hifadhi ya taifa ya jozani ni eneo maarufu duniani kwa kuwa na mbega wekundu ambao hawapatikani popote duniani ila zenj. mamia ya watalii toka ndani na nje ya nchi hutembelea msitu huo, na mie nilifanya hivyo karibuni wakati wa vekesheni. kwa habari zaidi bofya hapa
Home
Unlabelled
jozani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Sasa mwana misitu Michu! Mbona watu hapo wanaonekana wamevaa kama wanakwenda ofisini? Nadhani nguo za kwendea mbugani wanatakiwa wawe kwenye combati siyo suruali na vitenge!
ReplyDeleteHivi jamani kwa nini hawa kima punju, wasijaribiwe kupandikizwa kwenye maeneo mengine ambayo yana mbega wa kawaida kama misitu ya amani, bamba na maramba Tanga
ReplyDeleteHii naona itasaidia kuokoa viumbe hawa wasifutike duniani iwapo kutatokea chochote kisichofaa kwa maisha yao ndani ya msitu huu wa jozani
Sasa hao Mbega wanazungumza lugha gani na watalii???
ReplyDeleteDah huyo jamaa mwenye kipara(picha ya tatu) anaonekana kama uncle phil (James avery) wa kwenye ucheshi wa Willy Smith(Fresh Prince of Bel-air)
ReplyDeleteMbega wekundu wanapatikana pia Selous Game Reserve.
ReplyDeleteWadau mimi napenda kuuliza ni mkakati gani ufanyike ili kuhamasisha utalii wa ndani? (Yaani watanzania kutembelea vivutio vyao vya utalii)
ReplyDeletehawa kima wekundu (red colabus monkeys)duniani kupatikana brazil na zanzibar peke yake.
ReplyDeleteHIYO PICHA YA PILI TOKA JUU YENYE KIBAO CHA NO PARKING HAO WANYAMA WAKUBWA WANAPATIKANA WAPI LICHA YA JOZANI?
ReplyDelete"Rehema" ukija zenj salimia kaka zako, shauri yako!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeletemasahihisho!!!!!!! Jozani hakuna Mbega, kuna KIMA PUNJU (hao wanaoonekana katika picha) ambao duniani wanapatikana Zanzibar tu.
ReplyDeleteWanaowatunza hao ngedele wamejitahidi kuwawekea matunda mazuri naona mpaka fursadi , na mapera .hongereni kwa matunzo mazuri.Hawa wanyama (jamii ya kina kima) wamebarikiwa sana katika swala la chakula wanaweza kuishi na kula katika vipindi vyote iwe kiangazi au masika nilipata maelezo yao kwenye tvt wanasema anakula wadudu, mizizi ya miti, matunda, majani.pia wanapochambuana kupe(wadudu)kwenye miili yao si kutoa wadudu tu ila ni kupunguza hasira zao wanapokua wamecharuka.
ReplyDeleteMichu. nipelekee salamu zangu kwa huyo mfuga ng'ombe wa chwaka kua huyo mwanandama ana minyoo amtafutie dawa au mpaka aone anaporomosha mafua ndo astuke? ndio sotoka yenyewe hiyo.
anon wa 3 mar, 10:38 asante kwa mlishonyuma (feedback), mi nlikaa kimya sikutoa masahihisho juu ya hilo jina mbega ulotumia nkajua hicho ulichoongea ni kikwenu nikakusamehe bure.maana siku hizi mtu akishindwa kuongea kiswahili fasaha, mara utaskia mwanahuyu anaunganisha tuu sisi tunabaki tumeduwaa, tumepigwa na butwaa hatupati picha.
ReplyDelete