Maafisa wakuu 19 wapandishwa vyeo JWTZ
Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange tarehe 15-oct-07 aliwavisha vyeo vipya maafisa wakuu 19 wa JWTZ ambao walipandishwa vyeo hivyo na Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete.
Maafisa wanane kati yao wamepangiwa nyadhifa mpya.
Waliopangiwa nyadhifa mpya ni pamoja na Meja Jenerali Wynjones Kisamba aliyekuwa Kamanda wa Brigedi ambaye ameteuliwa Mkuu wa Kwanza wa Kamandi mpya ya Majeshi ya Nchi Kavu ambayo inaundwa kwa mara ya kwanza tangu JWTZ lianzishwe mwaka 1964.
Maafisa wengine waliopangiwa nyadhifa mpya ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanawake Jeshini, Meja Jenerali Zawadi Madawili ambaye anakuwa Mkuu wa Tawi la Mgambo, Brigedia Jenerali Vicent Mritaba anayekuwa Kamanda wa Brigedi na Brigedia Jenerali Charles Jitenga ambaye anakuwa Kamanda wa Brigedi badala ya Meja Jenerali Kisamba.
Wengine ni Brigedia Jenerali Patrick Mlowezi ambaye anakuwa Mkuu wa Shule ya Huduma, Brigedia Jenerali Charles Mzanila anayekuwa Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Mazao, Brigedia Jenerali Lilian Kingazi kuwa Mkurugenzi wa Utumishi Jeshini na Brigedia Jenerali Grace Mwakipunda kuwa Mkurugenzi wa Masuala ya Wanawake Jeshini nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Meja Jenerali Madawili.
Maafisa Wakuu waliobaki ambao wanaendelea na nyadhifa zao za awali ni Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Meja Jenerali Alfred Mbowe, Kamanda wa Brigedi ya Mashariki, Meja Jenerali Servas S. Hinda na Ma-Brigedia Jenerali Kelvin G. Msemwa, Albert Kigadye, Sebastian Chiwangu, Daniel Igoti, Salum Kijuu, Farrah Mohamed, Gerald Kiswaga, Julius Mbilinyi na Mabula Mashauri.
Kwa habari hizi na zingine za JWTZ tembelea bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. mbona 'diskriminesheni'waislam wako wapi?

    ReplyDelete
  2. Hapo inatakiwa shule. Wakati wakijiunga na jeshi hawa unaowasoma hapo juu, waislamu walikuwa wamelala. Labda sasa hivi ndo wameamka. Time tu itasema kila kitu.

    ReplyDelete
  3. Hapo inatakiwa shule. Wakati wakijiunga na jeshi hawa unaowasoma hapo juu, waislamu walikuwa wamelala. Labda sasa hivi ndo wameamka. Time tu itasema kila kitu.

    ReplyDelete
  4. Kaa, kuna wanaume huko kwa kweli! Najaribu kufikiria hawa jamaa wakikutana sehemu moja inakuwaje hapo? Panapendeza sana

    ReplyDelete
  5. wewe acha ushamba...unataka ugundue kuwa kuna waislam kwa majina???? mbona kuna majina ya asili kama Masanja,Rwegoshora n.k. nayo pia yanaashiria uislam au ukristo??? Usiwe mtumwa wa majina..

    ReplyDelete
  6. Hizi Mission au Vision zilishapitwa na wakati. Kulinda mipaka, tunapigana nani siku hizi? Adui gani na yuko wapi? Maadui wetu ni ujinga, umaskini na maradhi hasa ya UKIMWI. Formulate mission za namna hiyo

    Ulinzi wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya adui.

    Kutoa mafunzo ya kivita kwa maafisa na askari ili kumshinda adui.

    Kutoa msaada unaohitajika kwa mamlaka za Serikali katika hali ya hatari na maafa yatokanayo na nguvu za asili.

    Kusaidia uwezo wa mamlaka ya Serikali katika kudhibiti ghasia au vurugu ndani ya nchi.
    Kuendesha na kusimamia mafunzo ya mgambo.

    Kushiriki katika shughuli za kulinda amani duniani.

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Charles Jitenga ulistahili kupata hicho cheo maana ni mchapa kaza sana hapa makao makuu ya jeshi tulitamani sana upate hicho cheo kwa utendaji wako wa kazi mzuri.

    Anony: acheni mambo ya udini hivi vyeo vinaendana na kisomo cha mtu na utendaji kazi mzuri.

    ReplyDelete
  8. Hii nayo mpya! We annon Friday 18 12:33 umeshangza sana. Badala ya wewe mwenyewe kujitahidi upande ufike huko unasema ilikuwa unatamani mwenzako apande!? Hiyo hali sana Duniani haipo. Lbda kama ni mmeo!

    ReplyDelete
  9. huyu ni Jitenga yule aliyekuwa mkuu wa kikosi cha musoma? kule Makoko? kama ndie namfagilia kiafande! Jamaa mtu poa sana, ameenda shule alafu katulia, mjeshi wa uhakika, kama ni wewe kaka Jitenga tukutane afrilux hotel siku moja nikununulie walau lunch na bia moja!

    ReplyDelete
  10. Vyeo vya nini bwana?Wakati sisi Tanzania 'christendom'ni mmoja wa nchi maarufu za wapenda rushwa,wapokeaji zakaa kutoka magharibi na hata mashariki ya kati,tuko nyuma kielimu na hata matibabu muhimu wanatusaidia India,basi tusijivune...ni dua za Waislamu zilizoiweka taifa letu salama au hali yetu ingekuwa kama ya Burundi,Rwanda ,Congo nk...

    ReplyDelete
  11. Anony wa 11:49,bora Waislamu wamelala,wakiamka...jitahadhari,wewe baki nje tu ukiosha mitungi ya wazungu na kudoea makaratasi ya kuishi marekani / ulaya.

    ReplyDelete
  12. We annon Jan 19 6:14, kama bado walilala wanategemea wataamka, wakati huo wenzao watakuwa mchana katikati! Kusotea makaratasi ni sawa na wewe unayesotea chochote unachofanya hapo bongo. Hakuna tofauti. Mwenzako nina uhakika wa umeme na kula, wewe mashaka kila siku! Wote Watanzania

    ReplyDelete
  13. Bora nife maskini kwangu hapo ubongo nyumbani nikiwa bado nimelala na uhuru wa maarifa ya kupata riziki halali kuliko utoro na kuwa mchana katikati ambao mmefungwa na minyororo ya kudoelea cha wengine...endelea kusafisha vyoo na vyombo vya mzungu...na mengineyo!!!

    ReplyDelete
  14. We annon Jan 19 7;38 UTAKUFA BURE NA KIJIBA CHA ROHO. NAONSHA VYOMBO HUKU, LAKINI NIKIJA HUKO NAKUAOLEA DADA YAKO. UTAKULA PESA YA POSA YA VYOMBO NA MA-BOX HUKU. SHAURI YAKO WEWE LIA LIA TU HAPO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...