mama wa kwanza salma kikwete akihutubia katika mkutano wa amani ya dunia jana jijini seoul, korea ya kusini, jana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Hivi Mama wa Kwanza anahutubia kwa kutumia LUGHA gani? Ki-KOREA AU KI ENGLISH AU KISWAHILI?

    ReplyDelete
  2. anonymous hapo juu yani umeuliza swali ambalo wa kulitatuaa ni kaka michuzi tuu...michu ebu tupe clip ya huyo mama wakati anahutubia....tujue lugha iliyotumikaaa...

    ReplyDelete
  3. Nyie vipi hamjui kiswahili imekua lugha ya ki-inteneshno?Lazma alitumia lugha yetu ya taifa ebo!Kwani ki english lazma mtu ajue?Kwanza ni utumwa..teh tehteh teh!

    ReplyDelete
  4. hebu watuwekee mambo anayoongea uko, maana hata tukiwa hapa nyumbani tanzania tunahitaji kujua anayoongea uko, asante michuzi.

    ReplyDelete
  5. Mnafikiri mama lugha inampiga chenga? alikuwa mwalimu wa english shule aliyokuwa anafundisha

    ReplyDelete
  6. Kinachowasumbua ni ushamba wa kuona kuwa lugha duniani ni kiingereza tu. Kwenye mikutano ya kimataifa watu wote hawaongei lugha moja, wachina wataongea kichina, wafaransa wataongea kifaransa, wajerumani kijerumani, waarabu kiarabu, na lugha mbali mbali ndio maana kunakuwa na watu wa kutafsiri lugha. Na wote hao hawajilazimishi kuongea kiingereza ila sie waswahili tu na ushamba wetu ndio tunaabudu kiingereza sijui kwa sababu tulitawaliwa na waingereza? Na bado mabaki ya ukoloni yamo vichwani mwetu utaona watu huku nje wanawakataza watoto wao kuongea kiswahili, huwa nawaonea huruma sana hao watoto maana angalau hicho kiswahili cha kuwasogeza karibu na asili yao hawakijui sembuse lugha za wazazi wao za asili. Ndio wapo mnashangaa nini watu wanakana kiswahili wakati hicho kiingereza wanachoongea hakijulikani ni kipigini cha wapi.

    Anayedhani kuongea kiingereza ndio kuwa wa maana bado ametawaliwa kifikra. Amka na ujikomboe sasa.

    Nimesema hayo kwa sababu hii siyo mara ya kwanza kwa watu kuuliza huyu mama anaongea lugha gani. Ujinga mtupu kuabudu lugha za watu.

    ReplyDelete
  7. Acheni ushamba,kwani mmeona kuongea kiinglish ndo deal?kizamaani kweli,msiwe watumwa wa fikra,penda lugha yako na mama kikwete hiyo english mnayoona ni deal sana anaongea,dah kweli wabongo bado!

    ReplyDelete
  8. Kaka michuzi, nitafurahi sana iwapo siku moja utatutundikia CV (wasifu) wa mama wa kwanza. Kwa kweli nitashukuru sana. Ama kama kuna mtu yeyote yule anayeufahamu basi asisite kufanya hivyo. Imani.

    ReplyDelete
  9. Mama wa kwanza English, Kiswahili au Kiswanglish? Wenzetu huwa wana wapambe wa kumpolish Mzee na Mama mambo ya mavazi nk. na hata masuala mazima ya langueji.. At least wa kwetu ni mara kumi ya Mama Kibaki! duuh!! Wa kwetu hata kama English haijatulia hivyo lakini hatutii aibu!!

    Mdau - Boston, US

    ReplyDelete
  10. Wadau,

    Kufundisha lugha si lazima mtu uweze kuiongea . Nawajua walimu kibao wanafundisha Kiswahili ulaya na hawawezi kuongea hata sentensi moja na mswahili, lakini jaribu kuwauliza sarufi wanaijua kama maji

    teh teh teh nataka kumchokoza anony 12:24

    ReplyDelete
  11. Taratibu anony 9:07 mie sitaki uchokozi!

    ReplyDelete
  12. ukweli jamani, mama wa kwanza jitahidi basi na watanzania wote wapate ujumbe wako, haswa unapokwenda nchi za ulaya, uwe unafikisha ujumbe kwa watanzania wote basi.

    ReplyDelete
  13. TATIZO KAKA MICHUZI NUSU YA WADAU WA HII BLOG NI "MALIMBUKENI". ANACHOTAKIWA MAMA WA KWANZA KUFANYA NI PRESENTATION, KILICHO MUHIMU NI UJUMBE ULIOBEBWA KWENYE PAPER YAKE, SUALA LA LUGHA SIO ISSUE KWENYE VIKAO VYA INTERNATIONAL KWANI KUNA VIFAA MBALIMBALI VYA KUREKEBISHA MAMBO YA TAFSIRI. JAMANI KUWENI WATU WENYE BUSARA NA HEKIMA. ENGLISH SIO ISSUE KABISA KWENYE HIZO NCHI ZA ASIA HILO LAZIMA MTAMBUE

    ReplyDelete
  14. FIRST LADY ANAJUA LUGHA MBILI TU! KISWAHILI NA KIAMKONDE,KAMA MTU ANABISHA BASI MICHU TUWEKEE YUTUBE YA HIYO SPEECH YAKE MSIKIE JINSI HUYU MAMA YETU ALIVYO MZURI KWENYE KISWAHILI!

    ReplyDelete
  15. Nafikiri inabidi wakati wa uchaguzi tusiwe tunaangalia uwezo wa mgombe tu bali tuangalie na uwezo na mke wake kwani mama wa kwanza inabidi afanye majukumu ambayo yanahitaji uelewa kidogo. Hapo naomba nikusahihishe kidogo bwana Mchuuzi mama wa kwanza hahutubi bali anasoma hotuba. Lakini hongera mama wa kwanza kwa kuwa mwalimu wa shule ya msingi kwa miaka mingi kwa kujiendeleza kutoka UPE.

    ReplyDelete
  16. Hebu muacheni Huyo first lady, namuunga mkono anon hapo juu, Enlish sio issue, issue ni ujumbe gani anatoa TZ, AFR na DUNIA, cha maana Michu kimwagie hadharani alicho kisema kwa lugha yoyote ile hatutojali mradi kiwe cha maana.

    ReplyDelete
  17. Kazi kwelikweli... It's real interesting hii mada.

    Kwanza,nashindwa kujua limbukeni ni nani kati ya hawa waliochangia.Maana hata anaesema kiingereza siyo deal bado ameweka na vimaneno vya kiingereza.Au ndo ya wanasiasa kutuambia Kiingereza hakina neno ilhali wao wanawapeleka watoto wao nje, elimu bora,kiingereza juu na kazi nene wanachukua,wewe ulieambiwa soma kiswahili makampuni yanakupiga chini.

    Pili,mtu kujua lugha ya kimataifa kwa ulimwengu huu wa sasa ni muhimu,tusijidanganye kbs kwamba kiswahili kitatutoa.Tuna mabadiliko ya uwekezaji,utandawazi, soko huria etc,Kiswahili kufurukuta it'll take some time.

    Tatu,huyu first lady inabidi ajue kiingereza km hajui,ni muhimu kwake mno.Sawa atahutubia na kusoma hotuba kwa kiswahili in international conferences, inakuaje kama mgeni wa kitaifa amekuja na hajui(mgeni) hata kiswahili,ni kiingereza, kifaransa etc... Mama ataongea nini?

    Tusiangalie vitu kijuujuu na kishabiki.Lugha hii tuichukulie kwa uzito wa kipekee,km kweli tunataka kuendana na utandawazi huu. Ila tuhakikishe tunavyoenda na kiswahili chetu tunazidi kuki-boost.

    ReplyDelete
  18. Kwani mnaposema kiswahili ni lugha ya taifa, ina maana gani yaani utifa ni ndani ya taifa tu au hadi nje ya taifa. ikiwa mama Salma anaongea kiswahil nje ya nch huo ni utaifa wake ana haki ya kujivunia kinachotakiwa ni kuwa na wakalimani ili ujumbe anaoutoa uwafikie wote kwa lugha zao. mbona maris wanaokuja nchini wanapoongea lugha zao na kutafsilie aidha kwa kiswahil au kiingereza hamuwacheki na kusema si wasomi, inakuwa ajabu tu kwa mtanzania asipoongea kiingereza na kudharauliwa eti si msomi. HONGERA MAMA SALMA DUMISHA LUGHA YA TAIFA POPOTE UENDAKO HUO NI UTAMBULISHO WAKO ACHANA NA WATU WALIOTAWALIWA KIMAWAZO.
    tuwaombee ili wajisikie ni wananchi hao ni wale wasio ujuautaifa. wanhitaji kwenda tena shule.

    ReplyDelete
  19. Actually she is beuty and attractive I don't mind about language but they way she dress very undiplomatic

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...