasubiri kesho, hali ya kesho nayo ni ile ile, JE TUTAFIKA?

    Naomba kuwailisha (najua watu watanila nyama!)

    ReplyDelete
  10. napenda kumchallange KADA,wewe nadhani ni kada wa CCM kama ambavyo umejieleza mwenyewe,ninyi ndo watoto wa vigogo mlio-abroad mkisoma kwa kodi za walalahoi,tanzania umezaliwa masaki nakukulia huko masaki,ukaenda soma Tanganyika Int.xul na baada ya hapo huyo majuu,je wewe utapata wapi nafasi ya kuelewa kundani maisha duni ya mtanzania,jamani kuna watu tumekulia village natunaelewa hali duni hii inayozungumzwa,tusiende mbali pale pele Dar es salaam nenda sehemu kama,Mburahati,mansese,buguruni,mbagala,nenda jionee watu wanavyoishi maisha ya dhiki je wewe KADA hulioni hilo?acha ubinafsi ndugu yangu.okay umesema kwamba kila Mtz ana nafasi ya kuprosfer hili sio kweli kuna watu wanajitahidi sana kufanya hivyo but still kama haupo kwenye system and no body knows you its gonna b hard.watu wanamaliza chuo kikuu na hamna ajira wewe unataka wafanye nini?kazi nyingi ni kujuana kama huna God fathers umeliwa utasota hadi ukome.niambie aslimia 75 ya watu wanaoishi vijijini watajikwamua vipi na maisha magumu,kweli watalima pamba,kahawa,chai,korosho,machungwa,mananasi je kuna soka la uhakika la kuuza mazao hayo?plz KADA NIJIBU,JE WAMEWEZASHWWA KUEDESHA KILIMO CHA KISASA?ACHA UZUSHI KADA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...