Bro Michuzi,

Habari za masiku na pole na kazi. Naomba unipatie msaada kwenye tutazz kwenye blog yako natafuta ajira huwezi jua bwana labda naweza kubahatisha manaake nimezunguka hapa na pale lakini sijafanikiwa bado.

Naomba uweke ujumbe huu hapa chini, pamoja na picha niliyoattach.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kaka Michuzi, na Mungu akubariki kwa kazi nzuri unayofanya kutuhabarisha wadau.

Wasalaam,
Forgive.


---- mwanzo wa ujumbe -----

Je unahitaji mtu wa kupokea na kuchangamsha wateja wako? Naitwa Forgive Assenga, nina miaka 22 na elimu ya kidato cha nne, na ujuzi wa kutumia computer. Kabla hamjanishambulia kwa elimu yangu ndogo si mapenzi yangu bali ni mapenzi ya Mungu baada ya baba yangu kufariki nami nikashindwa kuendelea zaidi. Hata hivyo nina maono ya kujielimisha zaidi, sema kwa maisha ya sasa ni muhimu kufanya work-study la sivyo mambo hayaendi.

Uwezo wangu mkubwa ni kuongea na watu. Huwa siishiwi maneno na mtu yeyote akiwa nami hawezi kuboreka. Naamini naweza kumudu nafasi yoyote inayohitaji uwezo wa kuongea kama vile kutafuta wateja (sales/marketing), au kupokea wateja (receptionist). Ukinipa maelekezo ya kutosha kuhusu kampuni au biashara yako, na kazi husika naweza kuifanya kwa ufanisi tu. Kikubwa ni usichoke kunielekekeza katika miezi mitatu ya kwanza. Baada ya hapo nitakuwa fiti.

Vile vile kwa watu wanaohitaji models wa kuweka kwenye matangazo ya picha sura yangu naamini ina mvuto wa kutosha kuvutia wateja. Hivyo kama unahitaji sura yenye mvuto uweke kwenye tangazo lako tuwasiliane pia.

Asante kwa kusoma maelezo haya. Kwa maelezo zaidi tuwasiliane:

E-mail:
forgive.assenga@gmail.com
Simu: 0713 620 274

Asante na Mungu akubariki,
- Forgive

------ mwisho wa ujumbe ------

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 70 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2008

    Binti nakutakia kila la heri, ni jambo la busara kutafuta kazi na hasa kutumia kipaji ambaco unahisi unacho. Jamani wenye kazi msaidieni huyu binti.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2008

    madada wa kichagga kiboko !
    jk

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2008

    Kwa hakika umejaliwa sura ya mvuto, hongera! Wewe ni shujaa na inaonekana unajua nini kinakufaa ktk maisha. Hongera. Unapatikana wapi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2008

    Ujumbe kwa kaka michuzi hivi unategemea mtu kweli mwenye akili yake timamu akatuma huu ujumbe haya bwana ila mimi sidhani itakuwa walewale wazushi

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2008

    UNCLE MICHUZI, WANAKUINGIZA MJINI KIRAHISI MTOTO WA TOWN. HUYU ALIYEWEKA PICHA HAPA NI FEKI WALA SI MWENYE PICHA. NINA SABABU NYINGI TU. KAMA UNABISHA, NINA SABABU YA KUAMINI KUWA UMEWEKA PICHA HAPA MWENYEWE ILI UONE WAJINGA WANAVYOJIELEZA. HILI TANGAZO LIMEWEKWA NA MTU WA ZAIDI YA FORM 4. TENA ALISHAKAA NJE. KUNA USHAHIDI ANAVYOJIELEZA KWENYE MSTARI MMOJA HAPO JUU.

    POLENI MTAKAOPATIKANA. ISITOSHE MICHUZI ULIAHIDI HUTAPOKEA TENA PICHA. IMEKUWAJE UIWEKE HAPA. MICHUZI NAGUNDUA KAZI YAKO SASA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2008

    Nenda kijijini kwenu kashike jembe ulime wewe. Wacha kuomba kazi zisizo na msingi. Mjini shida. Kafungue mashamba uko kwenu uchagani, linma mchicha, fuga kuku na uuze maisha yatakwenda. Unachotafuta utaishia kwenye ngoma nakwambia na baada uanze kulia bure.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2008

    uskate tama mungu atakusaidia upate kazi mama eeh.jikaze

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2008

    Kaka Michu, kaka Michu- lengo ni jema kabisa ila jua ya kwamba umewachokoza waosha, ngoja uone comment zitakazofuata, mama yangu!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 07, 2008

    Hivi siku hizi wanawake wazuri wana nuksi au ni nini? Zamani msichana mzuri kama huyu unakuta tayari kapata mume mzuri tajiri kamuoa kamuweka ndani na anamtunza vizuri mno hata kama hajasoma wala hajui kusoma wala kuandika.

    Siku hizi wasichana wazuri kama huyu wanaume hamtaki kuwaoa kwa nini? au mnaogopa gharama? au ni ubahili wenu? hadi kusababisha mtu ahangaike kutafuta kazi namna hii?

    Wasichana wengi wazuri wa sura siku hizi hawana soko kwa wanaume waoaji sijui kwa nini? Wanaishia kuchezewa tu na kuzalishwa tu.Lakini kuolewa hakuna.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 07, 2008

    POLE SANA 4GIVE, NIMEPENDA UNAVYOJUA KUJIELEZA, NI BORA KUTAFUTA KAZI KULIKO KUJIUZA, NAKUSHAURI UJARIBU NAMBA HII KUNAWATU WANATAFUTWA KAMA SALES OFFICERS.0786402852. AU TUMA EMAIL emcdsm@yahoo.com. ALL THE BEST DADA!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 07, 2008

    NINGEPENDA NIKUSAIDIE LAKINI BAHATI MBAYA ULIKWISHA JITAZAMA KWENYE KIOO UKAONA KUWA SURA YAKO INA MVUTO, HIVYO NINAHISI KUTAKUWA NA MATATIZO BAADAE. POLE.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 07, 2008

    Michuzi una uhakika gani kwamba hiyo picha imetumwa na huyu dada???? Labda kuna mtu tu anataka KUMCHAFUA TU.Nakumba hapo nyuma ulisema kwamba huta post picha kama hizi.Ila kama ni yeye ndie aliyetuma hiyo picha Kila la kheri kwani ni full package.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 07, 2008

    Mimi nataka Secretary, lakini wewe hapana maana ni majaribu, umezidi urembo mama, kazi hazitakuwa zinaenda. Duh Mchagga mzuri kama nini! Bwana nimeandika kama Misupu utaibana shauri yako, kweli nahitaji mtu, lakini dada huyu, tehetehetehe

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 07, 2008

    Safi sana dada..keep up..maana biashara ni matangazo. By the way unaweza kuwa unasoma matangazo ya kazi kwenye magazetiya Dar yale maalum kwa ajili ya matangazo....Utafanikiwa why not!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 07, 2008

    Dadaangu Nakutakia kila la kheri na Pole na maisha, Najua ni vingapi ushapitia mpaka umeamua Kufanya jambo hili ambalo pengine likawa ni la maendeleo kwako..
    Yani Sina comment zaidi ya kukutakia kheri na fanaka kwenye maisha.. umejielezea vya kutosha na kweli unajua kujitangaza sijui ukiitangaza biashara itakuwaje..
    All the best Dadaa..
    Big Up kwa sana..
    NB: Tahadhari kwa wenye kupenda na tabia ya kurubuni watu kwa matatizo waliyonayo.. Wapo wengi wanaoweza kuoffer kazi kwa nia mbaya.. Stick to what u r goals r, dont turn back na kudhalilishwa kwa lolote hata kama iweje.. Fanya kitu moyo wako uko tayari na Muogope Mungu.

    narudia tena KILA LA KHERI.

    Maisha Bora kwa Watanzania Wote.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 07, 2008

    yangu macho dada,mawazo yako mazuri sana ila wadau watakuelewa

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 07, 2008

    forgive Assenga, teh!
    She looks like America Ferrera in the Ugly Bety series!.
    I am worried she must be talking and acting the same way!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 07, 2008

    kaka mishuzi sisi wadau humu kama kumpa mtu kazi basi ni wachache sana ila kama anataka kujulikana tu basi tutamjua na watu watapaka si unajua za wajomba zako kaka,ila huko kuongea kwake kusiwe sababu maana unaweza kuongea pumba muda wote na watu wakakkimbia so awe makini na sura sio kigezo siku hizi ni elimu ila ndio hivyo tena,poa sema sori analipa naona nitafungua massage pala soon na atakuwa muhudumu na mapokezi pia

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 07, 2008

    MAMAA ALIYE KUAMBIA UNAVUTIA KAKUDANGANYA! HIYO SURA C YA MATANGAZO..

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 07, 2008

    Mimi sina kazi ya kukupa lakini nimefurahishwa na kutambua kipaji ulicho nacho na unahitaji kukiendeleza.kwangu ina maana huna msuguano wa moyoni maana una ramani kamili.

    Unaweza kupata kazi ndani mwezi mmoja.Hii ni hakika!Mimi sio kajura

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 07, 2008

    Duuh! dada umependeza ila na hii ni mtindo mwingine wa akina manka mushi. Kila laheli utapata tu wa kuwaburudisha!!!!!

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 07, 2008

    Wewe unataka kazi za ofisi tu au kazi nyingine pia?. Mimi nina kioski changu cha juicy za miwa natafuta muuzaji au mparamiwa. Kama umependezewa nipigie namba 0744330220.
    Makame.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 07, 2008

    Michuzi,
    mbona hauna msimamo? si ulisema kuwa umesitisha kupokea matangazo yenye picha kwa sababu ya yaliyompata dada yetu wa London. au haukuwa siriasi?

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 07, 2008

    sawa dada tumekusikia na tumekuelewa,kazi zipo ila kazi zenyewe ni za ufisadi,je utaziweza?

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 07, 2008

    Michuzi mimi nashindwa kukuelewa sio wewe ambae wiki chache zilizopita ulitutangazia ku nabi hii biashara ya matangazo binafsi yenye sura za watu kwa sababu ya uchafuzi wa hali ya hewa , sasa kulikoni ?? Unataka tuu waoshwa vinywa waanze hapa ili usitoa comment zao hii si sawa kaka yangu kama umetoa uamuzi stick to it usijibadili badili kam kinyonga ! na naomba utoe comment yangu sinibanie kam kawaida yako mana umeyataka mwenyewe pls

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 07, 2008

    wish u all the lucky my little sister,utafanikiwa tu.
    Ms Bennett

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 07, 2008

    Ahh awesome... you are so cute kinda. All the best

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 07, 2008

    tehe tehe!Kazi ipo!Mwaka huu naona kina shimboni wamecharuka.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 07, 2008

    dada forgive.umependaza na kweli sura unayo na sidhani kama vibosile haWAtachanganyikiwa.unaweza ukapewa hata kazi ya kupokea cellphone LOOL maanake vibosile kwa kupenda vidogo vidogo.kwa fanya maneno mafupi maanake najua kuna mengi yanakuja kutoka kwa wadau JE ULIKUWA UNATEGEMEA MSHAHARA KIASI GANI KUANZIA?
    Wadau huyu anatafuta kazi jamani msije mkamwagia maneno makali dada wa watu mkajua anatafuta mchumba anyway kazi na dawa.
    Msomali

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 07, 2008

    misupu vipi bana? ulisema huweki haya mambo imekuwaje tena mazee?

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 07, 2008

    mdogo wangu yani nakuonea huruma sana, hayo matusi utayopata natamani kuitoa hiyo picha kabla hawajaamka hao watu wanaojifunza kiswahili, wasiojua maneno machafu na masafi ni yapi..ambayo hawapigi miswaki wanasafishia vinywa humu!! Pole sana dogo

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 07, 2008

    "Business without advertisement is like winking a girl in the darkness." (Walinena wahenga).

    Dada mimi nakushauri mambo makubwa mawili:
    1. Usikate tamaa; wakati unasubiri majibu ya wadau humu kijijini michuzi, endelea kuandika barua na cv nzuri... sawa?
    2. Usikubali kutoa rushwa!

    Ciao,

    Seve.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 07, 2008

    Kila la kheri Forgive kwa jitihada zako za kutafuta kazi, kwa mnao msaga kuwa atapataje kazi ndani ya blog hii then know this: "this is networking, big time". Hata sisi tunaoishi huku ughaibuni bila networking hupati kazi hata kama una elimu gani, ni rahisi mtu kukupendekeza kwani anaweza kuwa ameridhika na maelezo yako kuwa You are sincere.

    Wewe anonymous wa 12:01 unayesema eti wa kumuoa wako wapi wamtunze! Loh! huu sio wakati wa kutaka kuolewa for financial gain, wanawake wengi siku hizi tunataka "self reliance and financial capabilities" na ndio wanaume wanatueshimu.

    Go Girl, you might be successful in life and keep on your determination to advance your studies....PLEASE make sure you don't give up: beauty and brains will make you even more attractive. I believe you will understand me though I am using this language, when I was in form 4 I was good enough.
    God Bless sweetheart.

    JK - T.O.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 07, 2008

    Wabongo kwa ushauri tuu, utadhani wao maisha wameyapatia. Mambo ya muhimu hamjadili bali upuuzi ndio tunashikia bango.
    Dhana hii potofu haitufikishi popote.

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 07, 2008

    MH.MKUU WA WILAYA YA TEGETA NAONA SASA UNAKOSA MSIMAMO MAANAA ULISHATUELEZA KUWA AUTOPOKEA TENA NA KUZITOA PICHA ILI KUEPUKA UCHAFUZI WA HALI YA HEWA,YAANI HAPA ILIKUWA ZIBAKI ZILE PICHA ZAKO ZA ILE FULANA NA MIKONOZZZ SASA IMEKUWAJE TENA? NA HATA HIYO PICHA YA HUYO DADA MUOMBA "KAZI" NI YA KISANII SI YAKE.

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 07, 2008

    dada kwa hakika mie ni mzaliwa wa tabora na sasa naishi dubai lakini mwezi april nilikuwa bongo.

    nimeshamjulisha dada kama ni kweli yuko serious mimi nampango wa kufungua biashara kama vile real estate yaani developer pia nina plan ya kufungua hotel ya vibanda ambavyo huitwa challette kwahiyo mara nyingi hupata masikitiko makubwa pindi napoona binadamu au kiumbe kupata taabu.

    hata nilipokwenda kwenye club bongo nilikutana na baadhi ya kina dada wakijiuza nakawauliza jamani tumuogope MUNGU na maradhi.

    nikawauliza je tukifanikisha kupata pesa tukavungua mtaji ili kuendeleza maisha wengi hakika wakanicheka na kuniona kama mpumbavu.
    waliokubali ni wachache na mmoja wao namlipia ada anasoma namuombea MUNGU amjalie na wengine pia taratibu mambo yatakuwa mazuri.
    kikubwa ndugu watanzania tuwe na itikadi za kibinadmu na kupendana na kusaidiana.

    umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu MUNGU TUJALIE MAPENZI YAKUPENDANA BILA KIJALI DINI, RANGI. KIKUBWA NI KUJALI KUWA HUYU NI KIUMBE.

    ASANTENI MOHAMMED TOKA DUBAI

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 07, 2008

    Watu wangekuwa wanatoa comment kama hizi..watanzania tungekuwa mbali..leo kuna nini..mpaka watu wamekuwa decent hivi? (ofcourse wachache wapo wanaotoa maneno ya kashfa!), ila kwa mara ya kwanza...Watanzania tunaweza kubadilika. Yes we can!

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 07, 2008

    aah stori nyingine ya wanawake wa kichaga hiyo! Mnatuboesha bwana!kwani kwa elimu yako ya form 4 umekosa nini mpaka ukatake kuwa sekretari, modo, mpokea simu au utumie sura yako katika matangazo kupata fedha. Ni kweli akili ni nywele na kila mtu ana za kiasi chake kichwani. lakini ningependa kukushauri usijiunderestimate kiasi hicho dada, mimi pia ni msichana kama wewe lakini kama ningekuwa kwenye position kama yako pengine nisingechagua kazi kama hiyo, kwa elimu ya form 4 na kama vyeti vilikuwa vizuri kama ulivyojielea unaweza kuwa mwalimu mzuri wa shule ya msingi, na kama kingereza kinapanda vizuri unaweza pia kuwa mwalimu wa chekechea za english medium ambazo zinalipa vizuri zaidi kwa nchi yetu. Ni kweli umeeleza ujuzi uliokuwa nao wa kuzungumza na ukataja kazi unazopenda lakini ningependa kukuasa kuwa, angalia usije ukatumiwa vibaya na waajiri na mabosi wamiliki wa makampuni mafisadi, namaanisha mafisadi wa ngono..kwani wako tayari kuwapata wanaouza sura...kazi kama hizo kidogo ni rahisi kurubuniwa..na wakati wenyewe huu..angalia!
    nakutakia kila la kweli
    Msichana mwenzio

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 07, 2008

    kuna kazi pale ze comedy, sikiliza vizuri email ya masanja kisha mwandikie, ukiipatia tu kazi umepata, sikiliza kwa makini na mwandikie masanja mkandamizaji pekee!

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 07, 2008

    SHIMBONI 4GIVE.
    POLE SANA KWA UGUMU WA MAISHA NA MATUSI UTAKAYOYAPATA KWA WABEBA MOBOKSI
    MUNGU AWE NAWE

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 07, 2008

    Huyo dada asitake kutuzingua apa hakuna cha kutafuta kazi wala nini ila ana lake jambo tu.Anadai alishindwa kuendelea na masomo baada ya mzee wake kunanihii,ok sawa,but anaonekana ni binti mrembo kwa asili kama picha yake ilivyo na pia anaonekana mrembo zaidi kwa maana ya kufanya makeup,sijui izo nywele ni za kitanzania kweli au sioni vizuri,labda wigi.
    Sasa anapata wapi hela za kujikeep mrembo kiasi hicho paka mwenyewe anajikubali kwa kusema ye ni mzuri kiasi cha sura yake kuwekwa kwenye matangazo aagrrrryy!!
    Ok kama hizo hela za kujinyembuanyembua angezitumia kwa kusoma vijikozi(hotel mngt,ualimu,tourism...ect) kwa ngazi ya certificate kulingana na uwezo wake na baadaye diploma na kama akijaaliwa digrii kama kweli alikuwa na nia ya kujiendeleza kielimu.
    Asilete habari zake za kujua kuongea apa,kwani kuna mtu asiyejua kuongea?!What's kujua kuongea?Even bubu knows how to speak(gestures)Eti yeye ni mzuri,uzuri ndo nini? This is 21 century unaweza ukawin au ukaharibiwa life na huo uzuri wako ohooo mi simo mwenzio...
    Ebwana bro Michuzi uyo sis asikutie changa la macho iyo picha na maelezo havina uhusiano wa karibu hata kidogo kama vipi arudi kijijini akalime kama wadau walivyosema hapo juu,alah!!
    Upgrade elimu yako dada achana na kuongea na kijimwagia miujiko isiyo ya msingi kama kweli unataka kazi nzuri,watz matter in dis world is educ. Nothing else,may be if she needs ufisadi jobs.

    Mdau Potz.

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 07, 2008

    Kama kupima zali leo Michuzi umepima zali ila hali ni shwari kama unavyoiona. Kusema nako kunasaidia saa nyingine maana ni kukumbashana na nimeamini kuwa kweli watanzania ni wastaarabu ila kuna wachache waliokuwa wanataka kuharibu sifa yetu. Hongera wote mliotoa maoni yenu, ingawa mengine yanachekesha lakini yana mafunzo ndani yake. Bwana Mohamed wa Dubai shukran kwa maoni yako tukiwa nawatu wenye moyo kama wewe na wengineo humu basi tutafika mbali, yes we can.

    Dada Forgive, unaonekana una upeo mkubwa nacho ni kipaji, kama alivyosema mmoja wetu humu ndani usijilimit kwenye receptionists na usekeretari, panua wigo toka nje ya box angalia nyanja nyingine ambazo zina uhitaji mkubwa wa wataalam kama ualimu na unesi ingawa itabidi ujisomeshe, unaweza ukaanzia hapo kwenye receptionist halafu ukasoma jioni, lakini shortcut ya kimasomo ni kwenye sekta ya ualimu, huko kama unabidii utasoma wee mpaka darasa la kusoma litakapoishia.

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 07, 2008

    Makame hapo juu,
    Kwa nini unampatia dada wa watu namba ambayo haipo duniani!?
    Mwenzio yuko serious, wewe unamletea utani. Shauri lako, ukipigwa shavu usilalamike.
    Na wengine nyie mnaotoa comments mbaya, mmuogope Mungu! Nyie hamuangalii hata upepo uvumako? You can't even read the signs. Shauri zenu.
    Someni comments za watu mujionee au rudia tena kusoma maelezo za Forgive ili utoe comment kwa usahihi wa sindano.

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 07, 2008

    Kwanza dada nataka nikupe good luck... usi give up utapata tu kazi, na pili nyie wote mliyo msema kuwa ni muongo... mnajuwaje???? mnakaa tu kuwasema watu je wewe??? mjiangalie nyie kwanza...??? huyu dada ana tafuta ajira instead ya kumsaidia... jamani utajuwa tu roho za watu hamna aja ata ya kuona sura zao... alafu ni mijitu mizima na wanaheshimika... dahhhh Michunzi ingekuwa una weka picha za kila mtu ana comment utaona mijitu ambayo awana adamu wata kimbia wenyeweee unless awana akili timamu....

    From Mbongo

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 07, 2008

    YALL BUNCH OF HATERS. Kila la kheri mamy, Inshallah mungu atakusaidia utapata kazi lkn kua makini na tangazo lako na phone calls pamoja na email utakazo pata manake wengine hawakupi kazi bali watakufayia unyama tuu. Kazi za kuomba online nazo si kazi bt Inshallah mola atakua nawe katika maisha yako ya kutafuta.

    Na wewe (Tarehe May 07, 2008 1:40 PM, Mtoa Maoni: Anonymous) Una mfananisha huyu na ugly betty, wewe sura yako iko wapi? Acheni chuki,ufisadi na fitna jama. Kama mekosa kazi kasafisheni roho zenu msiwe na roho za kwa nini.

    To Haters: Why you waste ur time if you don't have nice thing to say? My mama always says "If you got nothing to say then don say it at all". And this applies to all of the HATERS. Stop bringing each other down. Try to motivate and encourage one another. Kila siku mkidharau mtafika wapi kwani? Leo kwake lakini kumbukeni kesho kwenu.

    KUMBUKENI KUPATA AU KUKOSA NI MAAJALIWA YAKE RABANA.

    Masalaam

    Ms.Thang

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 07, 2008

    Wewe Binti huko dar huna kazi ya kufanya au ndio unatafuta bwana?wewe nani kakuambia hiyo sura ya kufanyia biashara sasa hivi naona mmeshaona dili kuingia online na kufanya biashara au sio kazi kwako utakufa na ngoma na leo nimekosa mda tuu ningekupa vipande vyako vilivyo kwenda shule maana mnatuchosha sana na mmezidi bwana.

    Na pia kuna baadhi ya watu wamesema kwamba MICHUZI alikataa kuweka picha za watu au mtu ambaye anatuma salamu jamani elimu kweli ipo au mnalopoke tu!! kaeni mfahamu au mkumbuke yaliyopita sio mnalopoka tu bila kuelewa unaandika nini>>>>> MICHUZI ALISEMA KWAMBA HATOPOKEA SALAMU ZOZOTE ZILE KUTOKA MAHALI POPOTE PALE SASA HUYO DADA KUNA MTU KAMPA SALAMU AU KATANGAZA KITU ALICHOKUWA NACHO fikirieni kwanza ndio muongee sio mnaona bora mmetype keyboard ok thank.

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 08, 2008

    MAKOFI NA VIGELEGELE KWA msTHANG

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 08, 2008

    Wewe Makame hapo juu unamtangazia kazi za kuparamiwa huyu dada, wewe mwenyewe zimekushinda?

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 08, 2008

    Michuzi una lako jambo. najua unataka kuichangamsha blog. kuwa mbunifu bwana. hii imekaaje? usijichanganye. kwani hujajua kuwa blog yako ina wateja wengi?

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 08, 2008

    Mizimu ya Johnie Mashaka haya, kayaleta mwenyewe. Watoto sasa wameanza kuuza sura! Endeleeni, Yule kaka kazushi sana. amechanganya mademu na vijisenti vyake vya Wall-Street sasa wanauza sura kila eneo walipo wadau

    Mbeba Sanduku. Texas

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 08, 2008

    big up to makame!
    mpe ajira huyo sistaduu

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 08, 2008

    Dada Assenga
    ninarudi nyumbani siku za karibuni, na Mungu akijalia nitafungua mradi wangu, na kwa kweli nitahitaji mtu mwenye sifa zako haswa katika swala ma kutafuta masoko.
    Nimechukua contact zako tutawasiliana.
    God bless you

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 08, 2008

    Ile akili ya kusema uombe kazi kwa kutumia michuzi dot com inaonyesha jinsi gani ulivyo na malengo katika maisha yako. Kutafuta kazi haina maana kwamba umelosti kichizi hata mwenye kazi World bank anatafuta kazi hata senata hillary/Obama anatafuta kazi kwa kuomba na kunyenyekea sana. haina maana wamelosti. Huyu dada kasoma hadi form iv pia naonekana ni mkweli na hana haja ya kumuonea mtu aibu. Wabongo tafuteni kazi msijione mmefika na kazi zenu za kubeba mabox. Huyu dada angekuwa Marekani angekuwa mbali sana.Cheza lottery utawini greencard.

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 08, 2008

    KAZI UTAPATA 4GIVE, una experience gani? unajuaje utafaulu kuuza chochote? You must very smart and don't be afraid and keep up your courage and determination in life. you will be Oprah of Tanzania. Why not? Omba kazi ITV au Redio One,pia anaza kuwa mwandishi wa habari. Mi naweza kukupa kazi ya kuwa Wedding Planner.Utakuwa millionare usiogope makunyanzi.

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 08, 2008

    Duuuhh!! Michu!! Mambo yetu yaleeeeeeeeeeeeeeeee!!!

    Cheers 4Give, hutakosa!!

    ReplyDelete
  56. AnonymousMay 08, 2008

    MICHUZI MBONA UNAPENDA SANA KUTANIA WACHAGGA!!UMEKUWA MPARE NINI??HUYO DADA NI MSOMALI WA MTONI KWA AZIZ ALI UNASEMA MCHAGGA..USITANIE WACHAGGA TAFADHALI KWA KUTAKA SIFA..MDAU KYEKUE

    ReplyDelete
  57. AnonymousMay 08, 2008

    Wewe Issa MNAFIKI MKUBWA PICHA ZA MADEMU NDIO UNATOA wakati ulisema picha basi .. za madume kapuni

    ReplyDelete
  58. AnonymousMay 08, 2008

    hongera dada ulivyo jasiri. nafikiri unaweza. achana na wanaoona noma.

    cheers

    ReplyDelete
  59. AnonymousMay 08, 2008

    Makame, jina lako linanikumbusha muimbaji mmoja stadi mkongwe wa Taarabu huko zenjy(Makame Faki), huwa anaimba vizuri sana, na maneno yake huwa yana visa vingiiii, kwa umahiri wake anayafumba kwa lugha tauria na kama anamuimbia mlengwa huwa anatahayari au akikusifu kwa mafumbo yake kichwa huvimba kwa furaha. Ila wewe sentensi na mawazo yako, unatia kichefuchefu,bora kaa kimywa ujinyamazie tu.

    ReplyDelete
  60. AnonymousMay 08, 2008

    dada kazi inapatikana kwa Mungu piga magoti kwa Mungu wako mwambie hitaji lako nae atakusaidia.
    sweet,
    Arusha.

    ReplyDelete
  61. AnonymousMay 08, 2008

    Hivi wewe unayemwita michuzi mnafiki ulituma picha yako ikakataliwa au ulikurupuka tunduni hata ujapiga mswaki.Watch your mouth doug you gotta be serious.
    To you ma sis dont heed to what other people say life aint a gentle slope it git ups and downs so you fight.You got to make your dreams come true coz you are there to fight till the end.

    ReplyDelete
  62. AnonymousMay 08, 2008

    Hivi wewe unayemwita michuzi mnafiki ulituma picha yako ikakataliwa au ulikurupuka tunduni hata ujapiga mswaki.Watch your mouth doug you gotta be serious.
    To you ma sis dont heed to what other people say life aint a gentle slope it git ups and downs so you fight.You got to make your dreams come true coz you are there to fight till the end.

    ReplyDelete
  63. AnonymousMay 08, 2008

    For those who criticize her trying to get a job, I pity you. Here we have a young Tanzania, rather than begging for money she wants to work in a honest way to make a living. But we do what we are best at, criticize and make personal remarks.
    If you can help her in any way do it, if not at least be humane enough and give her some words of encouragement.

    My dear sister, all the best and may you look back one day and say it did work out for you.:)

    ReplyDelete
  64. AnonymousMay 08, 2008

    madume mnatisha! ndo mana mnatiwa kapuni! jilembeni kwa hereni na lipustiki!
    Good Luck Forgive inshaallah utapata kazi.

    ReplyDelete
  65. AnonymousMay 08, 2008

    dada nakushauri uende dar es salaam mjini posta karibu na Habib bank,au mlimani city kuna maduka yanaitwa AKS yanatafuta wadada kama wewe kwajili ya sales. je, nakumbuka jana nilikutumia namba ya simu na email ..ulijarubu kutuma!? jitahidi kuna wengi wamepata kazi nzuri kwa njia hii...KILA LA KHERI DADA!!

    ReplyDelete
  66. AnonymousMay 09, 2008

    NENDA REGENCY HOTEL MIKOCHENI AU PALE ROSE GARDEN KWA MLLATIE,LAZMA UTAPATA KAZI.UHAKIKA UPO,SEMA NDO USICHAGUE,KAZI NI KAZI.
    KILA LA KHERI

    ReplyDelete
  67. AnonymousMay 09, 2008

    jikaze dadaangu kazi utapata!ila angalia sana kuna vigogo ambao wanaweza wakakutumia kwa sababu ya shida zako za kutokua nakazi.good lucky sista.naomba usinibanie braza mithupu

    ReplyDelete
  68. AnonymousMay 09, 2008

    Watu wengine bwana kama zimetoka kichwani sasa wewe unaye mwita michuzi mnafiki kuna siku umetuma picha yako akuwekee akakuweka kapuni acha mambo yako ya kishamba wewe basi na wewe kama unataka jipake lispistiki vaa na gauni alafu mtumie michuzi akuweke basii mbona unakuwa na tamaa za kishamba hivyo wewe acha ujinga wewe mtoto wa kiume usiwe hivyo kama unataka wewe tuma tu picha sio unaongea ujinga wako mbele za watu umeamka asubuhi domo linanuka unakuja kulopoka hapa kaa chini na fikiria nini unaandika sio unakuwa kama mtu ambaye zimechomoka kidogo.

    ReplyDelete
  69. AnonymousMay 10, 2008

    Nimejaribu ku-foward kontakti zako kwa wadu nnaowajua wenye makampuni ya 'ROADSHOWS na MATANGAZO' wamenijibu kuwa ze namba z not richebo.

    Usomapo komenti hii wasiliana na michu atanistua nikupe namba upige wewe kama hii si namba yako.

    Asante

    Mdau wa Mayfair

    ReplyDelete
  70. AnonymousJune 26, 2008

    Wandu wekulamba ambia necha, kama nuere mbatu itutu yeparika iyoe tsia tsi cha mndu alaore mberi, omiicho, niinyi msacha opfo ngikyeri iha mrinyi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...