WADAU KUNRADHI.
KUNA MTU KANIPIGA SWALI NIMESHINDWA KUMJIBU; NIMEVUNGA KUFA NA KUJIFANYA NIKO BIIIIIZE ILE MBAYA, NA KWAMBA NITAMJIBU BAADAYE.
SASA NAOMBA MSAADA KWENYE TUTAZZZZZ....
KAULIZA HIVI: KWA KISWAHILI NENO 'LOVE' NI MAPENZI, SASA 'LIKE' NI NINI?
NA JE AKITAKA KUMWAMBIA MWENZIE 'I LIKE YOU' KWA KISWAHILI ASEMEJE?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 46 mpaka sasa

  1. Sisi hatuna like and love...wote ni upendo tu...ila inategemea una maana gani ukimwambia mtu ....I like you or I love you kwetu ni just ninakupenda....
    so mwambie rafiki yako awe carefull tu wakati anatumia hilo neno kwa kiswahili...

    ReplyDelete
  2. Usimjibu huyo mtu, na kama akiendelea kuuliza, basi mjibu kwa kipogolo, mwambie maana yake ni "nakufir ndiiyi mpaka kumoyo"

    ReplyDelete
  3. Mwambie aache kuiga na kulazimisha kiswahili na kiingereza viwe na maneno sawa, hali akijuwa kwamba lugha hizi zinatokana na tamaduni tofauti. Kwa taarifa yake sio kiswahili tu kinakosa neno 'like' lugha nyingi za tamaduni mbalimbali zinakosa neno hili.

    Mwambie afuate tamaduni zake katika mawasiliano ya kimapenzi. Ajuwe kwamba lugha inajengwa na kuhimiliwa na tamaduni.

    By the way...kama tayari anajuwa lugha zote mbili kwanini aliuliza swali hili? Si amwambie tu huyo anayemzimia kwa lugha yenye neno "I like"...mmhhhhh!

    ReplyDelete
  4. kwa kiswahili ni " dada unanivutia"

    ReplyDelete
  5. Love ni kupenda
    Like ni kutaka.
    Akitaka kusema I love u anasema nakupenda. Na akitaka kusema I lieke you anasema nakutaka.
    Wadau wa ung'eng'e mnasemaje hapo?

    ReplyDelete
  6. "nakuhusudu"

    ReplyDelete
  7. Kiswahili ni lugha ambayo bado inakuwa,

    I like you= Na kuzimia

    Ahsante
    Zero

    ReplyDelete
  8. Salaaale! Kaka hapa hata mie huwa najikwaa, ila sio kama wewe. Tuelewane kuwa sio kila neno la kidhungu linaweza kuwa na tafsiri dhahiri ya kiswahili. Na matumizi ya neno fulani hulingana aghalabu na 'mazingira.' Kama unakubaliana na mimi, soma tafsiri isiyo rasmi hapa chini, ila kama hukubaliani rudia hapahapa kwenye tuta!

    Neno 'love' sio tu lina maana ya "MAPENZI" bali pia "MPENZI". Neno hili mara nyingi hutumiwa kwa watu wa jinsia tofauti, lakini mara chache pia hutumika mwisho wa barua/kuaga (barua zetu zile); kwa mfano: love, michuzi

    Neno 'like' ni kupenda pia, lakini hasa kwa vitu na kwa watu wa jinsia sawa (HASA WANAUME). Lina maana nyingine, lakini kwa kuwa aliyeuliza swali alirandia LOVE basi tusimpoteze zaidi.

    Kama nilivyodadavua, neno 'love' ni kwa watu wa jinsia tofauti **mara nyingi** ila pia kwa ujumla, kama una hadhira kubwa yenye mchanganyiko wa jinsia ukiwaambia "I LOVE YOU" sio dhambi. >>>Mimi huwa nasita sana kuimba wimbo fulani kwenye kitabu cha kikristo, usemao "YESU MPENZI nakupenda .... moyo wako." Kadhalika, sijawahi/siwezi kumwambia mwanaume mwenzangu "I LOVE YOU" unless awe mmoja wa hadhira/mkusanyiko wa wengi.

    Tena, neno 'like' huwa linatumika kwa vitu. Mfano: I like that cow, chair, michuzi's crib, etc. I like you, and ..the way you are.

    I LIKE YOU kwa Kiswahili Misupu ni NAKUPENDA. Na I LOVE YOU kwa Kiswahili pia ni NAKUPENDA. Cha kuzingatia ni wakati/mazingira/hadhira\nani

    Wasalaam,
    SV

    ReplyDelete
  9. Like maana yake ni kama, hivyo basi, i like you tunaweza tafsiri kwamba: Mimi kama wewe.......

    Vinginevyo muulize mwalimu aliyekufundisha Kiinglish shule ya msingi.

    ReplyDelete
  10. unasema nimekutamani ndo maana ya like

    ReplyDelete
  11. like ni kuhusudu,

    nakuhusudu "i like u "

    yaani nikupendezewa na kitu au mtu

    ReplyDelete
  12. I like you michuzi hapo inamaana nakufananisha hakuna jingine, kwa hiyo mtu akikwambia i like you mwambie na nani simple like that

    ReplyDelete
  13. Like = Kutamani.

    I like you = Nakutamani.

    Nawasilisha.

    Edmas

    ReplyDelete
  14. Napenda kuwasilisha. Kuna kupenda na kuhusudu. Unaweza kumpenda mtu lakini usimhusudu.
    Love = kupenda hii inatumiwa sana kwa mtu wa karibu kama mama, dada, kaka, mjomba, shangazi au mpenzio nk.

    Like =Ni kuhusudu hasa inatumika kwa mtu wa mbali ambaye unamhusudu.
    So Wenyewe wanasema "You can love someone but not like him or her""

    ReplyDelete
  15. Like si KUTAMANI hata kidogo. Yaani inamaana mtu akisema I like eating... inamaana NATAMANI KULA?Mmmmmhhh... sidhani..

    Lkn pia Michuzi LOVE si MAPENZI tu, UPENDO ni LOVE pia.

    Ninachojua Love, its a feeling shown to someone you real feel... Meaning you cant LOVE forinstance someone/stranger you met in a day/couple of days. You can like him/her in the first place.. then baada ya kumjua and build trust n.k ndo LOVING HIM/HER will follow.

    So ni aina fulani ya feelings towards LOVE, lakini pia vitu km nguo, laptop etc are synonymiously used na LOVE too..

    Ulizaga na BAKITA pia Michuzi.. Ndo wataalamu wa Kiswahili wenyewe hao.

    ReplyDelete
  16. I like u maana yake Nakutamani.Hivyo mwambie aseme Nakutamani
    Naomba kuwasilisha

    ReplyDelete
  17. Like si KUTAMANI hata kidogo. Yaani inamaana mtu akisema I like eating... inamaana NATAMANI KULA?Mmmmmhhh... sidhani..

    Lkn pia Michuzi LOVE si MAPENZI tu, UPENDO ni LOVE pia.

    Ninachojua Love, its a feeling shown to someone you real feel... Meaning you cant LOVE forinstance someone/stranger you met in a day/couple of days. You can like him/her in the first place.. then baada ya kumjua and build trust n.k ndo LOVING HIM/HER will follow.

    So ni aina fulani ya feelings towards LOVE, lakini pia vitu km nguo, laptop etc are synonymiously used na LOVE too..

    Ulizaga na BAKITA pia Michuzi.. Ndo wataalamu wa Kiswahili wenyewe hao.

    ReplyDelete
  18. Washikaji eeh! Naona Kiinglish kinawapiga mweleka hapa. Lakini mmejitahidi.
    Ngoja niingie darasani sasa:
    Kwanza Anguje na wengine mliosema kama Andunje tafsiri ya neno kwa kawaida inaukiliwa (determined) na muktadha. Sasa, like katika muktadha huu haiwezi kuwa na maana ya neno "kufanana" katika Kiswahili.
    Pili, maneno haya love na like hayana tofauti kubwa kama ilivyo katika lugha ya Kiingereza. Hii ni kutokana na tofauti za kiutamaduni kati ya jamii hizi mbili. Wenzetu wakisema I LOVE YOU wana maana ile ya "kuzimia"=ninakuzimia. Na kwa hiyo akisema, I LIKE YOU ndiyo hiyo "kupenda"=ninakupenda.
    Sasa kutokana na utamaduni wetu pia "kupenda" limeshehenezwa sana. Mke unamwambia nakupenda, rafiki pia unamwambia nakupenda. Labda swali tu kwa waliooa, ni wangapi wanawaambia wake zao "ninakuhusudu au ninakuzimia"? Hapa kuna tatizo la tofauti baina ya lugha hizi mbili na wala si tatizo la mtu.
    Hapa kwa kweli mmemkumbuka mwalimu wangu wa tafsiri. Na kwahiyo nimetumia kidogo nilichopata kujibu hoja hii.

    Na kwa upande wa kaka yetu Michuzi, swali la huyo mtu linachanganya. Hiyo Love ni nomino au kitenzi? Maana amesema LOVE ni MAPENZI. Halafu akatumia like kama kitenzi. Najua pengine aliyeuliza si Mwanalugha, kwa hiyo nikianza kuzungumzia kitenzi na nomino nampa kizunguzungu tu. Sasa basi,
    Ukitumia love kama nomino (niwie radhi) ni PENDO lakini LOVE AFFAIRS ndio sisi tunasema MAPENZI. Lakini pia kwa wenzetu wanaweza kusema HE HAS A TRUE LOVE = ANA MAPENZI YA KWELI. Lakini sisi tunaweza kusema ANA UPENDO WA KWELI. Hii najaribu kuonyesha uelewa wangu wa maneno haya na matumizi yake.
    Huyo muuliza swali basi,
    Akitaka kusema I LOVE YOU kwa mwezi wake, asipate shida, aseme tu NINAKUPENDA, ila alainishe sauti na ikiwezekana na macho kama wanaonana ili iwe na maana ya MAPENZI (LOVE AFFAIRS. Vinginevyo hatuna jinsi. HAta hayo nakuhusudu na nimekuzimia hayana uasili, yanaonekana kama kitu cha kujifanya tu sio cha kweli. Sijui! Ila nadhani hata moyo wako utapasuka kama utaambiwa na mwenzi wako "NINAKUPENDA DAN!!!" Nadhani pia haitafanana na ile anayomwambia mwanamke mwenzie, NDIO MAANA NINAKUPENDA.
    Naomba niishie hapo na mniwie radhi kwa darasa refu.

    ReplyDelete
  19. Mnaosema LIKE ni KUTAKA,sasa WANT inamaanisha nini kama sio KUTAKA.Kiingereza kina asili ya Kirumi,wakati Kiswahili ni changanyiko wa lugah za Kibantu na Kiarabu kwa mbali (japo kuna maneno ya kuibia ya Kiingereza kama vile BASI,HOSPITALI,RADIO,HELIKOPTA,TELEVISHENI,nk.Hizi ni lugha zenye asili tofauti kabisa.Kwa maana hiyo basi,mtu anaweza kukesha kutafsiri neno HER au HIS kwa kiswahili kwa vile wakati kwenye kiingereza maneno hayo yanaambatana na jinsia,kwenye kiswahili ni YEYE tu.LIKE na LOVE yote yana maana moja kwa Kiswahili,nayo ni KUPENDA.Ukisema LIKE ni KUHUSUDU,je ADMIRE ni nini?Ukisema LIKE ni KUTAMANI,vp kuhusu WISH au LONGING FOR.Kama ananony wa hapo juu alivyosema,pengine umjibu huyo muuliza swali kwa Kipogoro ambapo I LOVE/LIKE YOU inatafsiriwa NAKUFIRA MPAKA KUMOYO (sio matusi,ni kipogoro hicho)

    ReplyDelete
  20. Like- Nakuhusudu
    Love-Penzi

    ReplyDelete
  21. neno husudu linatoka na hasada, kima chake ni hasidi, kama unamhusudu mtu wewe ni hasidi...hapo chacha, tuwe makini jamani. Sio kila neno zuri kutamkika mdomoni basi lina maana nyuri.

    I like sana sana linaendana na KUPENDEZEWA kama vile mtu anavyoweyz kulitumia neno dear kwa maana ya mpendwa. Sio kila mpendwa ni mpenzi.

    Wasalam

    ReplyDelete
  22. Ninavyo jua mimi,I love you in terms of boyfriend and girlfriend nikumpenda mtu kimapenzi and I like you nikumpenda mtu lakini si kimapenzi just as a mate.

    ReplyDelete
  23. Aliyepatia huyo mpogoro huko juu peke yake.

    ReplyDelete
  24. Hellow kaka Michu,
    Wadau wengi wamejaribu kuelezea kwa marefu na mapana lakini ukweli na maana halisi ya maneno hayo utabaki kuwa unabase kwenye tamaduni za lugha husika,kwani tamaduni ndiyo msingi mkubwa wa kila lugha yoyote Duniani,Neno "Love" kwa wazungu halina tafisiri ya moja kwa moja kuwa ni "Mapenzi" tu, No,ni neno pana sana,lina maana ya neno "upendo" pia.Neno "like" pia ni pana kama lilivyo mwenzake "Love","Like",lina maana ya...A-kufanana,A-kupenda,A-kutamani,ext.ILa kwa hapa Ughaibuni Msichana wa akikuambia "I like U" Anamaanisha anakutaka kimapenzi.........Hapo ujue kuna hisia za ngono tayari.......!!!!.Conclusion,Ni vizuri kutumia haya maneno kufuatana na utamaduni wa Lugha husika,umri,jinsia ya watu husika.........!!!!!!!.
    Nawasilisha.
    Mdau,
    USA.

    ReplyDelete
  25. raha sana, I like blogger aliyesema I like you = mimi kama wewe!!
    Ukinyambulisha neno "pend" unapata penda, pendwa, pendeza, pendea/pendelea. Kwa kiswahili neno "pend" linaonyesha kuvutia kwa aina moja au nyingine. Kwa mfano "nimependezwa na mwalimu wangu" inaweza kumaanisha kuvutiwa na ufundishaji wake, uvaaji wake, maumbile yake au hata kuvutiwa kimahaba. Ukisema "I love my teacher" hii inahusishwa na mahaba moja kwa moja wakati "I like my teacher" inahusishwa zaidi na vitu vingine ikiwemo ufundishaji, uvaaji nk. bila kujumuisha mahaba. Kwa hiyo inategemea jinsi unavyotumia neno hilo na kwa sasa hivi neno "love" na "like" yanatumika loosely kumaanisha kitu kimoja.

    ReplyDelete
  26. Like = (a) kuvutiwa; (b) kuwa karibu sawa;

    ReplyDelete
  27. I LIKE YOU MEANS NAKUTAMANI

    ReplyDelete
  28. achane na kingereza bora kisambaa amti nakuundisha nakata mzizi wa fitina

    ReplyDelete
  29. Like means to "find it satisfactory or agreeable" you can like someone but not Love them. but to love someone you must like them first...LOVE means "to have strong affection or deep tender feelings for" somehow attracted. Probably I LIKE YOU kwa kiswahili naweza kusema "Napendezewa nawe (na wewe)" but it doesn't mean I love you.

    Na mbeba box

    ReplyDelete
  30. I like you:
    -Navutiwa na wewe
    -Napendezewa na wewe
    -KOSHA

    sio kila neno la kiingereza linaleta maana sawa na kiswahili.Kumbuka lugha ni utamaduni, inabidi uendane na utamaduni na mazoea ya mahali hapo;

    KAMWAMBIE MWANAUME MWENZAKO NAVUTIWA NA WEWE AU NAPENDEZEWA NA WEWE---Unatafuta ugomvi.

    Lakini kwa sababu lugha inakua haya maneno tunayosema ya mtaani ndio huwa yanaleta maana kamili.

    Kwa mfano ukimwambia mwanaume mwenzako ;''nakufagilia inaleta maana nzuri zaidi''

    ReplyDelete
  31. angalia link below ya Yale university, kamusi project

    http://kamusiproject.org/cgi-bin/main.cgi?right_frame_src=http%3A//www.kamusiproject.org/cgi-bin/lookup.cgi%3FWord%3Dlike%26EngP%3D1%26SUBMIT2%3DLook+Up

    ReplyDelete
  32. NIMEPENDEZEWA NA WEWE...........
    LANKINI NI VYEMA UTUMIE LUGHA YA KWENU NA UACHANE NA HII LUGHA YA KITUMWA>>>>>>>>>>

    ReplyDelete
  33. Sheeeeee! we Mishu kweli ni bingwa wa habari umeishomoa wapi hii! Mimi kisungu yangu siyo nsuri. lakini wadau nyingi imesema uongo.
    Iko moja imesema kutamani UONGO
    nyingine imesema kufananinisha hii ndio imeshekesha kabisa, nyingine imesema LOVE ni kwa b/f na g/f imekosea saaaaaaana. Mollel imesema yote ni MAPENSI. mi nafikiri Mollel imepatia.

    Halafu kwa kilugha ya Baba ya taifa neno MAPENZI ni pana saaaana inajumulisha fitu yote inaendana nayo i.e kufutiwa, kupendeswa, kupenda, kupendeana, kupendwa kutamani kwa mazuri, na fitu nyingine nyingi kama hiso.

    Iko mdau nyingine imesema neno "pend" kwa kiswahili hakuna neno kama hiyo na kama iko mwalimu wetu hakusema

    ReplyDelete
  34. NYIE MNAOKATA KING'ENG'E HUMU TUWAELEWEJE? MTU ALIULIZA APEWE NAMNA YA KUSEMA I LIKE YOU KATIKA KISWAHILI. NINYI MNAZIDI KUMCHANGANYA NA KIZUNGU, WAKATI KIZUNGU CHENYEWE KINAWAPA KIZUNGUZUNGU.
    YANGU MACHO!
    Gumegume

    ReplyDelete
  35. "LOVE" na 'LIKE"

    1) "LOVE" = (noun) - mapenzi, upendo.

    2) "LOVE" = (verb) - kupenda, penda

    "3) LIKE" = (Verb) - kupenda, kuhusudu, tamani

    4) "LIKE" = (Adverb) - Kifananishi eg. Michuzi is like a
    journalist.

    'LIKE" Siyo kufanana kama wanavyosema baadhi ya watu. ISipokuwa vitu viwili ndio vinavyofanana. Hapo juu kwa mfano ni Michuzi v.s Journalist.

    KUFANANA = 'TO BE ALIKE", NA SIYO "LIKE".


    Kama alivyosema mdau mmoja matumizi yanategemea mahali, nani unayeongea naye, umri wake, cheo, mazingira, nk.

    WATAALAMU WA LUGHA TUNAITA "PRAGMATICS". Pragmiatocs is supposed to be about all aspects that you consider during communication eg. culture of the language, etc as mentioned above.

    MDAU,

    STATES.

    ReplyDelete
  36. Kwa kisukuma maana yake NIMEKUDONDOKEA.

    ReplyDelete
  37. KWA KISWAHILI FASAHA TO LIKE NI KUHUSUDU APO ZAMANI KABLA HATUJAWA WENGI MJINI HILO NENO LILITUMIKA SANA LAKINI TULIPOANZA KUWA WENGI KILA MTU KAJA NA LUGHA YAKE MWISHO KISWAHILI KINAZUNGUMZWA KILA AINA SASA

    ReplyDelete
  38. Michael Jackson alishatafsiri enz hizo na ule wimbo. "Nakupenda pia, nakutaka pia.." meaning?

    Cut the crap, tell ur friend to say what comes from his/her heart. U cant help translate feelings za mtu kwa mtu mwingine unless u know what chemistry is in there. If ur friend does not love/like the girl/boy, advise him/her to express in action

    ReplyDelete
  39. duuuhhhh!!!!!! wadauuuuuuuuu...

    kwanza naomba mkumbuke kuwa hii lugha ya watu imekuja na ndege.. yaan imelipiwa ma dolazzz na mapoundzzzz...

    so ni ngumu pia kuitumia... saaasaaa tutumie ya kwetu tuu kama vipiii mana hii ya watuuu ina gharama saanaaa

    LIKE ni KUHUSUDU..

    NAOMBA KUWASILISHA WADAU..

    ReplyDelete
  40. nimekuchunuku ndio maana ya kiingereza ya neno I like you.

    ReplyDelete
  41. CHIBILITI ANAJUA

    ReplyDelete
  42. Kwani Kamusi zimeenda wapi? Hebu rejeeni vitabuni kwani naona mpaka sasa hivi mnachemsha tu!! Eti like ni Kutamani!!!!! Nani kasema!!

    ReplyDelete
  43. love ni neno linalotumika kwa wapendanao wanapotaka kuambizana nakupena lkn kama mimi na wewe mjomba michuzi sio wapendanao basi tutatumia i like u au kama unaweza kukutana na mtu sio mpenzi wako lakini umempenda labda akisema au akicheka unawe kumwambia i like your smiley... mtu akikuambia i love you maana yake amekuzimikia ile mbaya hata usingizi haupati kwa ajili yako

    ReplyDelete
  44. KWA KISAMBAA TUNASEMA
    ..NVYEDII..
    ..NVITANA..

    ReplyDelete
  45. RUDISHA FEDHA ZA BOT

    Timu imewaomba wananchi wanaoelewa chochote kuhusiana na sakata hilo, waendelee kutoa taarifa moja kwa moja, kwa kupitia namba maalum ilizotoa ambazo ni 0713 223 362, 0784 213 928 na 0784 785 722.

    Miongoni mwa wanaounda timu hiyo iliyotokana na ubadhirifu ulioainishwa na Mkaguzi aliyekodioshwa na Serikali, Ernst & Young ni Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, PCCB.

    ReplyDelete
  46. Kweli Wabongo kiswahili hatujui,ila kwa jinsi hapo nene lilivyotumika I Like you Maana Yake NIMEVUTIWA NA WEWE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...