JK ANAINGIA UKUMBI WA TAMISEMI DODOMA SAA TISA NA DAKIKA 16 AKIONGOZANA NA MAKAMU WA RAIS DK. ALI MOHAMED SHEIN NA WAZIRI MKUU MH. MIZENGO PINDA. ANAKAA NA KUOMBA ABADILISHIWE KITI KWANI CHA AWALI HAKUKIPENDA. ANATOA MUHTASARI WA KILICHOPELEKEA KUTANGAZA BARAZA JIPYA. UFUATAO NI MUHTASARI WA HOTUBA YA JK
AMEANZA KWA KUTOA MAELEZO KWAMBA WAMEZINGATIA KAZI MBILI KATIKA KUAMUA
*KWANZA KUTAZAMA MUUNDO WA SERIKALI.
*YA PILI KUJAZA NAFASI ZA KUJAZA BARAZA LA MAWAZIRI.
KATIKA UTEUZI WALIZINGATIA MATATU.
1. JUKUMU LA SERIKALI KWA MUJIBU WA KATIBA
2. MAHITAJI YA MAENDELEO YA TAIFA NA WANANCHI KUFUATIA ILANI YA UCHAGUZI YA CHAMA TAWALA
3. UFANISI WA MAJUKUMU YA KISERIKALI.
YALIYOAMULIWA NI KUUNGANISHA NA KUPUNGUZA WIZARA
*OFISI YA RAISI SIASA NA USTAWI WA JAMII VINAHAMISHIWA PMO
*UCHUMI NA UWEZESHAJI INAUNGANISHWA NA FEDHA
*TUME YA MIPANGO KUWA OFISI
*MAMBO YA NDANI NA USALAMA WA RAIA NI WIZARA MOJA TENA
*MAMBO YOTE YA ELIMU YATAKUWA CHINI YA WIZARA MOJA BADALA YA MBILI KAMA ILIVYO SASA
*KUTOKANA NA ONGEZEKO KUBWA LA SHULE ZA SEKONDARI, IMEAMULIWA USIMAMIZI WAKE UHAMISHIWE TAMISEMI KAMA ILIVYO ELIMU YA MSINGI ILI KUSOGEZA MAAMUZI KARIBU NA SEHEMU HIZO.
*SHUGHULI ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIA NA SHUGHULI ZA MAWASILIANO KUTOKA WIZARA YA MIUNDOMBINU ZINAUNDIWA WIZARA YAKE, NA ITACHANGANYWA NA TECHNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO ILI KUTOA NAFASI STAHIKI KWA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA YA HABARI ILI
*USIMAMIZI WA KAMATI YA PAMOJA YA KUSHUGHULIKIA MASUALA YA MUUNGANO, MWENYEKITI NI MAKAMU WA RAIS.
*MAJI IMEUNGANISHWA NA KILIMO ILI WIZARA HII ISHUGHULIKE NA MIUNDOMBINU YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI.
*SEKTA YA UVUVI IMETOKA WIZARA YA MALIASILIN NA UTALII KWENDA WIZARA YA MIFUGO
*OFISI YA MANASHERIA MKUU WA SERIKALI; KATIBU MKUU WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA ASIWE NAIBU MWANASHERIA MKU, INATAKIWA NAIBU MWANASHERIA MKUU HUYO AMSAIDIE MWANASHERIA MKUU, WAKATI KATIBU MKUU AENDELEE NA MAJUKU YA WIZARA YA SHERIA NA KATIBA.
*UIMARISHAJI WA USHIRIKA NA BIASHARA YA NDANI NA BIASHARA YA NDANI KWA JUMLA; BADALA YA KUWA IDARA KATIKA WIZARA NA ENDAPO WIZARA INAHAMA MAKAZI INABAKI IDARA AMBAYO HAINA KITUO MAALUMU.
*BIASHARA YA NDANI AMBAYO INA BODI YA BIASHARA AMBAYO ZAIDI YA MAONESHO YA BIASHARA NA USHAURI WA BIASHARA YA SOKO LA NDANI, HAKUNA MFUATILIAJI WA KUTENGENEZA SOKO LA NDANI.
KWA HIYO BARAZA NI KAMA IFUATAVYO NA JK ANAKIRI HAIKUWA KAZI RAHISI:
AMESEMA MAWAZIRI KAMILI WATAKUWA 26 NA MANAIBU 21
WADAU KUNRADHI. AWALI NILITAJA WIZARA 29 KWA MAKOSA AMBAYO NIMEREKEBISHA. SPIDI 120 SI MCHEZO, SAMAHANI KWA USUMBUFU..SASA MAMBO NI MSWANO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. hiyo baadaye mwanagwa tupe majina kwanza

    ReplyDelete
  2. Mkuu Michuzi, mbona hujatuwekea majina, pressure inazidi panda, mkuu tupe majina na wizara tujue serikali yetu, ama nawe tukuundie tume.

    ReplyDelete
  3. wizara ya fedha na mipango ni nkuru
    wizara ya ulinzi mwinyi
    wizara ya elimu ni prof magembe
    Wizara ya umwagiliaji Prof mwandosya
    wizara ya mifugo ni magafuli
    wizara ya kazi Prof kapuya
    hayo ndiyo majina nayokumbuka
    ahsanteni

    ReplyDelete
  4. Michuzi mawaziri au wizara ni 26 na sio 29 kama ulivyosema. Hiyo figa ni ya zamani kaka.

    ReplyDelete
  5. Bro misupu tunakufuatilia kwa makini saaaaaaaaaaaaana tupe mambo hayo ya JK

    ReplyDelete
  6. Where are the names?

    ReplyDelete
  7. Kaka, alisema mawaziri 26 na manaibu 21!

    ReplyDelete
  8. WE WE KIJANA UTUKOME KABISA,WENZAKO TUNAOSUBIRI KUTEULIWA MATUMBO MOTO SAAHIZI....UNASUBIRI NINI KULITAJA JINA LANGU? SI UIIBE KARATASI HAPO MEZANI KWA JK KISHA TUHABARISHE WATU TUJIANDAE KUGOMBOA KASUTI KA KUAPISHWA NAKO....CHONDE CHONDE MICHUZI UTAUA BILA KUKUSUDIA...kila la heri wajameni mwe!!!

    ReplyDelete
  9. Niulize!kwa nini Dr Mohammed Shein hujamuanza na cheo mheshimiwa na Pinda umemuanza na cheo Mheshimiwa?????

    ReplyDelete
  10. Mhhh, Michuzi JK amesema wizara ni 26 au 29? mbona mimi nimesikia ni 26 ambazo amezipunguza kutoka kwenye 29 zilizokuwepo. inawezekana labda sikusikia vizuri. manaibu waziri uko sawa ni 21.

    ReplyDelete
  11. Kazi nzuri sana kaka Michuzi maana tulisubiri hii habari kwa hamu

    ReplyDelete
  12. michuzi,I thought Mr handsome boy oops sorry,the president said 26 ministries,are you sure you heard it right?

    ReplyDelete
  13. *MAJI IMEUNGANISHWA NA KILIMO ILI WIZARA HII ISHUGHULIKE NA MIUNDOMBINU YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI.
    ???????????????????????????????? angalia hilo kama ni kweli

    ReplyDelete
  14. Leo lazima nilale Bar Al maaruf Mramba kwisha......JK udumu

    ReplyDelete
  15. Ngeleja Waziri wa Madini? Malima msaidizi? Haya Mheshimiwa Raisi kila la heri na hilo baraza jipya eneo la madini.Nadhani, labda pengine Raisi anajua na hao mawaziri wa madini wanajua zaidi kuliko watu wengine wakiwemo wabunge wanavyojua.Haya weeeeeeeee! hongereni mawaziri wa madini.

    Kila la heri Raisi Kikwete.

    Mwenye macho haambiwi tazama.Tusubiri tuone.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...