Hi Bro.Michuzi!

Kwanza kabisa napenda kukushukuru sana tena na tena, kwa kazi nzuri unayo ifanya kutupatia habari mbalimbali kila siku. Pia wale wote wadau wanao kusaidia katika kazi hii, hongereni sana.

Pasaka hii kwa msemo wa zamani ni DOLE tuu...!!!Kama inavyo onekana hapo kwenye picha. Maana nimetembelewa na MTanzania mwenzangu, na kufahamiana kwasasa, baada ya yeye kunitafuta, kupitia mtandao huu yaani blog hii.

Yeye anaishi jirani na hapa Cesena nilipo, kupitia blog yako tumefahamiana nae. Ni furaha ilioje na tunafurahi pamoja Pasaka hii hapa Cesena. Ni jambo ambalo limenifurahisha sana sikutegemea.
Hongera sana Michuzi hii ni kazi nzuri sana unayoifanya. Naamini watu wengi wamefahamiana humu ndani na kujifunza mengi hapa, hongera sanaaaa...!!!!!

Basi narudi kwa Wapendwa na Wakeleketwa wote wa blog hii na WaTanzania wenzangu popote pale mlipo.

Ninawatakieni Heri nyingi kwa sikukuu hii ya Pasaka!

Tusherekee vizuri wote pamoja kwa upendo na amani tele kama kawaida yetu WaTanzania tulivyo na amani ya kumwaga, na iendelee zaidi na zaidi siku zote.

Salamu sana tena sanaaa....!!!!

B.F.CHIBIRITI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. BWANA CHIBIRITI WA ZAMANI SANA HIVI WEWE ULIONDOKA LINI BONGO NA TANZANIA ULIKUWA UNAKAA UPANDE GANI NINGEPENDA SANA KUJUA DU VIZURI SANA KUSHEREKEA NA MWENZIO MBONGO HAPO NIMEKUSIFU

    ReplyDelete
  2. Hi Bro Michu,
    Hey wewe Chibiriti naona siku hizi umekuwa mzee wa "kilajI" hilo banda lako la Mtwara utalimalizia kweli kwa mtido huu.....!!!.Na hao wazee uwaangalie vizuri,walivyokukalia hapo nyuma,wanakupiga busu la kichogoni inaonekana hawana nia nzuri na wewe,wasije wakawa ndiyo wanaprovide hivyo vinywaji kumbe wana mahesabu yao,Wazee kama hawa wa Ki-Italiano ni balaa Bro Chibe..!!!!!.
    Good Lucky,
    Baba Richard,
    USA.

    ReplyDelete
  3. Buona Pasqua a te e l'altro nostro fratello.
    Veneto.IT.

    ReplyDelete
  4. wabeba box wangapi wanapata fursa ya kunywa mvinyo na wananchi kama Bw. Chibiriti?

    Do your thing bro!

    ReplyDelete
  5. ha ha ha ha

    ReplyDelete
  6. mimi nikumuona chiribiti huwa nina furahi sana, ana confidence kama si mchezo yaani. kama mdau alivyosema the other day, inabidi chiribiti awekwe kwenye list ya Bongo Celebrities, watu wengi sana wanampenda. Hongera sana bwana chiribiti, na tunashukuru sana kwa salamu zako, ingawa pasaka yenyewe bado. Vipi mamaa hajambo?

    ReplyDelete
  7. Ushauri wa bure... kuna msemo wa wahenga unaosema 'NGOMA IKIVUMA SANA HATIMAE HUPASUKA'. Chibiriti itabidi umtafsirie kibibi naye apate ujumbe!!
    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  8. HUKO MTWARA WASAHAU WEWE KURUDI TENA SIDHANI YAANI UMENOGEWA KABISA UNACHELEKEA SASA TUNATAHISTORIA YAKO YA MAISHA KWA KIFUPI HUYU DEMU ULIMPATA WAPI NA ULIFIKAJE ITALI KWANINI SIO SWEDEN AU KENYA STATES AU ENGLAND WHY TUNATAKA MAJIBU BWANA CHIBIRITI

    ReplyDelete
  9. We no.3. wacha matusi yako ya kitaliano! PUS PAKA NYAU!

    ReplyDelete
  10. HUYO NDIO KAKA CHIBI /PASAKA NJEMA NA WEWE

    ReplyDelete
  11. Yaani Chibiriti kuoa ajuza basi company yako yote wazeeeeee....? Maana hapo naona wewe tu na huyo mbongo alikutembelea ndo vijana, hao wengine kama bongo unaamsha shikamoo....

    ReplyDelete
  12. Thumbs up chibiliti, hutishiki na vinywa vya watu wewe ndiyo mwanamme unaonyesha unayempenda bil kuficha na kupigana na Ukimwi. We waacha hawa wanaomsema mpenzi wako.Waulize waonyeshe wao tuwaone na wengine hata kuonyesha wanawake zao hawawezi kwa kukusoa confidence, wanafikiria mara mbili mbili. Be proud that u have someone u luv and to show off with, with out any obstacles. Dunia hii tunaishi mara moja tu maana wengine wanafikiria watarudi tena. Enjoy Man!!!!

    ReplyDelete
  13. Yaani Chibiriti nikiona jina lako tuu huwa nacheka sana , ila mbona huyo jamaa anakukiss kichwa halafu huyo jamaa mwingine anamkiss mwanaume mwenzake ? ...Chibiriti inaonekana kama mko San Fransico .

    ReplyDelete
  14. Chibiriti wewe ni kiboko....ukirudi Bongo kugombea ubunge nitajiandikisha kwenye hilo jimbo utakalogombea nikupe kura yangu!! Damn......una msimamo sio mchezo....keep it up!!

    ReplyDelete
  15. Huyo ndiyo Chibiliti senior care worker bila yeye nyumba haiendi kama inavyotakiwa vibibi na vibabu siku hiyo haviogi wala hakuna evening walking. Chibiliti habebi box yeye ni mlezi wa wale wazee wa town yake pale

    ReplyDelete
  16. Chibiriti Oyeeeeeeeeeee Chibiriti juuuuuu! Eee bwana watu wangu mimi namkubali sana Chibiriti huwa akibip tuu kwenye hii blog najikuta nacheka mwenyewe. Chibiriti bwana! ana confidence ya ajabu sana, keep it up man.

    ReplyDelete
  17. Bro. Chibby, you have no idea jinsi gani unatusuuza na roho zetu. Watu wengi tukiona tu post toka kwako tunafurahi kabla hata hatujasoma. Keep posting. Najua kila mtu ana purpose hapa duniani labda ya kwako ni kutufanya tutabasamu baada ya kubeba box za kutosha. HAPPY EASTER TO YOU TOO AND OTHER WADAUS.

    ReplyDelete
  18. SAME TO YOU KAKA CHIBIRITI, NILIJUA TU UTALONGA MAANA WEWE HUPITWI SALAMU NYINGI KWA SHEM WETU WAKITHUNGU BASI.

    ReplyDelete
  19. Pasaka njema chibiriti!!!

    ReplyDelete
  20. Pasaka njema na wewe bwana Chibiriti,ama wewe ni sugu la nguvu, watu wamekupigia kelele weee, lakini msimamo wako hauyumbi anyway mimi nafurahi sana kuona jinsi gani unavyo furahia maisha yako huko, naona waosha vinywa wameamua kukuacha umewapiga bao la kisigino, hahahahaha poa sana

    ReplyDelete
  21. tumefurahi chibiliti kwamba angalau umepata mtanzania mwenzio kuweni pamoja,kushirikiana na kubadilisha mawazo ktk kuleta maendeleo ya taifaUMOJA NI NGUVU.

    ReplyDelete
  22. We anonymous No.9 Mar 20.9:15EAT.Na kwako pia! Eti matusi ya kitaliano!Uanaongea nini?Kama nilichomwandikia Chibi lilikuwa tusi basi nadhani yeye angekuwa wa kwanza kujibu na si wewe usieelewa wala nini kilichoandikwa,hasa ukizingatia sikuwa nimekutakia we Buona pasqua,sio wote wanaongea ovyo na matusi kama wewe. Pilipili ziko shamba....!

    ReplyDelete
  23. Chibiriti bro angalia usirudi home mikono mitupu kwa ajili ya mashangingi wa kiburuda!!nyumbani wanakuhitaji...

    ReplyDelete
  24. mashemeji au? mmependeza sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...