Ndugu,
kwa mara nyingine tena ninayoheshima kukuomba ututangazie kupitia mtandao wako juu ya misiba mizito iliyoikumba familia ya wanajumuia mwenzetu hapa Dallas,Tx kwa kipindi cha wiki moja.
Wanajumuia wenzetu GEORGE MURO pamoja na mke wake JUDITH MURO wamepatwa na misiba miwili mikubwa katika kipindi cha wiki moja.Ndugu Muro alifiwa na mama yake mkubwa ANANDE HEZEKIEL MURO ambae mazishi yake yamefanyika jana tarehe 6.26.08 huko Masama Moshi.
Kwa bahati mbaya habari zingine za msiba wa baba yake mzazi JUDITH MURO ambae ni mke wa ndugu George Muro mzee MARTIN SWAI zikatokea katika hospital ya Mawenzi mjini Moshi siku hiyo hiyo ambayo kazi ya mazishi imefanyika.
Msiba huu umeleta simanzi ya aina yake huko nyumbani Tanzania na kwa wanajumuia wenzetu ambao tuko nao hapa Dallas.
Kutokana na hali ya misiba miwili kuikumba familia ya wanajumuia wenzetu tunaomba kila moja wetu atakaeweza kuwasiliana nao kwa ajili ya kuwafariji afanye hivyo kwani ni kweli wanahitaji faraja ya kila mwanajumuia katika wakati huu mgumu.
Kutakuwa na ibada nyumbani kwa wafiwa siku ya jumapili saa saba mchana.Tunapenda kawakaribisha wanajumuia wote wa Dallas pamoja na jumuia zingine hapa US katika ibada hii maalumu ya kuwafariji wanajumuia wenzetu.
Anuani; 1652 CROWN POINT DR. FRISCO,TX 75034
SIMU:Res;940 383 9556
Cell George; 940 465 5195
Judith; 940 465 5088
Email:Focusgm3@yahoo.com
Nawatakia baraka za Bwana.
Pastor Abisalom Nasuwa
214 554 7381
pole sana familia ya muro, nitamwabia mzee massawe wa kimara baruti, nitamwambia na mzee mashingiha wa marangu juu ,na vile vile nitamwambia mosha wa hapa uzuri. poleni sana aisee
ReplyDeletePoleni sana ndugu zangu kwa misiba hii mikubwa, Mungu mwenyewe atawapa nguvu na faraja katika kipindi hiki cha majonzi. Natamani ningekuwa karibu tuomboleze pamoja.
ReplyDeleteMy thoughts and prayers are with you.
Ni mimi binamu,
Ohio.
ooh my God.. dada judy and george poleni sana sana. I am so shocked kuingia kwenye blog ya michuzi kufind out kuhusu hii misiba .. i didn know and i truelly hope and pray that god will give u guys strength at this time. will definately call you guys kesho and Michuzi thanks for the good work u are doing.
ReplyDeleteits me (mtoto wa mama mkubwa)