Habari ambazo zinapita pita kama vile maji ya mfereji zinasema kuwa Mhe. Karamagi anatarajiwa kuwa mkutano na waandishi wa habari hapo kesho, atakachozungumzia hakijajulikana bado na kama kinahusiana na masuala ya TICTS au masuala ya Richmond.
Wakati huo huo Bunge linatarajiwa kutoa maamuzi kuhusu ombi la Dr. Mwakyembe kuhusu kanuni za Bunge.
Hii Alhamisi pia inatarajiwa Spika Sitta atatoa uamuzi wa kama kuruhusu Bunge lipige kura ya kutengua kanuni yake inayozuia kujadiliwa kwa azimio la Bunge au jambo lililotolewa uamuzi na Bunge hadi miezi 12 ipite.
Endapo Bunge litaridhia kutengua kanuni hiyo, basi mjadala wa ripoti ya Kamati Teule ya kuhusu Kampuni ya Richmond utaanza tena Bungeni.
Mojawapo ya waliouhisika na sakata hilo wamesema kuwa wanaisubiri kwa hamu siku ambayo wataweza kujitetea mbele ya Bunge.
"Hatukupata nafasi ya kujitetea, hivyo kanuni ikitenguliwa tutaweza na sisi kuelezea upande wetu" alisema mmoja wa Mawaziri ambao walijiuzulu kufuatia kashfa ya Richmond.
Hata hivyo, Dr. Mwakyembe na kamati yake wamesema wako tayari kusimama na kufafanua jambo lolote ambalo halikueleweka au kutoa hisia zao kuhusu yale ambayo yamekuwa yakifanyika.
Kwa mujibu wa mjumbe mmojawapo wa Kamati ile Teule, kitendo cha NEC na sasa Wabunge kujaribu kwa nguvu zote kuwasafisha na kuwatetea viongozi waliojiuzulu kina lengo moja tu nalo ni kuvuruga jitihada nzima za kurudisha fedha zilizolipwa Richmond na kuondoa mjadala kuhusu Dowans na kuufanya uwe unahusu Kamati Teule.
"Angalia ni nani aliyesimama kutetea kurudishwa kwa malipo ya mamilioni ya shilingi kila siku kwa Dowans? Angalia ni mjumbe gani wa NEC ambaye amesema anataka malipo yasimamishwe; hakuna!" alisema mjumbe huyo kwa jazba akizungumza na KLHN.
"Hili jambo halijafikia mwisho" alisema Mbunge mwingine ambaye anamwelekeo wa kuiunga mkono kamati teule.
Muda wote kesho KLHN itakuwa inakuletea taarifa kwa kadiri zinavyopatikana kufuatia maendeleo yoyote kuhusu masuala yote mawili ambayo yanahusiana.
Title: KLH News Episode: Sakata la Richmond kufumuka tena?
Sikiliza matangazo yetu "live" kupitia.
Enjoy!
mymedia/thumb/13384/300x300_1062781.jpg

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2008

    Mmmh!!! kama na Bunge lenye kutetea masilahi ya wananchi ni hili lakini si wote bali wachache wenye nia njema na taifa hili changa.Kimsingi suala la RICHMOND kwa kweli imefika hatua sasa hao waliyohusika wachukuliwe hatua kali za kisheria lakini baadhi ya Wabunge sijui ni ujinga au umasikini wa mawazo wamekuwa msumari kwa kamati teule ya Bunge eti wamewaonea wahusika!!! Inashaangaza sana iweje siku Dk. Mwakyembe anasoma taarifa mlipiga makofi kwa bashasha na isitoshe wengine mlimtumia meseji kumpongeza leo hii ndo wakwanza kumponda heeeee!!! mmepwa nini nyie kizazi cha nyoka!!!acheni unafiki!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2008

    Naona mnataka kuchokoza moto yataibuka makubwa zaidi. kwani uongo wewe lowasa hukuwa fusadi?hakuna anayekutana kabisaaaaaaaaaaaaa mwizi mkubwa.Hata huo ubunge unatakiwa uachie ngazi, Siku za mwisho zimefika yote mliotufanyia sis wananchi wa hali ya chini Mwenyezi Mungu atatufidia. Mnachotaka kujisafisha nini au unataka urais nini ilishatoka ikirudi pancha, Mwakyembe kaza buti baba usiogome tuko nawe na tunakuombea maisha marefu Mungu akujalie afya njema hakuna uchawi unakaokupata tuko katika sala usiku na mchana, safisheni mafisadi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2008

    Jamani jamani umasikini mbaya sana kwani unakunyima uhuru. hawa baadhi ya wabunge wanaotetea mafisadi wamepewa kitu kidogo wajaribu kuwakosesha mwelekeo watanzania. naomba bunge lianze kujadili upya ili tuwamalizie.

    Nantombe
    Moshi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 26, 2008

    I wish Hon.JK can be able to learn a thing or two on how to be "FIRM ON ISSUES" suppose to be.

    Yaani hawa mafisadi na chama chao wanavyotuchezea kama sisi shangazi zao nasikia hasira sana.

    Asante sana Dk. Mwak kwa kutufumbua macho tuone ni jinsi gani bunge letu lilivyojaza baadhi ya wabunge mafisadi, wanafki, wasiopenda maendeleo, wahujumu uchumi na masikini wa fikra.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 26, 2008

    Ama kweli kuishi kwingi ni kuona mengi haya tunajionea wanafiki na ufisadi unavyoingia mpaka watu wamenunuliwa ili wawasafishe mafisadi. Hivi jamani sisi tutakimbilia wapi? Hii serikali imekua kama genge la mafia. Watu wote wana njaa ina maana hawa wabunge wanaotetea ufisadi nao wengepewa nafasi wangekula vile vile. JK pole raisi wetu una kazi sio ndogo. Hata waziri wa ankara anawatetea mafisadi wa EPA eti pesa zilikua za wafanyabiashara sio za serikali. Mtakoma 2010. yaani mafisadi wamenunua wabunge karibia asilimia 60 ili wasafishwe mnaendelea tu kutumia hela zetu kutuchota akili na kutufanya wajinga. Lakini Mungu yupo Mwakyembe piganeni tuko nyuma yenu angalau mama Malecela na salelii wanajaribu ila jasho la mtu haliendi hivi hivi. Msipozirudisha ninyi watarudisha watoto wenu tena kwa kubembeleza. Acheni wizi mnakua kama Mugabe!

    MISOUP PLZ USINIBANIE MANAKE NASIKIA KUNA WAANDISHI WA HABARI WAMENUNULIWA ILI WASAFISHE MAFISADI. USIKUBALI MH. WA TEGETA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 26, 2008

    Huu ni upuuzi uliopitiliza, Hawa wabunge wetu wao kila siku ni 'kujadili' tu hata yale mambo ambayo yako wazi na yanatakiwa action..

    Mhe wa tegeta, hii issue ya ufisadi umeshakuwa mtaji wa kisiasa kwa wanasiasa wachovu kujipatia jukwaa la kuongea hata ujinga ili kuonekana kuwa ni 'wachangiaji' wakiwa bungeni. Hii nchi ilishapoteza mwelekeo 2005 na sasa ndio tumenasa kwenye tope tukiwa in the middle of no where!

    hapa kuna nini cha kujadili tena mpaka mjadala ufufuliwe. Hata Mwakyembe mwenyewe nae anaanza kuchemsha, kama anajua amefanya kazi sahihi kwanini aanze kutaka kuleta ligi zisizo za msingi. Anyamaze ili atakaejaa anga zake ampe kubwa ya kisheria au kinidhamu kwa mujibu wa taratibu na kanuni za Bunge.
    Noana nae kaanza kulewa sifa na sasa anaanza kujipakaza!


    Mume Wangu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 26, 2008

    mi nashauri tujitoe mhanga kwenye huo mkutano wao wa nec,tutakuwa tumesafisha mafisad kwa asilimia kubwa

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 26, 2008

    'mfisadi wana nguvu za ajabu sana' alisema PM Pinda. Na hapa hiyo nguvu inaanza kujidhihirisha kiasi cha kununua wahishiwa wabunge wetu ambao wakati ripoti inatolewa waliiunga kwa asilimia mia!!! Bongo hiyo!!!
    ninapendekeza mambo mawili, moja la kushughulikia tatizo la sasa na pili ni la muda mrefu. mosi, spika au rais auende tume ya kuchunguza kamati teule ilivyofanya kazi na ipewe muda wa miezi sita. pili, tupiganie mageuzi ya katiba na kipengee kimojawapo kiwe kwamba kila atakayetakiwa kugombea urais pamoja na kuwa na elimu (ya makaratasini) inayotakiwa, kuchunguzwa maadili yake, nk, pia achunguzwe IQ yake na chombo huru. lazima tuwe na viwango.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 26, 2008

    Nadhani hao wanaotaka kusafishwa waulizwe mali walizonazo wamezipataje na waonyeshe jinsi walivyolipia kodi. Hapa ndipo mahali pa kuanzia kama tupo serious, ni rahisi kukwepa suala na Richmond na mengine yanayohusu rushwa kwa kuwa ushahidi ni mgumu ila mali walizonazo zinadhihirisha kila kitu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 26, 2008

    rich wott??rich mond
    rich wottt?rich mond

    my cool people will know what i mean

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 26, 2008

    Rushwa,'CORRUPTION',ndugu zangu Watanzania haikuanza Jana wala Majuzi hapa nchini.Ina historia ndefu.Hivi sasa Rushwa hapa nchini umegeuka kuwa MBUYU ambao mizizi yake hivi sasa imeshafika mbali sana.'Kwa wenzetu hawa waliobobea katika Uongozi Uliokithiri kwa Rushwa'ukizungumzia kuhusu kitu kinacho itwa Rushwa hawakuelewi!Kwa kweli watakushangaa kwa sababu imeshakuwa sehemu ya kawaida kabisa ya maisha yao.Kuna Mzee wangu mmoja alipata kunifunda siku za nyuma kidogo kwamba ,'Mwanangu,katika Ulimwengu huu Ukitokea kuwa Kiongozi katika nafasi ya juu kabisa katika mahala pako pa kazi,ukajitambua kwamba Rushwa imekutawala,basi ili uweze kuwa salama zaidi na uhakika wa kudumu katika nafasi yako ya Uongozi,basi kitu cha kwanza kabisa hakikisha kwamba kila mfanyakazi na mtumishi aliye chini ya madaraka yako hakikisha na yeye anatopea katika maisha ya rushwa,wote mkiimba wimbo mmoja wa rushwa basi utawala wako utakuwa salama zaidi'.Leo hii hata ukisema Watnzania kateni huo Mbuyu,bila ya kuichimbua mizizi yake yote ni kazi bure,Mbuyu utachipua tena.Mtakapokuwa mkijadili EPA,RICHMOND,IMPORT SUPPORT,NYUMBA ZA SERIKALI,AIR TANZANIA,MIGODI,KAGODA AGRICULTURE,na kadha wa kadha kumbukeni kuitanabaisha Mizizi hiyo ya Mbuyu wa Rushwa imeatapakaa umbali gani na katika maeneo gani?Je, ni Shoka la aina gani litakalo himili kishindo hicho cha Panga moja tu Mbuyu chini!Hii Ngoma Watanzania ni Ngoma nzito sana.Lazima tuivalie KIBWEBWE NA MDUMANGE TUUCHEZE PASIPO MASIHARA! Mashetani lazima tuyapunge bila ya kuoneana haya!Wakati wa kuoneana haya umekwisha.Vinginevyo,kizazi kizima kitaangamia!Safari huanza kwa hatua moja.Mwakyembe amepiga hatua ya kwanza,Watanzania tumuunge mkono kwa nguvu zetu sote bila ya masihara!Kila siku wimbo wetu watanzania uwe huu huu mpaka waliohusika waachie ngazi kwa kuona aibu!2010 siyo mbali jamani,tuendelee kuimba wimbo wa Rushwa ni Sumu ya Taifa!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 27, 2008

    Hakuna mtu safi, rushwa ipo toka zamani toka enzi za WAJERUMANI kwani ndio hao waliowapa pesa machief ili watutawale, enzi za WAINGEREZA ndo hao waliokuwa wanasomesha watoto wa machief pekee tu ili kuendeleza utawala wao wa indirect rule, enzi za NYERERE ilikuwepo kama mtakumbuka waziri mmoja alipigwa viboko kwa kula rushwa, ni waziri wa mambo ya ndani wakati ule na alikuwa mwenyeji wa Tabora amekufa juzijuzi tu alikamatwa akichukuwa rushwa akafukuzwa uwaziri na viboko juu - NI FUNDIKIRA, enzi za MWINYI ndo usiseme viwanja vya Dar Mbezi Beach ni kero tupu, Enzi za MKAPA ovyoo, enzi za KIKWETE ovyoo pia lakini pamoja na yote hayo utawala wa haki na sheria lazima ufuatwe, watu waliotuhumiwa wana haki ya kuzikilizwa si kuwahukumu tu bila ya kuwasilikiliza, kwani hamna mtu safi hapa duniani 100% hata MWAKYEMBE mwenywe si safi nakumbuka alikuwa mjumbe wa board ya benki ya NBC na mara nyingi walikuwa wanachukuwa allowance ya vikao bila ya kufanya vikao au bila hata ya kuhudhurua vikao, kwani vikao vilikuwa vimepangwa kwa mwaka mzima na mara kadhaa vilikuwa havifanyiki, na siku ikifika cheque huandikwa na pesa walikuwa wanakula hawakurudisha, na sometimes mjumbe anaweza asije kwenye kikao na atapelekewa cheque na hakatai, nakumbuka mwenyekiti wa board alikuwa anakaa KAMPALA ni mfanyabiashara mkubwa mtanzania alikuwa akiandkiwa cheque kubwa na pengine alikuwa haji na pesa anachukuwa, je huo si wizi na ufujaji wa mali ya umma? so hata Mwakyembe si safi hivyo, wapeni nafasi ya kujitetea pengine tutapata wengine kutokana na tetezi zao na kujuwa full length of the whole issue.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 27, 2008

    Wewe anonym kapo juu wa June 27,1:55am huna lolote Mla Rushwa mkubwa wewe!Unacho kitetea hapo ni nini?Eti Mwakyembe mwenyewe siyo safi!Kwa hiyo?Asipige kelele kama nchi inateketezwa na mchwa!Mzee wa watu Mareh.Fundikira unamhusisha wa nini katika sakata hili?Ili iwe nini?Huyo aliyempiga viboko alikuwa mtu safi siyo kama mlivyozoea kuimba mchiriku!Msigeuze watanzania wajinga babu.Enzi hizo zishapita.Tunamjua Mbaya wetu aliyefuga hili dudde la Rushwa hapa nchini ni nani?Na ndiyo maana kupumzika wanashindwa japo wamechoka ile mbaya!Watafia mezani.Si yetu macho.Lakini,manyunyu ndiyo hayo,mvua iko njiani!Ajabu ya Mbaazi kusingizia Jua1

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...