Kaka Michuzi,

Nimeamua kukuandikia unisaidie kuomba radhi kwa wadau wa blog hii. Mwishoni mwa mwaka 2007 nilipokuwa nikitoa taarifa ya ushindi wa timu yetu ya Iringa dhidi ya SPUTANZA. Niliahidi kuwa baada ya ushindi huo wa Iringa, Mwaka huu tutaanza kuzitia adabu timu za mabenki. CRDB wakajilengesha wakaomba mechi na sisi tarehe 16/03/2008 (yaani jana) katika uwanja wao wa chuo cha ustawi wa jamii, sijui walishtuka vipi kama kiama yao imefika? Wakaingia mitini, hivyo hakukuwa na mechi.

Kwa kuwa CRDB wametunyima chance ya kutimiza ahadi yetu (kwa kuamua kuweka mpira kwapani) wadau watusamehe, tutafanya kweli kwa kabenki kengine kokote soon.

Siwalaumu CRDB football team kwani they are listeners na hakika walisikiliza moyo wao wakajua hawaliwezi game.

Tuntufye Abel
Secretary
NBC United

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. we timu yako hua inachezaga tu na mabenki tuu?? au pia makampuni mengine??

    Kama na inachezaga pia na makmpuni mengine basi omba mechi na vijana wa shirika la ndege la Precision Air,

    Wanapiga ball hakuna tena,
    nina uhakika baada ya mechi na hao jamaa hutakuja tena hapa bloguni kuleta tambo zako

    ReplyDelete
  2. We jamaa nawe mambo zako siyo kabisa.Jaribu kumba game na sisi watu wa airline uone kilicho mnyima mbuni manyoya.

    toka lini Arsenal A ikacheza na Arsenal B kisha ikajisifia twacheza siye.


    *KISODA*

    ReplyDelete
  3. NBC United tunaomba mechi na nyie. Tutatua Bongo muda si mrefu, tutacheza na timu za Yanga na Simba lakini kama muda utaruhusu tungependa kucheza na timu ndogo kama zenu. wwww.tanzanitefc.com

    ReplyDelete
  4. acha uzushi wewe CRDB chama wewe... watu walifiwa ndio maana hawakutokea, ombeni tarehe nyingine

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...