KABLA HAJATANGAZA JK KASEMA VIONGOZI WA MUDA MREFU WAMEOMBA KUPUMZIKA AMBAO NI:

1. JOSEPH MUNGAI

2. KINGUNGE NGOMBALE MWIRU


BARAZA LENYEWE NI:

1. WAZIRI OFISI YA RAIS (UTAWALA BORA SOFIA) SIMBA

2. WAZIRI OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UMMA) HAWA GHASIA

3. WIZARA OFISI YA MAKAMU WA RAIS (SHUGHULI ZA MUUNGANO) MOHAMED SEIF KHATIB

4. WIZARA YA UTALII NA MAZINGIRA DK. BATILDA BURIANI

5. WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS (SERA NA URATIBU WA BUNGE) PHILIP MARMO

6. WIZARA YA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA STEVEN WASIRA

7. WIZARA YA FEDHA MUSTAFA MKURO NA MANAIBU NI JEREMIAH SUMARI NA OMARI YUSUF MZEE

8. WIZARA YA AFYA PROFESA DAVID MWAKYUSA NAIBU NI AISHA KIGODA

9. WIZARA YA ARDHI JOHN CHILIGATI

10. ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI PROFESA JUMANNE MAGHEMBE NAIBU GAUDENSIA KABAKA NAIBU NI MWANTUMU MAHIZA


11. WIZARA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA SHUKURU KAWAMBA NAIBU NI DK. MAUA DAFTRI

12. WIZARA YA MIUNDO MBINU ANDREW CHENGE NAIBU DK. MAKONGORO MAHANGA

14. WIZARA YA UTAMADUNI NA MICHEZO GEORGE MKUCHIKA NAIBU JOEL BENDERA

15. WIZARA YA KAZI NA AJIRA POFESA JUMA KAPUYA NAIBU HEZEKIA CHIBULUNJE

16. WIZARA YA MAJI PROFESA MARK MWANDOSYA NAIBU CHIZA

17. WIZARA YA KILIMO NA CHAKULA MATHAYO DAVID MATHAYO

18. WIZARA YA MENDELO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MARGARETH SITTA NAIBU NI LUCY NKYA

19. WIZARA YA UVUVI NA MIFUGO JOHN POMBE MAGHUFULI NA MANAIBU NI
SHAMSA MWANGUGA NA EZEKIEL MAIGE

20. WIZARA YA MAMBO YA NDANI LAWRENCE MASHA NAIBU NI HAMISI KAGASHEKI

21. WIZARA YA MAMBO YA NJE NI BERNARD MEMBE NAIBU SEIF ALI IDDI

22. WIZARA YA NISHATI NA MADINI WILLIAM NGELEJA NAIBU ADAM MALIMA

23. WIZARA YA SHERIA MH. CHIKAWE

24. WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA DK. HUSSEIN MWINYI NAIBU DK EMMANUEL NCHIMBI

25. WIZARA YA AFRIKA MASHARIKI DK. E. KAMALA

26. WIZARA YA VIWANDA NA BISHARA DK. MARY NAGU NAIBU CYRIL CHAMI


KUNRADHI WADAU, KUNA WIZARA SIKUTAJA JINA NA JINA LA KWANZA LA MH. NKYA PAMOJA NA NAIBU DK. EMMANUEL NCHIMBI. SAMAHANI KWA USUMBUFU HUO NA WOWOTE UTAKAOGUNDULIKA KWANI NILIKUWA NAENDA KWA SPIDI 12O...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 104 mpaka sasa

  1. Hana jipya Kikwete.Anyway, u r doin'a great work Michu... Thanx 4 the info... Sura nyingi ni zile zile..more than 3/4 ni wale wale... Its a new wine in the old bottle... Will neva work out... Though namsifu kwa kumtoa mama Meghji...

    ReplyDelete
  2. asante kwa breking news, ila namba 22. hukuweka wizara husika.

    ReplyDelete
  3. MICHUZI,

    HABARI AISE. WEWE JAMAA NI 'SHARP'. MAANA NAFUNGUA TU BLOG NASOMA POSTING YA KWANZA, SIJAKAA SAWA UMESHSTUMA YA PILI, KUHUSU BARAZA LA MAWAZIRI.

    SAWA MZEE, ENDELEA KUTUPA HABARI ZA BONGO.

    MDAU

    ReplyDelete
  4. Maskini Lowasa na mama meghi. Sasa ina maana hawa ni wabunge tu wa kuwatetea wananchi?

    Sasa makosa yakifanywa tume iundwe na hawa waliotolewa kuwachunguza waliochaguliwa sasa.

    ReplyDelete
  5. Mramba, Karamagi, Msabaha, Meghji, Mungai, Kingunge, Rita Mlaki, Juma Ngasongwa wote nje.

    ReplyDelete
  6. JK bado safari ndefu anayo, hakuna tofauti kubwa na baraza lilolo pita

    ReplyDelete
  7. najiunaga na wantazania wengine wengi kumpongeza rais kwa nia yake thabiti ya kutuletea maendeleo!!!!!! Pia najiunga na mamilioni ya watumiaji wa blog hii kumkubali michuzi kuwa yuko fit na ni mwandishi wa habari ambaye yuko fastest kwa sasa kuliko mwingine yeyote tanzania!!!!! HEKO MICHUZI...... The speed of calculator!!!

    ReplyDelete
  8. Good selection. BUT nina wasiwasi na Andrew Chenge na Juma Kapuya. Sijui wamerudishwa kwa nini. Labda ndio hoja aliyosema raisi ya kuretain wazee.
    Pia nampa pole Magufuli, sasa ataanza kunuka samaki. Madili ya nyumba itabidi asahau kabisa.

    Kuhusu jenda issue....BRAVO KIKWETE!!!

    ReplyDelete
  9. Ngeleja ni wasziri wa nini na Malima ni naibu wa nini?

    ReplyDelete
  10. MAFISADI CHENGE NA KAPUYA..WAMERUDISHWA NAONA..

    ReplyDelete
  11. Ahsante Michu - lakini unaharaka kaka yetu na wewe??? Kisa kuwa wakwanza kutoa breaking news. Mhh... yatakushinda. Hadi umesahau kuandika wizara za mawaziri wengine. Hata hivyo ni kwa furaha kubwa na shangwe kuwaona watu wanao-deserve 100% kupata wizara za maana na haswa Batidla kuwa full Waziri na Hussein kupewa madaraka mazuri. She is a good woman and he a good man. Kikwete can be smart at times!!! Mhh....

    ReplyDelete
  12. Hakuna jipya lakini angalau kidogo amepunguza baraza lake

    ReplyDelete
  13. bazara poa, hawa nao wangen,goka A chenge C wassira na kapuya. sheka

    ReplyDelete
  14. michu No 22 ni wizara gani? ila nimefurahi kuona amepunguza balaza lake ila watu ni wale wale

    ReplyDelete
  15. kwei kikwete hataki utani,maana ni kawakimbiza wengi nishai....ndio vizuri,tumeshachoka na wizi wa umma

    ReplyDelete
  16. asante michuzi yaani nilikuwa hewani nikikusubiri wewe tu!! baraza linatisha sioni kama linaweza kazi. Vipi Anna kilango na Harison mwakyembe?

    ReplyDelete
  17. JAMANI HUYU ANDREW CHENGE AMERUDI KUFANYA NINI??????????????? UHHHHU WII!!!!!



    1. Zakia MEGHJI OUT
    2. RITA Mlaki OUT
    3. BASILI Mramba OUT
    4. JUMA Ngasongwa OUT
    5. BAKARI Mapachu OUT
    6. Msolwa OUT
    7. ZUBEID MHITA OUT

    ReplyDelete
  18. Wa TZ, namba 12 na 15 vipi hawa?

    ReplyDelete
  19. eh! dialo kapejwa? na mama meghji?

    ReplyDelete
  20. Ina maana twiga star wamepigwa chini? simuoni mama meghji au ndio mambo ya epa???? teteteee jk kweli ni thoooooooo,,,wizara ya fedha ni nani mkubwa??

    ReplyDelete
  21. Kweli Tumekwisha jamani yaani Kikwete anatoka na Baraza la Mawaziri la watu 60 anaamua kuweka watu 50?? Mbona watu kibao namna hiyo?? Hivi Kikwete hutusikii sisi wananchi wako kuwa hatutaki serikali kubwa ambayo inagharimu pesa nyingi sana kuiendesha??

    ReplyDelete
  22. Mkuu Michuzi tunashukuru kwa hili, lakini uliandika ukiwa una haraka, maana umesema kuna wizara 29, ila umetoa 25 tu, pia angalia majina kama William Ngeleja na Naibu kighoma Malima hakuna wizara, please tusaidie tulio nje ya TZ twafa kwa kuataka habari.

    ReplyDelete
  23. KINGUNGE NAKUBALI AMEKUBALI KUACHIA NGAZI ILA MUNGAI NA HAKIKA ALIPATA HOFU KWAMBA THIS TIME ATATUPWA WIZARA GANI KWANI HIYO YA MAMBO YA NDANI ALIKUWA KAMA VILE YUPO SHIMONI HASIKIKI KABISAAA KELELE KUFURUKUTA ZOTE ZILIKUWA BURE!!

    ReplyDelete
  24. kaka michuzi mbona umelipua kwenye kuandika?hapo namba 22 mbona tunaona majina tu bila kutuambia ni mawaziri wa wizara gani?rekebisha kaka!

    ReplyDelete
  25. ohh! still is big

    ReplyDelete
  26. jamani watanzania nisifurahie hao walioachwa wanapewa ubalozi soon!! subirini

    ReplyDelete
  27. michuzi umechapia baadhi ya sehemu...hujatuambia ngekeja na malima wako wizara gani...ila kwanini kikwete amemuacha chenge???

    ReplyDelete
  28. I would like to know the SECRET behind CHENGE??????????????

    ReplyDelete
  29. Chenge wa nini tena?

    ReplyDelete
  30. Hizo nyingine mi sisemi,

    lakin sijaelewa na kufurahi kuhusu wizara aliyopewa Bwana pombe magufuli john,

    Yule jamaa anafaa wizara zenye uozo azishughulikie, chiligati hataweza

    ReplyDelete
  31. WEWE UNAESEMA BARAZA HALIFAI TUPE SAFU YAKO SASA HIVI!!!

    ReplyDelete
  32. Michu,
    Nasherekea ushindi wa kuanguka kwa Zakia Meghji, Ritha Mlaki na Basil Mramba hapa nilipo

    Pia napongeza hatua ya kutuachia wasema hoja wetu bungeni, la sivyo angetuharibia kamati yetu

    Ikiwa ndo tumemaliza uchaguzi...sasa kazi inanza

    ReplyDelete
  33. HALIFURAHISHI,NI BARAZA LA KIRAFIKI
    ZAIDI,HAKUNA CHA AJABU TUSITEGEMEE MAAJABU

    ReplyDelete
  34. Masahihisho kidogo

    Waziri wa maji, kilimo na chakula ni Mhe. Msola naibu wake ni Mh. Mathayo.

    ReplyDelete
  35. ok wizara zinetufikia lakini naona kuna wizara mbili tatu zingweza kua pamoja.wizara hizo ni
    nadhani wizara ya sayansi na teknolojia ingeweza kuibeba hile wizara ya miundo mbinu hapo tungeweza kupunguza matumizi kiasi flani.
    nyingine ni wizara ya kilimo na chakula ingeweza kuibeba wizara ya uvuvi na mifugo.tena naona hii wizara ya uvuvi na mifugo imepewa ma naibu wawili akati ungetaka kupunguza gharama ungeweka wizara ya kilimo,chakula na mifugo ingekuwa poa tu kwani hizisekta ziko kwa ukaribu na uvuvi ungewekwa ndani yake tu.
    hayo ndio mawazo yangu na imekuwaje hile wizara mashughuli ya nishalti na madini sijaiona hapo juu imefutwa nini kaka michuzi?

    ReplyDelete
  36. WILLIAM NGELEJA; NAIBU ADAM MALIMA ni mawaziri wa issuez za Buzwagi? Weka list ya waliomwagwa!

    ReplyDelete
  37. UNITED KINGDOM OF TZ
    (1)Adam Kighoma Malima
    (2)Dk.Hussein Mwinyi
    (3)Masha

    ReplyDelete
  38. Safi sana Bro michuzi kwakuwa fast sana kutu update kuhusu hili baraza..nimeona baadhi ya vijogoo wapo bado wameng'ang'ania
    Andrew Chenge nashangaa sana kumwona kwenye baraza
    Juma kapuya nae si akapumzike tu
    Ngeleja naona kama the post is too senior to be handled by him..anyway ni mtazamo wangu tu

    ReplyDelete
  39. Kaka Michuzi you are very smart!!!
    ni alamost 5 minutes baada ya JK kumaliza kutangazo nikaiona kwenye blog. You are very reliable,
    JK amewapa shavu kina mama kwenye ofisi yake

    ReplyDelete
  40. Baraza safi, ila kwa kumhamisha Magufuli amechemsha

    ReplyDelete
  41. Usichoke Kuposti

    Tegemea critiques na comments kibao kutoka kwa wadau.

    Jamani nyiye wabeba boksi mkitoka kwenye boksi mmechoka mnakuja kucharua na kutapika maneno yenu humu,wanaotoka kwenye bangi nao ndiyo kabisaaa.

    Kikwete kateua amekwishawateua kama huwapendi, kateue wakwako nyumbani kwako.Mnachonga na mtachonga sana wabongo mwaka huu.Mbongo ni mbongo tu hata akiwa mwezini haachi jungu.

    ReplyDelete
  42. asante sana kaka michuzi, ila naomba ukipata muda utupe cv za hawa mawaziri wote, na ikiwezekana utuandikie majina yao in full, ili usaidie watanzania ambao hawaishi nyumbani kwa sasa waweze kuelewa zaidi, kazi njema mungu akubariki.

    ReplyDelete
  43. Jamani mbona Lowasa kaachwa tena, kwani yeye si alijiuzuru Uwaziri Mkuu na siyo Ubunge,naona hawajamtendea haki,angepewa tu hata wizara akishindwa ndiyo atolewe nje.

    ReplyDelete
  44. tunashukuru kwa kutupashahabari hizi za baraz Lakini kuna kosa moja umefanya, umekurupuka kuyaweka majina ya mawaziri na manaibu wao bila kutaja wizara mfano WILLIAM NGELEJA NAIBU ADAM MALIMA. Accuracy, clarity ni mambo muhimu ya kuzingatiwa katika uandishi. Mara nyingine usifanye kosa kama hili.

    ReplyDelete
  45. Hivi Sumaye siyo Mbunge!!Kama ni mbunge alifaa kupewa Kilimo ama Biashara kwani alikuwa Marekani akisomea Shahada ya Uzamili katika Uongozi Na Biashara

    ReplyDelete
  46. Mawaziri;- Dr.Kamala, Ngeleja, Masha na Dr.David Mathayo ni vijana zaidi katika baraza hili na bila shaka walikuwa kwenye kipindi chao cha kwanza cha ubunge. Nawapongeza na kuwatakia kazi njema. Rais Kikwete ameamua kuwapa shavu vijana kuingia kwenye Baraza.
    Excellent JK

    ReplyDelete
  47. Hapa lala michuzi nimekuvulia kofia kwa jinsi ulivoimuvuzisha ishu kwa speed...ile namalizia kulisikia live kwenye redio,kufungua michuzi ipo...au ulipewa in advance nini?Kweli unastahili pongezi kwa hili na mengine.Mjadala wa baraza hili baadae...Uncle Chenge amasevu,du!

    ReplyDelete
  48. Sawa kuna sura mpya katika baraza la mawaziri lakini kuna mapungufu hakuna CHACHU.Kwa wale wanaopika maandazi ,vitumbua wanaelewa nini maana ya CHACHU au amila kama hakuna amila katika unga unaoutayarisha kwa ajiri ya vitumbua au maandazi hata ubadilishe unga mara ngapi matokeo yatakua yale yale.Hapa cha kubadirisha sio unga tu bali CHACHU {amila}Hapa Rais amebadili unga tu.Chachu inayotakiwa hapa ingelikua vizuri kama katika baraza ili kukawa na mawaziri kutoka katika upinzani kwani wao ndiyo walioibua kashifa ambazo mawaziri na wabunge wa CCM hawakuziona.Hii inafahami ya kua wabunge na mawaziri wa CCM kitendo cha kukosoana hakipo kabisa kwani maamuzi yao ni ya jumla.Maamuzi yakitoka juu ya kua mfano Lowassa kiongozi safi wate watasema kweli ni safi kuliko wote,kama kauli itasema ni fisadi waote watajibu kweli ni fisadi kuliko wote.Katika hali hii hakuna lolote.Kama kungelikua na mawaziri kutoka katika kambi ya upinzani wasingelikaa kimya kuwakemea au kuwaonea aibu mawaziri Wa CCM wanaokwenda kinyume kinyume cha taratibu ana kadhalika Mawaziri wa CCM wasingeliona aibu kuwakemea Mawaziri kutoka kambi ya upinzani katika hali hii kunakua na challenge na discussions ambayo inazaa matunda.Hii ndiyo chachu inayotakiwa .Hapa imebadirishwa ijini ya gari lilonoki kwa sababu ya mafuta mabaya na kuendelea kutumia mafuta yalele.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  49. Duuh! Mambo hayo. Yaani na naniihii amechwa? Kwani na yeye yupo kwenye hao Maofisadi?

    ReplyDelete
  50. Mpira ulikuwa mkali sana. Sasa tupo kwenye extra time, score ni mbaya kwetu... JKTanzania 0 - Mafisadi Utd 5. Kwenye benchi la JKTanzania naona vipaji bado vipo, Mwakyembe na wengine wengi, sijui kwa nini hawakuingizwa kwenye mechi. Hii ni mechi ya kwanza, tunaelekea kushindwa nyumbani. Ya marudiano ni ugenini, tukumbuke Mafisadi Utd watakuwa wanaongoza kwa aggregate, kwa hiyo kibarua kigumu zaidi kwetu. Mashabiki wa Mafisadi Utd wanafanya rehersal ya kushangilia ushindi sasa hivi...
    Kwa maana nyingine, this is the same bullshit, same old games. Tusipokuwa makini tunapoteza mechi,na ligi vilevile!!!
    Bw.Michuzi heshima zako nyingi sana. Mwanafunzi wako kwenye sekta nyingi hapa.
    Bravo
    Karibuni www.upeowamtaa.blogspot.com

    ReplyDelete
  51. Kwa kweli mi JK amenisikitisha kitu kimoja,kumpa Magufuli wizara ya uvuvi ni bora asingemchagua kabisa.Magufuli anafaa sana kwenye wizara ya ardhi,anatakiwa mtu serious na asiyeogopa mtu kwenye wizara zilizo na harufu ya rushwa.Sasa Uvuvi ataenda kumpigia nani kelele.JK tunaomba badiliko tena kwenye wizara hiyo,Najua wengi wataguswa na post aliyopewa Magufuli.

    ReplyDelete
  52. SUBIRINI MKIWA NA MAMLAKA YA KUUNDA SERIKALI MUUNDE BARAZA LENU, MLITEGEMEA ATAWACHAGUA NYINYI? ALOWACHAGUA NDO KESHAWACHAGUA MKIWATAKA MSIPOWATAKA SHAURI YENU.

    HAPA WENGINE WALIKUWA WANASUBIRI WAJOMBA NA SHANGAZI ZAO NA MARAFIKI ZAO, SASA WAMEKOSEKANA WANAANZA KUPIGA KELELE. HEBU MUACHENI JK NA SERIKALI YAKE, NDIO MAANA MKAPA ALIWAFUNGA MIDOMO HAKUSIKILIZA NYOKO WALA FYOKO. MWISHO WENGINE MTATAKA HATA MPANGE RATIBA YA KAZI YA RAIS NA MAWAZIRI WAKE HUMU HUMU. KHA KABEBENI MABOKSI HUKU KURUDI BONGO HAIWEZEKANI HAKUNA MJOMBA WIZARANI WA KUKURUSHIA POST!

    KUNA WENGINE WANAOTA SERIKALI YA MSETO HUMU ETI ANGEWACHAGUA WABUNGE WA UPINZANI. HIVI NYIE MNASOMAGA KATIBA YA NCHI HATA KAMA INA VIRAKA AU MNAKURUPUKA TU. KASOMENI KATIBA KWANZA HALAFU MPIGANIE MABADILIKO YA KATIBA NDIO MTAWEZA KUZUNGUMZIA MSETO.

    ReplyDelete
  53. Aisee huu ni usanii wa mchana! hakuna jipya ni porojo tu. Sasa Chenge na kapuya wanafanya nini? halafu mbabaishaji kama malima naye kapewa uwaziri? mimi naona huu ni mwendelezo wa patronage! kulindana na kujuana. Mwinyi, bwana mdogo kapewa wizara ya ulinzi? are we serious? Magufuli kakosa nini yeye? mhandisi kwenye uvuvi? kwa nini wasimrudishe barabarani? kwa kweli hizi porojo za Jk zinaniboa sasa. We ngoja 2010 haiko mbali. halafu baraza la watu 50 ili iweje? Napata shida kuelewa huu usanii tutafanyiwa mpaka lini ili iweje? nachukia sana.

    ReplyDelete
  54. Michu,
    Vipi hapa mbona simuoni mama Mapesa??Zakia wa Maghji?
    WAMEMTEMA NINI?Ama wewe ndo umesahau kumuandika?

    ReplyDelete
  55. Kapuya,Chenge,Wassira???mmmmh. afadhali umetuondolea Sitta huku elimu,hakutusaidia chochote zaidi ya kuendeleza aloyakuta. lakini hapo kwa Magufuli loooh yasikitisha,kama hawamtaki si wamuache tu apumzike...uvuvi?upi?

    ReplyDelete
  56. Jamani mimi sijafurahia kuchaguliwa kwa Adamu Malima,sina uhakika na uwezo wake,hasa alipoongea pumba kuhusu Mengi na vyombo vyake vya habari.Kwani Baba yako akiwa waziri lazima na mtoto apate nafasi serikalini?

    ReplyDelete
  57. ubabaishaji hoyee! mafisadi mliobaki juuu, juu juuzaidi.

    ReplyDelete
  58. Michuzi Kwa nilivyosikia:

    Wizara ya Kilimo waziri ni Peter Msola.

    Kama ni mimi nimesikia vibaya tukumbushane, kama ni upande wako rekebisha.

    Ni hilo tu Mkuu!

    ReplyDelete
  59. Jk kafanya kazi nzuri ila kuna baadhi ya mawaziri wameweka post ambazo hawatazimudu mfano Dr Mwinyi kupewa wizara ya ulinzi hiyo ni hatari. Na huyo Chenge na Kapuya hawakutakiwa kabisa kuwepo katika baraza hili jipya nahisi ni washikaji wake Jk.

    ReplyDelete
  60. thanks for breaking the news as it happens..but......mie mkoa naotoka naona tumetoka patupu...may be ...tunaongoza kwa ufisadi!!

    au nimekosea........Iringa haijatoa waziri!

    ReplyDelete
  61. Kaka Michuzi nakufananisha na SHINKANSEN za hapa Japan jinsi ulivyokuwa faster kutuhabarisha mambo.
    Kwa mara nyingine tena" MUNGU IBARIKI TANZANIA"
    Mdau JAH-PAN .

    ReplyDelete
  62. Hongera kaka yaani leo mpaka saa hizi kwenye blogu yako wameshaingia watu 13,440 na hii ni namba ya leo peke yake wakati jana waliingia zaidi ya 14000.

    Hongera sana tena sana kwa utaoji taarifa ulio makini. Unafaa kuongoza kitengo cha e-government kwa spidi uliyonayo.

    ReplyDelete
  63. mambo yale yale wizara ya ulinzi na mambo ya ndani unapa daktari badala la askari!!!!!!

    ReplyDelete
  64. Umeruka 13, tuambiwe waziri na wizara ili kukamilisha mawaziri 26. Pia manaibu naona wako 17 tu na siyo 21

    ReplyDelete
  65. kwakweli nimefurahi sana mramba na mungai kutupwa nje, kwanza uyo mramba ndio hafai kabisa ni mwizi na fisadi mkubwa, na pia sijapendelea wizara aliyopewa magufuli, magufuli ni mchapa kazi anatakiwa apewe wizara zile zenye matatizo ili aweze kuzishugulikia kikamilifu sio kama wizara ya masamaki ya nini.

    ReplyDelete
  66. Brother Michuzi, hongera sana na asante kwa juhudi zako za kutuhabarisha kadri mambo yanavyojiri.

    Kwa haraka haraka nimeona yafuatayo:

    1. Watu wengi ni wale wale. Hii inaweza ikamaanisha mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutotegemea mapya au kuonyesha kuwa serikali iliyopita haikuwa chafu sana isipokuwa kwa wachache tu
    2. Baadhi wamepandishwa vyeo kutoka Unaibu kwenda Uwaziri kamili, ambalo ni jambo zuri
    3. kutokuwepo wapinzani kunaendeleza mapambano ya kuzidi fichua issues na kuleta challenges kwenye serikali lakini pia hakujahujumu kambi ya upinzani. Pia hakujaleta kasoro kwenye chama tawala kwa sababu kiitikadi chama tawala wasingeruhusu serikali yao ichangamane na wapinzani, wapinzani vivo hivyo. Ingawa inapokuja kwa maslahi ya kitaifa, haijalishi nani anatoka kundi gani, tunataka watu watakaoshirikiana na sisi wananchi kutuletea maendeleo.
    4. kutokuchaguliwa kwa Dr. Mwakyembe(na wengine wote waliowika wiki iliyopita) kunaonyesha ni ishara kuwa rais anategemea watu wazidi kuiibuka na kuikosoa serikali yake na he will take it constructively bila kuwaziba midomo kwa kuwapa uwaziri au mambo yafananayo na hayo. Ingawa ni angalizo pia kwa wote watakao simama kidete na kutetea hoja lakini wakiwa na hidden agenda kichwani i.e. kutegemea kupewa uwaziri nk.
    5. Nilisoma kwenye baadhi ya media kwamba kuna baadhi ya wadau watarudi kwenye serikali hii ingawa hawakutakiwa ili hapo baadaye waweze kuulizwa vizuri katika uchunguzi utakaofanyika kwenye wizara zao.

    Kwa vyovyote vile, serikali hii ina mkataba na watanzania mpaka 2010. Ikiwa agenda zao zitakuwa hazijatimilika….nafikiri mnajua nani ana nguvu za kumweka mwenzie madarakani. Watanzania tuamke !!!

    Mdau

    ReplyDelete
  67. Very impressed Michu wewe in CCN ya TZ! Yaani hata kama siasa ya nchi yetu inayumba yumba, kihabari tuna wewe unayetukeep up to date. Hizi habari haziko Daily News wala Ippmedia ni kwa MICHUZI TU, asante sana.

    Kuhusu Baraza jipya la mawaziri not impressed, amepunguza kidogo sana bado ni wengi. Ila inabidi tuelewe kwamba asingeweza kuvunja wizara nyingi bila mpanglio muda ulikuwa ni mfupi sana anahitaji muda zaidi. Inabidi apunguze pole pole kujua wizara gani iunganike na ipi, na ni nani ambaye anaweza kazi other wise itakuwa vurugu. Hivyo tumpe muda hopefully atapunguza zaidi.

    ReplyDelete
  68. Jamani wadau wenzangu hapa ukumbini nadhani kila mtu anatoa maoni yake. Mambo ya mtu ku-criticize hapa na pale na mwingine kumwambia... "wewe tengeneza baraza lako", hii si haki. Kila mtu yupo huru kutoa maoni yake kwa namna aonavyo. Na ikumbukwe kuwa wakati Rais anaunda baraza lake mwaka 2005, kuna watu walisema kabisa baraza kubwa na litashindwa kazi, na kweli tumeona hayo yametokea. Sasa na mimi nikirudi kwenye kuchangia, sitaweza bado kumsifu Kikwete kwa hili baraza jipya, ila "nitamuombea" angalau baraza hili liweze kwa namna fulani kufikia sehemu fulani ya matarajio ya wananchi. Kwa sababu si vizuri likavunjwa tena ndani ya miaka mitatu ya utawala wake iliyobakia kwa miaka mi-5 hii ya mwanzo. Hapa ni mambo yale yale tu, mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya. Bado damu changa na mpya zingeweza kutafutwa kuchukua nafasi za akina Chenge, Wassira, Kapuya. Na bado kwa mtazamo wangu baraza hili lingeweza kupunguzwa zaidi. kwa kuunga baadhi ya Wizara, kwa mfano Mambo ya Nje na Afrika Mashariki. Afrika Mashariki yaweza kabisa kuwa Idara ndani ya Wizara ya mambo ya nchi za nje na kufanya vizuri kabisa... labda kama ni uamuzi wa nchi za Africa mashariki, otherwise, hili ni eneo ambalo Rais angeweza kubana matumizi. Wizara ya Kilimo na Chakula, ingeweza pia kuunganishwa na ile ya Uvuvi na Mifugo sijui. Na pia Wizara ya Utamaduni Michezo, pia ingeweza kuunganishwa na kazi na Ajira. Kwa hiyo kulikuwa na uwezekano na Rais kuwa na kama Wizara 21 au 22 hivi tu. Nchi yetu ni masikini, hivyo na hata maamuzi yetu na mambo yetu lazima yaweze kwenda na uwezo wetu. Inashangaza kuona nchi ambazo ni tajiri, na kubwa kuliko Tanzania, zina wizara chache 15, 20hivi, lakini sisi masikini Wizara 26 sijui. Anyway, bado mjadala huu utaendelea, ngoja nifanye mambo mengine, baadae nirudi kwenye mjadala huu. Pia nikupongeze Michuzi kwa u-faster wako, japo na makosa kibao... lakini tunaelewa sababu..... unataka uwe wa kwanza...

    ReplyDelete
  69. Asante sana kaka Michu kwa kazi yako nzuri maana nilikua nategea kusoma hii habari kwenye glob yako.
    Kuhusu hili baraza kwa kweli sioni kama kuna lolote jipya hapa maana na sura zile zile za toka miaka ya sabini zinajirudia rudia tu toka wizara moja mpaka nyingine kwahiyo sijui kama kuna badiliko lolote la maana hapa.Ninachoweza kusema ni mungu ibariki Tanzania tu.

    ReplyDelete
  70. Mramba Njeeeeeeee teke kuleeeeee hafai kabisa huyo, lakini utasikia kapewa uablozi, au ukuu wa mkoa
    big Up Jk!

    ReplyDelete
  71. HONGERA SANA KAKA MICHUZI

    ILA KWANGU MIMI ZAKIA MEGHJI BADO NI CHUMA

    ReplyDelete
  72. Watanzania hebu tuache kashfa! Tushukuru mungu kwamba haya yote yametokea kidemokrasia na kwa amani. Watu tuliowachagua wamefanya kazi yao ya kuikabili serikali na kuwawajibisha viongozi walafi na mafisadi in public. Wote tulio nje ya nchi na wale walio Nyumbani tumeona LIVE jinsi demokrasi ilivyokomaa nchini mwetu, we have to be thankful for that. Kama kuna watanzania wanaoishi nje na hawajui kama unaweza kuona kila kitu live through www.jumptv.com. Nawajua wengi wao katika orodha hiyo wengine walikuwa walimu wetu Chuo kikuu cha Dar-es-salaam, na ninadhani ni team nzuri. Nyie mliowakalia kooni viongozi wa zamani lazima muelewe kuwa katika kila uongozi experience matters. Huwezi kuchagua watu wote wapya, na wakaendesha nchi. Hili ni jambo la utawala na siyo kila mtu anakipaji cha kuwa mtawala bali unaweza kujifunza kuwa mtawala mzuri kwa kujifunza kutoka kwa watawala waliopita na wenye uzoefu. Ndiyo maana Rais amejitahidi kuwaweka viongozi wapya na kuwachanganya na wazamani. wazungu wanasema "PHASING THEM OUT", muda utakapoendelea ndivyo atakapoanza kuwachomoa mmoja mmoja kama vile alivyofanya sasa kuwaacha baadhi ya viongozi wa muda mrefu ambao wameishasaidia vijana katika uongozi. Please watanzania tuwe makini tunapochangia hoja katika mtandao huu, au wale wakosoaji kwa nini msitoe list za mawaziri ambao ungechagua kama ungekuwa kwenye kiti cha JK?

    ReplyDelete
  73. Hwajaacha hakuna kuachwa katika huo mtandao watatujoin soon huku as mabalozi,uzamili au box. Imao

    ReplyDelete
  74. YAAP, asante michuzi sijalala leo huku canada natafuta habari hata bbc bado hawajaweka kwenye mtandao, i came to find info in you blg hongera kaka, will personall find you.

    Kuhusu new cabinet, it is good at least kuona mabadiliko, BUT I AM STILL WORRYING KIKWETE SIO MKWELI, tunafurahi ingawa kidogo.You see inabidi uwe mkali sio kusubiri report za bunge na presha za wananchi ndio ufanye mabadiliko, so bila mwakyembe, yasingetokea hapa,hata kama alifanya ujanja wa kumzunguka Lowassa kupitia bunge hapo ndio nasema ana udhaifu.

    Any way

    ReplyDelete
  75. Anon wa 4:45 pm Kwenye orodha ya United kingdom of Tanzania umemsahau Mathayo David Msuya. Huyu ni mtoto wa PM wa zamani. Ni jina tu linapinduliwa kila kukicha.

    ReplyDelete
  76. watanzania ni muhimu sana kuamka nakubaliana kabisa na usemi wa ndugu japhari.
    jk hayuko serious katika kuleta maendeleo ya wananchi kwa ujumla angalikuwa mwadilifu hapo angalichagua na wapinzani na ndiyo waliowezesha kutoa kashfa zote hizi za ufisadi.

    ama juzi nilikuwa nikiona interview CNN wa aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika Colin Power akiulizwa kuhusu election ya Amerika jinsi inavyokwenda na kuulizwa vipi atapigia kura yake kwa chama gani kati ya republican na Democrat jibu hakika lilinifurahisha sana na kusema ni muhimu watanzania waamke na wasishabikie chama wakawa kama bendera inafuata upepo, kura yako ndugu ni future ya taifa na vizazi vijavyo tusikubali kununuliwa na pesa zetu wenyewe yaani za Bot na Richmond na madini.

    yaani unakatwa kidole unalishwa damu yako.


    turudi nyuma kuhusu colin power ambaye hamna mtu asiyemjua ni mtu maarufu sana kuanzia amerika hadi dunia. alijibu kwa kusema japo yeye ni republican lakini hayupo kushangilia chama chake bila kutafakari.

    alisema yeye kura yake ataangalia sifa zifuatazo:
    mpigania uraisi mwenye uwezo wa kuleta maendeleo kwa waameraka
    chama kitakacholeta maendeleo kwa waaamerika
    hatojali kama mweupe, mweusi au mwanamke mana ukiwa ni mwamerika mambo ya matabaka hakuna, mwamerika ni mwamerika.
    hatojali kama ni chama chake au cha upinzani
    kwa kifupi amekubaliana na menge ya Democrat na hivyo dalili inaonekana kwamba atapigia democratic.

    yaani umaarufu wa colin power ni kama umaaruf wa mzee wetu kawawa japo yupo ccm lakini kuwa mkweli na apigie upinzani.


    nasisi watanzania muhimu inapokuja maslahi yetu, watoto wetu na taifa tumchangue mtu na chama kwa sifa zake siyo tu mie mpinzani basi napinga ccm au mie ccm napinga upinzani.

    kwanza kitu kikubwa cha watanzania ni kuwaeleza wabunge kila jimbo letu kuwa tunataka ratiba yote ya nchi iandikwe upya kwa kuwajumuisha vyama vyote tena.
    ikisha malizwa hapo wananchi wafahamishwe, leo raisi ana nguvu ya ajabu vipi unategemea aliowachagua watampinga.

    utaratibu wa america ni mzuri kulinganisha na mingine yote duniani. hapa nakusudia ukilinganisha na nchi zingine.
    leo obama ananguruma, angalia nchi zingine za ulaya kukuta mwenye asili ya kiafriaka au kiarabu au kihindi kupigania uongozi hamna.

    kwanza matunda yote ya haya mabadiliko yametokea kwa vyama vya upinzani kuvalia njuga kuhusu ufisadi maana serikali imeogopa yatakuwa makubwa maana hadi nchi za nje itayajua na kukata misaada.

    ni muhimu wananchi bunge letu liwe na vyama vingi na hiyo ndiyo demokrasi na tuchague viongozi wapya kutoka vyama vya upinzani ikiwa tunataka mafanikio.
    CCM hapa wanafanya kiini macho tu ukiangalia kwa watu wasomi watajua:

    bajeti ya tanzania 40% ni msaada toka nje
    mashule yanayojengwa ni msamaha wa madeni toka nchi za nje kwa masharti zitumike kujenga shule.
    barabara nyingi ni misaada
    ikiwa barabara imejengwa na serikari huwezi kusema kuwa CCM imejenga maana kodi ni ya watanzania wote na siyo ya CCM.
    badhi ya wana CCM wanaleana kwa mabaya na siyo mazuri, naimani vyama vya upinzani vikiingia madarakani madhambi mengi ya CCM yatatoka na hivyo kuwatoa wananchi kwenye umasikini, yote haya yanetegemeana nasisi wananchi kwenye majimbo yetu kuwajulisha wabunge na pia wakati wa uchaguzi muhimu.
    Salum Ahmed na mzee kawawa hawa ni watoto wa baba wa taifa na naimani hawa ni baadhi ya wana CCM wangalilileta maendeleo ya maana kwa vile wamekomaa na wamerithi mengi ya hayati baba wa taifa.

    lakini wengi walijua salum angalishika nafikiri kitu ufisadi tusingaliweza licha ya kulisikia hata kwenye kamusi ya tanzania lisingalikuwepo. na ndiyo hayati baba wa taifa alisema watu wanagombania kwenda ikulu huko hakuna pesa je hao waliokusaidia utawalipa nini pia alisema ikulu na mahala patakatifu.
    CCM wanasema wameleta amani leo tanzania kuna serikali mbili, mchana CCM ambayo serikali ya wananchi na usiku majambazi kazi kuua watu na kuwadhalilisha kwa kuwavua ngua nini serikali ilichokifanya cha maana hadi sasa. kiasi wananchi na mashirika yanabidi yafanye kazi mchana tu. leo nchi za ulaya zinafanya kazi masaa 24 na hayatoshi.
    haya CCM inasema imeleta usalama wa raia, tushukru tanzania haina makabila makubwa ya kuweza kuleta fujo, wewe unafikri ni rahisi kuleta amani kama burundi, rwanda na kenya wakati unakuwa na mafahari wawili katika zizi moja.
    ni muhimu kuona haki inakamilika kuona wote mafisadi wanafikishwa mahakamani, isiwe kubadilisha fanicha ndani ya chumba yaani nakusudia fanicha hiyo hiyo ila kiti hiki peleka pale na hiki paleka. hapa jamaa kutolewa uwaziri au ubunge bila kuwajibika itakuwa ni haramu hata kwa MUNGU.

    ReplyDelete
  77. Thanx bro Michu!! thanx a million times, wewe ndio 'yesu' wetu sisi tulioko ughaibuni. Nikija Dar nitakuleta zawadi (T-shirt). Nasita kusema BIG UP sababu sio kiingereza sahihi kama mnavyokitumia bongo. Bt thanks.

    ReplyDelete
  78. aisee,am so impressed with new cabinet.inaonyesha JK anajali mawazo na uhitaji wa wananchi wake.Am proud of him,tanzania inahitaji viongozi kama JK,uswahiba pembeni.

    ReplyDelete
  79. SASA JK TUNAOMBA UTURUDISHIE ZILE NYUMBA ZETU ZA OYSTERBAY.FISADI MKAPA ALIONA AWAPE WENZIE ILI WASIMSAKAME KWA WIZI WAKE.HIZO NYUMBA WAMEPEANA HAWAJAUZIANA.DHAMANI YA NYUMBA ZILE SI SAWA NA WALIVYOUZIWA.

    TAFADHALI SANA JK.

    ReplyDelete
  80. Afadhali JK ameonyesha hali ya kujali wananchi wake na kuwatoa viongozi ambao wanakashfa mbalimbali na kuchagua mbadala, Kwa mtu mwenye akili hataweza kulalamika sana kwani sio kosa lake bali ni mfumo mzima wa CCM na serikali yake,kwamba waziri ni lazima awe mbunge.Kwahiyo imembidi achague watu walewale ambao wapo bungeni na inamwia vigumu sana kuchagua outsider japo wapo ambao ni wasomi na wenyewe uwezo mkubwa kuendesha serikali hasa kwenye maswala nyeti ya uchumi,mipango miji na Fedha.

    Swali kwako Michuzi Hivi siku moja ikatokea wabunge wote wa CMM ambao wako Bungeni ni Vihiyo (kama unavyojua mtu yoyote anaweza kuwa mbunge) Je rais atachagua hao hao kuwa Mawaziri?

    Nadhani

    ReplyDelete
  81. We anony FEB 12, 4;46 PM mbona una hasira sana na unaowaita wabeba box, we kama sikosei ulidipotiwa halafu ulijaribu kurudi ukanyimwa visa...hapa watu wana diskasi mawaziri sasa wabeba box wametokea wapi? We kula vumbi lako ukalale.

    Mdau Holland

    ReplyDelete
  82. mnasema walioachwa watapewa ubalozi, ubalozi sio kazi raisi wakuu, inahitaji mtu mzoefu wa mambo ya diplomasia, nadhani pia kikwete abadili haraka, nchi za ulaya.

    ReplyDelete
  83. Nina furaha na baadhi ya sura ndani ya bunge isipokuwa wasiwasi wangu wizara ya fedha mabadiliko bado naona kikwete karuka mkojo kukanyaga mavi kwani mama meghji amenyoshe udhaifu wa maamuzi but huyo Mkulo ni fisadi nambari moja ameiifilisi NSSF na PPF hadi zikataka kufa. Alipokuwa yeye mkurugenzi mkuu Leo anateuliwa kuwa waziri wa fedha si fisi amepewa bucha????????????????? Mh. vita ya ufisadi naona inamgeukia kikwete mwenyewe

    ReplyDelete
  84. Sasa afadhali, nimefurahi sana kwa vikongwe kama meghji, mramba na vingunge wengineo wa zamani kutolewa. Lakini huyu Chenge kaponeaje? Na Magufuli wamempa wizara iliyolemaa. Huyu angepewa wizara ya fedha.

    ReplyDelete
  85. HEHEEEEEEEEEE!!!!
    MICHUZI NAMBA 13 NI WIZARA IPI HIYO AU NDIO KAAMUA KUONDOKA NAYO. WANAKIJIJI MSHTUENI NDUGU YETU

    ReplyDelete
  86. HIVI VIONGOZI WETU WANAFANYIWA BACKGROUND CHECK! WE REALY NEED TO START DOING THAT....AND PHYSICAL CHECKUP TOO....NISHAI BAADA YA SIKU WAZIRI KAANGUKA NA NGOMA.

    ReplyDelete
  87. the motherland,is on its knees,such that a mere change in cabinet positions raises,decibels of optimistic hope to biblical proportions,i fear for my country,land of my birth,when the truth finally dawns on the masses,and all their hopes are swept under the carpet.WHEN will we tanzanians be able to see ahead and not be hoodwinked by cosmetic changes,we must be bigger then this,personnel change as history has proved, has never beared fruits.kikwete should be taken to task be totally answerable on a given timescale the development of tanzania.its about time we woke up to the real task facing us.dancing to the tunes of the ruling class,i am afraid will do more harm then good

    ReplyDelete
  88. Mimi limenifurahisha swala moja la JK kugundua kuwa kazi ya uwaziri inahitaji vijana wenye nguvu na moto wa kufuatilia mambo. Namsifu kwa kuwapa wabunge vijana madaraka makubwa - full ministers. Kwa wanaojiuliza nawasema kina nani ni Dr Kamala, Dr Mwinyi, Ngeleja, Masha (full ministers) na Dr Nchimbi,Adam Malima na David Mathayo (deputy ministers). Sidhani kama kuna mbunge kijana wa CCM (between 30's and early 40's) ambaye hajajumuishwa (I stand to be corrected). This is the way to go!
    Mchemsho ni kwa kuwarudisha wazee sana kama Chenge, Wassira na Kapuya - I hope this is their last time na hawatakuwepo tena from 2010. Mdau - New Zealand

    ReplyDelete
  89. Bongo kweli nchi ya mtikasi
    i just wonder watu wanafurahia eti baraza jipya.For simple Tanzanian what are you going to gain from this new cabinet..????????kumbukeni waliondoka walikuwa hivyo hivyo Tanzania (nchi maskini in general )mtu atapewa post ili kuendeleza familia yake binafsi siyo jamii yake hiyo ndiyo tofauti yetu na nchi zilizo endelea ..hao watu watanza kujenga nyumba zao masaki.mikocheni..etc.ndugu zao na watoto wao wameisha jipanga kwenda oversease , kabla ya kutangaza hilo baraza magari yameisha order latest cars(luxury) siyo chini ya elfu sitini kila moja ukizidisha na 50 unapata thamani ya fedha inayo takiwa kujenga hospital ya Taifa (representable) siyo huu uchafu eti muhimbili watu wanalala chini hakuna vitanda , leo hii mnashangilia mawaziri wapya ....kweli nyerere alisema Tanzania ni kama kichwa cha mwenda wazimu kila mtu hujifunzia kunyoa kwetu...wabungu wa nchi za ulaya ambao hawana uchungu na sisi wanajitolea mishahara yao kusaidia watoto wa africa wanaokufa kwa malaria mie nimezaliwa bongo mpaka naondoka sijawahi kusikia eti bunge limetoa msaada hata 1m Tsh kusaidia watoto yatima..last time nilipo kuwa bongo (nilitembelea nyumba ya watu yatima ...nilimuuliza mtoto mmoja kitu gani akitoshereza hapa kwenu ??/ mto aliningalia na kusema uncle ...maji hapa kiu sana maji kwa wototo wote hayatoshi, kuoga mara moja kwa week.)anyway ni machozi sana nyie acheni mtoto wa Tanzania analilia maji wakati nchi imezungukwa na maji kama kuna mtu anajibu naomba atuwekee kwanye blog yetu hali kama hiyo mnaowaita waheshimiwa watembea 24 hours na magari ya kifahari bila kujali kupanda kwa mafuta dunia watoto yatima wanakufa kwa kukosa maji.....
    Jamani nafikiri mie mtazamo wangu uko tofauti na wengine.
    kama watanzania hatutafungua macho kwa bei usd 100 pipa la mafuta halafu waheshimiwa 50 kila siku wese aisee madeni hayataisha nchi hii na tusitegemee miujiza (kuna msema kwamba" kila serikali inastahili kwa watu wake") tuvumilie viongozi wetu kwasababu tunafanana nao...
    Doctor.

    ReplyDelete
  90. I'm very happy Zakia meghji is not there but am not happy where Magufuli is i think he is too beneficial to be where he is !

    ReplyDelete
  91. MASHA karudi kufanya nini si alikuwa naibu wa Msabaha huyu? naona wadau hawaliongelei hili!

    ReplyDelete
  92. what the hell is miundo mbinu?? kulikuwa hakuna umuhimu wa hiyo wizara?? kwanini isiwe chini ya wizara ya ujenzi..?What the hell is that...?

    ReplyDelete
  93. WE ANONY WA Tuesday, February 12, 2008 10:21:00 PM EAT,

    UNAWAZIMU, ROHO MBAYA AU NI NINI HASA?
    INAMAANA KWAKO WEWE MTU MWENYE NGOMA HANA HAKI SIYO? KWA TAARIFA YAKO MAGONJWA YA MOYO NA BLOOD PRESSURE NI HATARI KULIKO NGOMA HIYO, MWENYE NGOMA ANA HIARI YA KUFA BAADA YA 20 YEARS MWENYE BP HANA HIAI ANWEZA KUFA MUDA WOWOTE NYANG'AU WEE!!

    ReplyDelete
  94. embu niwaulize ndugu zangu,chenge,kapuya wa nini tena?chenge utendaji wake zero kabisa,kapuya ndo usiseme,yaani JK halioni hilo?bora angemrudisha mama meghji kuliko kuwaacha haya vihiyo...
    amepoteza ufanisi wa mtu kama magufuli kumweka wizara ya vilaza badala ya kumpa wizara nyeti,masha kawa uwaziri kwa ufanisi gani haswa?mtu amehamishwa wizara twice cause of underperformance then now unampa uwaziri?C'mon......
    Captain Mkuchika karudishwa kufanya nini?watu wanasinzia bungeni then unawapa uwaziri?get serious Jk...we need credentials not familiarity.

    ReplyDelete
  95. "THEM BELLY FULL BUT THEM HUNGRY"
    kazi ipo Tz jamani, it is the same people in different ministries, what a shame! Will see how long are you going to eat!

    ReplyDelete
  96. WADAU MICHUZI ANAWEZA AKAWA FISADI MAANA ZILE COMMENTS ZINAZOMLAUMU YEYE ANAZITIA KAPUNI, AU AKILAUMIWA KIONGOZI YEYOTE AMBAYE WATOTO WAKE WANA USHIKAJI KIAINA FULANI NA BWANA MICHU HAPOST HIZO COMMENTS DOH........ MI NSHAJICHOKEA NGOJA NIWE MSOMAJI TU MAONI YA WENZANGU, NAFIKIRI YULE JAMAA ALIYEFIKIA UAMUZI WA KUKUTUKANA KWA NAMNA NYINGINE ILISABABISHWA NA HASIRA MAANA AMETUMIA MUDA WAKE KUANDIKA ANACHOKIFIKIRIA ALAFU WEWE UNAZIWEKA KAPUNI, INAUMA SANA KWA KWELI SIO FRESH KAMA COMMENTS ZINAJENGA NA HAZINA MATUSI USIWE UNAZIBANIA BWANA.

    ReplyDelete
  97. Kwa ujumla baraza sio baya sana, dosari kubwa ni tatu tu, Chenge, Kapuya na Wassira hawakustahili kuwemo. Hasa Chenge ametajwa ktk list ya mafisadi.Kapuya ameboronga michezo na kazi na sasa karudishwa hukohuko, huo ni utani.
    Jambo la msingi sasa ni
    1. Kufuatilia wote waliohusika na Richmond na kurudisha pesa zetu ikibidi wafilisiwe akina lowasa,karamagi na rostam
    2. Kufuatilia kashfa ya EPA na kurudisha pesa zetu hata kwa kuwafilisi wahusika.
    3. Kufanyia kazi listi ya mafisadi kama ilivyotolewa na akina Slaa, ushahidi unaonyesha wazi kabisa kwamba wale jamaa wameiba hizo pesa kweli kwani tangu wametajwa hawajachukua hatua zozote na hali walitishia kushtaki.
    4. Ripoti ya Buzwagi nayo itolewe na wahusika washughulikiwe ipasavyo.
    5.Mkuu wa Takukuru na mwanasheria mkuu washinikizwe kujiuzulu kwani nao wanalea rushwa.
    Mwisho wanahabari msichoke kupigia kelele uozo wa viongozi kwani kelele zenu ndio zimesababisha tukio hili la kihistoria kutokea Tanzania tangu uhuru, yaani waziri mkuu kujiuzulu na cabinet kuvunjwa sababu ya rushwa,
    Tanzania oyee,Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki watetezi wa wanyonge, Mungu waumbue mafisadi, AMIIIIIIIIN!
    TANZANIA BILA UFISADI YAWEZEKANA TUKISHIRIKIANA.

    ReplyDelete
  98. Jk hana jipya sijaona badiliko la ajabu sura zilezile toka baba sasa mwana na atakuja na mjukuu, wengi tulitarajia haya tuloyasikia,urafiki,mtandao nk,

    ReplyDelete
  99. HAKIKA MIMI NIWAPONGEZE MAWAZIRI ILA PIA NAOMBA NICHUKUWE FULSA HII RASIMI KUMPONGEZA MICHUZI NADHANI KWA WEBSITE ZA TANZANIA NA PENGINE ULIMWENGU ALIKUWA WA KWANZA KUWEKA MAJINA KWENYE NET MUNGU ANDELEA KUKUPA NGUVU ZA KUTUMIKIA TAIFA LAKO AKUEPUSHE NA UFISADI NA UFEDHULI AMEN

    ReplyDelete
  100. Watanzania mnataka kuniambia nyie mnaijua serikali kuliko JK mwenyewe na washauri wake,Mwakayembe bado haja prove chochote kosa la kwanza tu ,Hakumuoji Lowassa kwenye uchunguzi hiyo pekee yake inamtoa kwenye baraza, siku zote mnachotegemea hakiwi,mtu anachagua uongozi anaona utaenda kwenda na matakwa yake kwa manufaa ya wananchi, alisema hato sita kumtoa waziri ambaye hafanyi vyema! England imekuwa na uhuru almost 700 years lakini hadi leo hamna waziri wanayempenda kwajili kila mtu ana opinion yake hayaa

    ReplyDelete
  101. napenda kumuunga mkono doctor kwa maelezo tanzania inajulikana kuwa wananchi na viongozi hali moja. kama baba wa taifa marehemu nyerere alisema Tanzania ni kama kichwa cha mwenda wazimu kila mtu hujifunzia kunyoa kwetu.

    nimepata habari baadhi ya mafisadi wanasema hayo ni maneno ya mtaani hayana uzito wowote. anazidi kusema kuwa jamaa ni njaa tu na sasa ndiyo kula zaidi maana ni sawa na simba kujeruhiwa.

    watanzania ni muhimu tushikamane nchi nzima kwa kutumia wabunge wetu wenye nia ya kusaidia taifa bila ya kujali chama ya kuwakilisha mada ya mafisadi ni lazima wapelekwe mahakamani na wataifishwe mali zote walizoiba.

    bila kufanya hivi tutabaki palepale na kama siyo kurudi nyuma na malaria na maji machafu wakati wenzetu wakila uhondo wa nchi.

    nachoomba tena sana huu ndio wakati wakuleta mabadiliko nchini kwa njia ya demokrasia.

    umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

    tanzania ina ufalme ila style yake tofauti na ufalme wa kawaida. maana hapa utakuta mtoto wa mkubwa fulani anatayarishwa ili kuja kushika ngazi hapo mbeleni ili aweze kuwahifadhi wazee wanachama.

    jk tunamuomba afanye haki kwa kiegesho cha kumuogopa MUNGU na kujua yote aliyo nayo kesho katika mahakama ya MUNGU itabidi kuyajibu duniani hapa ni mapito tu leo tupo na kesho hupo. hivyo cha kugombania ni akhera maana hii na katika kila dini inaeleza.

    leo jamani tunakula kiapo cha MUNGU halafu tunatenda vingine ni hatari kubwa ndugu zangu. ikiwa hatuogopi watu basi tumuogope MUNGU maana anatuona kila tunalolifanya. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA VIONGOZI WAKE PIA WANANCH WAKE AMEN.
    MSEMA KWELI

    ReplyDelete
  102. OPEN LETTER TO:
    Bi. Anne Kilango, Same Mashariki (CCM, Bw. Lucas Selelii, (CCM) Nzega, Dk. Wilbrod Slaa, Bi. Stella Manyanya na zitto napenda kuwashukuru sana kwa ukweli waliouweza kuutoa kwa kujali maslahi ya taifa na kujua cheo ni dhamana kwa wananchi.ninachowaomba ni kupigania haki ipatikane ya mafisadi wote wapelekwe mahakamani tusidanganyike na baraza la mawaziri tukasahau yaliyosababisha kuvunjika baraza.

    wazungu wanasema ukitaka kutibu ugonjwa ni muhimu kujua sababu za ugonjwa na siyo matokeo.

    chukulia mtu anaumwa kichwa anakunywa panadol hapo inakuwa hakutibu ugonjwa bali ametibu dalili za ugonjwa.

    kwa maana ingine kuumwa kichwa kunaweza kusababishwa na mambo mengi na ndiyo maana inabidi kwenda hospital kupimwa.

    hivyo hapa ugonjwa ni ufisadi na siyo baraza la mawaziri.

    hivyo ndugu zangu tunawaomba msiogope mtu bali muogopeni MUNGU.
    MUNGU ndio wa kuogopewa ikiwa watafanya madhambi ama binadamu wote ni sawa.

    pia ile kusema kuwa ya JK imebidi awache wazee kwa vile wanahitajika ukita ukweli , ikiwa hii ndio sababu basi tunarudi nyuma maana ujuzi wa viongozi wengi ulikuwa rahisi kwa vile dunia ilikuwa nyuma kiasi kiongozi anafanya anavyotaka na siyo watu wanavyotaka.

    kwa maana ingine chukulia biashara ambayo haina ushindani mara nyingi inakuwa hahitaji mbinu za kibiashara.

    lakini panapokuwa na maduka mengi hapo akili inabidi kufanya kazi.

    kwahiyo miaka mingi kufanya kazi haina maana mtu anakuwa mjuzi maana inategemeana alikuwa akijishughulisha kwa mambo gani kutetea maslahi ya nchi au ufisadi ili kujineemesha yeye na familia yake.


    pia inaweza kuwa jamaa anamiaka mingi kazini lakini udhoefu wake ni wa mwaka mmoja umejirudia miaka kadhaa aliyofanya kazi.

    mfano mwingine chukulia jamaa anaweza kuwa na driving license kwa miaka 30 lakini ukichukulia muda alioendesha gari ni miaka 3 muda wote license ilikuwa mfukoni.

    chukulia BARIKA OBAMA hata akishindwa lakini watu wameaamka na kuona ile kasumba ya muda wa kufanya kazi haina maana ndio uwezo wa maana.

    miaka isiwe sababu ya kumchagua mtu ni uhodari wake.

    mimi mara nyingi napofanya interview za watu siangalii kabisa experience ya karatasi naangalia usmati wa mtu.

    hivyo ndugu zangu tuikomboe tanzania kwa kuwa kitu kimoja inapokuwa maslahi ya nchi na rizki ni kwa MUNGU nasiyo binadamu napia kupata siyo hoja, hoja baraka hivyo msidanganyike maana hao mafisadi wako tayari kuhonga kiasi kikubwa cha pesa ili kuwanyamazisha watu kwa kutumia hizo pesa haramu ambayo ni damu ya watanzania, masikini hata maji safi hawana.

    tumkumbuke marehemu baba wa taifa bepari bi kama mnyama yeye hana rafiki na binadamu leo kakupa rushwa kesho atakupa sumu.

    tujiulize unaweza kufanya urafiki wa milele na simba???????

    asanteni mpenda kweli

    ReplyDelete
  103. Just for a record, Magufuli sio engineer, ni mwanasayansi Mkemia jamani. Tuache kukurupuka

    ReplyDelete
  104. Nakushukuru Kaka Michu,ila mimi nimesikitishwa na Wizara aliyopewa Magufuli hivi kamzibia mkubwa gani..mbona kama jamaa anajaribu kumfrastrate jamaa anapiga mzigo kama nini! lakini ni kama wanajaribu kum marginalise.Afu me nimemind sana Madini kupewa hawa jamaa ,wataweza kweli? maana wamekaa kisanii sanii anyway tusubiri tuone...na hivi Chenge kabeba mikoba ya nani? mi naona ni Mzigo tuu..........

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...