shule ya sekondari ya mzumbe, mji kasoro bahari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. JAMANI MOROGORO KUBAYA BWANA DU YAANI KWA KWELI IMAGINE UPATE KAZI HALAFU UPANGIWE MOROGORO SIUTALIA SANA MARA MIA NIPATE KAZI MOSHI NITASEMA NITAKUWA NAENDA KUJIRUSHA ARUSHA PIA KUNAUSTARABU KWA KINA MANGI ILA NDUGU YANGU MORO NI NGUMU SANA NA VUMBI LAKE MTANISAMEHEE NI NAFSI YANGU SIO YAKO

    ReplyDelete
  2. Hiyo ni Shaban Robert village. Kijiji hicho kilimlea Unguu na Mustahiki kwa miaka minne.John Mapinduzi na veterans wengine pia walikuwa hapo. Am coming to deliver back very soon to you Mzumbe and Ilboru, I promise.

    ReplyDelete
  3. sasa kaka Michu hapo ndio umefanya la maana. Umeweka shule ya watabe halisiwa Tanzania. Naiona mabweni ya Shaaban Robert hapo... hilo bweni lililo kwa mbele kabisa liliungua mwaka 2000 bahati nzuri hakuna alieathirika. Baada ya ukarabati ndio likaezekwa na bati jekundu tofauti na mabweni jirani ambayo yote yana vigae.

    Mpo wapi form 6 wa 2001? I am so proud of this class maana baada ya shule kuipoteza nafasi ya 1 kwa matokeo ya form 6 mwaka 99 na mwaka 2000; class of 2001 walirudisha heshima inapostahili. Na waliotufuatia hawakutuangusha kwani Mzube ilishikilia #1 mwana 2001 mpaka 2006 mfululizo.

    ReplyDelete
  4. michuzi saidia watanzania wenzangu kuingia site hii kusapoti tumu ya tanzanite fc ya atlanta, amaboa wanacheza ligi hapa atlanta ga.site yao hii
    http://www.tanzanitefc.com/
    www.wabongofc.blogspot.com

    ReplyDelete
  5. Malezi ya Mzumbe, Elimu yake ni kamilifu ya Kitanzania, daima mbele nyuma mwiko...

    Amour and Respicious Kundawa

    Sifael and ...

    Mrisho Amani and Said Nusura together with their discipline prefect.

    Rahim, Rajab and Daudi Mwani

    Mungu wabariki viongozi wa wetu.

    ReplyDelete
  6. Mi nilikaa kijiji cha Milambo maana mabweni yaitwa vijiji pale A-level 1992-94 PCB na headmaster wetu mzee Msuka ambaye alituhimiza kuimba mwimbo wa mdau hapo juu Zemarcopolo, Kuanzia hapo tulianza kuzishikisha adabu A-Level zote za wamissionari kushirikian na ndugu zetu wa Illboru na kuwaonyesha hata shule za serikali zikisimamiwa zina deliver, Ahsante Kaka Michu hizi picha zinatupa kumbukumbu nzuri

    ReplyDelete
  7. Oyaa Doc. Kondo(zemarcopolo) Sifael msaidizi wake alikuwa somebody SHIJA ambaye alini-preceed!
    By the way" DETERMINATION IS OUR MOTTO"
    Alumni-Houston-TX

    ReplyDelete
  8. Naililia mzumbe..elimu yake...ni kamilifuuu ...ya kitanzaniaaaa....!!!
    daima mbeleee ...nyumaaa ....mwiko..

    Determination is our motto...

    Wapi mzee msuka,mzee mwaisabila (....utaangukia pua chini mzee...angalia sana...)
    mzee wibo..(marehemu).....

    yaani hapa ndio wanapotoka vipanga wa tanzania

    ReplyDelete
  9. Ime2lia. Tuliimba pale (1995 hadi 1997)" Elimu ya Mzumbe, malezi ya Mzumbe, Daima mbele, nyuma mwiko". Na tulikuwa na ka-utamaduni ka kutaniana. Utamsikia mtu anasema " shauri yako wewe, utapata Dv II peke yako"!!! Just imagine, tukaweza kuitana majina kwamba ni "ABNORMAL" species.

    Pale Mwl Kabale, Mwl Msuka (HMaster), na walimu wengine kedekede wenye vipaji vya kujituma, walitufanya "tuwatengenezee nyali" (kwa wasomaji wapya, nyali ilikuwa ni special meal ya ubwabwa baada ya darasa lilotangulia kufanyiza mbaya kitaifa). Basi ng'wanawanne, tukapiga mzigo, hadi sasa tuna-flourish. Asante kwa picha hili. Wazumbe alumni iko wapi, au mimi nianzishe ya 1995-97? tuwasiliane hapa....ferrhyme@yahoo.ca

    ReplyDelete
  10. hello! Hii inanikumbusha mbali sana. Vijana wa 1996-1998 mpo? Nakumbuka tulikuwa waanzishaji wa mpira pale maana wazumbe walipenda sana buku. Games zilikolea mpaka mashindano yakaanza,
    Tupo pamoja wazee wa mzumbe na waTZ woteeee. hureeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  11. Mbona hakuwataji wasichana wenu wa kubugi nao dansi wa Kilakala? Au miaka yenu mlikuwa mnashindana tu na waseminary hamuendi kwenye disco Kilakala na Kilakala nao hawaji kwenu. Manake enzi za miaka ya 80 Mzumbe wakisikia Kilakala wamealika watu wengine kucheza nao mziki wanakuja juu!

    Utoto kaazi kweli kweli!

    ReplyDelete
  12. Michuzi umetukuna wengi na hii picha. Mimi nilikuwa nakaa Mkwawa...kipindi kidogo 1990-92. Wakati huo mwl wa Biology "A" level alikuwa mganda!! Ola wana Mzumbe!!

    ReplyDelete
  13. Mzumbe ni shule poa lakini mambo yapo PUGU, au siyo wazee wa POND: Kitabu mbele, fungus nyuma, maji kunywa Gongo la mboto! kilakishari, kilakishari, Pugu-kariakoo x2

    ReplyDelete
  14. leo Michuzi umenikumbusha mbali sana, hiyo ndo shule ambapo kweli tulijifunza kujituma, kupambana na mazingira magumu na kufanya vizuri badala ya kulalamika kila siku. unajua mazingira ya Mzumbe sio mazuri, lakini ukiangalia jinsi wanafunzi wanavyofaulu utashangaa sana, hii inanikumbusha msemo kwamba 'mchapakazi anakitumia hata kile kidogo alichopewa kufanya kazi nzuri, lakini mzembe atashindwa na kulaumu chombo alichotumia', mpo wapi form six 2000 akina Franc Mwega, Davis Binamu (Mkwawa 4) na kadhalika!! tukutane hapa hapa wakuu!! tehetehetehetehe!! anaeukumbuka wimbo wote wa Mzumbe naomba auweke hapa, nimeumiss sana, ila motto wetu ni mkali sana "determination is our motto"

    ReplyDelete
  15. Jamani msinikumbushe Mzumbe mie, shule ina watu wanapiga buku kama wametishiwa hukumu ya kifo. Hata kama hupendi kusoma hapo utasoma tu!! Pia nakumbuka vituko kwani kuna wakati kila kitu kiliitwa kwa kuanzia na "nyu" mf. uji -nyuji, wali-nyali(Hii haipatikani mpaka graduation).pia kuna kale kamtindo ka kuzomea kwa mlio wa nguruwe:chwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Kuhusu disco usiulize, lilikwepo tulikuwa tunakwenda na Lori letu na kibasi kidogo sijui bado kipo kile ki-isuzu.Pia yule bibi mpishi sijui mmasai yule sujui kama yupo maana sijatia timu toka nikamate gamba 1996 (PCB)

    ReplyDelete
  16. Sasa Michuzi hebu tukumbushie na Kibaha Secondary School, shule ya kitabu na kuku. Shule iliyomjenga JK.

    Wazee wa Pugu na Mzumbe nakumbuka mlikuwa mnakuja kuja sana kudoea kuku, huku mkidai mnafuata "utirio".

    ReplyDelete
  17. Michuzi ulikuwa Arusha hata hukupitia Ilboru...au ndio ilikuwa vekesheni fulani ..kule ndio kazi ilikuwapo sio hapo Mzumbe kwa hao waliokuwa watoto mayai!!

    ReplyDelete
  18. loooooong time saaaana,hapo ni shabaan Robert,ukishuka chini kidogo tuu unaingia mzumbe chuoni,salaam kwa wanamzumbe wote popote walipo duniani.
    mdau ndayo!

    ReplyDelete
  19. kwa bdygy zangu walioomba wimbo wa shule namba kuwasilisha:
    1. Shule yetu Mzumbe Sekondari, yasifika kote Tanzania,
    malezi ya Mzumbe, elimu yake,
    ni kamilifu, ya Kitanzania,
    daima mbele, nyuma mwiko

    2. Vijijini pia na mijini, matunda yake yaonekana,
    malezi ya Mzumbe, elimu yake,
    ni kamilifu, ya Kitanzania,
    daima mbele, nyuma mwiko


    ...kama kuna niliyosahau wadau waongezee

    ReplyDelete
  20. Yah nawakumbuka sana kina Mwega, William Mng'ong'ose, Mzee Madaha, Dula Tall, Wahabi matengo, Erick Nestory Felix John, Mko wapi vijana wa 2000 si mchezo wazee wa kumove

    ReplyDelete
  21. Basi Serikali na Wizara inayo husika kumbukeni Kujenga Majengo Mapya ya Ghorofa ili kuipanua shule hiyo muhimu yenye historia kubwa nchini.YATABAKIA HAYO MAGOFU hadi wajukuu zetu watayakuta,Aibu!Au tunasubiri KAMSAADA?wamesoma watu kama kina Mbaraka Mwinshehe katika shule hiyo pamoja na viongozi wengi hapa nchini!

    ReplyDelete
  22. Loooh hapo ni full malaria na typhod, hiyo ndo sifa ya Mzumbe, kama haitoshi joto kupita kiasi, yaani uko "prepo" huku unajipepea mbu na joto, adhabu tupu, haiyanani sijaona shule ya serkali ilokuwa na mazingira mazuri kama ILBORU, yaani kama upo nchi za scandanvia vile full kipupwe maji safi na salam kutoka kwenye mlima meru, ha ha ha! EDUCATION FOR SERVICE.

    Bablii

    ReplyDelete
  23. Mimi nakumbuka, Uji-nyuji, wali-nyali(hii haipikwi mpaka graduation) na ule mlio wa nguruwe-Chwiiiiiiiiii kama mtu akichemsha.Ila mzumbe noma jamani nilitaka kukimbia kuogopa watu wanavyopiga buku utadhani wametishiwa kuchinjwa!! Bila kuwasahau wachumba kutoka Kilakala na Disco letu la mchana jua kali.Tukitoka disco tunaingia kwenye lori au kile kibasi ki-isuzu.
    Mdau A-level 1995-1996

    ReplyDelete
  24. Asante Peter Nalitolela, umepatia, maana ungeshindwa kuandika huu wimba ningefuta kura yangu niliyokupigia uwe kiranja wa taaluma baada ya kuja na mkwara wa www. , kijana uliomba kura kwa mbwembwe nyingi sana, lakini ulijitahidi. mimi mdao form six 2000 na sasa hivi nipo ughaibuni!! tehetehetehe, uliyesema kiisuzu, tulikuwa tunakiita kiberiti hicho miaka yetu

    ReplyDelete
  25. dah nilisahau jambo la muhimu sana. Kuna alumni group iliyoundwa kwa ajili ya kujaribu kwuakutanisha wanafunzi na wahitimu wa Mzukila (Mzumbe + Kilakala).

    Kuna yahoo group ().
    Fuata link hiyo hapo juu na u-register ili uweze kupata updates mbalimbali toka kwa wazumbe wenzako na kwa vilei!!

    ReplyDelete
  26. jamanivijan wa 1996-1998 , mnakumbuka tulivyowakimbiza wana minaki walivyokuja kututembelea tukawapeleka prepo hadi sasa tisa usiku, teh teh teh teh teh teh teh
    ile wajameni kitabu kilikuwa kitamu , jamani OCCO MNAIKUMBUKA VIJANA WA PCB kule bondeni orange consuming organization, pia vijana wa 1995/1997 kina marauder , joka mkiuno , kina katili, ah ah ah ni noma
    karume namba mbili pale na mikungu ya ndizi ya majani ??
    michuzi umetufikisha mbali sana ,kiva

    ReplyDelete
  27. Hii picha inatukumbusha mmambo mengi.Mdau Nalitolela kiranja wangu wa elimu unapakumbuka vizuri sana.Bweni hilo liliungua 03-03-2000.Namkumbuka bro mmoja aliitwa Obote alilia sana kwa kupoteza jezi zake.Nalikumbuka lile kosi la mzee Obeda sijui wako wapi.Akina Onyango,Rama Mbiro ,Lipeleko nk.Nasi nakumbuka tulijiita kosi la Mzee Simbi(Our famous physics teacher tulipokuwa form two 2001).Nadhani form 4 graduates wa 2003 wanakumbuka vizuri.
    Mdau O-level 2000-2003

    ReplyDelete
  28. jamani mnamkumbuka shangazi wa Jikoni, uji alikuwa anasema "UCHI WANGU MUTAMU"

    ReplyDelete
  29. Yaap inanikumbusha mbali sana. Nilikuwa hapo SR 5 2002-2004 PCB. Sie ndo tulianza special school na mkuu Msuka. Mbona raha!!!! mZUMBE PAMELEA WATU HAPO NA UKUTOKA HAPO UMEKOMAA KISAWASAWA MAANA HAKUNA UMAYAI HAPO. CHEERS MA-ALUMS WOTE

    ReplyDelete
  30. Tunaomba picha za Tanga School (Tanga Tech). Shule kongwe kuliko zote nchini miaka 110. mPia ni shule aliyosoma Kikwete!

    ReplyDelete
  31. JAMANI JAMANI MBONA MWANIKUMBUSHA MBALI NAMNA HII,ASISEM MTU WAPI KAMA MZUMBE,KWELI ILE KAMBI MUHIMU SAANA,NAKUMBUKA NIMEFIKA NA HEADMASTER WETU MWASHA 1999 NA NIMEMWACHA 2005,KWELI MZEE ALIKUWA KIPENZI CHETU KWA MAPENZI YAKE KWA WANAFUNZI,WAPI O'LEVEL YA 1999-2002,KINA MATENGO SHARIFU,JOHN WILLIAM,MBABI PETER,ATHUR MSAFIRI,MWAZEMBE CHRAMADHA,NA WENGINE WENGI,MIMI VICE WENU KIZWI H,NIPO UCHINA,BIG UP SAANA MICHUZI KWA KUTULETA NYUMBANI,NIMEMISS SAANA NYALI NA UJI WA SHANGAZI(MWENYEWE AKIITA UCHI MUTAMU)HAHAAA,WAPI GWAKISA JOHN MTANGULIZI WANGU,MKUU SANA PENDI EZEKIEL,WAPI MAKAMU UNCLE BITO,HAHAAA,ELIUD SIMON,FELICIAN BALELE,STANFORD JOHN!EBWANA NILIKUWA MKAZI WA SHAABAN ROBERT SIX KABLA HALIJAAUNGUA NA NILIKUWA MUHANGA WA MARCH 3 2000 BWENI LETU LILIPO UNGUA,WAZEE WA FEDERATION MPO WAPI JAMANI,IKULU TUKUFU,SALAMU KWA WEZI WA MACHUNGWA NA WAKAAZI WA FUCULTY KINA MWINGIZI OBETH,ELHARD BILALO NA ADVAVACE WOTE WA 2003-2005!!!!!MALEZI YA MZUMBE ELIMU YA MZUMBE NI KAMILIFU YA KITANZANIA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO,DITERMINATION.......................

    ReplyDelete
  32. I am not a good member of this blog but the post (pic) really took me back far way long.That place used to be our home and it will always be,,was there from 2003 to 2005, May God bless the man of the house himself Baba Mwasha, the S.U.M and the greatest of all biology teacher Mr Malale(never seen anyone like him before and thereafter),,R.I.P baba Wibo the boys are missing u much!!As for you boys I got one word,,NYAYO!!

    ReplyDelete
  33. NiHao Mheshimiwa VP Hilali Kizwi...Nakumbuka siku hiyo SR6 yaungua nilikuwa nime dodge morning session "vilass",nimelala pale SR5.I was shocked,,,tukio moja la aibu nalikumbuka:wabongo tulishindwa kutumia fire extinguisher,,,teacher mmoja Mmarekani ndio alikuwa anaonesha ujasiri wa ku face moto..Mungu Atusaidie...ilikuwa ni ijumaa...vijana wa kosi la "obeda" wamehifadhi pamba na buti zao kali kwa ajili ya mzukila debe on the next...ikawa ndio mtihani tena.
    Huwa natumia msuliata mzumbeasis sometimes hapa versity...buku la Mzumbe aminia.Hapo juu kuna mtu kanikumbusha Malale Sir....ile kichwa ni noma.
    Ok vandugu SAYONARA

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 31, 2013

    Noma storiez Za bitwale na mwanafunzi mmoja lazima atoe morning speech asubuhi ... Mashindano ya Sunday Dominic na mwarabu ? Wazee Wa mabanda 10 wapi Fred Edson? Mkungume? Mfaume?..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...