kichwa kinachosadikiwa kukutwa na mtuhimiwa aliye chini ya ulinzi hapo chini


Kijana kama wa miaka 9 hadi 11, handsome, amekamatwa geti la kuingilia chuoni Muhimbili (leo asubuhi kama saa 2 asubuhi) akikatisha kuelekea Muhimbili Hospitali mkononi akiwa na kifurushi.

Kama kawaida, askari wa Muhimbili chuo alitaka kujua anaenda wapi na kashika nini?Yeye alisema anampelekea zawadi shangazi yake aliyeko wodi ya IPPM (sijui ni nesi au ni mgonjwa).


Askari akataka kujua zaidi kulikoni kabeba nini ndani ya mfuko wake, ndipo kijana (tumwite mtoto) huyu akatoa kichwa hicho hapo chini na kuanza kukitafuna live mbele ya askari.

Bahati mbaya walishikwa na butwaa na baadhi ya watu waliokuwepo hawakufikiria hata kupiga picha zaidi ya kushangaa kwa dakika kadhaa ndipo wakamshika.

Kichwa hicho ni cha binti kama wa miaka miwili na nusu hadi mitatu, kiko fresh kabisa (picha ya kichwa tume-itibu sababu yote iko too graphic). Ni mtoto mzuri sana na alikuwa amesukwa nywele, kwa bahati mbaya nilishindwa kuhakiki kama simu yangu ilichukua picha vizuri maana kulikuwa na msongamano mkubwa wa watu na ilikuwa ngumu kupata picha nzuri.

Bwana mdogo alipigwa kidogo na akaanza kung’aka kwa nini wanamshika yeye wakati watu kibao tu wanakula watu. Akasema wamegawana mtoto huyo na wenzake wawili ambao walimwacha na kupanda ungo, ila yeye akaona akampelekee shangazi yake kazawadi.

Picha za chini hapa utakuta kuna damu midomoni mwa dogo huyu ambaye aliendelea kujilamba na kutafuta kumalizia vile alivyokuwa navyo mdomoni

Mpaka naandika hizi habari, polisi wa Selander bridge wamemchukua dogo huyu na kumpeleka kituoni pamoja na mlo wake (inasikitisha sana). Kuna umati mkubwa wa watu wakishangaa kilichotokea.

Huwezi amini kwamba kijana mzuri kama huyu ataweza akawa ameingizwa kwenye ushirikina. Hapo anajilambalamba masalia.


Haki ya Mungu huwezi amini kwamba alikuwa akiongea kama ana haki kabisa ya kula kale kabinti ka watu. Ana jeuri ya kichawi.Kwa wale wanaodhani kwamba ni kichaa, wajue bwana mdogo alikuwa fully conscious, na pia oriented to time, place and person.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Mambo mengine bora uwe unahisi tu..... lakini inapofikia hatua ya kuona live kama hivi.... inanifanya niogope na kujiuliza mangapi yanaendelea......
    Inaonekana Tanzania TUNA AMANI ya JUU JUU tu.. lakini yanayoendelea chini kwa chini... KAMA UCHAWI, nk ni mengi na ya kutisha...
    Inatisha!!

    Mdau, London

    ReplyDelete
  2. Mmh michuzi.Umeshuhudia kwa macho yako au ni tarehe ya wajinga nyingine.Habari mbaya sana,fuatilia sana huyo mtoto huko polisi hicho kichwa alikitoa wapi?

    ReplyDelete
  3. ni habari ya kusikitisha sana huwezi amini kama inatokea bongo huyo mtu kwa vyovyote atakuwa ana wazimu, wadau tuwalinde watoto zetu kwa karibu sana maana watu kama hawa tunaishi nao humuhumu mtaani. tujuze habari zaidi bwana michuzi

    ReplyDelete
  4. Of course kama nchi yote inaliwa na Balali, Lowasa, Sumaye, Kikwete, Chenge na Mkapa; sisi tule nini? inabidi tulane wenyewe kwa wenyewe

    ReplyDelete
  5. Mbona Story na picha zimekaa kisanii?Aliyelala ni nani?mbona anaonekana kama mtu mzima na sio kijana wa miaka 9 au 10?
    Kichwa hapo chini ni cha yule mtoto wa kike au huyo kijana?
    Maelezo na picha haviendani jaribu kuelezea kwa uzuri na uwazi.
    Ngurubange

    ReplyDelete
  6. Jamani dunia imeisha. jamani hembu fatillien hii stori zaidi. labda huyo shangazi yake ndio kamtuma huyo kijana. na huyo binti wa watu mdogo ni wa nani? Jamani Mungu Baba yetu wa mbinguni unayaona hayo

    ReplyDelete
  7. nimeshikwa na butwaa hata sijui ni comment nini,

    hivi tunaelekea wapi jamani?, huu si ubinadamu kabisa, kuna mambo mengine inakuwa vigumu kuamini ati,

    mungu tusaidie, tunakuhitaji sasa kuliko tulivyokuhitaji awali,

    ReplyDelete
  8. Meu Deus! Vampire live! Hii ni kali. Lakini ndivyo ilivyo kwenye ulimwengu ambao watu fulani wanauita Ulimwengu wa Giza! Watoto wengi wanaopotea katika mazingira ya kutatanisha huwa wanaliwa na wachawi-vampire wa jinsi hii.

    Lakini naomba tu ufuatilie suala hili ili uendelee kutufahamisha kinachoendelea. Naaamini uzuri wa kisa ni ujuwe mwanzo, ujue kinavyoendelea na hatimaye ujuwe mwisho wake. Matukio mengi TZ yanatokea lakini likiashaanikwa mwanzoni tu huwezi juwa tena liliendeleaje.

    Natumaini watakuwa walimpata shangazi wa vampire huyo!

    ReplyDelete
  9. NIMEPAGAWA NASHINDWA KUSEMA WETHER NI ZILE TABIA ZA KITAPELI KAMA YULE MTOTO MWINGINE AU NI KICHAA SIDHANI KAMA MZIMA BAHATI MBAYA MIMI SIAMINI

    ReplyDelete
  10. Inalilah Waina Ilahi Rajiun! jamani tusomeshe watoto zetu dini na elimu ya dunia, sio ushirikina na tabia mbovu inasikitisha watu wazima kuwafundisha watoto kama hao jamani tena anasema anampelekea bibi? police kweli wanamafunzo atakuwa kaona au anajuwa kuna watu wapo kama hao.

    ReplyDelete
  11. Michu,
    This photo is very disturbing. Please remove it.

    Mdau

    ReplyDelete
  12. JMANI KUNA HAJA YA KUWA NA SALA MAALUM DUNIA IMEKWISHA SASA DUH!!

    ReplyDelete
  13. Jamani ni ushirikina au ukichaa huo?sasa huyo mtoto ni wa nani?mungu wangu...michuzi hii ni kweli au sinema za kinageria?mie siamini kabisa kama imetokea tanzania
    mdau anayelia

    ReplyDelete
  14. Polisi hawawezi pata solution ya issue hii. Nashahuri labda wamshirikishe yule mgambo wa getini aliyemkamata yule dogo. Kwakuwa inaonyesha lazima yule mgambo anaohujuzi na mambo yale....ktk hali ya kawahida kama huna ujuzi wa mambo ya ushirikina ungeweza mwachia yule dogo ukijuwa ni mwema na anaenda kutembelea wagonjwa kama wengine.

    ReplyDelete
  15. Astaqhfir lah wallah tumezoea kuona ama kusikia kwenye news media disturbing news kama hizi inasikitisha kusikia hii imetokea kwetu,nijuzi niliona kwenye discorvery chanel jamaa marekani alikua anachukua wanaume wenzie kwake anawaua kisha anarep maiti for two days alafu anakatakata parts za mwili ana sevu kwenye freza anakula,hata alipokamatwa walihisini mgonjwa wa akili lakini test zikaonyesha ni mzima..leo naona nchini kwangu ..ewemungu zilinde familia zetu(amin)

    ReplyDelete
  16. Muhimbili kuna vimbwanga wa kutembelewa na wachawi kila siku tena hasa wodi za watoto, masikini jamani sijui alikuwa binti ya nani huyo kapotea wazazi wake wamemtafuta wee kumbe kaliwa nyama. Hapo Dar kuna kundi kazi kuiba watu wazima na watoto pia, kuna kaka mmoja alisalimiwa na mtu kama anayemfahamu vile akampa mkono (nyie mnaopenda kutoa toa mikono hovyo mjifunze) basi yule kaka naye akampa huyo mtu mkono basi fahamu zikamruka, kaka wa watu kutoka Ubungo karibu na Trafiki light akajikuta yuko Chang'ombe nyuma ya maduka mawili lakini hakujua yuko wapi kwa kipindi hicho. Alipozinduka akaanza kusoma aya za Quran, kama ayat kursiy na sura nyingine alizoweza kukumbuka, fahamu zikamrudia akaona kwenye hicho chumba alichopo kuna watu wengi wamekaa watu wazima na watoto pia. Akatoka nje kama anaenda msalani akaona mlango wa uwani akatoroka. Basi kilichotokea hapo watu walikuwa wanamuona kama kichaa, maana wale watu waliomchukua walikuwa wanamfuata, sasa anapiga kelele jamani nisaidieni wananifuata, watu wanamuona yeye ndio chizi mpaka akaingia ndani ya basi mwisho wanamfuata bado akawa anapiga kelele, akashuka akaingia ndani ya taxi na kumuamuru dereva taxi ampeleke kwa jamaa zake! Lakini humo ndani ya taxi anawaona bado wanamfuata, cha ajabu ni yeye tu peke yake alikuwa anawaona wengine hawawaoni wanamshangaa anavyopiga kelele. Ndio akafika kwa jamaa zake, wakamsadia kwa dua na maombi zaidi.

    Huyo mlinzi lazima ama atakuwa mcha mungu sana ama atakuwa na yeye fundi lakini si mchawi maana angekuwa mchawi asingemuumbua huyo mchawi. Na kisha huyo mwamuona kijana mdomo wa miaka 11 pengine ni babu wa miaka 80 au kijana wa miaka 30, kajibadilisha.

    Cha msingi ndugu zanguni ni kufanya ibada sana. Kabla hujatoka nje ya nyumba yako fanya ibada na umuombe Mungu akukinge na mabalaa yaliyopo duniani. Kama ni mwislamu hakikisha unakuwa na udhu kabla hujatoka nje ya nyumba yako na kama unaweza muda wote mwili wako uwe na udhu. Na kuomba na kufanya nyiradi muda wote na pia kuwafundisha watoto wetu sala na dua.

    Shetani anatembea siku hizi mchana hadharani!

    ReplyDelete
  17. michuzi hii umeona wewe au kuna mtu kakuletea ujumbe huu. naona utufahamishe hilo plz.

    ReplyDelete
  18. KAMA SI KUMUUA HUYU UNADHANI ANASTAHILI HAKI IPI YA BINADAMU!

    HUKO POLISI ATAPOTEA NA ATAENDA KWAO MUTABAKI NA COPY: well huenda hata mukamua copy or kumfunga copy yake!

    Hii ni style mbaya ya ufisadi!

    G7
    UK

    ReplyDelete
  19. jamani dunia imekwisha kijana mdogo kama huyu anaanza mambo yasiyokuwa na msingi kama hayo ni muda gani anakuwepo shule ni kijana mdogo sana anatakiwa asome awe taifa la kesho leo anakula watu liko wapi taifa la kesho polisi wasimuachie awataje na wenzie washikishe adabu waende shule sio mambo mengine

    ReplyDelete
  20. Yaaaaaaaaaaaaaarabi mola tustiri sie waja wako. Jamani ulimwenguni kunani hivi. Mbona mambo ya ajabu yanatokea? Kaeni makini na kujua kwamba mungu ndo aja sasa watu wamefanya mengi ya ufuska. Kaka Michuzi hii story ni kiboko na inatisha. Sasa hao ni wanga kma wanapaa na ungo lkn duh balah si dogo. Mwenyezi Mungu Ataenda Kumuhukumu kesho akhera.

    ReplyDelete
  21. Iko haja ya jeshi la polisi kuweka kitengo cha askari wenye ujuzi wa mambo ya Giza maana issue hii haitakuwa na solution . Na huyo kijana huko Segerea ataishi kwa raha maana hakuna askari jela wala mbabe atakaemgusa kwa kuogopa kuliwa.

    ReplyDelete
  22. Mh! nahisi ntaota usiku sasa!

    Mdau- Amsterdam!

    ReplyDelete
  23. Asiwadanganye mtu....uchawi hupo duniani, I have seen it with my own eyes. Miaka ya nyuma mimi mwenyewe nilikuwa siamini kitu kama hiki kipo duniani japo nilikuwa nahisi lakini yalinikuta. Niliumwa sama ,iaka hiyo mpaka watu wakawa wanaongea mambo ya ngoma juu yangu lakini nilijijua kuwa sina baada ya kupima Muhimbili na sehemu zingine (Hindu mandal) mara kadhaa. Baada ya kukosa jibu sahihi toka hospitali zetu ilibidi nikimbizwe na wazazi wangu nyumbani Iringa (Mufindi). Kule yaliyonisibu ni ajabu hata kuandika hapa siyawezi....nikatibiwa na sasa nadunda kinoma. Cha kushangaza nilipokuwa pale nilionana na mawaziri wawili wa Mkapa pale na wote tulikuwa tunalala chumba kimoja kwa yule mganga. Amini usiamini, uchawi (juju) upooooooo!

    ReplyDelete
  24. jamani wadau imetokea kweli,wameonyesha picha ya kichwa cha mtoto kilicholiwa na kiwiliwili kwenye luninga zetu za bongo,inasikitisha sana.wengine tumelia kuona huo ukatili.

    ReplyDelete
  25. Namkumbuka kijana huyuhuyu alishatokea katika mazingira ya kutatanisha wakati maombi ya waumini wa kanisa walipokuwa wakiomba kwa ajili ya wachawi. Jana mch/mhe. Getruder Rwakatale alisisitiza na kukumbusha kuwa madaktari walipinga na kusema wale vijana waliotokea porini walikuwa wanatabia ya uwongo na kutoroka nyumbani kwa siku na kurudi sasa Mungu alitaka kumdhihirisha huyohuyo kijana waliyesema ni mzima na timamu alirudi tena na kidhibiti cha kuchwa cha mtoto wa binaadamu, sijui watatuambiaje kupindisha usemi ule wa yule doctor aliyeonyeshwa kwenye luninga siku za nyuma kidogo.

    Wadau mliombali hii kitu ni sahihi/kweli wameonyesha kwenye station zote za Tv huku bongo,na kijana alikuwa analia kwa mayowe na uchungu akisema wamemnyang'anya nyama yake.Inasikitisha kuona kichwa cha binti mdogo wa miaka mitatu asiye na hatia ameuwawa vibaya vile. Tunashukuru walitoa onyo la picha watakazoonyesha kuwa mbaya wakati wa taarifa ya habari, nilifanikiwa kumziba macho toto wangu mmoja mdogo na mwengine alikuwa mbali aliona alishindwa kulala chumbani kwake alikuja usiku chumbani akasema naogopa vampire.

    ReplyDelete
  26. michuzi umekosea ulivyoandika kijana handome...huyu ni shetani,hatakiwi kusifiwa kwa aina yoyote,he is not worth it,complimenting him its like shaking hands with the devil..thats just my opinion...mdau,uk.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...