gazeti la daily news linaripoti leo kwamba mke wa aliyekuwa waziri wa nishati na madini nizar karamagi, nadia, ametinga kizimbani jana mahakama ya hakimu mkazi kisutu, dar, kujibu shtaka la wizi wa cheni ya dhahabu na simu ya mkononi. kwa habari zaidi bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2008

    Hee tena? Hii kali kweli kweli

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2008

    Wahenga wa joti walisema,

    Tish tashi tata tatita,

    tishita titata,



    Yani ukiishi na mwizi nawe utakua mwizi.


    NI HAYO TU!!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 27, 2008

    Mwe aibu yaani mke wa waziri naye anakuwa kibaka,wameishiwa namna hiyo au ni tamaa tu,zote zile alizochukua mume wake haziwatoshi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 27, 2008

    Makubwa haya!Sasa TICTS itakuwaje?Si itabidi Bandari yetu ifungwe siku moja ili kuomboleza kadhia hii ifilie mbali?Wenye Tuta nisaidieni....mamaweeeee....mbavu.....kichomiii...nakufa mwenzenu...aaah

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 27, 2008

    Haiwezekani hao wana mambo yao mengine. Labda huyo aliiacha kwnye mgahaw awa huyo mama aliporudi akaikosa sasa anamdai mmiliki. shhs 250,000 hata mimi ningelipa asingekubali adhalilishwe. KIBAO KITAGEUKA WE NGOJA TUONE MAMILIONI YATAKAYODAIWA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 27, 2008

    Hizi ni njama za Karamagi kumdeal ex maiwaifu. Huu ni mtindo wa wabongo wa kutaka kuwaondoa wake zao hasa wa kirusi. Wenye kumbukumbu watakumbuka yule mama wa kirusi wa wizara ya pesa alivyokuwa akisumbuliwa na mume wake kwa kesi zisizo na kichwa wala mkia. Ex Mrs. Karamagi shika uzi hapa umefika ndio kwenu sasa, umevumilia sana yale maziwa ya Wazo Hill, kumchukulia chakula keshasahau? Leo asikuletee za kuleta, shika uzi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 27, 2008

    ina maan yule mke wake Raia wa Urusi ndiye mwenye msala

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 27, 2008

    Hivi inaingia akilini meneja wa mgahawa na mke wa tajiri kama karamagi kuiba kicheni na kisimu uchwara vyenye garama ya tshs 200,000? Hata mwendawazimu hawezi kuafiki kirahisi madai hayo. Mimi sitoi hukumu ila i am thinking loud, hapo kuna mambo siyo wizi! Mrusi wa watu anaweza kuiba lakini siyo cheni na simu isiyozidi £100. Mliotoa maona na kumhukumu mama huyo mnaweza mkawa hamkumtendea haki kwani siasa ni mchezo mchafu sana!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 27, 2008

    Mi sitaki jamani, nini?????

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 27, 2008

    Namfahamu sana Nadia,huyu mama wa Kirusi tangu alipokua na mume wake kitambo hicho Twiga cement,kipindi hicho ikiwa chini ya saruji cooperation,na Karamaji alimpata alipoenda kusoma Urusi,aliporudi huyu mama tulikua tunakula nae kantini ya wafanyakazi,tena msosi wa foleni,waliosoma boarding kipindi kile ,hasa siku inapopikwa wali nyama watakumbuka vurugu yake inakuaje,lakini huyu mama alikua anakomaa hadi anapata msosi,hadi mumewe alipopandishwa cheo akawa C'D wa kampuni,naye akakata mguu kantini.
    Hapa hawa wifi zake naona wamemchoka na yaonekana hawampendi sasa wanaamua kumdhalilisha mama wa watu,haiingii akilini mama huyu leo aibe simu na cheni vyote havifiki hata laki mbili na nusu.Hii ni namna tu ya kumdhalilisha mama wa watu.Kama matatizo ni mume wake ndiye mwenye matatizo kwani hata alipokua wazo aliiba cement zaidi ya tani alfu 4 akauza Uganda na Paul Rwegasira aliyekua waziri wa viwanda enzi hizo alimlinda asipate balaa.
    Mimi sitaki kuamini kwamba huyu mama anaweza kweli kwa kudhamilia eti aibe simu na cheni ya dhahabu vyenye thamani hiyo,haijaniingia akilini,isipokua ninachoweza kusema ni kwamba hao wifi zake ndio wameamua kumpaka matope huyo Mrusi
    Hapo nipo tofauti,

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 27, 2008

    you people dont be hipocrites..mke wa waziri,aibe?mshahara wa waziri mnaujua?eti cheni ya goldi na simu,i bet anavyo vyote hivyo nyumbani kwakwe na zaidi..huyu amekuwa set up..kama walivyomset up michael jackson..

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 27, 2008

    hiko kitu hakipo,kwani mimi nipo Urusi sasa na kwa mda mrefu tuu na nawajua vizuri warusi,kwa kifupi ni kwamba hawa watu hasa wanawake wao hawana kabisa tabia za wizi nina uhakika wa asilimia mia moja huyo mama hajaiba sema kuna kitu nyuma yake jina lake lenyewa(Надежда kwa kirusi)inamaanisha(Hope kwa kiingereza)na (Tumaini kwa kiswahili)wengi wao wenye majina kama lake hapa urusi wanaendana na maana ya hilo jina kwa hiyo hiko kitu hakipo na waache kumpakazia mama wa watu

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 28, 2008

    we wa juu yangu jina linaendaje na tabia ya mtu?! Sasa mnakuwa watu wa ajabu sana! Hata kama asimilia nyingi yao si wezi inamaana huyu hawezi kuwa mwizi? Hizo ni conclusion za kipumbavu! Kama evidence itaonyesha kaiba...ina maana kaiba! Kama ndi iyo kuwa-set up basi imekula kwake! Life goes on... Haya mambo ya kutoa hukumu sijui kutokana na tabia za watu wa huko na majina ni fikra duni!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...