JK leo amemuapisha Jaji Salum A.L. Massati (58, pichani) kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Taarifa iliyotolewa leo Ikulu, Dar Es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo inasema kuwa uteuzi wa Jaji Massati ulianza Alhamisi iliyopita, Januari 31, mwaka huu. Jaji Mkuu ndiye kiongozi wa shughuli zote za Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kabla ya uteuzi wake, Jaji Massati alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuanzia mwaka 2002.
Jaji Massati anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Kiongozi Amiri Ramadhan Manento ambaye alistaafu kutoka utumishi wa umma kuanzia Januari 31, mwaka huu.
Jaji Massati alizaliwa Desemba 25, 1949 katika kijiji cha Kilama, Ifakara, Mkoa wa Morogoro.
Alisoma shule za msingi na kati huko huko Ifakara, kabla ya kujiunga na Shule ya Sekondari ya Kwiro iliyoko Mahenge, mkoani humo humo Morogoro mwaka 1966.
Alisoma kidato cha tano na sita katika Sekondari ya Mkwawa, Mkoa wa Iringa, kabla ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa mwaka 1972.
Alikuwa mwanafunzi katika Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 1972 na alipata shahada ya kwanza ya sheria mwaka 1975. Alipata shahada ya pili ya sheria (LLB) mwaka 1980.
Jaji Massati aliajiriwa kama Mwanasheria wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kupata shahada yake ya kwanza.
Mwaka 1979, alihamia Mamlaka ya Pamba – Tanzania Cotton Authority ambako alifanya kazi kama Ofisa Sheria wa shirika hilo la umma.
Kuanzia mwaka 1985 hadi alipochaguliwa kuwa Jaji alikuwa akiendesha kampuni yake binafsi ya sheria mjini Morogoro. Aliteuliwa kuwa Jaji mwaka 2002.

shahada ya pili ya sheria ni ll.m na sio ll.b. tafadhali rekebisha
ReplyDeletesasa mbona sielewi maana huyu mteule ana miak 58 umri wa kustaafu ni 60 inakuwa vipi, yaani huyu mshkaji ameteuliwa kufanya kazi miaka miwili tu!! naomba msaada kuhusiana na hili.
ReplyDeletehongera mh. Masati na familia yako.
ReplyDeleteMatua Masati uko wapi nowdays??? bongo au?? long time
kweli watu wanatoka mbali.hicho Kijiji cha Kilama nakijua sana hapo Kibaoni Ifakara.lakini nadhani Jaji kwa mara ya mwisho kufika hapo itakuwa zamani sana.japo aende siku moja kuwasilimia japo hata jamaa zake wa hapo na kuwapa changamoto wanafunzi wa s/msingi hapo kuwa unaweza soma mpaka juu kabisa kama ukizingatia taratibu za shule.najua hapo hata walimu hawatoshi au hakuna kabisa.
ReplyDeletehongera kwa nafasi hiyo lakini ndo umri mzee ushakwenda malizia tu matunda ya uhuru bwana.