Kaka Michuzi,
Nimeamua kukuandikia unisaidie kuomba radhi kwa wadau wa blog hii. Mwishoni mwa mwaka 2007 nilipokuwa nikitoa taarifa ya ushindi wa timu yetu ya Iringa dhidi ya SPUTANZA. Niliahidi kuwa baada ya ushindi huo wa Iringa, Mwaka huu tutaanza kuzitia adabu timu za mabenki. CRDB wakajilengesha wakaomba mechi na sisi tarehe 16/03/2008 (yaani jana) katika uwanja wao wa chuo cha ustawi wa jamii, sijui walishtuka vipi kama kiama yao imefika? Wakaingia mitini, hivyo hakukuwa na mechi.
Kwa kuwa CRDB wametunyima chance ya kutimiza ahadi yetu (kwa kuamua kuweka mpira kwapani) wadau watusamehe, tutafanya kweli kwa kabenki kengine kokote soon.
Siwalaumu CRDB football team kwani they are listeners na hakika walisikiliza moyo wao wakajua hawaliwezi game.
Tuntufye Abel
Secretary
NBC United
we timu yako hua inachezaga tu na mabenki tuu?? au pia makampuni mengine??
ReplyDeleteKama na inachezaga pia na makmpuni mengine basi omba mechi na vijana wa shirika la ndege la Precision Air,
Wanapiga ball hakuna tena,
nina uhakika baada ya mechi na hao jamaa hutakuja tena hapa bloguni kuleta tambo zako
We jamaa nawe mambo zako siyo kabisa.Jaribu kumba game na sisi watu wa airline uone kilicho mnyima mbuni manyoya.
ReplyDeletetoka lini Arsenal A ikacheza na Arsenal B kisha ikajisifia twacheza siye.
*KISODA*
NBC United tunaomba mechi na nyie. Tutatua Bongo muda si mrefu, tutacheza na timu za Yanga na Simba lakini kama muda utaruhusu tungependa kucheza na timu ndogo kama zenu. wwww.tanzanitefc.com
ReplyDeleteacha uzushi wewe CRDB chama wewe... watu walifiwa ndio maana hawakutokea, ombeni tarehe nyingine
ReplyDelete