WADAU KUNRADHI.
KUNA MTU KANIPIGA SWALI NIMESHINDWA KUMJIBU; NIMEVUNGA KUFA NA KUJIFANYA NIKO BIIIIIZE ILE MBAYA, NA KWAMBA NITAMJIBU BAADAYE.
SASA NAOMBA MSAADA KWENYE TUTAZZZZZ....
KAULIZA HIVI: KWA KISWAHILI NENO 'LOVE' NI MAPENZI, SASA 'LIKE' NI NINI?
NA JE AKITAKA KUMWAMBIA MWENZIE 'I LIKE YOU' KWA KISWAHILI ASEMEJE?
Sisi hatuna like and love...wote ni upendo tu...ila inategemea una maana gani ukimwambia mtu ....I like you or I love you kwetu ni just ninakupenda....
ReplyDeleteso mwambie rafiki yako awe carefull tu wakati anatumia hilo neno kwa kiswahili...
Usimjibu huyo mtu, na kama akiendelea kuuliza, basi mjibu kwa kipogolo, mwambie maana yake ni "nakufir ndiiyi mpaka kumoyo"
ReplyDeleteMwambie aache kuiga na kulazimisha kiswahili na kiingereza viwe na maneno sawa, hali akijuwa kwamba lugha hizi zinatokana na tamaduni tofauti. Kwa taarifa yake sio kiswahili tu kinakosa neno 'like' lugha nyingi za tamaduni mbalimbali zinakosa neno hili.
ReplyDeleteMwambie afuate tamaduni zake katika mawasiliano ya kimapenzi. Ajuwe kwamba lugha inajengwa na kuhimiliwa na tamaduni.
By the way...kama tayari anajuwa lugha zote mbili kwanini aliuliza swali hili? Si amwambie tu huyo anayemzimia kwa lugha yenye neno "I like"...mmhhhhh!
kwa kiswahili ni " dada unanivutia"
ReplyDeleteLove ni kupenda
ReplyDeleteLike ni kutaka.
Akitaka kusema I love u anasema nakupenda. Na akitaka kusema I lieke you anasema nakutaka.
Wadau wa ung'eng'e mnasemaje hapo?
"nakuhusudu"
ReplyDeleteKiswahili ni lugha ambayo bado inakuwa,
ReplyDeleteI like you= Na kuzimia
Ahsante
Zero
Salaaale! Kaka hapa hata mie huwa najikwaa, ila sio kama wewe. Tuelewane kuwa sio kila neno la kidhungu linaweza kuwa na tafsiri dhahiri ya kiswahili. Na matumizi ya neno fulani hulingana aghalabu na 'mazingira.' Kama unakubaliana na mimi, soma tafsiri isiyo rasmi hapa chini, ila kama hukubaliani rudia hapahapa kwenye tuta!
ReplyDeleteNeno 'love' sio tu lina maana ya "MAPENZI" bali pia "MPENZI". Neno hili mara nyingi hutumiwa kwa watu wa jinsia tofauti, lakini mara chache pia hutumika mwisho wa barua/kuaga (barua zetu zile); kwa mfano: love, michuzi
Neno 'like' ni kupenda pia, lakini hasa kwa vitu na kwa watu wa jinsia sawa (HASA WANAUME). Lina maana nyingine, lakini kwa kuwa aliyeuliza swali alirandia LOVE basi tusimpoteze zaidi.
Kama nilivyodadavua, neno 'love' ni kwa watu wa jinsia tofauti **mara nyingi** ila pia kwa ujumla, kama una hadhira kubwa yenye mchanganyiko wa jinsia ukiwaambia "I LOVE YOU" sio dhambi. >>>Mimi huwa nasita sana kuimba wimbo fulani kwenye kitabu cha kikristo, usemao "YESU MPENZI nakupenda .... moyo wako." Kadhalika, sijawahi/siwezi kumwambia mwanaume mwenzangu "I LOVE YOU" unless awe mmoja wa hadhira/mkusanyiko wa wengi.
Tena, neno 'like' huwa linatumika kwa vitu. Mfano: I like that cow, chair, michuzi's crib, etc. I like you, and ..the way you are.
I LIKE YOU kwa Kiswahili Misupu ni NAKUPENDA. Na I LOVE YOU kwa Kiswahili pia ni NAKUPENDA. Cha kuzingatia ni wakati/mazingira/hadhira\nani
Wasalaam,
SV
Like maana yake ni kama, hivyo basi, i like you tunaweza tafsiri kwamba: Mimi kama wewe.......
ReplyDeleteVinginevyo muulize mwalimu aliyekufundisha Kiinglish shule ya msingi.
unasema nimekutamani ndo maana ya like
ReplyDeletelike ni kuhusudu,
ReplyDeletenakuhusudu "i like u "
yaani nikupendezewa na kitu au mtu
I like you michuzi hapo inamaana nakufananisha hakuna jingine, kwa hiyo mtu akikwambia i like you mwambie na nani simple like that
ReplyDeleteLike = Kutamani.
ReplyDeleteI like you = Nakutamani.
Nawasilisha.
Edmas
Napenda kuwasilisha. Kuna kupenda na kuhusudu. Unaweza kumpenda mtu lakini usimhusudu.
ReplyDeleteLove = kupenda hii inatumiwa sana kwa mtu wa karibu kama mama, dada, kaka, mjomba, shangazi au mpenzio nk.
Like =Ni kuhusudu hasa inatumika kwa mtu wa mbali ambaye unamhusudu.
So Wenyewe wanasema "You can love someone but not like him or her""
Like si KUTAMANI hata kidogo. Yaani inamaana mtu akisema I like eating... inamaana NATAMANI KULA?Mmmmmhhh... sidhani..
ReplyDeleteLkn pia Michuzi LOVE si MAPENZI tu, UPENDO ni LOVE pia.
Ninachojua Love, its a feeling shown to someone you real feel... Meaning you cant LOVE forinstance someone/stranger you met in a day/couple of days. You can like him/her in the first place.. then baada ya kumjua and build trust n.k ndo LOVING HIM/HER will follow.
So ni aina fulani ya feelings towards LOVE, lakini pia vitu km nguo, laptop etc are synonymiously used na LOVE too..
Ulizaga na BAKITA pia Michuzi.. Ndo wataalamu wa Kiswahili wenyewe hao.
I like u maana yake Nakutamani.Hivyo mwambie aseme Nakutamani
ReplyDeleteNaomba kuwasilisha
Like si KUTAMANI hata kidogo. Yaani inamaana mtu akisema I like eating... inamaana NATAMANI KULA?Mmmmmhhh... sidhani..
ReplyDeleteLkn pia Michuzi LOVE si MAPENZI tu, UPENDO ni LOVE pia.
Ninachojua Love, its a feeling shown to someone you real feel... Meaning you cant LOVE forinstance someone/stranger you met in a day/couple of days. You can like him/her in the first place.. then baada ya kumjua and build trust n.k ndo LOVING HIM/HER will follow.
So ni aina fulani ya feelings towards LOVE, lakini pia vitu km nguo, laptop etc are synonymiously used na LOVE too..
Ulizaga na BAKITA pia Michuzi.. Ndo wataalamu wa Kiswahili wenyewe hao.
Washikaji eeh! Naona Kiinglish kinawapiga mweleka hapa. Lakini mmejitahidi.
ReplyDeleteNgoja niingie darasani sasa:
Kwanza Anguje na wengine mliosema kama Andunje tafsiri ya neno kwa kawaida inaukiliwa (determined) na muktadha. Sasa, like katika muktadha huu haiwezi kuwa na maana ya neno "kufanana" katika Kiswahili.
Pili, maneno haya love na like hayana tofauti kubwa kama ilivyo katika lugha ya Kiingereza. Hii ni kutokana na tofauti za kiutamaduni kati ya jamii hizi mbili. Wenzetu wakisema I LOVE YOU wana maana ile ya "kuzimia"=ninakuzimia. Na kwa hiyo akisema, I LIKE YOU ndiyo hiyo "kupenda"=ninakupenda.
Sasa kutokana na utamaduni wetu pia "kupenda" limeshehenezwa sana. Mke unamwambia nakupenda, rafiki pia unamwambia nakupenda. Labda swali tu kwa waliooa, ni wangapi wanawaambia wake zao "ninakuhusudu au ninakuzimia"? Hapa kuna tatizo la tofauti baina ya lugha hizi mbili na wala si tatizo la mtu.
Hapa kwa kweli mmemkumbuka mwalimu wangu wa tafsiri. Na kwahiyo nimetumia kidogo nilichopata kujibu hoja hii.
Na kwa upande wa kaka yetu Michuzi, swali la huyo mtu linachanganya. Hiyo Love ni nomino au kitenzi? Maana amesema LOVE ni MAPENZI. Halafu akatumia like kama kitenzi. Najua pengine aliyeuliza si Mwanalugha, kwa hiyo nikianza kuzungumzia kitenzi na nomino nampa kizunguzungu tu. Sasa basi,
Ukitumia love kama nomino (niwie radhi) ni PENDO lakini LOVE AFFAIRS ndio sisi tunasema MAPENZI. Lakini pia kwa wenzetu wanaweza kusema HE HAS A TRUE LOVE = ANA MAPENZI YA KWELI. Lakini sisi tunaweza kusema ANA UPENDO WA KWELI. Hii najaribu kuonyesha uelewa wangu wa maneno haya na matumizi yake.
Huyo muuliza swali basi,
Akitaka kusema I LOVE YOU kwa mwezi wake, asipate shida, aseme tu NINAKUPENDA, ila alainishe sauti na ikiwezekana na macho kama wanaonana ili iwe na maana ya MAPENZI (LOVE AFFAIRS. Vinginevyo hatuna jinsi. HAta hayo nakuhusudu na nimekuzimia hayana uasili, yanaonekana kama kitu cha kujifanya tu sio cha kweli. Sijui! Ila nadhani hata moyo wako utapasuka kama utaambiwa na mwenzi wako "NINAKUPENDA DAN!!!" Nadhani pia haitafanana na ile anayomwambia mwanamke mwenzie, NDIO MAANA NINAKUPENDA.
Naomba niishie hapo na mniwie radhi kwa darasa refu.
Mnaosema LIKE ni KUTAKA,sasa WANT inamaanisha nini kama sio KUTAKA.Kiingereza kina asili ya Kirumi,wakati Kiswahili ni changanyiko wa lugah za Kibantu na Kiarabu kwa mbali (japo kuna maneno ya kuibia ya Kiingereza kama vile BASI,HOSPITALI,RADIO,HELIKOPTA,TELEVISHENI,nk.Hizi ni lugha zenye asili tofauti kabisa.Kwa maana hiyo basi,mtu anaweza kukesha kutafsiri neno HER au HIS kwa kiswahili kwa vile wakati kwenye kiingereza maneno hayo yanaambatana na jinsia,kwenye kiswahili ni YEYE tu.LIKE na LOVE yote yana maana moja kwa Kiswahili,nayo ni KUPENDA.Ukisema LIKE ni KUHUSUDU,je ADMIRE ni nini?Ukisema LIKE ni KUTAMANI,vp kuhusu WISH au LONGING FOR.Kama ananony wa hapo juu alivyosema,pengine umjibu huyo muuliza swali kwa Kipogoro ambapo I LOVE/LIKE YOU inatafsiriwa NAKUFIRA MPAKA KUMOYO (sio matusi,ni kipogoro hicho)
ReplyDeleteLike- Nakuhusudu
ReplyDeleteLove-Penzi
neno husudu linatoka na hasada, kima chake ni hasidi, kama unamhusudu mtu wewe ni hasidi...hapo chacha, tuwe makini jamani. Sio kila neno zuri kutamkika mdomoni basi lina maana nyuri.
ReplyDeleteI like sana sana linaendana na KUPENDEZEWA kama vile mtu anavyoweyz kulitumia neno dear kwa maana ya mpendwa. Sio kila mpendwa ni mpenzi.
Wasalam
Ninavyo jua mimi,I love you in terms of boyfriend and girlfriend nikumpenda mtu kimapenzi and I like you nikumpenda mtu lakini si kimapenzi just as a mate.
ReplyDeleteAliyepatia huyo mpogoro huko juu peke yake.
ReplyDeleteHellow kaka Michu,
ReplyDeleteWadau wengi wamejaribu kuelezea kwa marefu na mapana lakini ukweli na maana halisi ya maneno hayo utabaki kuwa unabase kwenye tamaduni za lugha husika,kwani tamaduni ndiyo msingi mkubwa wa kila lugha yoyote Duniani,Neno "Love" kwa wazungu halina tafisiri ya moja kwa moja kuwa ni "Mapenzi" tu, No,ni neno pana sana,lina maana ya neno "upendo" pia.Neno "like" pia ni pana kama lilivyo mwenzake "Love","Like",lina maana ya...A-kufanana,A-kupenda,A-kutamani,ext.ILa kwa hapa Ughaibuni Msichana wa akikuambia "I like U" Anamaanisha anakutaka kimapenzi.........Hapo ujue kuna hisia za ngono tayari.......!!!!.Conclusion,Ni vizuri kutumia haya maneno kufuatana na utamaduni wa Lugha husika,umri,jinsia ya watu husika.........!!!!!!!.
Nawasilisha.
Mdau,
USA.
raha sana, I like blogger aliyesema I like you = mimi kama wewe!!
ReplyDeleteUkinyambulisha neno "pend" unapata penda, pendwa, pendeza, pendea/pendelea. Kwa kiswahili neno "pend" linaonyesha kuvutia kwa aina moja au nyingine. Kwa mfano "nimependezwa na mwalimu wangu" inaweza kumaanisha kuvutiwa na ufundishaji wake, uvaaji wake, maumbile yake au hata kuvutiwa kimahaba. Ukisema "I love my teacher" hii inahusishwa na mahaba moja kwa moja wakati "I like my teacher" inahusishwa zaidi na vitu vingine ikiwemo ufundishaji, uvaaji nk. bila kujumuisha mahaba. Kwa hiyo inategemea jinsi unavyotumia neno hilo na kwa sasa hivi neno "love" na "like" yanatumika loosely kumaanisha kitu kimoja.
Like = (a) kuvutiwa; (b) kuwa karibu sawa;
ReplyDeleteI LIKE YOU MEANS NAKUTAMANI
ReplyDeleteachane na kingereza bora kisambaa amti nakuundisha nakata mzizi wa fitina
ReplyDeleteLike means to "find it satisfactory or agreeable" you can like someone but not Love them. but to love someone you must like them first...LOVE means "to have strong affection or deep tender feelings for" somehow attracted. Probably I LIKE YOU kwa kiswahili naweza kusema "Napendezewa nawe (na wewe)" but it doesn't mean I love you.
ReplyDeleteNa mbeba box
I like you:
ReplyDelete-Navutiwa na wewe
-Napendezewa na wewe
-KOSHA
sio kila neno la kiingereza linaleta maana sawa na kiswahili.Kumbuka lugha ni utamaduni, inabidi uendane na utamaduni na mazoea ya mahali hapo;
KAMWAMBIE MWANAUME MWENZAKO NAVUTIWA NA WEWE AU NAPENDEZEWA NA WEWE---Unatafuta ugomvi.
Lakini kwa sababu lugha inakua haya maneno tunayosema ya mtaani ndio huwa yanaleta maana kamili.
Kwa mfano ukimwambia mwanaume mwenzako ;''nakufagilia inaleta maana nzuri zaidi''
angalia link below ya Yale university, kamusi project
ReplyDeletehttp://kamusiproject.org/cgi-bin/main.cgi?right_frame_src=http%3A//www.kamusiproject.org/cgi-bin/lookup.cgi%3FWord%3Dlike%26EngP%3D1%26SUBMIT2%3DLook+Up
NIMEPENDEZEWA NA WEWE...........
ReplyDeleteLANKINI NI VYEMA UTUMIE LUGHA YA KWENU NA UACHANE NA HII LUGHA YA KITUMWA>>>>>>>>>>
Sheeeeee! we Mishu kweli ni bingwa wa habari umeishomoa wapi hii! Mimi kisungu yangu siyo nsuri. lakini wadau nyingi imesema uongo.
ReplyDeleteIko moja imesema kutamani UONGO
nyingine imesema kufananinisha hii ndio imeshekesha kabisa, nyingine imesema LOVE ni kwa b/f na g/f imekosea saaaaaaana. Mollel imesema yote ni MAPENSI. mi nafikiri Mollel imepatia.
Halafu kwa kilugha ya Baba ya taifa neno MAPENZI ni pana saaaana inajumulisha fitu yote inaendana nayo i.e kufutiwa, kupendeswa, kupenda, kupendeana, kupendwa kutamani kwa mazuri, na fitu nyingine nyingi kama hiso.
Iko mdau nyingine imesema neno "pend" kwa kiswahili hakuna neno kama hiyo na kama iko mwalimu wetu hakusema
NYIE MNAOKATA KING'ENG'E HUMU TUWAELEWEJE? MTU ALIULIZA APEWE NAMNA YA KUSEMA I LIKE YOU KATIKA KISWAHILI. NINYI MNAZIDI KUMCHANGANYA NA KIZUNGU, WAKATI KIZUNGU CHENYEWE KINAWAPA KIZUNGUZUNGU.
ReplyDeleteYANGU MACHO!
Gumegume
"LOVE" na 'LIKE"
ReplyDelete1) "LOVE" = (noun) - mapenzi, upendo.
2) "LOVE" = (verb) - kupenda, penda
"3) LIKE" = (Verb) - kupenda, kuhusudu, tamani
4) "LIKE" = (Adverb) - Kifananishi eg. Michuzi is like a
journalist.
'LIKE" Siyo kufanana kama wanavyosema baadhi ya watu. ISipokuwa vitu viwili ndio vinavyofanana. Hapo juu kwa mfano ni Michuzi v.s Journalist.
KUFANANA = 'TO BE ALIKE", NA SIYO "LIKE".
Kama alivyosema mdau mmoja matumizi yanategemea mahali, nani unayeongea naye, umri wake, cheo, mazingira, nk.
WATAALAMU WA LUGHA TUNAITA "PRAGMATICS". Pragmiatocs is supposed to be about all aspects that you consider during communication eg. culture of the language, etc as mentioned above.
MDAU,
STATES.
Kwa kisukuma maana yake NIMEKUDONDOKEA.
ReplyDeleteKWA KISWAHILI FASAHA TO LIKE NI KUHUSUDU APO ZAMANI KABLA HATUJAWA WENGI MJINI HILO NENO LILITUMIKA SANA LAKINI TULIPOANZA KUWA WENGI KILA MTU KAJA NA LUGHA YAKE MWISHO KISWAHILI KINAZUNGUMZWA KILA AINA SASA
ReplyDeleteMichael Jackson alishatafsiri enz hizo na ule wimbo. "Nakupenda pia, nakutaka pia.." meaning?
ReplyDeleteCut the crap, tell ur friend to say what comes from his/her heart. U cant help translate feelings za mtu kwa mtu mwingine unless u know what chemistry is in there. If ur friend does not love/like the girl/boy, advise him/her to express in action
duuuhhhh!!!!!! wadauuuuuuuuu...
ReplyDeletekwanza naomba mkumbuke kuwa hii lugha ya watu imekuja na ndege.. yaan imelipiwa ma dolazzz na mapoundzzzz...
so ni ngumu pia kuitumia... saaasaaa tutumie ya kwetu tuu kama vipiii mana hii ya watuuu ina gharama saanaaa
LIKE ni KUHUSUDU..
NAOMBA KUWASILISHA WADAU..
nimekuchunuku ndio maana ya kiingereza ya neno I like you.
ReplyDeleteCHIBILITI ANAJUA
ReplyDeleteKwani Kamusi zimeenda wapi? Hebu rejeeni vitabuni kwani naona mpaka sasa hivi mnachemsha tu!! Eti like ni Kutamani!!!!! Nani kasema!!
ReplyDeletelove ni neno linalotumika kwa wapendanao wanapotaka kuambizana nakupena lkn kama mimi na wewe mjomba michuzi sio wapendanao basi tutatumia i like u au kama unaweza kukutana na mtu sio mpenzi wako lakini umempenda labda akisema au akicheka unawe kumwambia i like your smiley... mtu akikuambia i love you maana yake amekuzimikia ile mbaya hata usingizi haupati kwa ajili yako
ReplyDeleteKWA KISAMBAA TUNASEMA
ReplyDelete..NVYEDII..
..NVITANA..
RUDISHA FEDHA ZA BOT
ReplyDeleteTimu imewaomba wananchi wanaoelewa chochote kuhusiana na sakata hilo, waendelee kutoa taarifa moja kwa moja, kwa kupitia namba maalum ilizotoa ambazo ni 0713 223 362, 0784 213 928 na 0784 785 722.
Miongoni mwa wanaounda timu hiyo iliyotokana na ubadhirifu ulioainishwa na Mkaguzi aliyekodioshwa na Serikali, Ernst & Young ni Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, PCCB.
Kweli Wabongo kiswahili hatujui,ila kwa jinsi hapo nene lilivyotumika I Like you Maana Yake NIMEVUTIWA NA WEWE
ReplyDelete