jk akikutana na baraza jipya la mawaziri leo ikulu, dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Duh...sikujua hapo kwetu tuna meza ndefu kama hii...basi imagini ndafu na nyama choma baadae!!!

    ReplyDelete
  2. Sijui atakuwa anawaambia nini kipya!?Kwa maana alipoingia tu ikulu alitembelea wizara zote na bado walimuangusha!ndio itakuwa sasa!!??kuna jipya gani?kwa maana asilimia kubwa ya mawaziri ni walewale wamebadilishwa wizara tu ila ndio hawabebeki wataiba tuuu,wameishazoea kama wakiiba ni kujiuzulu na kukana tuhuma hamna kushtakiwa wala nini!!

    ReplyDelete
  3. JAMANI RAIS WETU HANDSUM BOI...

    ReplyDelete
  4. JK wape mkwara mzito hao mawaziri wako

    ReplyDelete
  5. Bado baraza ni kubwa!!Lakini afadhali vile vizee vimetoka..vimekaa kwenye cabinet hadi watoto wao nao wamestaafu kazi vyenyewe bado vipo!!! Duh

    ReplyDelete
  6. Hivi hakuna Award za Waandishi wa HABARI. Maana Michu Nakukubabali sanaaaaa.

    ReplyDelete
  7. Too many people! we have been running budget deficit for 10 years in a row, our budget cashflow depends on donors to inject 40% capital. why cant our government be sensible enough to merge correlated ministries and appoint smart individual to run them? It doesnt make sense at all..wake up JK, how can you maintain and sustain all those crooks?

    ReplyDelete
  8. Kumbe hata Rais anavaa saa mkono wa kulia kama mimi tehetehete...

    ReplyDelete
  9. Jk hao uliokuwa nao hapo baadhi yao bado ni MAFISADI hata ukiwaambia kitu kitakuwa kinaingia sikio la kulia na kutoka kushoto hapo ni sawa unampigika mbuzi gitaa au kutwanga maji kwenye kinu sisi wananchi tungefurahi kama ungetuambia MAFISADI wa kwanza umefikia uamuzi gani? katika kuwawajibisha hao uliokaa nao kuna wengine wanafikiria jinsi gani nao watatuRICHMOND au kutu EPA
    A.H.W (From B)

    ReplyDelete
  10. Hakuna kitu hapo,ni ubabaishaji mtupu!Kikwete usipowaondoa Mawaziri wako walioguswa na tuhuma za Epa na nyinginezo,mathalani Masha,Hosea,Mgonja,Mwanyika,nakupunguza wizara zako kwa kuziunganisha ziwe chache zaidi,Ripoti ya Epa kuwekwa hadharani kabla ya Bunge la Bajeti Juni 2008,Basi ujue umekula hasara uchaguzi ujao wa 2010.Hata sisi tuliokuwa nyuma yako sasa tumechoka na kinachoendelea!

    ReplyDelete
  11. Lakini mh.Jakaya utukumbuke nasi tulio huku masomoni kwani hao mabwana waliopo hapo hata kama siwaaminihivi.Imaging mtu anamaliza chuo anakaa zaidi ya miaka tano hajapata kazi kwani hana uzoefu wa kazi sasa sijui uzoefu utaupatia shuleni au?.Hilo lazima ulijue nasi tunataka kutumikia Inchi na bodi inataka kurudishiwa hela zao baada ya mwaka mmoja sasa bila kazi tutazipata wapi?Hilo lazima ulifikirie kwa makini zaidi .Mawidhara mengi kuna watu wazee zaidi ya hata miaka 80 na bado wanafanya kazi tu na elimu yenyewe ni form 4 what the meaning?.Hilo fikiria lazima mtu akitoka chuo aandaliwe mazingira ya kazi la sivyo tutabaki kuwa nyuma milele.

    Student(MP)

    ReplyDelete
  12. Naogopa saana hawa jamaa kwani nishaona mtu kakosa kazi at the same time huyo boss anazungumza na rafiki yake kumtaka amlete mwanawe aliyekataa kuendelea shule baada ya kumaliza form4 ili ampe kitengo kimojawapo hapo offisini.Imaging huyo aliyeambiwa hakuna kazi ni msomi wa chuo tena mtaalam wa section hiyoyo.
    Swali hivi hii country ni ya watu fulani fulani au ni ya wote na kama ni ya watu wote basi give us the chance to handle some of the sector
    student(MP)

    ReplyDelete
  13. Mafanikio ya nchi yetu si Rais kutembelea wizara zote au kuwa na kikao cha mawaziri wote Ikulu isipokuwa ni kuwapiga chini CCM na serikali yake kisha kuchagua chama kingine. Tanzania itaendelea, angalieni Kenya Moi na KANU wameondoka nchi inapiga maendeleo kama nini.Tanzania inawezekana pia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...