
Kamishina wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja akimshukuru Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya BARCLAYS Bernabas Waziri kwa Benki hiyo kutengeneza vitabu 2400 na vipeperushi 9000 vya ulinzi shirikishi vyenye thamani ya Tshs. 4,000,000/= vitavyogawiwa kwa jamii


Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya BARCLAYS Bernabas Waziri akiwaonesha kitabu cha Polisi Jamii kilichotengenezwa na Benki hiyo kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi kuhusiana na swala zima la ulinzi shirikishi huku Kamishina wa Polisi wa Operesheni na Mafunzo Paul Chagonja akimuangalia kwa makini

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya BARCLAYS Barnabas Waziri akiongelea leo katika makao makuu ya jeshi la polisi juu ya Benki hiyo kutengeneza vitabu 2,400 na vipeperushi 9,000 vyenye thamani ya Tshs. 4,000,000/= vya Mpango wa Ulinzi Shirikishi baina ya wananchi na Jeshi la Polisi . shoto ni Kamishina Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja na kulia kwake ni Msemaji wa Jeshi la Polisi Kamishina Msaidizi wa Polisi Esaka Mugasa.
Bwana Michu,huyu jamaa mkurugenzi wa fedha utakuwa umekosea jina,alikuwa bosi wangu stan chat one time jina lake ni Samuel Nyaki unless awe amebadili jina..
ReplyDeleteHajabadili jina, hata mimi alikuwa bosi wangu wakati fulani!!!!!! Michu umefanya makusudi au ni bila kukusudia? Anaitwa Sam au Bombaaa!!!!!!
ReplyDeleteMdau Issa Muhidini kweli umeMIX majina. Bwana Waziri B ni Mkuu wa Finance. Pse correct.
ReplyDeleteMdau wako, UKEREWE.
kaka michuzi mimi nauliza, je huyo mkurugenzi ameoa au? maana sioni kale kapete wanachovaa walioa. kama hajaoa niunganishie kaka yangu mchuzi, maana natafuta mume mimi hasa aliye kwenye sehemu kama hizo za pesa fezwa ahahahaha, who doesn't like money?
ReplyDeletebro michuzi.. huyu mshikaji anaitwa samuel nyaki.. waziri barnabas ndiye mkuu wa finance hapo barclays lakini siyo yeye huyo kwenye picha..
ReplyDelete