Huwezi kuzungumzia historia ya disco nchini Tanzania na kuacha kumtaja DJ Bonny Luv (pichani). Ukifanya hivyo,wanaoielewa historia, ladha na utamu wa disco, enzi hizo lilipokuwa disco haswa, watakuona una lako jambo.

Na katika tukio la nadra, tarehe 5 mwezi wa saba (5th of July 2008) ndani ya jiji la Columbus katika jimbo la Ohio(Columbus,Ohio) nchini Marekani, DJ Bonny Luv kwa kushirikiana na wakali wengine kama DJ Mix Master Luke kutoka Washington DC na TNT Jackson wanatarajia kutoa burudani ya aina yake.
Waandaji wameliita tukio hiloOld School Party of The Century. Ukikosa,usije kumlaumu mtu na kusema hukuambiwa.Habari ndio hiyo.
nenda http://bongocelebrity.com/kujua mengi juu ya DJ huyu mahiri ambaye kaahidi kufanya makubwa huko Columbus na vibao kama 'maiko jekson njoooo.....sitakiiii.... kama hutaki nenda...'

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2008

    Sema Mtu wangu..i got everything rollin man..wewe tu ukifika powa. Dj Boni Luv, Boni Mapenzi..

    By the way kwa wanaokumbuka disco la ghorofa ya 7, New Africa Hotel,Twiga na Kilimanjaro. Motel Agip jee?? USIPIME!! This guy ndo aliekua akiturusha wote tangu za zile songi kali kama "ekoo maa heart..." na "I gotta get the best of you now baby...

    Je Mrope dereva wa double cabin ya Kusaga, Bouncer Dabo Difu? Jamaa alikua anabeba Amps mbili peke yake duu..Bouncer Martin jee Tazara..jamaa alikua ukimkatia umeingia tazara nusu kiingilio. Mnakumbuka ukumbi wa DI? haa haa haa Hii ni down memory lane for sure!! Mambo ya Boni Vencha..
    haa haa haa

    DONT MISS HII KITU OHIO..SIO MCHEZO!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2008

    hawa watoto wa juzi. Kina Choggy sly John Peter wako wapi? hiyo ni maiaka ya 79/80? Huyu anwafaa old skul watoto wa Bilicanas!
    kama Bonny Luv mtu wa zamani basi ni kwa watoto wadogo wa kilimanjaro Pool side. Yuko wapi Dj wa Cave disco Arusha? NK Disco Sound Dodoma?
    Kina Nene Cherry na Buffalo Stance! Colonel Abrahams wataonekana wa zamani hao pia ni wa juzi! Kina Puala Abdul wa American idol kina Gerald Levert (Sp)!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2008

    BONY SIJUI NIKUSIFU VIPI JAPO JAMAA ANASEMA WE NI YOUNG ! NIKWAMBIA NENDA KAWACHENGUE WAAMBIE ULIANZA ZAMANI WAKATI UKO TAMBAZA , VI BOTLE PARTY VYA REGENT EST. KWA KINA MAREHEMU ANORLD (RP) KAKA YAKE BENNY MWAMASAGE. KUENDELEA KWENYE VIWANJA VINGINE.

    WAPE ZA SILENT INN, TAZARA , PICK COCONUT NENDA KAWAPAGAWISHE KWELI KWELI WAJUE KUA HABARI NDO ISHAWAFIKIIA SIYO KILA SIKU VITOTO VIDOGO TU VINAENDA TUNATAKA UWAPE EEEEH ACHALI ACHALI TO BLIND TO SEE....

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2008

    BONI LOVE LAZIMA UWEKE KONYAGI HAPO... NIMESIKIA ITAKUWEPO?? NI KWELI JAMANI...
    NA MIX KONYAGI NA REDBULL SASA HIVI!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2008

    Anon wa June 06, 2008 8:09 AM,KWA KUONGEZEA BILA KUWASAHAU DJ CHRIS PHABBY,DJ KALIKALI(RIP) NA WENGINEO WEENGI TUUUU

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2008

    madude ya kina Ray parker jr, Joyce sims,'Shuga sei yes ,shuga sei no" SAIIN o ZE TAIM, pRINCE,Rick Ashley, London beats etc. ilikuwa bab kubwa.enzi za Manikiniki, Msasani beach, Kawe beach , palikuwa hapatoshi.
    Mdau mtoni, kijichi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 06, 2008

    ndio maana yupo dj Luke atakae wakilisha hao madj wazamani,unakumbuka disko la stirio II,basi huyu dj alianzia hapo akishirikiana na dj Agib show na madj enzi hizo pamoja na hao ulio wataja pia walikuepoakina Kalikali na Niga jay(ymca),saydou na jeri koto(mbowe)dj Roma popjuice na jb(rungwe oshenik)dj clement disko la gogo chris phaby(msasani bichi)dj joe wa studio 35amani chalenja(bs korogwe)

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 06, 2008

    Daah hivi KalikaLi alituacha lini hebu nipeni taarifa hii kwangu ni mpya.(R.I.P) KAMA NI KWELI

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 06, 2008

    huyo anon wa june6 time 8.09 hapo juu ni mzushi Dj Kali Kali yu hai .pengine anasema Kalikawe ndio aliyefariki kitambo. dogo unaweza kufungwa kwa uzushi.mdau Zee la Bandari

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 06, 2008

    Yaani mambo ya seven floor,Twiga n.k ndani ya house dj Steve Punk(R.I.P),dj Charles Mwamiji,Wazee wa tazara club kidengule, mambo ya pili pili weeee!!!!!!!!!!!!kuna jamaa mmoja alikuwa famous sana lakini hatujui kapotelea wati jamaaa alikuwa wakwanza kuvaa beli la OPP by naughty by nature alikuwa anakaa chuo kikuu anaitwa BIYE.....msikose jamani kwani nitakuwa nauza miswaki na dawa wewe tu.............

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 06, 2008

    Dj Bonny Luv ni dogo tu kwa kina Dj Chogole Selemani (Choggy Sly), Ajib Show,Kali Kali (double K double A double L double I, Dj Bonny alikuwa akiwapigia watoto wa shule tu wakati huo mnazungumzia time ya pink coconut ,new africa na tazara ? old school ilikuwa wakati wa Sea view, Mbowe, na Bahari beach na wakati huo Dj bonny alikuwa akipiga kwenye vi bottle party na akija kwenye madisko basi atapewa kazi ya kusafisha mavumbi santuri. ama kweli tumetoka mbali.
    mdau Zee la Bandari -UK

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 07, 2008

    Dah mmenikumbusha mbali, siku moja nilikuwa mwaingu studio mwenge na Columba Mwingira, Mzigo umeingia toka USA Kusaga pembeni, mzigo ukafunguliwa na 12 inch za majaribio kibao pale nje mawingu studio by then siku hiyo ilibamizwa I wanna be down, Brandy damn! mbona majirani walikuja kulalamika kelele IoI alafu ilikuwa mchana maana Bonny alifanya... I am happy he still...by the way, nani anafahamu Dj David Joseph yuko wapi these days? IoI Enzi za onex 7th floor
    Londoner

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 07, 2008

    Anoy June 6, 9.28PM Sasa BIYE..ama BIYENGO hilo beli la OPP nilimpiga nalo mimi mwaka kama 91 hivi kuanzia enzi za KRIS KROSS..jamaa inasemekana kafariki(RIP)MSUMBIJI akiwa njiani kwenda Bondeni sio.
    Dj Boni ila kaaniza mbali tangu enzi za ku rewind kanda bwa peni..upo hapo.
    Hii inakumbusha enzi za ma Beach Party kabla watoto wa uswahili hawajazishtukia na kuanza kuharibu zile party. daaa!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 07, 2008

    Maneno kina Chris Phabby Kalikali, Choggy Sly na wengine wa enzi hizo. Sasa hawa kina Luke na Bonny Luv ni wabangaizaji tu. MaDj Kawawa na Karume, eee bwana tumitoka mbali nyie enzi za kina Nyerere kabla ya uhuru tulikuwa tunajirusha Oysterbay Beach Club na Sumbawanga!!
    MaDj hawapo nyimbo bado zipo!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 07, 2008

    Isiwe taabu michuzi mixers 1975 to 2009 zitakuwepo!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 07, 2008

    Duh,hii must kuzuka.Inaelekea itakuwa patashika nguo kuchanika.Ila lazima waandaji wahakikishe kunakuwa na gari la ambulance kabisa nje ya ukumbi kwa sababu kuna watu hivi sasa washakuwa watu wazima sana na ma high blood presha nk.Akinogewa mtu na muziki anaweza kuanguka.

    Halafu Michuzi nadhani umekosea hiyo link ya bongocelebrity,hebu icheki tena.By the way,kazi nzuri sana Michuzi na bongocelebrity.Hizi ni blog mbili ambazo kwa kweli they worth visiting hata mara kumi kwa siku.Endeleeni hivyo hivyo wakubwa.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 08, 2008

    oldskool ni mlolongo mrefu,kuna mdj,wateja ambao walikua nevamisi,madansa,mabaunsa nk.kwa kumbukumbu zangu mdj enzi nikama ifuatavyo:kalikali na niga jei,chogy sly na joni pita pantalakisi,roma pop juice na jb(joni bure),mc hope na kate,yang milionea na joni kitambi,edi sali,mc gee,deo compoza,super deo,switi kofi,chriss phaby,jeri koto na seidu,clement,laulance,joe holela,mr a,richie dillon,charles na sure boi,washinton,joe wa studio 35,bush dctor,jesse,mehbub,franco kabigi na viatu vyake vyekundu,kulikua na madj wa madisco ya xtc na jet set majina yamenitoka na oldskool haijakamilika bila wa tu hawa,charles mbowe,bob rich,makochela(makojozi),ray abdu,sabri kube,spia,jimi chacha,wandiba,toni,abdul shalamaa,ali baucha,black moses,athuman digadiga,omy sidney,shabani sato,pailonga n.k.wapiga picha michuzi na mzee mpiga picha na wengineo wengi

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 08, 2008

    Inabidi watu wakavae kizamani pia,ie; kung fu shoes,dont touch, mocasin bila sox, scuna mtambo wa fungus,wanyoe mabwenzi au push back,stonewash,Raba za kuchumpa,nyanya pensi,fulana za carwash.Hii inanikumbusha misemo ya kizamani pia ie;shingo feni macho balbu.Masisterdu wenye majina ya kiswahili walikuwa wanajiita Rose, Mary, Jackline etc.Machecksister wa kitizii walikuwa na nyodo sana miaka hiyo kama huna guruwe(peogeot 504) la kupiga msele hakieleweki.
    Mdau, mtoni kijichi.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 08, 2008

    dj kalikali ni marehemu,halikadhalika mdogo wake reggae man kalikawe ni marehemu

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 09, 2008

    justin kalikawe amefariki?WHEN?

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 09, 2008

    Michuzi, halafu haya mambo ya kudanganyana Bonny Luv anakuja watu tunapoteza hela zetu na muda wetu, only kuishia kuentertainiwa na kina DJ Luke. I mean Luke ni DJ mzuri, but they advertised that Bonny will be visiting, so I really expected to see Bonny Luv. July 2007 Washington DC hiyo. Please tunaomba organizers watupe information za kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...