Bwana Michuzi habari yako.
Hii siyo comment bali ni tangazo nakuomba ututangazie kwenye blog yako kwa wabongo wanaoishi London Uingereza.
TANGAZO LA SHUGHULI.
FAMILIA YA KINA KILEMELA YA GREAT ORMOND STREET LONDON, INA FURAHA KUWATANGAZIA SHUGHULI YA NGOMA YA BINTI ZAO, ASIA NA FATMA KILEMELA ITAKAYOFANYIKA 65 ORDE HALL STREET, GREAT ORMOND, HOLBORN, LONDON.
SHUGHULI ITAANZA 27 APRIL 2008 NDOWEKA, TAREHE 1 MAY MBIGA, TAREHE 2 MAY MKOLE, TAREHE 3 MAY MKESHA, TAREHE 4 MAY KUTOKA.
HAKUNA MCHANGO WOWOTE WA KIFEDHA UNAOHITAJIKA.
SARE NI KHANGA ZIMEANDIKWA "HI HIVIHIVI TUU", AU KITENGE CHA WAX, AMBAVYO VIMESHAAGIZWA KUTOKA BONGO NA UNAWEZA KUVIPATA KWA £7:50.
VANGA, MDUNDIKO, MKINDA NA GOMBE SUGU VIMEALIKWA KUTOKA BONGO.KWA MAELEZO ZAIDI FIKA NYUMBANI (ADRESS HIYO HAPO JUU), AU PIGA SIMU NAMBA 07826007942.
KUFIKA KWENU NDO UKAMILIFU WA SHUGHULI HII.
AHSANTENI.


Mimi nimemiss mkole na mkinda sana tu, sijui Gombe Sugu litakuwepo siku ya kutoka? Au ndio siku hizi mwali anatolewa na rusha roho?
ReplyDeleteKingine nataka kuja kuhudhuria hiyo sherehe, na mimi ni mkazi wa Ukerewe ila ninaishi kijijini, yaani kijijini kama ambavyo unajua maana ya kijiji. Swali nikiendaga ngomani nikiwa TZ kutokea kijijini huwa sina wasi wasi wa mahali pa kula wala pa kulala, maana ntakula na kulala ngomani. Sasa hali itakuwaje na hii ngoma ya uzunguni? Ntakula na kulala ngomani? Mbona mkole mnafanyia holini, hakuna miti mikubwa huko? Au mje mfanyie huku kijijini kwetu maana kuna miti mikubwa tu au mkaombe ruhusa mfanyie kwenye park! Si mambo ya mila bwana! Wadau mnashangaa nini? kwenu hamna mila?
Swali la mwisho, turudi kwenye mila, je siku ya mkole hao wali watawekwa matiti nje kama nyumbani au huku inakatazwa? Wakitoka wanaolewa kabisa kama nyumbani au bado hawajapata wachumba ili wachumba waje mkoleni kujichagulia?
Nina maswali nyie lakini midamu mumeweka address yenu ntakuja huko huko kwenu kama hamtanijibu, ila swali la kuhusu kula na kulala ngomani jamani naomba mnijibu haraka, ili nisije nikafunga safari nikalala vibarazani.
Mwayangu mwayangu!
YAANI HADI ULAYA WANATOA MWALI ? HAYA KWA MTINDO HUU KAZI IPO
ReplyDeletesio mchezo, ngoma mpaka ughaibuni!!! ama kweli mwacha mila ni mtumwa, sasa ngoma ya unyago inatangaziwa kina mama tu, leo iweje kila mtu aambiwe!! haya jamani, kina braza men kaeni mkao wa kula, wari hao, mshindwe wenyewe, hadi mdundiko na mchiriku toka bongo wamealikiwa, langu jicho!!lakini nawatakia kila la kheri wari
ReplyDeleteSafi sana mila na desturi razima zifanyike,I wish ningekuwepo ningekata kiuno na bingibingi kiunoni naamanisha shanga.Halooo mwanamke kuchezwa bibi yaaani kutoka unyago.Nashukuru nilitoka unyago maana sisi wanawake wa uswahilini kita........... baraa mama.Mdau
ReplyDeleteRose Norway
Hama kweli ukishangaa ya musa basi ya firauni yaja.wazaramu kwa ngoma kiboko.mnge chukua hall mjifungie ndani kabisa mcheze ngoma vizuri manake msije mkaitiwa polisi bure kwa kupiga kelele.alafu vikuindi vya ngoma vinatoka bongo au mnatumia kanda? Simchezo hili mtu lazima ulichukulie vacation.UNAJUA hii blog inavituko vya kila haina kila kukicha kutoka kwa manka mushi mpaka kwa wazaramu wa london. He he he he mnastahili pongezi lakini kwa kuendeleza utamaduni na sasa hivi tutasikia sherehe za kutailiwa london.
ReplyDeleteWHAT???!!!! HII NI JOKE KAKA MICHUZI??!!! SIAMINI KABISAAAAAA!!!
ReplyDeleteungejua kama wax zinatengenezwa Holland usingepata taabu ya kuagizia Bongo na vile vile kuna kikundi cha mdundiko kinachoongozwa na mzee Kamogola siku ingine usiangaike kufata Bongo njoo Holland. mambo yote hayo tembele kamogola@gmail.nl
ReplyDeleteNgoma hadi UK? kazi ipo
ReplyDeleteNa lini natakiwa kuja kuchagua mchumba. Ila inabidi waangalie wakiwaweka matiti wazi kama bongo watashitakiwa.
ReplyDeletehivyo 'ngoma za binti zao'maana yake nini?
ReplyDeletekwa jinsi ninavyofahamu mimi ngoma kama hizo wanaohudhuria ni wanawake tena ambao walishawahi chezwa ngoma kama hizo sasa inakuwaje mwaliko hausemi kuwa ni shughuli ya kina mama na haijuishi wanaume? mmh....
ReplyDeletemila zingine kazi kweli kweli....laiti mngejua wanachofundwa hao mabinti
ReplyDeletehakuna la maana zaidi wanayofundishwa kwenye hiyo ngoma sana sana kuhusu wanaume,sometimes i hate mila
ReplyDeleteWote feki, hakuna mume hapo!
ReplyDeleteOOOoooH ACHENI HIzooo, HIYO SHUGHURI NI YAKUWATOA NDANI BAADA YA KUKEKETWA? kama hivyo niko njiani nakuja.
ReplyDeletejamani huo mdundiko na vanga mtavipigia ktk uwanja gani?maana ni vitu vinavyohitaji nafasi, na hayo makelele yake,kweli mtawapona majirani?au ndio ngoma itabidi tu izimwe?mimi ninawatakia mafanikio mema kwakuendeleza mila na desturi hata ugenini,ingawa nadhani itakua ngumu kutokana na mazingira.Mdau Sevensisters,Tottenham.
ReplyDeleteDuh!! hii kali, ngoma mpaka mantoni?
ReplyDeletewallah siamini,ngoja nichangamkie visa UMOJA HOUSE nikashuhudie mambo ya wazaramo kwa watasha!!!
ReplyDeleteHuo ni uzaramu pure!!kuleta ngoma ugenini!!kwanini usiende kuowa kijijini kwenu?kama kweli unapenda ngoma na vikorombwezo?acha ujinga wewe.
ReplyDeleteHongereni sana maana naona mnaendeleza culture... je na maadili m nawafunza au ni shuguli tu ili tupate shuguli???
ReplyDeleteMachui
shughuli hadi ukerewe?
ReplyDeleteHayo maneno kwenye hizo Kanga Pekeyake yanatosha Kufikisha Ujumbe kwa Walengwa: HIV i HIV i tu!!
ReplyDeleteNaelewa hizi ni TAMADUNI/JADI kwa baadhi ya Makabila Tz,lakini naelekea kufikiri Ngoma(Kumtoa mwali,Mdundiko)huchangia sana Maambukizo ya VVU Tanzania!
TUNAKUITIKIA TUTAKUJA LKN KABLA YA YOTE HUJATUFAFANULIA VIZURI KAMA HIYO NGOMA NI YA HARUSI AU NI UNYAGO HUO? TUTAKUJA BWANA SIO TUPO TUSIOPENDWA KUPITWA. JE NGOMA YA SEGELE IPO NA MATARUPETA?
ReplyDeleteMZARAMO HAACHI ASILI YAKE! HADI UGHAIBUNI!
ReplyDeleteMZARAMO HAACHI ASILI YAKE! HADI UGHAIBUNI!
ReplyDeleteANNONIMOUS ULIETANGULIA, HAWA NI WAZARAMO. HII NI NGOMA YA KUMTOA MWALI.
Segere mama eeeeh. Hii ngoma ya kizaramo tuu....mmmh mwe natafuta flight sasa hivi ya kutoka Canada to UK. Pakufikizia ninako ilobaki niende kwenye hiyo sherekhe niwaone kina fatuma wanatolewa nje. Hii sio harusi....sasa hiyo khanga ya Hi HiviHivi ina maana gani?
ReplyDeleteuswahili wenu mje fanyia kwenu,siyo kuwapigia makelele wasio na hatia!
ReplyDeletegongo na bangi navyo mnavyo vya kutosha au mnataka ngoma isichangamke?
MZARAMO HAACHI ASILI YAKE! HADI UGHAIBUNI!
ReplyDeleteANNONIMOUS ULIETANGULIA, HAWA NI WAZARAMO. HII NI NGOMA YA KUMTOA MWALI.
Nikitaka kucheka, huwa naingia humu kwenye tovuti ya kaka michu, yaana nimecheka hadi machozi yamenitoka. wazaramu wana watani wengi basi hapa inaburudisha mno, aunt NAILA imekaaje hiyo?
ReplyDeleteAcheni zenu za kitanesco hapa, mbona "bethdei, get tugetha, vipaimara, n.k" vinafanyika kila siku hapa London? Cha ajabu nini sasa? Ongereni bwana na bibi Vilemela kwa kudumisha jadi yenu.
ReplyDeleteUnaweza kumtoa mzaramo kutoka katika Uzaramo, Lakini kamwe huwezi kuutoa Uzaramo kutoka katika Mzaramo.
Kuna kufunga madogoli na somo ni nani jamani. Navyojua mimi wapiga ngoma lazima wanye changaa sijui itakuwaje manaake ukiwapa hivi vinywaji vya kigeni. Vilevile mwalike Kikwete na mkewe kwani wao pia ni watu wa pwani. Otherwise hongereni kwa kuendeleza mila hilo ndilo la msingi.
ReplyDeleteMpiga dogoli akikata hakawii kumba mama mwenye nyumba ....... Ulaya ataambulia address tu. Na huo mdundiko mtakujajikuta mko mahakamani shauri noise pollution.
ReplyDelete"Dizogolo ndyangu wadiba eheee.....!!!" Jaje....????
HII NGOMA NI DANGANYA TOTO,HAWA MA BINTI WATAKUA WAMEZALIWA BONGO WAMEISHI UK LABDA KAMA MIAKA 10,WENGI WAO WAMESHA CHEZWA NJE(I HOPE YOU KNOW WHAT I MEAN)SASA TENA WANACHEZWA NINI KWENYE HALL WAKATI UHAKIKA SHUGHULI PEVU WANAZIJUA.MAANA WATOTO WAKIBONGO WOTE WALIOLETWA HUKU UINGEREZA HAWASHIKIKI,WANA TABIA KAMA VICHANGU DOA NA KUNA MDAU KASEMA KUCHEZWA KWA WASICHANA WENGI BONGO KUMECHANGIA VVU NAKUBALIANA NA WEWE 200%.
ReplyDeleteNAJUA MNADUMISHA UTAMADUNI LAKINI ANGALIENI NCHI YENYEWE NA JINSI WATOTO WETU WALIVYO HARIBIKA HALAFU MUONE KUWACHEZA HUKO KUTAWASAIDIA HAO WATOTO AU KUTAZIDI KUWAHARIBU.NYINYI KINA MAMA HAMSHIKIKI MNA BEHAVE KAMA MA-TEENAGER ITAKUA HAO WATOTO.
UK KUMEKUCHA, MAREKANI NA CANADA MABISHOLOLO WENGI HUWEZI KUPATA MAMBO KAMA HAYA, WAO HATA HUKU WAKIANDIKA NI MAMBO YA YO YO,...UK MASSIVE..FANYENI ASILI YENU NDIO UTAIFA HUO.
ReplyDelete..NITAKUJA CHEZA GOMBE SUGU..
ReplyDeletekweli huyu Kalemela anataka kuwa ingiza ktk April 1st, 'Fools'Day'.
ReplyDeletekwa anayeijua London haiwezekani mtu kufanya sherehe siku Nne nzima ikiwemo 'mkesha'.
Huyu jamaa hajui ASBO(Anti-social Ban Order)itakayomfanya afikishwe kortini kutokana na kukera majirani. Pia wote wahudhuriaji baada ASBO mtafungwa kufuli miguuni yenye 'navigator' ili mfuatiliwe msijefanya 'shughuli' nyingine ya kero kwa jamii. Labda ukoo wa Kalemela muhamie shamba(county)jirani na David Beckham, ambapo utakuwa na hekalu lenu na shamba kubwa kufanya 'mkole' bila bughudha kwa wabeba boxi wachovu baada ya kazi wa katikati ya jiji la London maeneo ya Holborn.
Mdau
Guruwe
Kimanzichana