Bwana Michuzi habari yako.
Hii siyo comment bali ni tangazo nakuomba ututangazie kwenye blog yako kwa wabongo wanaoishi London Uingereza.
TANGAZO LA SHUGHULI.
FAMILIA YA KINA KILEMELA YA GREAT ORMOND STREET LONDON, INA FURAHA KUWATANGAZIA SHUGHULI YA NGOMA YA BINTI ZAO, ASIA NA FATMA KILEMELA ITAKAYOFANYIKA 65 ORDE HALL STREET, GREAT ORMOND, HOLBORN, LONDON.
SHUGHULI ITAANZA 27 APRIL 2008 NDOWEKA, TAREHE 1 MAY MBIGA, TAREHE 2 MAY MKOLE, TAREHE 3 MAY MKESHA, TAREHE 4 MAY KUTOKA.
HAKUNA MCHANGO WOWOTE WA KIFEDHA UNAOHITAJIKA.
SARE NI KHANGA ZIMEANDIKWA "HI HIVIHIVI TUU", AU KITENGE CHA WAX, AMBAVYO VIMESHAAGIZWA KUTOKA BONGO NA UNAWEZA KUVIPATA KWA £7:50.
VANGA, MDUNDIKO, MKINDA NA GOMBE SUGU VIMEALIKWA KUTOKA BONGO.KWA MAELEZO ZAIDI FIKA NYUMBANI (ADRESS HIYO HAPO JUU), AU PIGA SIMU NAMBA 07826007942.
KUFIKA KWENU NDO UKAMILIFU WA SHUGHULI HII.
AHSANTENI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. Mimi nimemiss mkole na mkinda sana tu, sijui Gombe Sugu litakuwepo siku ya kutoka? Au ndio siku hizi mwali anatolewa na rusha roho?

    Kingine nataka kuja kuhudhuria hiyo sherehe, na mimi ni mkazi wa Ukerewe ila ninaishi kijijini, yaani kijijini kama ambavyo unajua maana ya kijiji. Swali nikiendaga ngomani nikiwa TZ kutokea kijijini huwa sina wasi wasi wa mahali pa kula wala pa kulala, maana ntakula na kulala ngomani. Sasa hali itakuwaje na hii ngoma ya uzunguni? Ntakula na kulala ngomani? Mbona mkole mnafanyia holini, hakuna miti mikubwa huko? Au mje mfanyie huku kijijini kwetu maana kuna miti mikubwa tu au mkaombe ruhusa mfanyie kwenye park! Si mambo ya mila bwana! Wadau mnashangaa nini? kwenu hamna mila?

    Swali la mwisho, turudi kwenye mila, je siku ya mkole hao wali watawekwa matiti nje kama nyumbani au huku inakatazwa? Wakitoka wanaolewa kabisa kama nyumbani au bado hawajapata wachumba ili wachumba waje mkoleni kujichagulia?

    Nina maswali nyie lakini midamu mumeweka address yenu ntakuja huko huko kwenu kama hamtanijibu, ila swali la kuhusu kula na kulala ngomani jamani naomba mnijibu haraka, ili nisije nikafunga safari nikalala vibarazani.

    Mwayangu mwayangu!

    ReplyDelete
  2. YAANI HADI ULAYA WANATOA MWALI ? HAYA KWA MTINDO HUU KAZI IPO

    ReplyDelete
  3. sio mchezo, ngoma mpaka ughaibuni!!! ama kweli mwacha mila ni mtumwa, sasa ngoma ya unyago inatangaziwa kina mama tu, leo iweje kila mtu aambiwe!! haya jamani, kina braza men kaeni mkao wa kula, wari hao, mshindwe wenyewe, hadi mdundiko na mchiriku toka bongo wamealikiwa, langu jicho!!lakini nawatakia kila la kheri wari

    ReplyDelete
  4. Safi sana mila na desturi razima zifanyike,I wish ningekuwepo ningekata kiuno na bingibingi kiunoni naamanisha shanga.Halooo mwanamke kuchezwa bibi yaaani kutoka unyago.Nashukuru nilitoka unyago maana sisi wanawake wa uswahilini kita........... baraa mama.Mdau
    Rose Norway

    ReplyDelete
  5. Hama kweli ukishangaa ya musa basi ya firauni yaja.wazaramu kwa ngoma kiboko.mnge chukua hall mjifungie ndani kabisa mcheze ngoma vizuri manake msije mkaitiwa polisi bure kwa kupiga kelele.alafu vikuindi vya ngoma vinatoka bongo au mnatumia kanda? Simchezo hili mtu lazima ulichukulie vacation.UNAJUA hii blog inavituko vya kila haina kila kukicha kutoka kwa manka mushi mpaka kwa wazaramu wa london. He he he he mnastahili pongezi lakini kwa kuendeleza utamaduni na sasa hivi tutasikia sherehe za kutailiwa london.

    ReplyDelete
  6. WHAT???!!!! HII NI JOKE KAKA MICHUZI??!!! SIAMINI KABISAAAAAA!!!

    ReplyDelete
  7. ungejua kama wax zinatengenezwa Holland usingepata taabu ya kuagizia Bongo na vile vile kuna kikundi cha mdundiko kinachoongozwa na mzee Kamogola siku ingine usiangaike kufata Bongo njoo Holland. mambo yote hayo tembele kamogola@gmail.nl

    ReplyDelete
  8. Ngoma hadi UK? kazi ipo

    ReplyDelete
  9. Na lini natakiwa kuja kuchagua mchumba. Ila inabidi waangalie wakiwaweka matiti wazi kama bongo watashitakiwa.

    ReplyDelete
  10. hivyo 'ngoma za binti zao'maana yake nini?

    ReplyDelete
  11. kwa jinsi ninavyofahamu mimi ngoma kama hizo wanaohudhuria ni wanawake tena ambao walishawahi chezwa ngoma kama hizo sasa inakuwaje mwaliko hausemi kuwa ni shughuli ya kina mama na haijuishi wanaume? mmh....

    ReplyDelete
  12. mila zingine kazi kweli kweli....laiti mngejua wanachofundwa hao mabinti

    ReplyDelete
  13. hakuna la maana zaidi wanayofundishwa kwenye hiyo ngoma sana sana kuhusu wanaume,sometimes i hate mila

    ReplyDelete
  14. Wote feki, hakuna mume hapo!

    ReplyDelete
  15. OOOoooH ACHENI HIzooo, HIYO SHUGHURI NI YAKUWATOA NDANI BAADA YA KUKEKETWA? kama hivyo niko njiani nakuja.

    ReplyDelete
  16. jamani huo mdundiko na vanga mtavipigia ktk uwanja gani?maana ni vitu vinavyohitaji nafasi, na hayo makelele yake,kweli mtawapona majirani?au ndio ngoma itabidi tu izimwe?mimi ninawatakia mafanikio mema kwakuendeleza mila na desturi hata ugenini,ingawa nadhani itakua ngumu kutokana na mazingira.Mdau Sevensisters,Tottenham.

    ReplyDelete
  17. Duh!! hii kali, ngoma mpaka mantoni?

    ReplyDelete
  18. wallah siamini,ngoja nichangamkie visa UMOJA HOUSE nikashuhudie mambo ya wazaramo kwa watasha!!!

    ReplyDelete
  19. Huo ni uzaramu pure!!kuleta ngoma ugenini!!kwanini usiende kuowa kijijini kwenu?kama kweli unapenda ngoma na vikorombwezo?acha ujinga wewe.

    ReplyDelete
  20. Hongereni sana maana naona mnaendeleza culture... je na maadili m nawafunza au ni shuguli tu ili tupate shuguli???

    Machui

    ReplyDelete
  21. shughuli hadi ukerewe?

    ReplyDelete
  22. Hayo maneno kwenye hizo Kanga Pekeyake yanatosha Kufikisha Ujumbe kwa Walengwa: HIV i HIV i tu!!
    Naelewa hizi ni TAMADUNI/JADI kwa baadhi ya Makabila Tz,lakini naelekea kufikiri Ngoma(Kumtoa mwali,Mdundiko)huchangia sana Maambukizo ya VVU Tanzania!

    ReplyDelete
  23. TUNAKUITIKIA TUTAKUJA LKN KABLA YA YOTE HUJATUFAFANULIA VIZURI KAMA HIYO NGOMA NI YA HARUSI AU NI UNYAGO HUO? TUTAKUJA BWANA SIO TUPO TUSIOPENDWA KUPITWA. JE NGOMA YA SEGELE IPO NA MATARUPETA?

    ReplyDelete
  24. MZARAMO HAACHI ASILI YAKE! HADI UGHAIBUNI!

    ReplyDelete
  25. MZARAMO HAACHI ASILI YAKE! HADI UGHAIBUNI!

    ANNONIMOUS ULIETANGULIA, HAWA NI WAZARAMO. HII NI NGOMA YA KUMTOA MWALI.

    ReplyDelete
  26. Segere mama eeeeh. Hii ngoma ya kizaramo tuu....mmmh mwe natafuta flight sasa hivi ya kutoka Canada to UK. Pakufikizia ninako ilobaki niende kwenye hiyo sherekhe niwaone kina fatuma wanatolewa nje. Hii sio harusi....sasa hiyo khanga ya Hi HiviHivi ina maana gani?

    ReplyDelete
  27. uswahili wenu mje fanyia kwenu,siyo kuwapigia makelele wasio na hatia!
    gongo na bangi navyo mnavyo vya kutosha au mnataka ngoma isichangamke?

    ReplyDelete
  28. MZARAMO HAACHI ASILI YAKE! HADI UGHAIBUNI!

    ANNONIMOUS ULIETANGULIA, HAWA NI WAZARAMO. HII NI NGOMA YA KUMTOA MWALI.

    ReplyDelete
  29. Nikitaka kucheka, huwa naingia humu kwenye tovuti ya kaka michu, yaana nimecheka hadi machozi yamenitoka. wazaramu wana watani wengi basi hapa inaburudisha mno, aunt NAILA imekaaje hiyo?

    ReplyDelete
  30. Acheni zenu za kitanesco hapa, mbona "bethdei, get tugetha, vipaimara, n.k" vinafanyika kila siku hapa London? Cha ajabu nini sasa? Ongereni bwana na bibi Vilemela kwa kudumisha jadi yenu.

    Unaweza kumtoa mzaramo kutoka katika Uzaramo, Lakini kamwe huwezi kuutoa Uzaramo kutoka katika Mzaramo.

    ReplyDelete
  31. Kuna kufunga madogoli na somo ni nani jamani. Navyojua mimi wapiga ngoma lazima wanye changaa sijui itakuwaje manaake ukiwapa hivi vinywaji vya kigeni. Vilevile mwalike Kikwete na mkewe kwani wao pia ni watu wa pwani. Otherwise hongereni kwa kuendeleza mila hilo ndilo la msingi.

    ReplyDelete
  32. Mpiga dogoli akikata hakawii kumba mama mwenye nyumba ....... Ulaya ataambulia address tu. Na huo mdundiko mtakujajikuta mko mahakamani shauri noise pollution.
    "Dizogolo ndyangu wadiba eheee.....!!!" Jaje....????

    ReplyDelete
  33. HII NGOMA NI DANGANYA TOTO,HAWA MA BINTI WATAKUA WAMEZALIWA BONGO WAMEISHI UK LABDA KAMA MIAKA 10,WENGI WAO WAMESHA CHEZWA NJE(I HOPE YOU KNOW WHAT I MEAN)SASA TENA WANACHEZWA NINI KWENYE HALL WAKATI UHAKIKA SHUGHULI PEVU WANAZIJUA.MAANA WATOTO WAKIBONGO WOTE WALIOLETWA HUKU UINGEREZA HAWASHIKIKI,WANA TABIA KAMA VICHANGU DOA NA KUNA MDAU KASEMA KUCHEZWA KWA WASICHANA WENGI BONGO KUMECHANGIA VVU NAKUBALIANA NA WEWE 200%.
    NAJUA MNADUMISHA UTAMADUNI LAKINI ANGALIENI NCHI YENYEWE NA JINSI WATOTO WETU WALIVYO HARIBIKA HALAFU MUONE KUWACHEZA HUKO KUTAWASAIDIA HAO WATOTO AU KUTAZIDI KUWAHARIBU.NYINYI KINA MAMA HAMSHIKIKI MNA BEHAVE KAMA MA-TEENAGER ITAKUA HAO WATOTO.

    ReplyDelete
  34. UK KUMEKUCHA, MAREKANI NA CANADA MABISHOLOLO WENGI HUWEZI KUPATA MAMBO KAMA HAYA, WAO HATA HUKU WAKIANDIKA NI MAMBO YA YO YO,...UK MASSIVE..FANYENI ASILI YENU NDIO UTAIFA HUO.

    ReplyDelete
  35. ..NITAKUJA CHEZA GOMBE SUGU..

    ReplyDelete
  36. kweli huyu Kalemela anataka kuwa ingiza ktk April 1st, 'Fools'Day'.
    kwa anayeijua London haiwezekani mtu kufanya sherehe siku Nne nzima ikiwemo 'mkesha'.
    Huyu jamaa hajui ASBO(Anti-social Ban Order)itakayomfanya afikishwe kortini kutokana na kukera majirani. Pia wote wahudhuriaji baada ASBO mtafungwa kufuli miguuni yenye 'navigator' ili mfuatiliwe msijefanya 'shughuli' nyingine ya kero kwa jamii. Labda ukoo wa Kalemela muhamie shamba(county)jirani na David Beckham, ambapo utakuwa na hekalu lenu na shamba kubwa kufanya 'mkole' bila bughudha kwa wabeba boxi wachovu baada ya kazi wa katikati ya jiji la London maeneo ya Holborn.
    Mdau
    Guruwe
    Kimanzichana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...