timu ya taifa ya bara kilimanjaro stars imeibenjua somalia 1-0 katika mchezo wake wa pili wa chalenji kwa nchi za afrika mashariki na kati. mfungaji alikuwa ni mike chuma (pichani) katika dakika ya 56 baada ya kupewa pande na nizar khalfani nje ya 18 na kuachia mkwaju mkali uliokwenda kimiani moja kwa moja. mpira umeisha dakika kama 10 zilisopita, hata hivyo bado kiwango cha mchezo wa staaz si cha kufurahisha sana kwani pamoja na ushindi huo wapenzi wamelalamika fomu ya vijana hao...


Somalia sio nchi ya kushangilia ushindi. Nchi haina serikali kwa mwaka wa 20 sasa tunachekelea ushindi wa 1-0??
ReplyDeleteTatizo sio fomu.Kwani fomu inaweza kuwa mbya siku mmoja na ikabadilika mcehzo mwingine.Tatizo ni kwamba timu ni mbovu sana na hakuna nayediriki kusema ukweli.Maximo ameishiwa mbinu au wachezaji aliowachagua ni wabovu.Waandishi wa habari ondokeni kwenye coma na muulizeni huyu kocha maswali magumu kuhusu timu yake.Kwa standard niliyoiona timu haifiki mbali.Timu ya Somalia ni timu ya kuokoteza wachezaji kutoka sehemu mbali mbali na bado tunashindwa kuwafunga kisawa sawa.Kagoli kamoja ka mbinde.It is time to wake up and smell the coffee.
ReplyDeleteAsante sana Michuzi, maana niliku anataka kumuona huyu Mike Chuma, kumbe ni kijana anye vutia , yaani wa kileo, nili wahi kumuona zamani, ila nilikwua sijui ama ni yeye, asante
ReplyDeleteNow I believe that we don't have a coach, and therefore we don't have a team, this is nonsense. Huwezi kuwaacha wachezaji bora waliojikusanya Simba na Yanga halafu ukategemea miujiza. Tabia ya watu kuchukia wachezaji wanaotaka timu hizi mbili ni kutokujua mpira wa Tanzania. Hizi timu ndizo hukusanya wachezaji bora wa taifa letu, ukiwaaacha umeacha wachezaji bora, basi!!!
ReplyDeleteKweli watoa maoni hapo juu hamjui mnachokiongea, ule umaarufu wa simba na yanga hauna kitu, kitu ni ushindi tu, sasa kocha kawaletea ushindi nyie bado mnaongelea wachezaji wa simba na yanga ambao miaka yote walikuwapo na taifa stars ilikuwa ikifungwa na kila kibonde.
ReplyDeleteKocha wa timu ya ugiriki iliyoshinda last european cup alikuwa anapata criticism pia kuwa timu yake inacheza mchezo wa kizamani, yeye alijibu mchezo wa kisasa ni ushindi na timu yangu imeshinda kwa hiyo inacheza kisasa.
Tuwape support wachezaji wetu na tuwaambie waongeze biddi, lakini kuwaambia hawana kitu wakati mechi mbili walizocheza wameshinda ni mambo yaleyale yakufurahia kufungwa na kusema lakini chenga tumewala, ni wakati umefika wa kupima watu kutokana na perfomance na majibu sio mbwembwe au sura nzuri.
Hata Msomali katubana!!!
ReplyDeleteDuh! Kuwafunga Somalia bao moja tu ni aibu ya hali ya juu ukichukulia kwamba sisi tulikuwa na maandalizi ya muda mrefu katika kampeni za kwenda Ghana na kocha anayelipwa mafedha chungu nzima. Somalia ni nchi ambayo haina siri kali na wanauana kila kukicha na hawakuwa na maandalizi yoyote ya maana.
ReplyDeleteHii timu haionyeshi kama itaweza kufurukuta katika safari ya SA hapo 2010.
Kichwa cha mwendawazimu kama kazi.
We anony wa 11:31 ndo kumbe hujui kitu,hivi weye kwa mtaji huo unadhani tuna timu hapo?Nadhani hata kocha sasa kwa wengine tushaanza kuwa na wasiwasi nae huyu ni mbabaishaji tu,kuna Mtanzania mmoja aliwahi kuishauri TFF isimwachie achague timu peeke yake ahusishe hata makocha wazalendo na waandishi wa habari za michezo lakini hili TFF hawalioni!kwa timu hiyo hata chalengi tutaishia robo fainali kwa baba Madiba ndo kabisa tufute mawazo!
ReplyDeleteNdugu watanzania.Tupende tusipende hatuna wachezaji nguli katika muongo huu.Ni mara kibao kocha ame recrut wachazaje wa simba na Yanga lakini yaleyale (Hawana kitu ndungu yangu).Tutabadilisha makocha tutabadilisha wachezaji lakini ola hamna kitu.Kumbukeni enzi za akina Zamoyoni waliweza kupasua ngome wanavyotaka lakini leo wachezaji kama hao wako wapi?Mta bisha bure,hata kama wewe unaijadai kumsaga kocha wakupe hiyo timu ya Taifa sanasan utadumu wiki tu.Na nawathibitishia bora huyo kucho amejaribu kuwakumbuka wachezaji wa mikoani na pia mbalimbali kuliko kocha mwengine aliewahi kuifundisha taifa.Yanga na simba pia uozo tuu.Tuendelee kuwa na maumivu ya kisoka labda kwa miaka 20 ijayo.endeleeni kulumbana,fukuzeni wachezaji,fukuzeni kocha,jifukuzeni wenyewe but HATUNA VIPAJI.
ReplyDeleteMaximo kajichokea, hana jipya wala manufaa yeyote. Na hapo ndo mjue wabongo jinsi tulivyowababaikaji. Kwa timu hiyo tuliyo nayo, mwisho wetu robo fainali. Tunao makocha wazuri hapa ambao wanaweza kuelewana hata lugha na wachezaji wetu na wakafanya maajabu lakini mnawabania. Aliongea Mziray kuwa serikali ijaribu kuwawezesha kama inavyowawezesha hao makocha wa kigeni ijionee habari yake! Lakini jiii!!! mpaka leo. Maximo anakula raha mjini hapa minyau kwa sana, mishahara mingi, na lazima atakuwa anapeleka kwao, lakini kama wangepewa wazawa mshiko ungebaki hapahapa na kuendeleza nchi yetu na soka lingekwenda juu. Akina Tenga amkeni sio enzi zile za akina Ndolanga, jengeni heshima kwa kumstukia mbangaizaji huyu Maximo. Unawaacha wachezaji kama akina Kaseja, Machupa, Kaniki, Nsajigwa n.k unategemea nini. Lazima tuwe wakweli. Leo hii mzawa Mkwasa kapewa timu ya wanawake amekuwa kama yatima hakuna msaada wowote! Hata akipiga ukelele hasikilizwi lakini angekuwa foreigner hapo ungeona habari yake. Aaa Acheni Hizooo.
ReplyDeleteTatizo nyie watanzania mnataka mcheze mpira kama wa wabrazil.Kweli manachekesha ndungu zangu na poleni.Kwa taarifa yenu,huo mpira mnaocheza ndio kiwango chenu.kwani huyo kocha mnaemlalamikia amewashusha au amewapandisha kwenye kiwango/rank ya FIFA?Watanzania nyie mnahitaji miaka 30 zaidi ili muweze kupata maendeleo ya mambo mengi wala sio soka tu.mjifikirie ni nini mko juu?ni Elimu (kiwango chenu je,enrollment per year,wahitimu je?),Afya (Leg-head mix operation),Madini?(mikataba ya London)Miundo mbinu (Maujaji tu wanalala uwanja wa ndege mwezi,Dar ni mashimo),Maji(Mawaziri awalipi bili),Umeme(IPTL,Richmond saga,giza nchi nzima)MNAHITAJI MUDA NDUGU ZANGU.NADHANI BORA SOKA MNAJITAHIDI.
ReplyDeleteMimi ni mnigeria,nafanya tafiti UdSM.
Huyu anaonymous wa hapa mwisho kanichekesha kweli, ingawa kweli Tz tumechoka lakini imebidi nicheke kwa data zake za kiudaku-udaku.
ReplyDeleteDa! hii inapendeza nakumbuka ktk makala au habari za nyuma tuliongelea sana huyu kocha mpya na value for money lakini kuna watu waliopinga na kuona tunaongea utumbo sasa nafikili yanajionyesha na kuna kila sababu ya watu kulalamika kocha analipwa vizuri lakini mabadiliko ni kiduchu yaani washikaji mpira wanaocheza ni bora liende!!!!!
ReplyDeleteMpira wa sasa umebadilika, hao wajinga wote wanaojidai wanaweza kufundisha vizuri walishafundisha na hawakuinua uwezo wa timu hii zaidi ya kujaza majungu,urafiki na upendeleo wa wachezaji wa hizi timu mbili za mitaani hapa Dar. Timu ya sasa ni nzuri na ni mchanganyiko wa vijana wenye ari na nia ya kufanya vizuri.Hao wachezaji wenu ambao hawana nidhamu hatuwataki ktk timu, watatuletea matatizo wabaki huko huko, na nyie mnaowapigia debe/chepuo hamna nia njema.
ReplyDeleteMaximo endelea na kazi ya kujenga timu. achana na washamba wa hizo Yanga na Simba hawana mpango timu zao zinawashinda kuziendeleza halafu wapewe national timu. njaa inawasumbua na watakiona mpira umechange watalipwa watendaji sio wasimama milangoni na viongozi uchwara. Timu ipewe muda na sasa ndio tuna wachezaji sio wahuni.