kibao cha jozani maeneo ya chwaka
watalii wakifaidi mandhari ya jozani
lugha za kimataifa
msitu wa jozani unafaa kuchezea filamu za kama za tarzan
mapokezi
mbega haogopi binadamu, huyu nilimsogelea kiasi cha mita moja na akapozi
mbega mwekundu na mwanae
asili ya kuitwa mbega wekundu ni hayo manyoya mgongoni
mbega hawana noma
jozani ni kama mizitu ya amazoni
hifadhi ya taifa ya jozani ni eneo maarufu duniani kwa kuwa na mbega wekundu ambao hawapatikani popote duniani ila zenj. mamia ya watalii toka ndani na nje ya nchi hutembelea msitu huo, na mie nilifanya hivyo karibuni wakati wa vekesheni. kwa habari zaidi bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Sasa mwana misitu Michu! Mbona watu hapo wanaonekana wamevaa kama wanakwenda ofisini? Nadhani nguo za kwendea mbugani wanatakiwa wawe kwenye combati siyo suruali na vitenge!

    ReplyDelete
  2. Hivi jamani kwa nini hawa kima punju, wasijaribiwe kupandikizwa kwenye maeneo mengine ambayo yana mbega wa kawaida kama misitu ya amani, bamba na maramba Tanga

    Hii naona itasaidia kuokoa viumbe hawa wasifutike duniani iwapo kutatokea chochote kisichofaa kwa maisha yao ndani ya msitu huu wa jozani

    ReplyDelete
  3. Sasa hao Mbega wanazungumza lugha gani na watalii???

    ReplyDelete
  4. Dah huyo jamaa mwenye kipara(picha ya tatu) anaonekana kama uncle phil (James avery) wa kwenye ucheshi wa Willy Smith(Fresh Prince of Bel-air)

    ReplyDelete
  5. Mbega wekundu wanapatikana pia Selous Game Reserve.

    ReplyDelete
  6. Wadau mimi napenda kuuliza ni mkakati gani ufanyike ili kuhamasisha utalii wa ndani? (Yaani watanzania kutembelea vivutio vyao vya utalii)

    ReplyDelete
  7. hawa kima wekundu (red colabus monkeys)duniani kupatikana brazil na zanzibar peke yake.

    ReplyDelete
  8. HIYO PICHA YA PILI TOKA JUU YENYE KIBAO CHA NO PARKING HAO WANYAMA WAKUBWA WANAPATIKANA WAPI LICHA YA JOZANI?

    ReplyDelete
  9. "Rehema" ukija zenj salimia kaka zako, shauri yako!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. masahihisho!!!!!!! Jozani hakuna Mbega, kuna KIMA PUNJU (hao wanaoonekana katika picha) ambao duniani wanapatikana Zanzibar tu.

    ReplyDelete
  11. Wanaowatunza hao ngedele wamejitahidi kuwawekea matunda mazuri naona mpaka fursadi , na mapera .hongereni kwa matunzo mazuri.Hawa wanyama (jamii ya kina kima) wamebarikiwa sana katika swala la chakula wanaweza kuishi na kula katika vipindi vyote iwe kiangazi au masika nilipata maelezo yao kwenye tvt wanasema anakula wadudu, mizizi ya miti, matunda, majani.pia wanapochambuana kupe(wadudu)kwenye miili yao si kutoa wadudu tu ila ni kupunguza hasira zao wanapokua wamecharuka.

    Michu. nipelekee salamu zangu kwa huyo mfuga ng'ombe wa chwaka kua huyo mwanandama ana minyoo amtafutie dawa au mpaka aone anaporomosha mafua ndo astuke? ndio sotoka yenyewe hiyo.

    ReplyDelete
  12. anon wa 3 mar, 10:38 asante kwa mlishonyuma (feedback), mi nlikaa kimya sikutoa masahihisho juu ya hilo jina mbega ulotumia nkajua hicho ulichoongea ni kikwenu nikakusamehe bure.maana siku hizi mtu akishindwa kuongea kiswahili fasaha, mara utaskia mwanahuyu anaunganisha tuu sisi tunabaki tumeduwaa, tumepigwa na butwaa hatupati picha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...