Makamu wa Ris Dk Ali Mohamed Shein na Mama Mwanamwema Shein wakimfariji Mbunge wa Mbeya Vijijini Mh. Richard Nyaulawa ambaye amelazwa katika Hospitali ya Indraprastha Apollo kwa matibabu ya kamsa ya utumbo wakati Dk Shein alipotembelea hospitalini hapo leo kuona huduma mbalimbali zinazotolewa hapo.
Mama Mwanamwema shein akisalimiana na Mama Salma Ansari Mke wa Makamu wa Rais wa India Mohamed Himid Ansari wakati Mama Mwanamwema na Makamu wa rais Dk Ali Mohamed Shein walipoalikwa katika dhifa ya Kitaifa iliyofanyika Ikulu kwa Makamu wa rais wa India.Nyuma ni Dk Ali Mohamed Shein,Makamu wa Rais wa Tanzania na Mohamed Himid Ansari Makamu wa Rais wa India.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ni utaratibu mzuri kwa viongozi wetu kuwatembele wabunge na viongozi na wananchi wawapo katika zira zao ugenini.Marekani au USA ni eneo amablo viongozi wetu uzuru mara kwa mara hapo tunae balozi wetu,Mama mingiro n.k.kwanini hatujamuona hata kiongozi mmoja akimtembelea Gavana wa zazmzni au hata alipokua gavana wa BOT Balali au hii ni agenda ya siri jamaa huyu amefichwa ili asiibue mambo mengi yanayo wahusu viongozi wetu wa JUU.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  2. My goodness this picture just shocked me!! Jamani life is unpredictable. I knew mr nyaulawa years ago when he was healthier/handsome!! Du my insides are running!!!

    Mungu ampe uponyanji wa haraka!!

    ReplyDelete
  3. Mungu akurejeshee afya yako baba wa watu masikini

    ReplyDelete
  4. Oooh My Goodness!!! Am Shocked!!! Mr Nyaulawa use to be my Boss at Business Times those days mama yangu!! Mungu amsaidie apone arudi kwenye hali yaake!! Duh!!
    Get well soon Baba...

    ReplyDelete
  5. Duuuh,kweli kansa ni balaa jamani! Yaani Mh.Nyaulawa nilikutana naye pale mjini Dodoma wakati wa mkutano wa bunge la bajeti la mwaka jana akiwa mwenye afya njema kabisa. Na zaidi ya hapo nilimshuhudia kwenye mtandao kupitia luninga ya Star Tv iliyokuwa ikirusha matangazo ya mkutano mkuu wa CCM,moja kwa moja toka Kizota,Dodoma mwezi Novemba mwaka jana akiomba kura za ujumbe wa NEC kupitia kundi la wazazi,ambako kwa bahati nzuri alishinda.Leo hii ndani ya miezi 3 yuko hivyo?? Mungu akusaidie Mheshimiwa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...