JK na Rais wa Senegal Abdulaye Wade katika majadiliano.
jk akijadilaiana na Rais wa Sauzi Mh. Thabo Mbeki na na Rais wa Ghana Mhe. John Kufuor wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika na India leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Good JK.Viongozi wa Africa(wa sasa) kwa kweli wanaboa kitu kimoja-"kung'ang'ania"(sina uhakika na spelling) madaraka.Wako wapi akina Nyerere,Mandela,Nkrumah n.k.Mijitu imezeeka,haipendwi lakini bado tu inawapelekesha wananchi.

    ReplyDelete
  2. acheni kuchenguka wananchi wenzangu tv moja leo india imeonyesha mawaziri kumi na nne wa india hivi waligomea huo mkutano kwani wanadai haukustairi ulikua na mapungufu makubwa kwani ni wanahisi huwenda ni propaganda ya biashara binafsi kati ya waziri mkuu wa india na hao marais wa africa haya kazi kwenu walalahoi wa africa tunazidi kudanganyika ny wahenga wanasema wanakula kwa urefu wa kamba yao

    ReplyDelete
  3. Nyerere amekaa madarakani zaidi ya miaka 20. Sasa unaposema hakung'ang'ania madaraka hapo nakushangaa sana.

    ReplyDelete
  4. Mzee Msafiri,je ulitembelea Taj Mahal au Bollywood!!!hizo ndizo vivutio kabambe,usirudi bila shopping rahisi...

    ReplyDelete
  5. hata hao mawaziri wakigoma sisi inatuhusu nini,sisi sida yetu wawekezaji,mradi tu mikataba ile makini kwenye kusainiwa,ctually huo uwekezaji ni wakilimo,so wanaingia mikataba na wakuliwa,wawasaidie kitechnologia,now india ni moja ya nchi inayokuja juu sana kwa technology,wao na china ni kwamba tu population ni kubwa mno other wise wangekuwa mbali.kwenye first world country.brazo jk,uwekezaji ndo uloziinua nchi kama dubai na malaysia na thailand,tena wao hawana dhahabu wala tanzanite,muhimu ni ziwanda ili zitoe ajira kwa wananchi.ndo uchumi utakuwa,kenya wanafanya vizuri kutokana na viwanda,tz tuna soko kubwa,tukiwekeza kwenye viwanda tutafika mbali.

    ReplyDelete
  6. Namuunga mkono anonymous 7.29pm...mimi nadhani Nyerere hata aliko anasikitika, kwani anasingiziwa mambo mengi...kwasababu kama siyo sera yake ya ujamaa na kujitegemea kupoteza mwelekeo na hivyo kuogopa joto la vyama vingi, hiyo miaka 20 aliyokaa madarakani ingeongezeka na angeendelea kutawala kuliko hata Mugabe.
    Tuliimba nyimbo za mchaka mchaka za kuwatokomeza watu wengine wenye busara zao kama akina Kambona, wewe unafikiri ilikuwa kheri ile!!! Nakumbuka nikiwa na miaka 7 naimba kuwa kambona ameolewa ulaya...wimbo wa mchaka mchaka huo....nikamuuliza mama yangu hivi Kambona ni mdada..ilimpa shida sana mama yangu kunielezea kwani picha ya Kambona tulikuwa nayo nyumbani...hivyo alitumia busara kunielezea na mwishoni kwa ubishi wangu tuliishia kwenye maamuzi ambayo wazungu wanasema "let's agree to disagree". Hiyo haikuwa kheri ndugu zangu.
    Kama unataka kujua ukweli, tembelea maktaba za nje au Vituo vyenye vitengo vya "African Studies", tafuta vitabu vya akina Profesor Babu na Kambona na wengineo...hivyo vitabu vinahusu siasa ya Tanzania na sera za ujamaa na kujitegemea, ukivisoma na ukaelezwa hivi vitabu hata leo Tanzania huwezi kuvikuta maktaba..utagundua kwanini Profesor Babu na Kambona walikimbia nchi.....Nakuapia Tanzania hizi shida zote za uchumi tulizo nazo wala msiwalaumu wanaoongoza sasa hivi (sijasemea ufisadi), kama sera zile zingefuatwa tungekuwa mbali sana. Nakueleza hata Kikwete angevichukua na kuanza kuvisoma sasa hivi, kuna machache anaweza kubadili, ijapokuwa vitabu vyenyewe ni vya 60's...hivyo pamoja na sifa tunazo mpa mwalimu nadhani sera zake nyingine ndizo zimetufanye tuwe tulipo leo.
    Nakwambia tungekoma, tungekuwa kama Cuba, watu wanashangaa just mwezi uliopita ndipo wameruhusiwa kuwa na TV, DVD na Computer.
    Tumushukuru Ruksa wakati mwingine.
    Kwa kifupi Nyerere alikuwa na mema yake, kama Mwinyi alivyokuwa na Mkapa alivyokuwa na vilevile wote wanamapungufu yao kama binadamu wengine...ila Mkapa na Mwinyi muda wa Miaka 10 haukuwa mzuri kufanya mengi mema kama Mwalimu aliyekaa miaka zaidi ya 20 madarakani.

    ReplyDelete
  7. Hapo agenda kuu ni MUGABE...najua ndiye watakuwa wanamuongelea hapo kwenye picha!! kwamba sasa itakuwaje jamani?? tufanyeje kuficha hii aibu??

    ReplyDelete
  8. Mbeki: Washkaji,mie nakiri kuwa nimeshindwa kuwapatanisha ndugu zangu Bob na hasimu wake,nifanyeje? nisaidieni
    Kufour: Usikonde, hiyo wala siyo inshu mie mwenyewe nilibwaga manyanga kwa Kibaki na Odinga, after all tuna mambo kibao ya kushughulikia home
    JK: Kudadadeki, hiyo mbona kama kumsukuma mlevi tu, si mliona wenyewe nilivyowachimba biti Nairobi mpaka wakatia saini, usifanye mchezo na mimi,hata kule Zanzibar wananijua
    Wote:hahahahahahahahahahahahah

    ReplyDelete
  9. michuzi hebu mpe huyo mbeki au bekisalamu zangu,raisi gani huyo wa ki sauzi?wakati walpokuwa na shida wamesaidiwa na raia wengi wa kizimbabwe heti sasa yuko na mugabe NO CRISIS???!!!!we mtu achoma nyumba za raia wake na kuwafanya wakimbie nchi no crisiss,mtaniwia radhi lugha lakini hawa viongozi wetu wa africa wanajijali wao tu na sio raia wao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...