
HABARI TOKA DODOMA SASA HIVI ZINASEMA KUWA SPIKA WA BUNGE MH. SAMWEL SITTA AMETANGAZA KWAMBA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA AMEAMUA KUJIUZULU UWAZIRI MKUU.
MH. SPIKA BAADA YA KUTANGAZA HILO AMESEMA MJADALA WA RIPOTI YA RICHMOND, NA SIO MJADALA WA LOWASSA, NDIO UENDELEE. NA NDICHO KINACHOFANYIKA HIVI SASA HUKO BUNGENI.
HABARI ZAIDI ZINASEMA KWAMBA MH. LOWASSA AMESEMA KWAMBA INGAWA HAJAMTAARIFU JK UAMUZI WAKE HUO, AMEAMUA KUJIWEKA KANDO
Whaaaaaaaaaaaaaaaaaaat!!!! Is this for real? OMG! what is going on there?
ReplyDeleteAsante kwa kaka Edo kuonesha initiatiave. Na wengine wafuate nyayo, Nazir, Ibra, Arthur na wengineo wote waliotajwa.
ReplyDeletePia warudishe hela zetu. Tuna machungu sana.
Michuzi big up kwa kutupa "livescores". Nakukubali sana kaka.
Bado ripoti ya BOT- EPA na madini kina Zitto.
Mungu ibariki Tanzania.
HUREEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE! Mungu wangu nchi yako tunakufa maskini kwanini?!! Jamani, hata aibu alikuwa hana!
ReplyDeleteNilishangaa! Alikuwa anasubiri nini toka jana?! Ni ajabu sana kwa kweli. Wengine wa chini wana hali mbaya sana. Kikwete kweli ni kiboko!
ReplyDeleteSio sababu,
ReplyDeleteWala Hajakwepa bado,
Tutakutana nae huko huko mitaan na mahakamani
Hureeeeee, uamuzi wa busara sana huo Mr. Edo, kama inawezekana jiuzulu na ubunge tu
ReplyDeleteimekaa vizuri hiyo, hawa watu walishatakiwa kuachia ngazi sio leo. na hao akina Karamagi na Msabaha wanangoja nini mpaka sasa hivi? waondoke haraka sana na baada ya hapo tunachosubiri ni kuona wanapelekwa mbali zaidi ya hapo. watu tunateseka kila kukicha kwa sababu zao hawa fisadizi. naona kaamua kumpunguzia kazi JK, au anatuyeyusha tu inawezekana kamwambia japo sio kwa maandishi maana ni mshikaji wake. Aluta continua, wadumu akina Slaa wanaojua kuibua mambo bila woga
ReplyDeleteI tell you this is more than GOOD NEWS na bado ni lini tuanze kumfilisi. kikwete should know that the man was a spoiler.Congrats to Dr. Mwakiembe and the Team
ReplyDeleteHaya ndio tulioyategemea haya safari njema wasalimie Kighoma.
ReplyDeleteEheee mambo yamekuwa mambo... Kujiululu kwa Lowassa hakutoshi...bado wengine wengi wanatakiwa kufanya hivyo na vile vile wanatakiwa wafidie gharama tunazoingia watanzania kwa kuingia mikataba feki..
ReplyDeleteKweli Lowasa amefanya uamuzi wa busara.
ReplyDeleteNinachumshauri Mwakyembe akihadhari na lolote lile litakalotia doa umaarufu wake. Ninakumbuka suala la Prof.S.Mbilinyi (alikuwa waziri wa fedha) lilivaliwa njuga na Mh. Iddi Simba, baadaye Mh. Iddi Simba naye akavaliwa njuga na akina Mzindakaya naye akajiuzulu.
Bila kusahau hadithi niliyoisoma nilipokuwa mdogo ya: "Mtego wa Panya huingia waliomo na wasiokuwamo" kutoka kitabu cha hekaya za Abunuasi.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake
Ni uamuzi wa msingi kwa heshima yake binafsi, ya mwenza wake JK na CCM kwa ujumla.Bado, wengine.
ReplyDeletekachukua uamuzi wa busara mie sikuona namna yeyote ambayo angeendelea kuwa hapo alipo kutokana na kashfa hiyo tena ilitakiwa jana hiyo hiyo ajiuzuru na wengina nao wote wawajibike kama yeye.
ReplyDeletehata kiwira waliohusika nao wachukuliwe hatua na hata hawa wa uungo gesi wanaolipwa pesa ya bule wachukuliwe hatua huwezi klipwa bila kudeliver mambo ya kihuni bayo
Ebwana eeh!Michuzi unatisha,you r just so current.
ReplyDeleteSiwezi kusema natoa pongezi kwa Mh. kuamua kujiuzulu..No way..he already has accumulated lots of wealth for himself and the entire family..wacha akapumzike after all he has never been that much of a mchapa kazi.
Shemejio M.M
nakasikia ka wimbo ka AKUDO kwa mbaaali"ukisikia nimejiuzulu usifanye msiba ila sheherekea kwasababu nina roho mmbaya"...Oops nimekosea wimbo!!!!
ReplyDeleteboys 2men imesambaratika.Kwa kweli mlitufanya wajinga umeme tulipie bei kubwa kwa ulafi wenu hizo pesa nani kakwambia utakufa nazo? Na washikaji wako waombe msaada ktk tuta kama wewe.
ReplyDeleteNgoja niwe wa kwanza kuchangia!!
ReplyDeleteMichu nimemsikiliza vizuri sana EL wakati wa hoja yake ya kujiuzulu! Nimeamini Tanzania kweli hatutaweza kupambana na rushwa, jamaa anagoma kwamba ahusiki! Anadai kwamba amesingiziwa! Hivi ni kweli? Mbona kila kitu kilikuwa wazi? Kamati ile ilifanya kazi yake bila upendeleo na yeye anadai kwamba wanamwone wivu na uwaziri mkuu wake!!!!!
kwa nini mjadala kuhusu Lowasa usiwepo? Kwani Richmond ilijirich yenyewe?
ReplyDeletembona mjadala ulikuwa juu ya kuunda tume kuhusu Buzwagu ukageuka na kumuhusisha aliyeleta hoja mpaka akasimamishwa?
Kama mimi ni mbuge nisingekubali kirahisi ningependa rohasa aseme yeye anavyohusika au kutohusika tusikie to kinya chake.
Pili hili si tu suala la kustep down ni mtuhumiwa kuanzia sasa hivyo afikishwe mahakamani.
JK ana kazi sana pole kini ndio ukuu kwa hili utajijengea heshima.
Hii ni habari njema kwangu!
ReplyDeleteSASA NIMEKUMBUKA HAYATI BABA WA TAIFA KUWA KAMA UNAMPENDA MTU NENDA KANYWE NAE CHAI KWENU.
ReplyDeleteKWA USHAURI MH.RAIS HILO BARAZA LAKO WENGI NI WABABAISHAJI ONDOA. KIDONDA CHENYE USAHA LAZIMA NZI AKIFUATE.
Napenda kutumia fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Edward Lowassa (Mb) kwa uamuzi mgumu na wa ujasiri aliouchukua wa kujiuzuru wadhifa mkubwa aliokuwanao. Ni jambo la nadra sana kwa viongozi wa bara letu kufikia uamuzi wa jinsi hii. Nasema hivyo kwa sababu pamoja na kuwa ripoti ya kamati ya Dr Mwakyembe haikuwa na ushahidi wa moja kwa moja wa kuhusika kwa Mh Lowassa katika kuibeba kampuni ya Richmond bali ushahidi wa kimazingira tu, bado Mh Lowassa ameamua kujiuzuru ili kutoa nafasi kwa Mh Rais kufanya kazi yake kwa uhuru zaidi.
ReplyDeleteTutaukosa sana uzoefu na uongozi wa kijasiri alionao Mh Lowassa. Hata hivyo Mh Rais kwa uzoefu wake na kwa jinsi anavyoufahamu utendaji kazi wa kiadilifu wa Mh Lowassa, pengine akamrejesha katika serikali yake.
Ni hayo tu kwa sasa
Mmmmmm! mimi chimo kabicha
ReplyDeleteMungu ibariki TANZANIA na watu wake
ReplyDeleteaaa..sipati picha katuni ya kesho ya KP...
ReplyDeleteEne wei..Safari moja uhanzisha nyingine.
Ni matumaini yangu mawaziri wengine wiki hii watafuata nyayo za Edo.
Ene wei,Tutafika tu
HILO HALIKWEPEKI NAOMBA WADAU MNISOMESHE.BADO TUNAWEZAJE KUCHUKIUA HATUA ILI KIRANJA HUYO APATE STAHILI YAKE?MDAU UK
ReplyDeleteAmelazimishwa kujiuzuru. Ngoma ilikuwa ngumu kwake. Kama anavyosakamwa Balali kwamba arudishe mali zetu, Lowasa naye arudishe. Hatuwezi kupandishiwa bei ya umeme wakati wachache wanaitafuna Tanesco.
ReplyDeletehuyu mjamaa lazima ajiuzulu kwani ripoti imesha sema wizara yake imehusika sana,sasa hakuna mjadala tena we umeme unapanda bei kama vile hatuwezi kutumia vibatali bwana,na wengine lazima wafuate tu hakuna kuoneana haibu sasaivi,na bora walikua wamerekani nasasa wapopo wakijua tu kuna mazoba bongo lazima watakuja na ya kwao.....
ReplyDeleteMICHUZI NAOMBA NISHAHIHISHE USEMI WAKO, TENA KWA HERUFI KUBWA KABISA. HAJASEMA KWAMBA HAJAMTAARIFU RAIS, KASEMA KAMWANDIKIA BARUA RAIS YA KUJIUZULU, NA BADO HAJAPATA MAJIBU. SASA KAMA BARUA IMEANDIKWA LEO ASUBUHI KABLA YA KWENDA BUNGENI, UNATAGEMEA MAJIBU YA RAIS YAWE YA HARAKA KIASI HICHO.
ReplyDeleteKWA KIFUPI JAMAA KAJIUZULU....TUNAMSHUKURU SANA KWA KUTUIBIA PESA ZETU. UBAYA UNALIPWA HAPA HAPA DUNIANI. MAMBO YA MBINGUNI NI MENGINE.
Du Hatimaye tembo kaanguka. Naipongeza tena kamati teule kwa kuweza kuweka mambo hadharani mapka kisiki kikang'ooka. BIG UP Mwakyembe and your Team. Kwani huyo jamaa kujiuzulu ni nini? Aende zake tumechoka, tuna majiko ya umeme tumogopa hata kutumia kumbe yeye ndiyo mpandishaji umeme
ReplyDeleteGOOD RIDDANCE!! ANNA MAKINDA FOR NEW PM.
ReplyDeleteAkafie mbele, fisadi mkubwa.
ReplyDeleteWatanzania tumeamka sasa, nawashangaa sana hao wabunge wanaomtetea Lowasa, mwacheni aondoke, we are tired the the shames
ReplyDeleteMichi kazi safi endelea kutuma news maana wengine tuko makazini hakuan Radio wala Tv. Vipi yaliyojiri Dodoma kwa JK?
ReplyDeleteHongera Michuzi kwa kuwa 'sharp' katika kutupa habari wasomaji wa blog yako. Bila shaka hii habari ya Waziri Mkuu umeipata katika chanzo ambacho si 'credible' kwa kuwa inatofautiana kidogo na taarifa halisi.
ReplyDeleteWaziri mkuu ametangaza mwenyewe kujiuzuru baada ya kudai kuwa kamati ya Dr. Mwakyembe imemtuhumu bila kumpa nafasi ya kujitetea. Na kwamba ameshamwandikia Rais uamuzi wake huo, ambao alisema Rais bado hajaujibu.
Kutokana na mkanganyiko huo, spika amelazimika kusimamisha shughuli za bunge hadi saa 11 jioni, si kwamba bunge linaendelea kama ulivyoandika.
Pamoja na kasoro hizo bado nakupa hongera!
Bwana Michuzi kwanza kabisa napenda kuchukua fursa hii kukupongeza wewe binafsi kwa kuwa shapu sana kutuwekea habari mbichi kabisa.Nimekuwa kwenye mjadala mkali na wadau wenzangu huko nyumbani juu ni nini kitafuatia baada ya report ile.Hata kwenye blog yetu ya hii ya jamii jana nilitoa maoni na kuelezea nini watanzania wategemee.Sasa kama dakika 20 zilizopita kuna mdau alinitumia sms alinijulisha kuwa Mh.Waziri Mkuu Lowasa kajiuzulu.Kwa kuwa nipo nakamua book kufukuzia nondoz kando na computer yangu ikiwa ni saa 9.30 usiku kwa hapa Ohio-USA, nimekuwa nafungua blog yetu kila baada ya dakika ili nione kama kuna breaking news kuthibitisha kama ni kweli.Hatimaye nakutana na maandishi mekundu kwa herufi kubwa yakithibitisha hilo.Sasa hatua ya Mh.Lowasa kujiuzulu.Kama kada wa CCM nampongeza kwa uamuzi huo ambao kimsingi ni mzito sana na ambao pengine wengi hawakuutarajia.Napongeza kwa kuwa likuwa ni lazima kufanya uamuzi huo mchungu sana ili kutuliza hali ya mambo ambayo dhahiri,shahiri ilikuwa inakipeleka chama na serikali yetu mahali ambapo tusingepatarajia kabisa.Kama alivyosema kwenye taarifa yake kuwa sasa wabunge waijadili Richmond na sio Lowasa,ni kweli kabisa.Maana nina hakika kabisa joto lake sana limeshuka kabisa na inawezekana kabisa siku 2 walizotengewa wabunge kuijadili report zikawa ni nyingi.Nasema hivyo kwasabu sitegemei kuona kama bwana mkubwa amejiweka pembeni mawaziri wake wabaki.Ndio kusema mapendekezo ya kamati yameanza kuzaa matunda kiasi cha kuuzima mjadala.Ndio,maana inajadili nini tena wakati wahusika wamekubali kuwajibikika? Ndio maana nasema mjadala haupo tena.Labda kutoa maangalizo kwa siku sijazo.Nampa pole sana Mh.Lowasa,maana ni ukweli kwamba matatizo yanampata binadamu.Na kwa kweli,kwa wanaCCM tunapaswa kulia wote.Waswahili wanasema "mchuma janga hula na wa kwao".Kwa hiyo hatuwezi kufurahia jambo hili japo katika mantiki yake ni uamuzi busara kwa maslahi ya taifa na kukirejeshia chama heshima,hadhi na imani kwa watanzania.Mzee wangu JK,naomba uupokee uamuzi wa Mh.Lowasa kwa ujasiri bila hofu yoyote.Najua ni majaribu makubwa sana.Hatahivyo,jipe moyo mkuu.Chukulia kama ni changamoto kubwa na muhimu katika utawala wako.Mungu aliyekuinua kuwatumikia watu wake ana makusudi mema nawe.Kumbuka umma wa watanzania wana imani nawe sana.Na hao ndio ulioingia nao ubia wa kuongoza nchi na kuwatumikia.Tunatambua nia yako ilikuwa njema kabisa,lakini unapofungua dirisha kuruhusu hewa safi iingie,sio ajabu kuona inzi na mbu wakiingia pia.Hakuna kurudi nyuma.Songa kifua mbele kwa ukakamavu wananchi tuko nawe.
ReplyDeleteMungu Ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wetu!
Namuonea huruma sana muheshimiwa kikwete kwani sasa ile kasi mpya na ari mpya inabidi ibadilike anyway ni uamuzi wa busara muheshimiwa kujiuzulu unfortunately tunataka na ufatiliaji wa tuhuma hizo huku ulaya zinaanzishwa probes kuchunguza hizo tuhuma.
ReplyDeleteNa sio kutaarifiwa basi mtu kajiuzulu then anaendelea kula kuku tu lazima afilisiwe na kama ikiwezekana kufungwa kabisa!!!!!!!!!! Tuwe kama Thailand, Malaysia, Singapore kwa kasi kikwete tuko Ulaya sio tunamalizia nondo zetu tunakuhakikishia tunairudisha Tanzania katika ramani ya dunia kiuchumi na kimaendeleo
Kaza Buti Mzee JK
Usirudi Nyuma
Tuko nyuma yako
Wako
Mwenye uchungu
Karamaji na mwenzio Msabaha , haya mfuaate upesi kujiuzuru, hahahaha, karamaji safari imewadia sasa, Mkuu ameshaanza usijifanye kuzuga wewe mfisadi mkubwa!!1
ReplyDeleteKwakweli Sasa Hii ndio Tanzania tunayoitaka;
ReplyDeleteTanzania Blia Mafisadi
Tanzania Bila Rushwa
Tanzania Bila Wezi ;
Mungu Ibariki Tanzania
Watu WeeeeeeeWeeeeeeeeeeeee
Afadhali sana huyu jaamaa kajitoa maneke kulikuwa na Fununu anataka kugombea urais mwaka 2010 kwa kumpika Chini Jakaya katika kura za ndani ya CCM,
na alikuwa ameshaaandaa kambi nzito ;
Swali JE ATAENDELA KUWA MBUNGE AU NDO NAUBUNGE GOODBYE??
kwa kweli waendeleekujiuzulu hawa ni wanyonyaji wasio na huruma hata kidogo mtu unamyonya mpaka mfupa ,wale kidogo wabakizie na wenzao
ReplyDeletemimi bill pale nyumbani nalipa postpaid, nilikua nalipia tshs 30,000 per month hapo situmii jiko la umeme wala birika ,wala ni pasi mafridge matatu, tv na feni moja tu basi mwaka huu jan
matumizi haya haya nimepata bill ya elfu 92,000/= kwa kweli nimechanganyikiwa taa zetu ni tube light, nasema hivi sbab mimi ni mtanzania wa kawaida tu
bei imepanda mno jamani
kikwete akae akijua kua mimi sina imani nae tena ,anatumia kodi zetu kwenda nje kila siku,
nasema hivi watu wameelevuka kwa sasa tumechoka na kuibiwa ,tunaishi maisha ya kuhangaika, kwa ajili ya manufaa ya watu wachache
mlioko ulaya komaeni hukohuko huku serikali hii ni ya wezi wenye njaa kali
JAMANII NGOJENI WAOSHA VINYWAA NA WADAU WAAMKE WAANZE KUTAPIKAAA??
ReplyDeleteHivi kwani kujiuzuru na ubunge haiwezekani? asijitetea chochote, ni bora ameachia ngazi..kama mbwai,mbwai bwana!
ReplyDeleteSIKU ZOTE TUNAONGEA KWENYE BLOG HII. KUNA WATANZANIA WENGI VIONGOZI MAFISADI NA WASIO WAADILIFU. WATU WAMESAHAU KABISA MAMILIONI YA WATANZANIA WANAOKUFA KWA KUKOSA "BASIC SERVICE" KAMA HUDUMA ZA AFYA NK.
ReplyDeleteNDIYO MAANA TUKIFIKIA HATUA KAMA YA KENYA KWENYE UCHAGUZI UJAO SITASHANGAA. MAANA WANAIBA KURA KUINGIA MADARAKANI WATUIBIE.
MUNGU WABARIKI HAWA:-
1. Mhesh. SLAA, ZITTO KABWE, Mch. MTIKILA nk.
2. DAKTARI MWAKYEMBE NA KAMATI YAKE YOTE.
3. WABUNGE WOTE WALIOONESHA UCHUNGU SAFARI HII KATIKA MIJADALA MBALIMBALI.
4. WATANZANIA WENYE UCHUNGU NA NCHI YAO.
Anony,
MAREKANI KWA BUSH.....
SIKU ZOTE TUNAONGEA KWENYE BLOG HII. KUNA WATANZANIA WENGI VIONGOZI MAFISADI NA WASIO WAADILIFU. WATU WAMESAHAU KABISA MAMILIONI YA WATANZANIA WANAOKUFA KWA KUKOSA "BASIC SERVICE" KAMA HUDUMA ZA AFYA NK.
ReplyDeleteNDIYO MAANA TUKIFIKIA HATUA KAMA YA KENYA KWENYE UCHAGUZI UJAO SITASHANGAA. MAANA WANAIBA KURA KUINGIA MADARAKANI WATUIBIE.
MUNGU WABARIKI HAWA:-
1. Mhesh. SLAA, ZITTO KABWE, Mch. MTIKILA nk.
2. DAKTARI MWAKYEMBE NA KAMATI YAKE YOTE.
3. WABUNGE WOTE WALIOONESHA UCHUNGU SAFARI HII KATIKA MIJADALA MBALIMBALI.
4. WATANZANIA WENYE UCHUNGU NA NCHI YAO.
Anony,
MAREKANI KWA BUSH.....
HALELUYA, HALELUYA, HALEYUYA HALELUYA HALELUYA. Mungu Mwenyezi ametutendea mema HALELUYA!!! Niacheni niimbe HALELUYA KUU japo ni wakati wa KWARESMA mana nimefurahi sana.Kweli mambo ya Mungu ni ya poleple lakini akiamua kujisdhihirisha, matendo yake ni makuu na yanatisha kama nini. Ah KAKA KAJIUZULU AMA KWELI HAKUNA MAREFU YASIYOKUWA NA NCHA!! Ngoja niwahi zangu nikajipongeze na kuhitimisha furaha yangu kwa kitimoto na ndovu baridi pale JJ SINZA MAPAMBANO.Karibuni sana wadau wote mliofurahishwa najambo hili. Mapambano bado yanaendelea na Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
ReplyDeleteSAMAHANI ANON HAPO JUU WA ohio samahani tena ila naomba nikwambie kwamba nchi yetu inazidi kuwa maskini kwa ubinafsi na uzandiki wa watu wachache wenye mawazo yako. Lowassa is a thief simple! Big time theif! Yaani huyu jamaa na kodi zetu anazolipwa marupurupu na mishahara mamilion bado anatufanyia haya madudu? eti kafanya uamuzi wa busara? which uamuzi, hapa kinachofuatia apelekwe kwenye vyombo vya sheria! This is way too much.
ReplyDeleteAu mkubwa kwa vile uko OHIO hujui machungu ya watanzania hapa nyumbani? mtu analipwa mshahara wa elfu sitini halafu taifa linamlipa Million 152 kila siku Lowassa kupitia kampuni yake hewa? eti tumuonee huruma? Huyu ni muuaji zaidi ya INTERAHAMWE!
Eti hakupewa nafasi ya kusikilizwa? Mwakyembe alitutangazia watanzania wote wenye chochote/maoni waende kwenye kamati yake! Mbona hakwenda? People wote sio wajinga kama mnavyotufikiria. Huu UFISADI wa kuiweka mbele CCM kuliko taifa letu ndo unatufikisha hapa!
Nasema hivi, Lowassa na wote waliotajwa waondoke na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. Watanzania tumechoka, kuibiwa na watu wale wale, siku zote. Mpaka wengine wameshaamini kwamba walizaliwa wawe maskini! Mdau wa Ohio Iam sorry I thought because you are in western countries ungekuwa na uelewa zaidi ya huo, but unfortunately you are worse off!
Lowassa has done more damage and He has proved right Nyerere aliyetwambia kwamba huyu jamaa si muadirifu! YAMETIMIA.
Tanzania ni ya watanzania wote, masha bora si kwenu tuu watoto wa wakubwa na viongozi! CCM watch out, watu tuna hasira na nyinyi...Iko siku kitaeleweka tu, ngoja tusake nondo!
Hongera lowasa kwa kujiuzuru
ReplyDeleteNimepokea kwa furaha sana kwa kujiuzulu mh lowasa ni jambo la kujiheshimu sana, na kukbali matokeo, ni ushujaa na mapenzi ya dhati ya kuwajibika ktk nchi ili kutoa nafasi kwa watu wengine kufanya kazi kwa mapenzi ya dhati toka moyoni ktk nchi hii
Sikuona sababu ya kusubiri report ya Mwakyembe ungeachia ngazi mapema sana tangia mwanzo
Ulizoiba zinatosha nenda katumie na mke wako sasa kwani maisha bora ya lilenga zaidi ktk mfuko wako binafsi. sijaamini kama mtu kama wewe ulikuwa unaitumbukiza nchi ktk janga la kifo namna hii,maisha yamekuwa magumu sana kila mahali nchini Tz, wewe unashika uchumi wa nchi hii ktk mikono yako.
naomba uombe msamaha kwa wananchi wa wazawa wa Tanzania, kwani kila kilio chao hutobaki salama kabisa.
Mungu ibariki Tanzania
Email:moshaalexus@yahoo.com
Tuwalinde Mwakyembe na Michuzi dhidi ya Tindikali
ReplyDeletemimba tayari tumeanza kuona watoto na badooooooooo!!kwani wako wengi sana,kajitoa kigogo wao bado vifaranga sasa!!!!!WADANGAYIKA OOOOOOOOOOOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE MUKAMA~SEOUL
ReplyDeleteKIKWETE ANAPONZWA NA USHKAJI NA WAKO WENGI WATAKAO KUANGUSHA.....
ReplyDeleteANGALIA KAKA JIPANGE TENA
"Haya Edward sisi tulikupenda lakini Richmond wamekupenda zaidi...wasalimie Kighoma"
ALL IN ALL KIWETE IS THE BEST TO ME HOW MANY PRESIDENTS HAVE PASSED WHAT HAVE THEY ACHIEVED THAN RUSHWA ANGALIA ANAVYOPAMBANA WAZI ALIWAAAMBIA ALIVYOANZA TU KAMA UNAFANYA KAZI KAMA INAVYOSTAHILI ULL STAY UNLESS OTHERWISE ULL BE KNOCKED OFF SASA HAYO MAJIMAMBO.JAMANI WATANZANIA TUJALINI AMANI PIA OHHH HAYA MAMBO YANATISHA SANA ASWA WALALA HOI MAANA NDIO WANAKUWAGA WABAYA SANA KWASABABU YA HAKI YAO.NDIO MAANA UJAMBAZI BONGO KILA SIKU WATAHAWANA NJIA YA KUISHI
ReplyDelete"Because I have been linked to this scandal, I have decided to write to the president asking to be relieved of my duties," Edward Lowassa told MPs.....vp kuhusu kuturudishia mkwanja wetu??? kujiuzuru siyo issue kwa wananchi tunataka asongeshwe mbele na afilisiwe
ReplyDeleteWakubwa! msimpe huyu jamaa sifa za bure! Huyu hakujiuzulu huyu! Jana usiku kuliwaka moto huko kwenye vikao vyao vya ndani vya sisi-M! huyu atakuwa ametakiwa AANZE kwa kwenda mbele!
ReplyDeleteWaziri mkuu mzima utaachiaje ngazi kwa maneno unayosema ni ya kusingiziwa!!!
Take five, Mhesimiwa Mwakyembe!!
good riddance!
Haya, na wengine waanze kutia maji mabichwa yao...!!! I am SOOOOO happy!
Thanx Bro Michu for this info. Sasa kilichobaki ni kuwaunganisha Lowassa,Karamagi,Yona,Mkapa,Msabaha nk kwenye kuadabishwa,they should be accountable.
ReplyDeleteAhsante sana Bwana michuzi kwa habari hizo.Mh.Lowassa na wote waliohusika sio kwamba wanapaswa wajiuzulu bali wanapaswa kukamatwa moja kwa moja kutoka jumba la bunge nakufikishwa katika vyombo vya sheria.Accounts zao kuzuiwa pia mali zao wakati sheria inachukua mkondo.Hii itafanya kwa kila kiongozi yeyote kua makini anapokua madarakani,kwani ikiishia kujiuzulu tu kutampa nafasi kiongozi yeyote kujichotea mapesa na baadaye kujiuzulu na kuendelea kutumbua pesa zake alizozipata kwa ufisadi.KUJIUZULU HAKUTOSHI,MUNGU IBARIKI TANZANIA.
ReplyDeleteJAMANIII.....NASKIA RAHAAAA..UTAM!! ME NASUBIRIA ZE COMEDY WATAKAVYOHARIBU..HA HA HA HAAAA!!! UUWIIII..
ReplyDeleteNIMEFURAHI SANA JAMANI, YANI NIMEPIGA KIGEREGERE KIKUBWA SANA, HAWA WATU WAMETUFANYA MAHANITHI SANA!! YANI NINA MACHUNGU MIE JAMANI SIJUI NIKAWARIPUE NA GOBOLE LANGU WOTE?? NAFUU MUANZE KUVAA KIZUIA RISASI!! PUMBAFFFF..MICHU USIBANE!!
Wapendwa Hizi ni Habari Njema. Narudia HABARI NJEMA. Kwani Imeandikwa 'NI LAZIMA MTU MMOJA AFE KWA AJILI YA WENGI' 2010 SI MBALI, ccm wameshatoa kafara tumeliona, lakini si lazima tulikubali. mafisadi wako wengi, tunataka mikataba migine pia ipitiwe hasa wa buzwagi.
ReplyDeleteHILI PIA NI CHANGA LA MACHO. ili tuseme wanafanya kazi na tuwachague tena, hatutaki kufukia mashimo wakati viazi vimeshaliwa, tunataka tule viazi wote, haisaidii chochote, bado hawa jammaa ni wazembe, Kikwete mwenyewe a step down, najua naye anahusika tu. si bure. pesa zinarudi vipi? akijiuzulu inatosha? afungwe tu ili anangalau asizitumie tena. Tena nasikia aliiba mashine za kufulia za hospitali akkanzisha dry cleaning business, arudushe zile mashine mount meru hospital pia. Jamaa ni MWIZI kabisaaaaa.
SAmaki Mmoja akioza Fridge bovu mwaga wote nunua ingine. Tuwamwage wote na fridge CCM bovu, 2010 tupigie Kura wengine Yaani Upinzani, Chadema, NCCR au wengine wowote.
SASA NEXT PM NI NANI WADAU?
ReplyDeleteafadhali amejitoa, mi mnaniudhi sana, haya na wengine jitoeni, mana nina hasira na nyie, UFISADI WENU NDO UNATUFANYA WENGINE TUNAISHIA KUBEBA MABOKSI NCHI ZA WATU....bila ya hivyo, tungekuwa nyumbani kwetu tunaishi kwa raha musratehe, ila kila tukifirikia namna ya kuanza kusettle nyumbani ni headache kubwa, wenyewe wachache wamejilimbikizia mali, nchi wameishikilia utadhania ya kwao binafsi...watoto zenu tumesoma nao huku nje, wamemaliza mmewaambia warudi upesi, bado mko kwenye system mtawasaidia, haya wamesharudi mmewapa kazi, nafasi nzuri nawao wanajijenga, tumebakia watoto wa mbwa, tunabeba maboksi tu ughaibuni....
ReplyDeleteSINA HAMU, WATANZANIA KAENI CHONJO, UCHAGUZI 2010 KUNA VITA KAMA YA WAKENYA YAJA........
we blog yako sasa leaves much to be desired. uliyobreki newzz partly ni kweli partly si kweli. Ni kweli kuwa amewasilisha barua ya kujiuzulu. lakini bunge limesitisha kikao hadi saa 11 jioni ili kuamua ni namna gani bora ya kuendelea na mjadala. mind you kwa mujibu wa katiba ombi lake likikubaliwa ina maana nafasi za mawaziri ziko wazi kwahiyo hakuna serikali bungeni.its advisable kuwa uwe na namna ya kupata taarifa sahihi.
ReplyDeleteWaapsss jamani wamemuonea Lowasa kijana wa watu mbona hawakumhoji akatoa kile alichokuwa nacho moyoni?This is not fair kabisa Lowasa is innocent na saga hili aliingizwa mkenge tu.
ReplyDeleteBOOOOOOOOOOOOM!!!!!!!!!
ReplyDeleteUKIPORA HAKI Ya maskini Mungu atakutandika hapa hapa duniani.Ndiyo maana mijizi mingi na mifisadi ina migonjwa kama visukari,BP,na haiwezi kula chumvi wala sukari Mungu kaikomesha kaachia sukari na chumvi wafaidi maskini wanaowaibia kodi zao.
ReplyDeleteNa ndiyo maana mingi inaishia kuadhirika.Kweli Mungu si Athunmani.Hawafanani kabisa na Athumani.
Hongera mheshimiwa Mungu kutusaidia kupigana na mifisadi.
"Kioo, kioo, alikivunja nani, sijui sijui, wa mwisho akamatweeeee!".
ReplyDeleteNadhani sasa Mh. JK atakapokuwa katika ziara za kikazi nje ya nchi, akiulizwa mbona nchi yako ina kila namna ya nanihii, lakini nyinyi mko nanihii, sasa atakuwa na jibu.
[Vyungu vinatokota Buzwagi na EPA, ambayo ni maeneo madogo tu].
Lakini naamini kwa asilimia kubwa tu, kuwa kuna Waandamizi fulani fulani katika wizara nyingi tulizonazo kwamba sasa hivi matumbo yako MOTO!.
Ombi kwa Bunge Tukufu, and of course kwa Mh. JK, tumalizane na hizo kwanza halafu wapinzani waibue na nyingine, nazo mzishughulikie. Heshima itarudi tu.
Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote................
ANNA MAKINDA ndio the next PM.
ReplyDeleteNakubaliana na anony mmoja hapo juu.
Nyie subirini tu
Hiyo nimekubali. Sasa tuanze mahakama haraka sana. Takukuru nao wawemo!
ReplyDeleteSAMAKI mmoja akioza basi wote latika kapu wameoza.Haitoshi kujiuzuru kwa waziri mkuu pekee yake,RAIS naye anatakiwa kujiuzuru kwani ni yeye alie wateua hao watenda kazi wake.Wamemlet down basi naye aondoke jukwaani ili kupisha waigizaji wengine.
ReplyDeleteANNA MAKINDA ndio the next PM.
ReplyDeleteNaungana na anony mmoja hapo juu.
Nyie ngojeni tu!
Wana Blog, yaani hapa Univ of Dsm wanafunzi wanaandamana na kuimba Lowassa rudisha hela zetu, huku wameshika mabango mengi sana yanayoorodhesha mafisadi wa Richmond. Zaidi ni kuwa Kilio cha mafisadi! Mimi natamani nijiunge nao maana bei ya umeme inanitatiza. Usiku nikisikia hata feni limewashwa nawagongea mlango watoto wazime maana ugali utakuwa haupatikana kwa jinsi Richmond anavyonitafuna kwa nguvu! Aondoke na arudishe fedha zetu na wengine wote waliohusika.
ReplyDeleteHistoria inajirudia: Hii ni mara ya pili sasa! Mara ya kwanza yalimkuta Ndugu Rashid Mfaume Kawawa na MV Rajpar! safari hii yanamkuta Manywele na Richmond Development!
ReplyDeleteMtiMkubwa.
Kwa kweli yametufika sasa ni wakati wetu sasa UAMUZI WA KUJIUZULU NI POA
ReplyDeleteKama wazungu wanavyosema it is about the time. Kwa wale ambao mnadhani Lowassa asinge jiuzulu nawasupport kabisa kwani hii ni shock news, hasa kwa wengi wetu tulio nje ya Tanzania. Going back kwenye point, Lowassa hakuwa na ulazima wowote wa kuhojiwa, however yeye ndie aliyekuwa mstari wa mbele kutetea scandal yote ya Richmond, kumbukumbu zangu zinaniambia aliwaambia wabunge wa CCM wache kushangilia swala la Richmond.
ReplyDeleteHii ni move nzuri sana kwake, kwani nina baadhi ya wadau wenzangu tulikuwa tunaplan kufanya maandamano hapa ughaibuni tukiomba Muheshimiwa ajiuzuri. Again, point yangu sio kusema kwamba bwana Lowassa is guilty, kwani hakuna litigation zozote zilizo failiwa, point muhimu ni kwamba muheshimiwa waziri alishindwa kufanya maamuzi muhimu pindi swala hili la Richmond lillipo lipuka. Kama muheshimiwa Lowassa angekuwa wa kwanza kuomba bunge liunde tume pindi tuu swala hili lilivyo bumbuluka basi leo tungekuwa tunaongea mengine.
Hongera zangu ziende kwa Dr Mwakyembe, kwani ameonyesha ufanisi wa juu kabisa katika kuorganize the whole report spectrum. Vile vile Prof Tenende wa pale Houston, Texas kwani aliweza kuonyesha doti hadi doti la majambazi hawa wa Richmond. Hili ni swala la kitaifa, i hope JK atavunja baraza zima la mawaziri kwani wananchi hawana imani nalo. Vile vile napenda kuwashukuru wandishi wa magezeti mbali mbali ya hapo nchini, ndugu michuzi kwa kutupa snap shot of what happening in day to day basis. I believe each Tanzanian who participate on this movement needs special Thanks.
Hakuna maendeleo pasipo mabadiliko.More to come, i believe we will see Zitto report about Madini which will be a slum dunk.
The next thing i believe ni sheria kuchukua mkondo wake. This people creaple our country, our economy, our hearts, our moral and our respect on global manner. They need to stand infront of Judge. I am so Happy leo. This is our time, this is our Era, Tanzania the Come back Kid,
Mdau wa US
Yap yap, aibu kubwa, watoto wake huwa wanajidai mno, at least sasa hivi watanyamaza kimya, serikali inastahili kurudushiwa hela yote na hawa mafisadi, ianzishe tume ya kusaka mali na fedha zinazohusiana na hizi hela za wizi kwani wnaoiba sasa hivi hawana wasiwasi hadi wakamatwe. Bila kuwa na tume maalum wizi wa fedha za serikali utaendelea.
ReplyDeleteeh kwa kweli hii inatuonyesha kuwa maombi ya watu wa mungu yanajibiwa,maombi yaliyomguruma uwanja wa taifa kabla ya mwaka huu yalikuwa kiboko,tumemwona mungu nchi hii ipate viongozi waadilifu Rwakatare kachomoza tayari,Rais kikwete wape watu kama hawa wizara nyeti hawatakubali mlungula,kwa kweli watanzania wengi tulio hapa Oslo tunaipongeza kamati ya mwakyembe kwa kazi pevu ,nzuri na ya kina,Bot nayo tunaomba wengine wapewe kadi nyekundu sio balali tu
ReplyDeleteRugaitika Revocatus
jk usipokuwamakini utatupeleka kenya hayo mambo ya kupeana kisa friend of mine yatakutoa hata wewe kwenye upresident nadhani kwenye hilo umejifunza chagua kiongozi kwa kuzingatia sifa sio sura wa urafiki
ReplyDeleteHeads will roll, kudadeki. Na bado!
ReplyDeleteNyani haoni shaurile, walivyomsakama Zitto bila kumpa nafasi ya kujitetea hawakuona hilo sasa umefikia kwake ndio imekuwa hivyo. waht goes around always comes back around. Ukikosa bora ujinyamazie taratibu usiseme hovyo mwisho utasema na visivyo kuwepo maana hata kama unasingiziwa ndio unazidi kuonekana mwongo, achukue desa kwa Ben na makelele yote kanyamaza kimya hataki bugudha mzee wa watu. Kujikosha ndio kunawafanya watu waseme ambayo hata hayapo kwa kutaka kuonekana hawana hatia.
ReplyDeleteMIMI MAMBO YA KUJIUZULU BILA KUCHUKULIWA HATUA SIPENDI.HUYO KIONGOZI WA SERIKALI NA KUTUHUMIWA KWENYE UFISADI LAZIMA APELEKWE MAHAKAMANI HILI HELA ZA WANANCHI ZIRUDI NA YEYE APEWE ADHABU KWANI WOTE HAO WALIKULA KIAPO KUTUMIKIA TAIFA LETU KWA UKWELI.MAMBO HAYA KUJIUZULU TU NA KUKACHIWA NDUGU ZANGU HAWA SIO MAKOCHA WA MICHEZO AMBAO TIMU IKIBORONGA TUNA WAFUKUZA AU WANAJIUZULU NA KOCHA MWINGINE ANALETWA TIMU INAENDELEZA LIBENEKE.HAPANA HAWA NI VIONGOZI WA NCHINA WASHITAKIWE.
ReplyDeleteOh hii ni habari nzuri sana yenye uzuri kupita kiasi, sasa naona Watanzania wameamka. Ukweli ni kwamba wakubwa walizidi kula na kasahau wananchi wao sasa ni wakati wao wa kuwajibishwa. Na sisi wananchi tunaomba awajibishwe kama wengine walivyowajibishwa. Na pia umeme upunguzwe bei ili watanzania wote waweze kutumia umeme, umeme ulikuwa unatumiwa na wao wenyewe tu maana ulikuwa bei juu sana kumbe zilikuwa ni hela zao za mifukoni. Na kama walivyopiga kelele kuhusu Balali na kudai alipe, tunaomba na Mh. Edo alipie hasara yote aliyoisababishia taifa. Tunaamini hasara si hii tu kuna mengine yatakuja mengi tu huko siku za usoni. Mfano mwingine kijana mh. wa watu Kabwe walijifanya kumpa adhabu eti kwa kusema waziri ni "muongo" ikapitishwa apewe adhabu ya kuacha kuwatumikia wananchi wake kwa uwakilishi wake bungeni, je sasa na hawa waliosababishia hasara kubwa ya mabilioni serikali pamoja na kuwatesa wananchi ambao ndo waliowaweka hapo walipo kwa kulipia umeme bei za juu zisizo halali, je apewe adhabu gani ya kufanana na alichokitenda??
ReplyDeleteJamani Watanganyika wenzangu,mnaonaje hapo tukamweka JOHN POMBE MAGUFULIII????
ReplyDeleteNdugu wadau wenzangu mliobobea kweny masuala ya sheria
ReplyDeleteHuku ng'ambo kuna mashitaka ya abuse of power
ambapo adhabu yake ni kurudisha mshahara woot tuliomlipa au kufilisiwa kiki ambatana na kifungo jela
sasa hili suala mnalionaje kwani ni wazee wetu ndio wanaoumia mpaka sasa kwa ufisadi wake
Vema kajiuzulu, waziri mkuu ajaye asitoke kwenye recycling plant. JK unao watu wengi wenye uwezo na nia ya kuijenga nchi si kama JK alivyosema enzi zake hapakuwa na wasomi na wanasiasa wakutosha
ReplyDeleteHaitoshi kujiuzulu..inabidi ahukumiwe na kurudisha pesa za walalahoi na wananchi wenye kuvuja jasho wa Tanzania. Baada ya hukumu pia bila kujali kuwa alikuwa waziri mkuu wa nchi mlafi..ahukumiwe na akakione cha mtemakuni huko jela! Vilevile afilisiwe ili uwe mfano wa viongozi wengine wafisidi na waroho wenye kukalia viti ili kujaza matumbo yao!
ReplyDeleteNawakilisha ....Kudumu Kujenga Nchi!
Serikali ya Valafi hoyiiiiiiiiiiiii!
Je mkataba wa richmond hausitishwi baada ya kuthibitika kuwa walidanganya kwenye zabuni? Tutaumizwa mapaka lini. Au nchi imekuwa ya vichaa kujifunzia kunyoa?
ReplyDeleteMagufuli si ndiye aliyemwomba rushwa Karamagi wakati wa uchaguzi wa NEC kule kwao, eti awagawie tumadini kidogo watu wa jimbo lake ili wamchague?? Rose Garden ameiwekea kifua.HAFAI ananuka turushwa tudogotudogo
ReplyDeleteMungu atupe nini tena.....labda aendelee kuwafichua.Maana mpaka kujitoa keshaona hali mbali.Tanzania we need to be serious na nchi yetu esp makini katika uchaguzi.
ReplyDeleteeeeeeebwanaeeeeeeeeeeeeeeeee duuuuu sasa boys 2 men imebaki sijui tuseme "boys 1 men" au vipi? na je huyu JK jamaa Lowassa si bonge la swahiba wake na tuone atamfanyaje, TZ kumekucha sasa na hii ni "kazi kwelikweli"
ReplyDeletemmoja mmoja ataondoka, mafisadi nyie, sasa Raisi si na wewe ujitoe maana uliwachagua mafisadi ina maana ulikua unapata cha juu
ReplyDeletena wewe tunaomba ujiuzulu tumekuchoka, hatuoni maisha bora wala nini
patachimbika mwaka huu
umenichekesha sana BABU MZEE REVO wa 2:12,,kawimbo katamu sana....
ReplyDeletekioo,kioo alikivunja nani....sijui sijui ,,waongo ndio wote....PITENI,PITENI...wamwisho akamatwe,atiwe gerezani..
kawimbo kaminikumbusha mbali,,kanafaa sana hapa....
INFWAKT MANY OF THE TOP GOVERMENT OFFICIALS, NEED TO LOWASALISE THEMSELVES, BEFORE ITS TOO LATE.
OOH, GO LOWASA ITS YOUR BADDAY..
GO KARAMAGI ITS YOUR BADDAY, GO MSABAHA ITS YOUR BADDAY...AMAKWELI ZA MWIZI 40
Inasikitisha lakini ili kupata maendeleo ya kweli lazima haya yatendeke vinginevyotutakuwa tunafanya kazi bure, ikiwa unahusika mtu anahusika na uhalifu kweli hatua zichukuliwe kwani huyu moja kwa moja ni mbadhilifu wa mali ya umma hatufai , na hapo Rais anakazi kweli kwani Kuchaguliwa kwake mara ya pili kutategemea busara yake katika uamzi wa suala kama hili, akifanya kinyume amevunja imani ya Watanzani, Naomba Mungu utumie hekima na busara katika kuamua hili, ikiwa kunauhakika katika tuhuma za viongozi basi wapewe sitaha zao. Maana wanastahili na walikusudia kufanya hivyo. Kwani nini wasiwajibishwe hakuna kutazamana usoni, mmoja atoke mwingine apone na wewe unayetoka jilaumu mwenyewe na tamaa yako, na wala usianze kuunga vikosi vya ujambazi na kuwadhuru wengine haitasaidia.
ReplyDeleteASANTE MUNGU, WASHINDWE NA WALEGEE VIONGOZI WOTE WEZI WANAOTUIBIA HAKI ZETU, UWALEGEZE MUNGU KWANI WAMETUFANYA TUISHI KIMASIKINI SANA KWA WIZI WAO, WAONDOSHE VIONGOZI WOTE WEZI KWA NGUVU ZAKO MUUMBA, MUNGU KWELI U MTUPI KIUMBE WAKO, HII NDIYO HASA WATANZANIA TULIKUWA TUNAOMBA, ONDOKENI WEZI WOTE MUWAACHIE VIONGOZI WAZURI WAONGOZE NCHI KIMAENDELEO, BADO MOTO SASA UNAWASUBIRIA MAANA KUIBA NI DHAMBI KUBWAAAAAAA.
ReplyDeletenadhani prof mark mwandosya anafit ktk position iyo ya PM,wadau mnaonaje?
ReplyDeletemambo hayooooooooo, mafisadi wote matumbo joto
ReplyDeletekwakwakwaaaaaaaa...ahahahaaaaaaaaaaa. jamani jamani jamani. sasa nadhani watachaguliwa wenye akili zao timamu. Watakaoangalia maslahi ya kila mtanzania na si maslahi ya kila kiongozi wa CCM. Hahahahahahaaaaaaaaaaaaaa!! Acha nicheke mieeeee!!!!!! wameumbuka haooooooooooooooo. na JK ndio atajifunza. Kwanza kwa nini bunge linaendelea wakati waziri mkuu kajiuzulu. Au sheria za bunge nazo zimejiuzulu jamani. Waziri mkuu ndio kiongozi wa bunge tukufu. Kama hayupo, that means na bunge lisiwepo hadi hapo atakapochaguluwa PM mwingine. hahahahahahahahahahahahahaaaaaaaaaaaa!! AIBU!!
ReplyDeleteMungu ni mwema sana!!! Sasa JK amepata nafasi ya kuchagua baraza la mawaziri ambao hawana biashara za kishenzi za kuwaumiza wananchi.
ReplyDeleteNamuwaza sana Salim Ahmed Salim...
Dr. Asha-rose Migiro ndio awe the next PM!! Mama yule yupo serious na kazi yake.
ReplyDeleteKUNA POSSIBILITY MHESHIMIWA BENALD MEMBE(MB) WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIKIANO WA KIMATAIFA (MFAIC) KUWA WAZIRI MKUU, MTANIAMBIA
ReplyDeleteWABILLAH TAWFIQ
TANGAZO LA KAZI..... VACANCY
ReplyDeleteNAFASI NYINGI SANA ZA UWAZIRI. TUM CV KWA MH JAKAYA jakayak@hotmail.com
CLOSING DATE TAR FEB 09TH 2008
baba wa taifa alisema tukome kuchagua "mahandsome boy "mnaona sasa ??
ReplyDeleteKikwete give me hug,jamaa msela wako lakini kachemsha umemwaga,powa kishenzi. Na wewe Lowasa mwanaku........yo mwanaku......na umenifanya kwa njaa nije ulaya nijilipue, na sasa kusugua mavi na kuosha vibibi vizee, ili niweze kuleta pesa za kumuhudumia mama yangu. wewe umekaa ma.......u juu ya kiti umestaree kwa wizi, wenzenu tunateseka huku jamani,baridi, ubaguzi. tunatamani kurudi kwetu lakini tunashindwa kwa hali ngumu ya nyumbani.
ReplyDeleteAnon feb 8, 12:35 ingawa umetukana kidogo ila nimecheka sana nimeweza kupima hasira iliyomo kifuani kwako, hata sisi tunauchungu sana pale unapoenda tanesco na kulipa sh 94 elfu kwa mwezi au zaidi eti unalipa umeme pekee bado mengine unakua na vyombo vya umeme unavirundika kabatini jikoni na kuvifungia ili watoto wasivitumie kwa hofu ya kushindwa kulipia umeme. huona wivu sana nikienda nchi jirani na kukuta wenzetu wanatesa na umeme hiter zinawaka kila kitu umeme kwa sana,
ReplyDeleteMh. tusubiri sasa hiyo kesi ya ngedele ilopelekwa kwa nyani.
kwa kupendekeza mi ningefurahi wangefilisiwa ili iwe fundisho kwa waroho, walafi wengine wote
Sijui hela nyengine wameshazimovuzisha wameshaficha mivunguni mwa vitanda vyaoooo???
Hichi ndo kile kisa cha mwanambuzi tunalipa fidia kwa kosa la mwengine.
Kwa kweli hili suala la waziri mkuu kuhusika katika ufisadi uliofanyika katika mkataba wa richmond ni kitendo cha aibu na ambacho hakina uzalendo kabisa. Kusema kweli mtu kama lowassa hafai kabisa kusika nyadifa yoyote kwa sababu ya kuweka maslahi mbele kuliko ya wananchi. Viongozi bora uwa na legacy ambayo inadefine uongozi waka na kama ni nzuri basi itakumbukwa na daima na vizazi vijavyo
ReplyDelete